fidel castro wapili
JF-Expert Member
- Mar 18, 2017
- 3,497
- 2,919
Kweli adui hawezi kujua siri yako pasipo usaliti wa mtu wa karibu
Stalin alizingua Spanish civil war peke yake ila huku kungine alienda toe to toe na WestSifahamu matokeo yangekuwaje, lakini kitu ninachofahamu ni kwamba vita ile ingekuwa ndefu sana na ingevaa sura mpya kwasababu ya Uchina kuingilia ile vita. Pia nadhani ingefika kipindi nchi kama Japan na Taiwan zingehusishwa moja kwa moja na kugeuzwa uwanja wa vita. Wakina Jenerali Douglas McArthur walipendekeza kwamba Marekani itumie hadi silaha za Kinyuklia dhidi ya Uchina ambao waliingilia vita ili kuwasaidia Korea Kaskazini.
Kama wasingekaa chini na kutafuta suluhu nadhani na vita ingeendelea nadhani basi tungeshuhudia silaha za kinyuklia zikitumika na kusingekuwa na mshindi kwasababu pande zote hazikukubali kumwachia kila mtu achukue vyote.
Achana na General Yuri Drozdov wa Illegals Program.
Huyu alikuwa ni Counter Intelligence Officer based in Japan.
Yaani yeye alikuwa ni msomi wa Chuo Kikuu na alikamata sana majasusi wa CIA na MI6 kwa wingi.
NATO walichanganyikiwa sana wakawa wanahisi labda kuna watu wanatoa siri za CIA na MI6; kumbe jamaa katembelea nchi zote za Warsaw Pact na zile za Kikomunisti duniani akafanya utafiti mkubwa kuhusu tabia za kipekee (Peculiar Human Behavior) za majasusi wa CIA na MI6 na akatengeneza Bango-Kitita (Matrix) kubwa kweli akawapelekea KGB.
Hivyo mle ndani kukawa na somo kabisa wanafundishwa majasusi wa KGB-Counter Intelligence kuhusu CIA behaviour. Wanakwambia zaidi ya asilimia 85% ya tabia zilizoorodheshwa mle zilikuwa ni za majasusi wa CIA na MI6. Baada ya kuanguka Urusi ya kisovieti CIA walimfuata awaeleze alitumia mbinu gani kuwakamata wengi vile. Baadae wakaja kuambiwa ni kutumia Peni, Karatasi na kuangalia kwa jicho la tatu tu......!
NB 1: Tafuta kitabu cha Oxford kinaitwa "Near and distant neighbours: A new history of soviet Intelligence (The Extraordinary achievements of Yuri Totrov Page 251 na Page 252)" kimeandikwa na Jonathan Haslam. Sasa huwa najiuliza sana maswali kama: Hivi miaka ya 70's na 80's KGB walikuwa wanafanya hivi unategemea leo ndiyo nchi yenu inakutana na majasusi wa namna hii hivi kuna kupona kweli ???
NB 2: Yuri Totrov ni uthibitisho tosha kwamba hakuna silaha kubwa duniani kama Ubongo wa mwanadamu, pia hakuna kitu chenye nguvu kama Human Intelligence. Aliweza kufanya ujasusi kwa kutumia COMMON SENSE na kuweza kushindana na CIA ambayo ilikuwa iko mbele sana kwenye swala la teknolojia na fedha.
Watanzania tuna nini cha kujifunza hapa ???
Tunaweza tusiwe na pesa nyingi na teknolojia kubwa sana lakini tukafanikiwa kwa kiasi kikubwa mno katika kulinda maslahi mapana ya nchi. Japo ni kweli kwa dunia ya sasa tunahitaji pesa na teknolojia lakini hili halitakiwi kutufanya tulemae na kutegemea kuomba msaada wa taarifa au kununua vyombo vya kijasusi kutoka nchi za nje: Ni hatari sana kwetu.......
NB: Ukitaka hiki kitabu kinachomzungumzia Yuri Totrov utakipata kwenye bandiko namba [HASHTAG]#120[/HASHTAG], tunamshukuru sana Mkuu Palantir kwa kufanya jitihada za ziada kututafutia nakala yake (Softcopy) ili wengi wakisome.
