Declassified KGB documents: Churchill alimuua Stalin

Hata Marekani nayo ilikuwa kubwa mara mia ziadi ya Japani, hapa utasemaje ???
Marekani ilishambuliwa ghafla kwa kushtukiza (japo kuna baadhi hudai shambulio hilo liliachwa litokee makusudi ili ipatikane sababu ya kuingia vitani)

Ila kwa upande wa Warussi baada ya Poland kuvamiwa hiyo ilikuwa ishara tosha kuwa wao pia hawakua salama, Ina maana gharama walizolipa ni kubwa mno kwa nchi iliyojiandaa vizuri
 
Hapana siyo kweli na hili umelitoa wapi mkuu ??? Wakati Ujerumani anavamia Poland, Umoja wa Kisovieti ulikuwa umesaini mkataba wa amani na Ujerumani. Umewahi kusikia kitu kinaitwa The NAZI-SOVIET PACT au The Non-Aggression Pact au The Molotov-Ribbentrop Pact ???

Huu mkataba ulisainiwa mwaka 1939 na Hitler na Stalin walikubaliana kugawana Poland na kutovamiana kijeshi kwa muda wa miaka 10, hivyo uvamizi wa Ujerumani kule Poland uliwekwa kwenye maandishi na kubarikiwa na Wayahudi wa Moscow.

NB: Halafu naomba chanzo kinachosema kwamba Marekani aliacha ashambuliwe maksudi ili apate sababu ya kuingia vitani........
 
Hapo kwenye hoja yako ya kwanza nakubaliana na wewe kwamba Pogroms/Purges ziliondoa wale wataalamu wenye uzoefu wa vita ya kwanza ya dunia na vita ile ya wenyewe kwa wenyewe. Maana wataalamu waliopigana vita ya pili ya dunia kwenye nchi kama Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani wote walikuwa ni maveterani wa vita ya kwanza ya dunia.
Ukianza kumuangalia Adolf Hitler, Winston Churchill na Charles De Gaulle wote walikuwa ni wazoefu sana na vita.

Wataalamu wa Historia wanakwambia Lavrenty Beria peke yake aliamuru vifo vya majasusi na wanajeshi wazoefu wa Urusi zaidi ya eflu kumi na nne hivi (14,000). Leon Trotsky ndiyo aliyeunda jeshi la Urusi pamoja na chombo cha ujasusi wa jeshini (The Main Intelligence Directorate/ The GRU), lakini kwenye vita ya pili ya dunia hakuwepo kabisa. Wataalamu wengine kama Lev Kamenev na Zinoviev nao hawakuwepo. Hivyo jeshi lilikuwa na ombwe kubwa sana wakati wa maandilizi ya vita ya pili ya dunia.

Hoja yako ya pili, kuhusu Muingereza na Mfarasansa kumchangia Mrusi wangemshinda nadhani umeiangalia juu juu sana. Mbona hujajiuliza kwanini Mfaransa na Muingereza pamoja na mataifa zaidi ya ishirini (20) walimchangia Mjerumani kwenye vita zote za dunia lakini bado wakashindwa vibaya japo Mjerumani alikuwa hana rasilimali nyingi kama wao ???

Sidhani ni rahisi hivyo, na kama ingekuwa inawezekana kwao nadhani wangekuwa washaivamia Urusi miaka mingi iliyopita ili kuchukua rasilimali zake. Nasema hivi kwasababu mwaka 1853-1856 Ufalme wa Uingereza, Jamhuri ya Ufaransa, Ufalme wa Sardinia na Dola la Kikalifeti la Uturuki waliuchangia Ufalme wa Urusi kwenye Vita Ya Krimea (The Crimean War), madhara yakawa makubwa sana kwa Urusi lakini wote wakakubali kusaini mkataba wa amani huko Ufaransa (1856, Treaty of Paris).

