Ushawahi kumsikia mtu anaitwa Jenerali Alexandr Sakharovsky ???
CIA wanadai mwaka 1969 yeye ndiye aliyewaagiza KGB kuyatumia makundi kama Palestinian Liberation Organisation (PLO) na mengine kuteka ndege kama 82 hivi. Halafu likawa linajisifia "Airplane Hijacking is my own invention" teh teh teh teh teh, yaani hili jamaa ndiyo liliwashauri KGB ujinga kwamba kupigana vita vya nyuklia haitasaidia bali kutumia Ugaidi ndiyo njia pekee ya kuweza kupigana vita na mataifa ya magharibi. Kama ukifuatilia utakumbuka kuna kikosi kama The Red Army Faction (RFA) cha ujerumani kilishawahi kuua majenerari wakubwa wa NATO, wakina Sanchez A.K.A Carlos The Jackal alishawahi kuvamia mkutano wa OPEC na kusababisha madhara, baada kutafuta vizuri wakakuta Carlos ni KGB..teh teh teh.
NB: Mimi ndiyo maana mpaka leo nawaheshimu sana CIA, kupigana na Urusi ya Kisovieti ilikuwa siyo kazi ndogo aiseee. Warusi tabia ya Ushushushu imekuwa kama sehemu ya utamaduni wao, and they are very good at it tokea kipindi cha Tsarist Russia. Kuna kipindi walipigana Vita Baridi (Cold War) na Ufalme wa Uingereza tokea mwaka 1813-1907, kama Karne moja hivi, wenyewe wakawa wanaita The Tournament of Shadows (The Great Game). Walikuwa wanagombania kutawala Bara la Asia hasahasa Asia katikati, Urusi alikuwa anataka kuvamia Ottoman Empire ili afike atawale bahari ya Mediterania, Ghuba ya Uajemi, Afghanistani na Bahari ya Hindi.
Baada wa Waingereza kusanua mchezo walimchangia vibaya kweli Mrusi, huku wakiwa na Wafaransa na Waturiki kwenye Vita vya Crimea mwaka 1853-1856. Baada ya kupigwa vibaya mirusi ikachoka kweli kiuchumi ikaamua kumuuzia Marekani Alaska na baada ya hapo, mfalme wa Urusi akaona njia nyepesi kabisa ni Ushushushu na Ujasusi tu. Wanahistoria wanasema Tsarist Chekas walikuwa na Agents of Influence kwenye ukanda wote ule Ulaya Mashariki na Asia katikati (Miaka kama 200 iliyopita). Ukisoma Historia ya Warusi na Waingereza haya yanyotokea leo hayatakushangaza, yameanza mbali sana na wanachogombania ni kile kile.