CC: Consigliere, Red Giant , zitto junior , chige , mng'ato, Mbimbinho, Da'Vinci , Dragoon , mngony , Bukyanagandi
Siyo Uhispania tu, Joseph Stalin na Umoja wa Kisovieti walishindwa kufanikisha uvamizi wa Ufinishi (Finland) mnamo mwaka 1939 hadi wakaishia kusaini mkataba wa amani mwaka 1940 huku Umoja wa Kisovieti ukiwa umedhalilishwa na kupewa adhabu ya kufukuzwa kwenye Jumuiya ya Umoja wa Mataifa (The League of Nations). Hii vita ilikuwa inaitwa The Winter War, na walikufa wanajeshi wa Urusi zaidi ya 40,000.Stalin alizingua Spanish civil war peke yake ila huku kungine alienda toe to toe na West
Chini Wachina waliingia front huju juu Stalin kapeleka marubani kabisa wa Soviet Red Army
Siyo Uhispania tu, Joseph Stalin na Umoja wa Kisovieti walishindwa kufanikisha uvamizi wa Ufinishi (Finland) mnamo mwaka 1939 hadi wakaishia kusaini mkataba wa amani mwaka 1940 huku Umoja wa Kisovieti ukiwa umedhalilishwa na kupewa adhabu ya kufukuzwa kwenye Jumuiya ya Umoja wa Mataifa (The League of Nations). Hii vita ilikuwa inaitwa The Winter War, na walikufa wanajeshi wa Urusi zaidi ya 40,000.
Kushindwa kufanya vizuri kwa vikosi vya Umoja wa Kisovieti kule Uhispania na Ufinishi ndiyo moja za sababu zilizomfanya Adolf Hitler avamie Urusi mwaka 1941 kutekeleza kile wanaita The Drang-nach-osten au A March to the East. Hivyo mara nyingine unaweza ukawa mkubwa na bado ukazidiwa: Vita vina mambo mengi sana.
Hapo kwenye hoja yako ya kwanza nakubaliana na wewe kwamba Pogroms/Purges ziliondoa wale wataalamu wenye uzoefu wa vita ya kwanza ya dunia na vita ile ya wenyewe kwa wenyewe. Maana wataalamu waliopigana vita ya pili ya dunia kwenye nchi kama Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani wote walikuwa ni maveterani wa vita ya kwanza ya dunia.Mwamba Stalin madhaifu yake alikuwa katili kupitiliza
Ila kwa Finland sidhani kama kulikuwa na namna ya kukwepa kichapo, Purges iliondoa wenye uzoefu jeshini halafu prior to wwii USSR hawakuwa na zana nzuri za kivita
I couldnt Imagine kama France akiteam na Britain wangeamua kuivamia USSR before world war two Kama USSR angesurvive uvamizi kama huo given how these two country how they had the access to vast resources unlike Germany maana nilikuwa nacheki Brits wa WW2 aisee walikuwa vizuri kwa zana sasa sijui kama Wangeshindwa kuiangusha USSR hasa kufuafia upumbavu wa Stalin kuua maafisa wa jeshi tena karibia wote
Dah!...hawa mabeberu bhana...hivi mkuu bila uingiliaji wa Marekani (baada ya pearl harbor) unadhani ingekua rahisi kwa USSR na UK peke yao kuyashinda majeshi ya Wajapani na majeshi ya Hitler?Hapo kwenye hoja yako ya kwanza nakubaliana na wewe kwamba Pogroms/Purges ziliondoa wale wataalamu wenye uzoefu wa vita ya kwanza ya dunia na vita ile ya wenyewe kwa wenyewe. Maana wataalamu waliopigana vita ya pili ya dunia kwenye nchi kama Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani wote walikuwa ni maveterani wa vita ya kwanza ya dunia.
Ukianza kumuangalia Adolf Hitler, Winston Churchill na Charles De Gaulle wote walikuwa ni wazoefu sana na vita.