Napoleon Bonaparte alifika hadi Moscow mwaka 1812 lakini alikiona cha moto, Urusi inalindwa na jiografia yake kama nchi nyingi za Ulaya Mashariki (Eastern Europe) na Asia ya Kati (Central Asia). Baridi na ile milima itakukatisha tamaa tu, hasahasa pale ambapo utaamua kutumia jeshi la ardhini (Infantry).

Hoja yako ya tatu, nayo siikubali sana kwasababu unaposema Muingereza na Mfaransa walikuwa na rasilimali nyingi nashindwa kukuelewa. Rasilimali nyingi ni zipi hizo mkuu Masamila ??? Maana kama wangekuwa na rasilimali nyingi sidhani kama Mfalme wa Uingereza na Waziri Mkuu wa Uingereza wangehangaika kwenye kukopa mabilioni ya pesa kwa Wamarekani. Vita ya kwanza ya dunia, Mjerumani mwenye rasilimali chache alikuwa anadaiwa dola za kimarekani milioni 3 mpaka kufika mwaka 1917 huku Muingereza alikuwa anadaiwa dola za kimarekani milioni 26 hivi.

Kwenye vita ya pili nako Muingereza alikimbilia kukopa pesa kwa Marekani, ambapo alikopa dola za Kimarekani Bilioni 3.7 ambapo ni sawa na dola za Kimarekani Bilioni 53 kwa mwaka 2020. Mikopo ambayo Muingereza alipewa na Marekani wakati wa vita ya pili ya dunia 1941 amemaliza kulipa mwaka 2006, baada ya kufanya marejesho hamsini (50 Installments). Hizo rasilimali nyingi unazozisema Mkuu Masamila ni zipi ????

NB: Ukitaka kuthibitisha hili nisemalo hebu pitia historia ya Njaa ya Bengali (The Bengal Famine) ambayo iliua wahindi zaidi ya milioni 5 baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza Winston Churchill kusema kwamba chakula chote kilichozalishwa kwenye koloni la India kitumike kulishia wanajeshi wanaopigana Vita ya Pili ya dunia. Walipomwambia kwamba akifanya hivyo itatokea njaa kwa Wahindi yeye akajibu akasema hivi "hakuwalazimisha wahindi wazaliane kama panya" au Kiingereza "It's not my fault that Indians breed like rats"

Mkuu Masamila hizo rasilimali za kupigana na Umoja wa Kisovieti wangezitoa wapi hawa Waingereza na Wafaransa ???

Mkuu access to resources ilikuwa ni factor kubwa iliyodetermine uelekeo wa WW2

Mjapan kwa mfano kuna Operesheni muhimu alitakiwa azifanye ndani ya WW2 lakini hazikufanyika sababu ya ufinyu wa resources ambapo mJapan kama ilivyo kwa mjerumani alikuwa hana mafuta(petroleum) mfano Australia ingekuwa eneo muhimu lakini Opereshini ya kuvamia Australia ilikuwa abandoned sababu ya limited oil resources for Japs during that War

Tukija kwa Muingereza na mfaransa hawa jamaa wote wawili by 1930's walikuwa makoloni sehemu zote duniani kiasi kwamba Resources zilikuwepo za kutosha Manpower Uingereza alikuwa anachukua Wahindi,Watu weusi halafu USSR hana tena ubavu

Nadhani tunaofuatilia historia tunafahamu jinsi UK alivyowatumia Wahindi first world war and by second world War koloni la muingereza la India likikuwa na population ya watu milioni mia tatu na hamsini

France akiteam up na UK walikuwa na access to huge resources from Manpower,oil,minerals,food na kila kitu

Tukija kwenye silaha pale Ulaya aliekuwa kidogo anaweza kumatch na Hitler kwenye zana alikuwa UK ushahidi ni ndege za kivita za UK kama Spitfire na Hurricane

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Hapana siyo kweli na hili umelitoa wapi mkuu ??? Wakati Ujerumani anavamia Poland, Umoja wa Kisovieti ulikuwa umesaini mkataba wa amani na Ujerumani. Umewahi kusikia kitu kinaitwa The NAZI-SOVIET PACT au The Non-Aggression Pact au The Molotov-Ribbentrop Pact ???

