Wakuu,
Asalam aleykum,Tumsifu Yesu Kristo,Mwana kondoo ameshinda,Bwana Yesu asifiwe na wale wengine, Mambo vipi......
Rejeeni kichwa cha habari hapo juu wadau sio siri jambo hili limekuwa likinipa shida kulielewa ktk siasa za Tanzania linawezekanaje. Nimekuwa nikisikia malalamiko mengi sana kuhusiana na jambo hilo kwa namna moja ama nyingine nimekuwa silielewi. Mathalani, unakuta mtu analalamika uwepo wa mfumo kristu kwasababu ya kwamba,shule zinafunguliwa siku ya ijumaa (siku ya ibada kwa Waislam) na hufungwa siku ya Jumapili (siku ya ibada kwa Wakristu). Wengine wanadai kuna MOU iliyowekwa kati ya madhehebu ya dini ya kikristo na Serikali kwaajili ya kuendesha Shule na Mahospitali za madhehebu hayo.
Na ktk thread ya ndugu
MZIMU kwenye jukwaa la Katiba hivi majuzi, alijaribu kuelekeza shutuma zake kwa Kanisa na mfumo kristu kwamba ndivyo vilivyosababisha kutokuwepo kwa Mahakama ya Kadhi ktk Rasimu pendekezi ya Tume ya mabadiriko ya Katiba. Na si huyo tu, Wengi wamekuwa wakihusisha mafanikio ya madhehebu ya dini ya kikristu ktk huduma mbalimbali hapa Tanzania na uwepo wa mfumo Kristu. Ikumbukwe hata Marehemu shehe
Ilunga aliwahi kwa nyakati tofauti kulipigia kelele jambo hili kwamba ndilo limekuwa kikwazo kwa madhehebu ya dini ya Kiislam kushindwa kusonga mbele kimaendeleo.
Katika hali ya kawaida ni rahisi sana kuyapuuza madai haya kutokana na ukweli kwamba ni ngumu kwa Tanzania kuwa na kitu kama hicho ukizingatia ukweli kwamba, Tanzania duniani kote inajinasibu kwamba haina dini bali wananchi wake ndio wenye dini. Na pia kukubaliana na jambo hilo ni ngumu vilevile kutokana na ukweli nilioubainisha hapo juu kwamba Tanzania haina dini. Sasa uwepo wa madai haya na uwingi wake huwezi kusema tu kwamba mtu anadanganya ama kupotosha. Na pia huwezi kusema kwamba anasema ukweli kutokana na ugumu wake wa kuyatekeleza ndani ya siasa za Tanzania.
Ningeomba kwa wale wenye taarifa za kweli na zenye uthibitisho usio na shaka waje hapa watujuze jambo hili liliingiaje nchini Tanzania na linafanyaje kazi na ktk misingi ipi? Kwamba hiyo MOU Iliyofungwa na serikali na hayo madhehebu ya dini ilifungwa lini? Na Je mkataba wake ni wa wazi au kificho? Kama ni wa wazi je wanaweza kutuletea hapa copy ya mkataba huo? Kama ni siri je waliwezaje kujua kama kunakitu kama hicho ilhali jambo hilo limefichwa? Wakitutatulia jambo hili watakuwa wametusaidia sana sisi kizazi cha juzi kati hapa kwani tutaweza kujua ni nini mababu zetu walikikosea ktk siasa za hapa nchini petu, na sisi tufanye nini ili tuweze kuondokana na malalamiko haya ya upande mmoja wa dini kuulalamikia upande mwingine kwamba unapendelewa.
Katika mjadala/Mnakasha huu niwaombe wafuatao ili wawe nguzo na mwongozo wa majadiriano haya
mohamedi Saidi
FaizaFoxy mkandala Mzee Mwanakijiji Pasco Eiyer Ishmael Nguruvi3 Mag3
Pia wake wazee wa "makavu live" kama
MZIMU Ritz THE BIG SHOW Boko haram Matola Ngongo Kigogo Remote na wengineo,Kama mkiweza kutupisha au mkachangia kwa staha kile mnachokijua kuhusiana na mada hii itakuwa vyema sana.
BACK TANGANYIKA