Wataalamu wa Historia wanakwambia Lavrenty Beria peke yake aliamuru vifo vya majasusi na wanajeshi wazoefu wa Urusi zaidi ya eflu kumi na nne hivi (14,000). Leon Trotsky ndiyo aliyeunda jeshi la Urusi pamoja na chombo cha ujasusi wa jeshini (The Main Intelligence Directorate/ The GRU), lakini kwenye vita ya pili ya dunia hakuwepo kabisa. Wataalamu wengine kama Lev Kamenev na Zinoviev nao hawakuwepo. Hivyo jeshi lilikuwa na ombwe kubwa sana wakati wa maandilizi ya vita ya pili ya dunia.
Hoja yako ya pili, kuhusu Muingereza na Mfarasansa kumchangia Mrusi wangemshinda nadhani umeiangalia juu juu sana. Mbona hujajiuliza kwanini Mfaransa na Muingereza pamoja na mataifa zaidi ya ishirini (20) walimchangia Mjerumani kwenye vita zote za dunia lakini bado wakashindwa vibaya japo Mjerumani alikuwa hana rasilimali nyingi kama wao ???
Sidhani ni rahisi hivyo, na kama ingekuwa inawezekana kwao nadhani wangekuwa washaivamia Urusi miaka mingi iliyopita ili kuchukua rasilimali zake. Nasema hivi kwasababu mwaka 1853-1856 Ufalme wa Uingereza, Jamhuri ya Ufaransa, Ufalme wa Sardinia na Dola la Kikalifeti la Uturuki waliuchangia Ufalme wa Urusi kwenye Vita Ya Krimea (The Crimean War), madhara yakawa makubwa sana kwa Urusi lakini wote wakakubali kusaini mkataba wa amani huko Ufaransa (1856, Treaty of Paris).
Napoleon Bonaparte alifika hadi Moscow mwaka 1812 lakini alikiona cha moto, Urusi inalindwa na jiografia yake kama nchi nyingi za Ulaya Mashariki (Eastern Europe) na Asia ya Kati (Central Asia). Baridi na ile milima itakukatisha tamaa tu, hasahasa pale ambapo utaamua kutumia jeshi la ardhini (Infantry).
Hoja yako ya tatu, nayo siikubali sana kwasababu unaposema Muingereza na Mfaransa walikuwa na rasilimali nyingi nashindwa kukuelewa. Rasilimali nyingi ni zipi hizo mkuu Masamila ??? Maana kama wangekuwa na rasilimali nyingi sidhani kama Mfalme wa Uingereza na Waziri Mkuu wa Uingereza wangehangaika kwenye kukopa mabilioni ya pesa kwa Wamarekani. Vita ya kwanza ya dunia, Mjerumani mwenye rasilimali chache alikuwa anadaiwa dola za kimarekani milioni 3 mpaka kufika mwaka 1917 huku Muingereza alikuwa anadaiwa dola za kimarekani milioni 26 hivi.
Kwenye vita ya pili nako Muingereza alikimbilia kukopa pesa kwa Marekani, ambapo alikopa dola za Kimarekani Bilioni 3.7 ambapo ni sawa na dola za Kimarekani Bilioni 53 kwa mwaka 2020. Mikopo ambayo Muingereza alipewa na Marekani wakati wa vita ya pili ya dunia 1941 amemaliza kulipa mwaka 2006, baada ya kufanya marejesho hamsini (50 Installments). Hizo rasilimali nyingi unazozisema Mkuu Masamila ni zipi ????
NB: Ukitaka kuthibitisha hili nisemalo hebu pitia historia ya Njaa ya Bengali (The Bengal Famine) ambayo iliua wahindi zaidi ya milioni 5 baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza Winston Churchill kusema kwamba chakula chote kilichozalishwa kwenye koloni la India kitumike kulishia wanajeshi wanaopigana Vita ya Pili ya dunia. Walipomwambia kwamba akifanya hivyo itatokea njaa kwa Wahindi yeye akajibu akasema hivi "hakuwalazimisha wahindi wazaliane kama panya" au Kiingereza "It's not my fault that Indians breed like rats"
Mkuu Masamila hizo rasilimali za kupigana na Umoja wa Kisovieti wangezitoa wapi hawa Waingereza na Wafaransa ???