Huu mkataba ulisainiwa mwaka 1939 na Hitler na Stalin walikubaliana kugawana Poland na kutovamiana kijeshi kwa muda wa miaka 10, hivyo uvamizi wa Ujerumani kule Poland uliwekwa kwenye maandishi na kubarikiwa na Wayahudi wa Moscow.

NB: Halafu naomba chanzo kinachosema kwamba Marekani aliacha ashambuliwe maksudi ili apate sababu ya kuingia vitani........
Hayo ya Marekani kuacha ashambuliwe makusudi siyo chanzo rasmi.

Kuhusu Poland ina maana uvamizi wa Ujerumani huko haiwezi kuwa moja ya chanzo cha kuzuka Vita vya pili vya dunia?
 
Kwahiyo Mkuu Masamila unataka kusema kwamba Hawaii nalo lilikuwa ni Koloni ???
Invasion of Pearl harbour Mjapan alilenga kuangamiza naval fleet fulani ambayo ilikuwa kubwa na ya kutegemewa na USA sio Kukamata eneo

NB:Nimesahau jina la fleet

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Hayo ya Marekani kuacha ashambuliwe makusudi siyo chanzo rasmi.
Kwanini unatumia vyanzo visivyo rasmi kufanya mijadala ???
Kuhusu Poland ina maana uvamizi wa Ujerumani huko haiwezi kuwa moja ya chanzo cha kuzuka Vita vya pili vya dunia?
Vita ya pili ya dunia ilianza pale Uingereza na Ufaransa walipomtangazia vita Mjerumani baada ya kuvamia Poland. Joseph Stalin hakuwa na shida yoyote na Wajerumani kwa kipindi hiki....
 
Mkuu umeitoa wapi hii ???
Halafu kama KGB ndiyo imefanya ku-declassify hizi nyaraka utasemaje kwamba Counter=Intelligence ya Urusi ya Kisovieti ilikuwa dhaifu, wakati walikuwa wanajua mpango wote ??? (Hapa pana ukakasi sana) Hizi nyaraka zingetolewa na MI6 ndiyo zingekuwa na uhalisia kidogo, kuna mengi yana walakini hapa.

Siwezi kukupinga sana lakini tukitumia Common Sense tutabaki na maswali mengi sana:
1. Kwanini walisubiri wamuue Joseph Stalin wakati ameshakuwa mzee na miaka 73 ??
2. Kwanini mnawasahau maadui zake wakubwa wa ndani kama Nikita Khrushchev ??
3. Kwanini hao MI6 hawakuwaua Leonid Brezhnev na Yuri Andropov ??

NB: Kama KGB walikuwa na Intelijensia kinzani dhaifu basi hujawahi kumsikia mtu anaitwa Yuri Totrov (The most ruthless spy catcher in KGB history)..CIA walimfuata kumhonga mabilioni ya pesa baada ya kuanguka Urusi ya Kisovieti ili kujua alikuwa anatumia mbinu gani kukamata CIA na MI6 wengi vile.....
Walipo mfuata aliwapa mbinu na mikakati aliyokuwa akitumia?
 
Kwahiyo Mkuu Masamila unataka kusema kwamba Hawaii nalo lilikuwa ni Koloni ???

Unaweza nisaidia hizi gaps?
George malenkovy..
Inaonekana alimrithi Stalin kabla ya Krushev.
What happened?
Na Yuri alikaa miaka miwili tu
Why?Aliemrithi pia miaka miwili tu?
Why?Why Mikhail alikaa mda mrefu?

Halafu wakati wanamfata Yuri awape Siri za why aliweza kamata spies wengi ilikuwa lini?
 
Georgy Malenkov, Vyacheslav Molotov na Lavrentiy Beria ndiyo walikuwa watu wa karibu sana wa Joseph Stalin. Baada ya Stalin kufariki hawa jamaa ndiyo waliongoza nchi na kutengeneza kitu kama kile cha Roman Triumvirate cha Julius Caesar, Pompey na Crasus. Hawa ndiyo walioisaidia Urusi kupata silaha za kinyuklia kwa kuiba teknolojia kutoka Ujerumani na Marekani.

Malenkov ndiyo alikuwa anasimamia teknolojia ya roketi huku Beria akiwa kiongozi wa NKVD/ The old KGB ambayo ilipenyeza wengi majasusi nchini Marekani kama The Rosenbergs ambao walipeleka siri za nyuklia kule Umoja wa Kisovieti. Hawa watatu walikuwa ndiyo wateule wa Joseph Stalin kwasababu walikuwa wanampa kile anataka.

Malenkov alikuwa ndiyo katibu wa chama (Party Secretary) na kiongozi wa mawaziri (Premier) akisaidiwa na Beria ambaye alikuwa ni waziri mkuu msaidizi (Deputy Premier) na Molotov ambaye alikuwa Waziri wa mambo ya nje (Foreign Minister). Bahati mbaya sana kulikuwa na kundi jingine ambalo lilikuwa na nguvu sana kule Urusi ambalo liliongozwa na Nikita Khrushchev na Marshal Georg Zhukov na watu wengine ambao walitoa mchango mkubwa sana kwenye vita ya dunia.

Hili kundi lilimlazimisha Malenkov avue kofia ya Katibu Mkuu wa chama na kubaki na ile ya uwaziri tu. Baada ya hili Nikita kwa msaada wa Zhukov waliamua kumuua Lavrentiy Beria wakati wa kikao kwa kusema kwamba alikuwa ndiyo msimamizi wa Purges za Joseph Stalin ambazo ziliua mamilioni ya raia. Nikita wakati huu ndiyo alikuwa Katibu Mkuu wa Chama na akajijengea nguvu kubwa mno ambapo baadae mwaka 1955 alimfukuza kazi hadi Georgy Malenkov ambaye alikuwa ndiyo Waziri Mkuu.

Kwenye hili kundi aliyepona alikuwa ni Vyacheslav Molotov kwasababu hakuonesha namna yoyote ile kutaka madaraka. Pia alifahamu ukweli mmoja kwamba yanaweza kutoka mazito kama angefanya hivyo: Joseph Stalin alishawahi kuwaambia hivi "Siku nikitoka mnaweza kupata sana shida" Kweli hakukosea maana hawa jamaa walikuwa ndiyo wanatumiwa kuua na kuteka maadui wa Joseph Stalin.
 
Shukran sana..
Hiyo ya mtu kuuwawa kwenye kikao hatari sana.

Kuna swali la pili hapo
Hawa waliomrithi Krushev mbona wakikaa miaka 2 each?Halafu huyu aliepewa ofa akakataa na USA .why urais ulimshinda?
Na why hakuuwawa? Why miakhail alikaa mda mrefu?
 
Unaweza nisaidia hizi gaps?
George malenkovy..
Inaonekana alimrithi Stalin kabla ya Krushev.
What happened?
Na Yuri alikaa miaka miwili tu
Why?Aliemrithi pia miaka miwili tu?
Why?Why Mikhail alikaa mda mrefu?

Halafu wakati wanamfata Yuri awape Siri za why aliweza kamata spies wengi ilikuwa lini?
Yuri Andropov wakati wa utawala wote wa Leonid Brezhnev yeye ndiye alikuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la ujasusi la K.G.B. Alivyofariki tu Brezhnev basi Yuri akajikuta ndiye mtu mwenye nguvu katika Umoja wa Kisovieti. Nakumbuka niliwahi oneshwa jarida la TIME la mwaka 1982 pale mbele waliweka sura ya Andropov wakisema maneno haya "Meet the new boss". Sasa Andropov alifariki mwaka 1984 na kurithiwa na Konstantin Chernenko: Wanahistoria husema hawa ndiyo walikuwa watawala wa mwisho kutoka kizazi kile cha zamani cha wabolsheviki (Old Bolsheviks)