Hapa ndo naskiaga Mahatma Ghandi alilaani kwa kutumia chumvi?..Hapo kwenye hoja yako ya kwanza nakubaliana na wewe kwamba Pogroms/Purges ziliondoa wale wataalamu wenye uzoefu wa vita ya kwanza ya dunia na vita ile ya wenyewe kwa wenyewe. Maana wataalamu waliopigana vita ya pili ya dunia kwenye nchi kama Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani wote walikuwa ni maveterani wa vita ya kwanza ya dunia.
Ukianza kumuangalia Adolf Hitler, Winston Churchill na Charles De Gaulle wote walikuwa ni wazoefu sana na vita.
Wataalamu wa Historia wanakwambia Lavrenty Beria peke yake aliamuru vifo vya majasusi na wanajeshi wazoefu wa Urusi zaidi ya eflu kumi na nne hivi (14,000). Leon Trotsky ndiyo aliyeunda jeshi la Urusi pamoja na chombo cha ujasusi wa jeshini (The Main Intelligence Directorate/ The GRU), lakini kwenye vita ya pili ya dunia hakuwepo kabisa. Wataalamu wengine kama Lev Kamenev na Zinoviev nao hawakuwepo. Hivyo jeshi lilikuwa na ombwe kubwa sana wakati wa maandilizi ya vita ya pili ya dunia.
Hoja yako ya pili, kuhusu Muingereza na Mfarasansa kumchangia Mrusi wangemshinda nadhani umeiangalia juu juu sana. Mbona hujajiuliza kwanini Mfaransa na Muingereza pamoja na mataifa zaidi ya ishirini (20) walimchangia Mjerumani kwenye vita zote za dunia lakini bado wakashindwa vibaya japo Mjerumani alikuwa hana rasilimali nyingi kama wao ???
Sidhani ni rahisi hivyo, na kama ingekuwa inawezekana kwao nadhani wangekuwa washaivamia Urusi miaka mingi iliyopita ili kuchukua rasilimali zake. Nasema hivi kwasababu mwaka 1853-1856 Ufalme wa Uingereza, Jamhuri ya Ufaransa, Ufalme wa Sardinia na Dola la Kikalifeti la Uturuki waliuchangia Ufalme wa Urusi kwenye Vita Ya Krimea (The Crimean War), madhara yakawa makubwa sana kwa Urusi lakini wote wakakubali kusaini mkataba wa amani huko Ufaransa (1856, Treaty of Paris).
Napoleon Bonaparte alifika hadi Moscow mwaka 1812 lakini alikiona cha moto, Urusi inalindwa na jiografia yake kama nchi nyingi za Ulaya Mashariki (Eastern Europe) na Asia ya Kati (Central Asia). Baridi na ile milima itakukatisha tamaa tu, hasahasa pale ambapo utaamua kutumia jeshi la ardhini (Infantry).
Hoja yako ya tatu, nayo siikubali sana kwasababu unaposema Muingereza na Mfaransa walikuwa na rasilimali nyingi nashindwa kukuelewa. Rasilimali nyingi ni zipi hizo mkuu Masamila ??? Maana kama wangekuwa na rasilimali nyingi sidhani kama Mfalme wa Uingereza na Waziri Mkuu wa Uingereza wangehangaika kwenye kukopa mabilioni ya pesa kwa Wamarekani. Vita ya kwanza ya dunia, Mjerumani mwenye rasilimali chache alikuwa anadaiwa dola za kimarekani milioni 3 mpaka kufika mwaka 1917 huku Muingereza alikuwa anadaiwa dola za kimarekani milioni 26 hivi.