Yuri aliingia kwenye utawala wakati mbaya sana, tena alikuwa mzee wa miaka 73. Umoja wa Kisovieti ulikuwa umeanza kuporomoka kiuchumi, Vita ya Afghanistani haiwaendei vyema, Bei ya mafuta imeanguka duniani, Poland wakawa na Papa John Paul wa pili na bahati mbaya sana kule upande wa pili wakamchagua Ronald Reagan kuwa raisi.

Yuri alivyoingia tu alijaribu kufanya mabadiliko makubwa sana hasa kwenye uhuru wa kupata habari, teknolojia ya jeshi na uchumi lakini alikuwa ni mzee aliyechoka na afya yake haikuruhusu. Kama unakumbuka kipindi hiki ndiyo alimwandikia hadi Barua mtoto wa Kimarekani aliyeitwa Samantha Smith ambayo ilichapishwa duniani kote na kubadilisha kidogo sura ya Utawala wa Kisovieti mbele ya dunia. Lakini haya hayakusaidia maana nchi ilikuwa ishaporoka baada ya miaka 18 ya kudorora kwa uchumi kulikofanywa na Brezhnev.

Andropov akiwa anafahamu fika madhaifu ya Umoja wa Kisovieti mbele ya Marekani alikuwa kila siku anauliza watu wake kama Marekani anaweza kuwafanyia shambulio la kinyuklia. Maana baada ya ile hotuna ya The EVIL EMPIRE na Ronald Reagan kusema anataka kuanzisha S.D.I (The Strategic Defense Initiative) au Star Wars, Umoja wa Kisovieti walimuita Reagan "A Bellicose Lunatic".

Kitu kikubwa alichofanya Yuri japo alichelewa sana ni kuwaingiza vijana kwenye mfumo na sehemu nyeti. Mikhail Gorbachev ni moja ya vijana waliotumiwa sana na Yuri katika kufanya mabadiliko makubwa wakati Yuri yupo kitandani: Kuna kipindi wakati Yuri yuko kitandani anaumwa sana, Gorbachev alienda kumuona na kumuandikia ujumbe kwamba angependa kufanya mabadiliko makubwa zaidi lakini Yuri alikataa na kumuambia "You are asking for too much".

Hadi Yuri anafariki mwaka 1984 Mikhaili Gorbachev alikuwa ameshajijengea msingi mkubwa sana ndani ya chama na mbele ya kizazi kipya ambacho kilikuwa kinapenda mabadiliko. Baada ya Chernenko naye kukata moto, basi Gorbachev ndiyo akawa ni moja kati ya vijana ambao waliaminika kwamba wangeleta mabadiliko ya kiuchumi na kumaliza vita baridi. Lakini nalo hili halikufaa Umoja wa Kisovieti ulikuwa ushafikia njia mbaya sana ya kutoweza kupona kirahisi. Gorbachev alilirithi bomu akitegemea angeweza kulitegua kumbe likamlipukia.
 
Unaweza nisaidia hizi gaps?
George malenkovy..
Inaonekana alimrithi Stalin kabla ya Krushev.
What happened?
Na Yuri alikaa miaka miwili tu
Why?Aliemrithi pia miaka miwili tu?
Why?Why Mikhail alikaa mda mrefu?

Halafu wakati wanamfata Yuri awape Siri za why aliweza kamata spies wengi ilikuwa lini?
Mikhail Gorbachev hakukaa muda mrefu kwenye madaraka, sema yeye alidumu kuliko Andropov na Chernenko kwasababu alikuwa ni kijana mdogo wa miaka 54 tu wakati anakuwa Katibu Mkuu wa Chama (The General Secretary) mwaka 1985. Kipindi hili watu walisema wanataka vijana wenye mawazo mapya na siyo wale wazee wa zamani (The Old Bolsheviks). Mikhail akaoneka kwamba ndiye anafaa maana alikuwa na mawazo ya tofauti kidogo na wale wazee wa zamani.