Kwenye vita ya pili nako Muingereza alikimbilia kukopa pesa kwa Marekani, ambapo alikopa dola za Kimarekani Bilioni 3.7 ambapo ni sawa na dola za Kimarekani Bilioni 53 kwa mwaka 2020. Mikopo ambayo Muingereza alipewa na Marekani wakati wa vita ya pili ya dunia 1941 amemaliza kulipa mwaka 2006, baada ya kufanya marejesho hamsini (50 Installments). Hizo rasilimali nyingi unazozisema Mkuu Masamila ni zipi ????
NB: Ukitaka kuthibitisha hili nisemalo hebu pitia historia ya Njaa ya Bengali (The Bengal Famine) ambayo iliua wahindi zaidi ya milioni 5 baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza Winston Churchill kusema kwamba chakula chote kilichozalishwa kwenye koloni la India kitumike kulishia wanajeshi wanaopigana Vita ya Pili ya dunia. Walipomwambia kwamba akifanya hivyo itatokea njaa kwa Wahindi yeye akajibu akasema hivi "hakuwalazimisha wahindi wazaliane kama panya" au Kiingereza "It's not my fault that Indians breed like rats"
Mkuu Masamila hizo rasilimali za kupigana na Umoja wa Kisovieti wangezitoa wapi hawa Waingereza na Wafaransa ???
Naomba nikujibu kwa kukuuliza swali hili: Hivi unadhani Marekani na mapesa yake yote yale angeweza kupigana peke yake na vikosi vya Ujerumani na Japani bila msaada wa Uingereza na Mrusi na akashinda ???Dah!...hawa mabeberu bhana...hivi mkuu bila uingiliaji wa Marekani (baada ya pearl harbor) unadhani ingekua rahisi kwa USSR na UK peke yao kuyashinda majeshi ya Wajapani na majeshi ya Hitler?
Mkuu nadhani Marekani (hasa jeshi lake la anga na majini/navy) ndiyo iliyotoa upinzani mkubwa kwa majeshi ya Wajapani na vikosi vya Hitler huko Ulaya na ukanda wa Pacific.Naomba nikujibu kwa kukuuliza swali hili: Hivi unadhani Marekani na mapesa yake yote yale angeweza kupigana peke yake na vikosi vya Ujerumani na Japani bila msaada wa Uingereza na Mrusi na akashinda ???
NB: Pia unapozungumzia mchango nadhani uangalie haya mambo yafuatayo:-
- Urusi walikufa watu milioni ishirini na sita. (26,000,000)
- Marekani watu lakini nne na elfu kumi na nane na mia tano. (4,185,000)
- Uingereza watu laki nne na nusu. (4,500,000)
Mkuu nadhani Marekani (hasa jeshi lake la anga na majini/navy) ndiyo iliyotoa upinzani mkubwa kwa majeshi ya Wajapani na vikosi vya Hitler huko Ulaya na ukanda wa Pacific.
USSR pia ilichangia ila kumbuka mkuu kwenye mkutano wa Yalta( kama sijakosea) Stalin alimshinikiza Roosevelt na Churchill kupanua zaidi uwanja wa Vita huko Ulaya magharibi ili kupunguza hujuma za majeshi ya Wanazi huko Ulaya mashariki maana ingemlazimisha Hitler kupunguza shinikizo huko mashariki ili ajihami zaidi.
Na hata kwenye uvamizi wa Ulaya (D-day) ni Marekani ndio iliyochangia askari wengi kuliko washirika wengine wa Ulaya magharibi.
Ukija kwenye ukanda wa Pacific ni jeshi la maji la Marekani (US navy) ndio liliotoa upinzani mkubwa kwa Wajapani mpaka kufanikiwa kulishinda jeshi la wanamaji la Japan na hata baada ya vita kumalizika, jeshi la wanamaji la Marekani (US Navy) limebakia kuwa jeshi la wanamaji lenye nguvu zaidi duniani kuliko lolote lile mpaka leo.
Hapa mkuu unaona jinsi Marekani alivyokuwa na mchango mkubwa kwenye kuwashinda Wanazi na washirika wao (Italy na Japan).
Nchi kama Uingereza ilitegemea Sana makoloni yake (India na Africa) kutoa nguvu kazi/askari wapiganaji.
Nadhani bila Marekani hata USSR na Uingereza wasingeweza kushinda vile Vita.