Upande wa pili aliwaahidi Wasovieti kwamba angemaliza vita baridi, jambo ambalo pia liliwafurahisha maadui wa Wasovieti. Margaret Thatcher alinukuliwa akisema kwamba "Gorbachev is a man i can do business with" kwamba ni mtu wa kuaminika. Sasa hii taswira nzuri aliyoijenga nyumbani na nje ya mipaka ndiyo ilimfanya akae muda mrefu madarakani, japo K.G.B na The Red Army hawakupenda jinsi alivyokuwa anaongoza nchi.

Gorbachev kuna mambo hakuyatilia maanani kama kushughulikia watu kama Boris na walevi wenzake wa Ukraine na Belarus ambao ndiyo walipata nguvu kubwa sana na kupelekea kwenda kusaini Mkataba kwenye msitu wa Belovezhva (The Belovezhva Accords) ambao ndiyo uliua kabisa Umoja wa Kisovieti. Kuna sehemu ananukuliwa akisema hivi "Ningejua ningesikiliza ushauri na kumteua Boris Yeltsin awe balozi wa kwenye nchi ya ulimwengu wa tatu, huko angeenda na kufa kwa ulevi" Wachina wana utani mmoja hivi kuhusu Gorbachev ambao wanasema hivi "Gorbachev is a good example of things not to do here in China"
 
Halafu wakati wanamfata Yuri awape Siri za why aliweza kamata spies wengi ilikuwa lini?
Hili lilifanyika baada ya Jamhuri ya Kisovieti kuanguka, wakurugenzi wa C.I.A walitaka kumkamata muhusika mkuu aliyechoma majasusi wengi wakihisi labda kuna mtu ndani ya C.I.A alikuwa anatoa siri, kumbe kuna jamaa tu lina akili nyingi limejifungia sehemu linawachora tu.
 
Mkuu access to resources ilikuwa ni factor kubwa iliyodetermine uelekeo wa WW2

Mjapan kwa mfano kuna Operesheni muhimu alitakiwa azifanye ndani ya WW2 lakini hazikufanyika sababu ya ufinyu wa resources ambapo mJapan kama ilivyo kwa mjerumani alikuwa hana mafuta(petroleum) mfano Australia ingekuwa eneo muhimu lakini Opereshini ya kuvamia Australia ilikuwa abandoned sababu ya limited oil resources for Japs during that War.

France akiteam up na UK walikuwa na access to huge resources from Manpower,oil,minerals,food na kila kitu

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app

Mkuu Masamila umetoa hoja nzuri sana na naomba nijibu hii hoja yako katika sura tatu. Suya ya kwanza ni mkakati wa kijiografia na sura ya pili ni mkakati wa kisiasa na kiusalama na sura ya tatu ni makakati wa kiuchumi. Naomba nianze na sura ya kwanza ya mkakati wa kijiografia.

SURA YA KWANZA: Kimkakati nchi kama Ufalme wa Uingereza ambazo zinakuwa na makoloni mbali kabisa na mipaka yake kuzungukwa na bahari huwa tunaziita (A Thelassocracy). Uingereza ndilo dola kubwa kuwahi tokea duniani na lilimiliki asilimia 22% ya ardhi hadi kufika mwaka 1922: Lakini bahati mbaya sana lilikuwa ni A Thelassocracy. Tofauti na madola mengine makubwa kama Urusi na Mongolia ambayo majimbo yao yalilikuwa yameungwanisha hili kimkakati tunaita (A Contiguous Empire), ilikuwa ni lazima Uongereza avuke bahari ili kuendesha makoloni yake.

Hatari ni kwamba pale unapokuwa na makoloni mengi na ukapambana na adui mwenye mkono mrefu kama Umoja wa Kisovieti au Marekani unaweza kweli kuyalinda kwa urahisi hayo makoloni yaliyo maelfu ya kilomita mbali na wewe ???

Uhalisia wa kimkakati sasa ni huu: Muingereza na Mfaransa ili kwenda kwenye makoloni yao ya Afrika na Asia walikuwa lazima wapite kwenye mfereji wa Gibraltar (The Strait of Gibraltar) kisha waingie bahari ya Mediterranea hadi mfereji wa Suez Misri ndipo wafike Pasifiki. Sasa Adolf Hitler alipanga kitu kinaitwa The Mediterranean Strategy ambapo alitaka kumtumia rafiki yake Franco Dikteta wa Uhispania ili kufunga mfereji wa Gibraltar na kukata mawasiliano baina ya makoloni na nchi mama. Hili halikufanyika kwasababu Franco alisema kwamba Uhispania haitafungamana na upande wowote wakati wa vita.

Lakini lingefanikiwa sidhani kama Uingereza na Marekani wangeweza kupambana na Ujerumani hata zaidi ya mwaka maana wasingeweza tena kupita pale Gibraltar. Naomba nikupe mifano hai ya hichi nachokisema na udhaifu wa Muingereza: Kipindi cha Vita Baridi, Wasovieti wakifahamu fika juu ya huu uadhaifu, Mwaka 1956-1957 Gamal Abdi Nasser akishauriwa na Wasovieti aliamua kutaifisha mfereji wa Suez Canal. Ulaya nzima walichanganyikiwa kwamba utajiri wao kutoka kwenye makoloni ungetumia njia gani kufika Ulaya hivyo ikabidi Muingereza, Mfaransa na Muisrael wavamie Misri.

Mfano wa pili, mwaka 1942 Mjapani alivyokamata Singapore unadhani lilikuwa ni jambo rahisi kwa mataifa ya Ulaya kama Uingereza na Ufaransa ??? Wote tunafahamu umihimu wa mfereji wa Malacca kibiashara na kiusafiri ukiunganisha Ulaya na Asia. Sasa hizo ndizo hatari za kijiografia kwa nchi ambayo ni A THELASSOCRACY kama Uingereza kutaka kupigana na A CONTIGOUS EMPIRE kama Umoja wa Kisovieti

SURA YA PILI: Kisiasa kuwa na makoloni ni sawa na kuweka mzinga wa nyuki maeneo ya nyumbai, akitokea mtu tu kautingisha lazima hadi wewe mfugaji utang'atwa tu. Adolf Hitler anasema hivi "ningejua ningefanya kama Wasovieti wanavyofanya, nisingetawala watu wa ulimwengu wa tatu bali ningeunga mkono harakati zao za kudai uhuru ili kusambaza hujuma ambazo zingeweza kufanya nchi za Ulaya zianguke"

Haya maneno aliyasema mwaka 1945 siku chache kabla Ujerumani haijasalimu amri na aliyasema kwa majuto mengi. Kama angeunga mkono juhudi za wapigania Uhuru kuanzia miaka ya 1933 basi sidhani kama Muingereza angeweza kupambana na Ujerumani hata kwa mwaka moja. Sasa VITA BARIDI (The Cold War) ilipiganwa na mashirika ya kijasusi ya Kisovieti (INO, COMINTERN na NKVD) kwa sura ya kufadhili harakati za wapigania uhuru.

Marekani nao walifahamu huu udhaifu wa Muingereza ndiyo maana wakaamua kuanza kuunga mkono juhudi za Uhuru chinichini kwenye makoloni yote ya Muingereza. Mwishowe Muingereza alitikishwa kwenye makoloni yote na akaamua kuachia. Ubaya wa hili ni kwamba endapo pale nchi mama (The Metropolitan State) inapokataa kutoa uhuru basi ni lazima usalama wa raia wake na mali zake kwenye kwenye makoloni hayo utakuwa kwenye hatari kubwa kubwa sana.

Naomba nikupe mfano hai wa hili: Mwaka 1946 Wadi uhuru wa Kiyahudi walilipua Hotel Waingereza (King David Hotel) ili kutuma ujumbe kwamba hili eneo ni letu na mtoke. Mwaka huohuo tena kule Vietnam (Indo-China) wapigania Uhuru walianza kupigana na Mfaransa na kusababisha vita kubwa ambayo vilidumu hadi mwaka 1975.

Huu ujanja alikuja kufanyiwa Umoja wa Kisovieti kuanzia miaka ya 1980's na mabepari wakisaidiwa na Kanisa Katoliki chini ya Papa John Paul II. Nchi za Ulaya Mashariki ziliahidiwa kupewa uhuru kama ule wa nchi za Ulaya Magharibi ambazo zilikuwa zimefanikiwa sana kiuchumi. Wasovieti walipotaka kutumia nguvu ndipo wadai uhuru wakaanza kufanya hujuma dhidi yao, mara unasikia The Solidarity Movement, mara hiki, mwisho wa siku kapoof. Sasa kama A Contiguous Empire kama Umoja wa Kisovieti ilifanywa hivi unadhani nchi ambayo iko mbali na makoloni kama Uingereza wangepona kweli kwa kutegemea makoloni ???

Mfano wa mwisho kwenye hii hoja: Mapinduzi ya Haiti (The Haitian Revolution) 1791-1804 yalifanyika kipindi Ulaya nzima inapigana vita na Mfalme Napoleon wa Ufaransa. Haiti ilikuwa ni moja ya koloni tajiri na muhumu sana kwa Ufaransa. Sasa ili kuiumiza Ufaransa Waingereza na Wahispania chini kwa chini waliwaunga mkono watu weusi na kumshawishi sana Toussaint Louverture kuua mamia ya walowezi wa kifaransa kule Haiti na kujitangazia uhuru ili Wafaransa wapate hasara. Kweli wafaransa walipata hasara kubwa sana maana koloni halikutawalika tena kwasababu watu washaonja uhuru. (Mfaransa naye alifanya hivihivi kwa Muingereza kipindi Marekani anadai uhuru wake kwa mtutu wa bunduki)

SURA YA TATU: Hoja yarasilimali za kwenye makoloni haziwezi kukusaidia sana kwasababu mwisho wa siku makoloni hata uyawekee pesa nyingi ni lazima yatakuwa huru tu. Ndiyo maana Waziri Mkuu wa Ujerumani Otto Von Bismarck alikuwa hayapendi sana, akisema kwamba unapowekeza sana kwenye makoloni jua kwamba kuna siku yatakuwa huru tu. Hili ndilo ukichanganya na sababu ya pili, ni njia tosha kabisa kufanya usitegemee rasilimali za makoloni, hasahasa pale kipindi cha vita kubwa kama zile za dunia.

Ina maana adui yako akikamata makoloni basi na uchumi wako ni lazima uyumbe pakubwa tu. Pia Muingereza na Mfaransa wasingeweza kutumia zile rasilimali za kinyonyaji kwa wingi bila kusababisha hasara kwa wazawa wa kwenye makoloni. Mfano Mzuri ni njaa ya Bengal ilivyoua mamilioni ya watu: Lakini ukiangalia unaweza kusema Muingereza anasifiwa kwamba yeye ndiyo alikuwa kitovu cha kuzalisha wakati wa vita ya pili ya dunia, ukweli ni kwamba alikuwa kwenye hali mbaya sana ambayo hakuweza kusimama hata baada ya vita kuisha.

RASILIMALI ZA MAKOLONI SIYO ZA KUTEGEMEA HATA KIDOGO, HAKUNA TAIFA AMBALO HAZIJAWAHI KUWATOKEA PUANI...........
 
Mkuu ASANTE sana.hii ni Elimu kubwa.
 
Back
Top Bottom