Kuhusu USSR kuwa na vifo vingi nadhani ilichangiwa sana na mbinu zao walizotumia hapo awali isitoshe wakati wamevamiwa na Ujerumani majeshi yao yalisambaratika sana mpaka baadae huko Stalingard walipoweza kuwashinda Wanazi kwa msaada wa hali ya hewa (Japo siwezi kuthibitisha hili maana chanzo changu si rasmi).
Tunaweza kusema Vita viliwakuta USSR wakiwa hawajajipanga vya kutosha ndio maana waliingia sana hasara ya maisha ya raia wao.
Hapana, kwa wakati ule na nguvu walizokua nazo ingekua vigumu kuyashinda hayo mataifa mawili makubwa akiwa peke yake.Nimeuliza swali rahisi sana lakini bado hujanijibu: Hivi unadhani Marekani na mapesa yake yote yale angeweza kupigana peke yake na vikosi vya Ujerumani na Japani bila msaada wa Uingereza na Mrusi na akashinda ???
Wakati wa Uvamizi wa Normandy Ujerumani alikuwa na vikosi thelathini (30) tu ambavyo aliviweka kule Ufaransa ili kupigana na Marekani, wakati huohuo pia alikuwa na vikosi zaidi ya mia mbili ishirini (220) vyenye uwezo huohuo vikiwa kwenye eneo la Umoja wa Kisovieti vikipambana na Warusi. Ukifanya mahesabu utatambua kwamba Urusi alipambana na vikosi 190 zaidi vya Ujerumani kuli ambavyo Marekani alifanya.Hapana, kwa wakati ule na nguvu walizokua nazo ingekua vigumu kuyashinda hayo mataifa mawili makubwa akiwa peke yake.
Hili uliloandika hapa halina ukweli wowote na linapingana na historia na tafiti zilizofanywa na wataalamu. Professor Stephen Kotkin anasema hivi kuhusu Umoja wa Kisovieti kabla ya Vita ya Pili ya dunia:Tunaweza kusema Vita viliwakuta USSR wakiwa hawajajipanga vya kutosha ndio maana waliingia sana hasara ya maisha ya raia wao.
Angalia jinsi majeshi yake yaliposhindwa vibaya kwenye hatua za mwanzo baada ya kuvamiwa na Wanazi.Hili uliloandika hapa halina ukweli wowote na linapingana na historia na tafiti zilizofanywa na wataalamu. Professor Stephen Kotkin anasema hivi kuhusu Umoja wa Kisovieti kabla ya Vita ya Pili ya dunia:
Hili la kusema kwamba Umoja wa Kisovieti hawakujipanga vya kutosha ndiyo maana waliingia hasara umelitoa kwenye chanzo gani mkuu ???
- Umoja wa Kisovieti ndiyo nchi iliyokuwa na jeshi kubwa kuliko wenzake wote.
- Umoja wa Kisovieti ndiyo nchi iliyokuwa na kambi kubwa ya vifaru.
- Umoja wa Kisovieti ndiyo nchi iliyokuwa na kambi kubwa ya ndege za vita.
Mbona hata Marekani naye mwanzoni alishindwa vibaya na Wajapani ???Angalia jinsi majeshi yake yaliposhindwa vibaya kwenye hatua za mwanzo baada ya kuvamiwa na Wanazi.
Mkuu kwa ukubwa ule wa USSR na jinsi Wanazi waliposonga mbele zaidi na kuteka maeneo ilionekana dhahiri Hitler alikuwa anaelekea kupata ushindi dhidi ya Warussi, ukiangalia hata ushindi uliopatikana huko Stalingard ulilipiwa gharama kubwa sana ya maisha.Mbona hata Marekani naye mwanzoni alishindwa vibaya na Wajapani ???
Tatizo liko wapi hapa ???
Hata Marekani nayo ilikuwa kubwa mara mia ziadi ya Japani, hapa utasemaje ???Mkuu kwa ukubwa ule wa USSR na jinsi Wanazi waliposonga mbele zaidi na kuteka maeneo ilionekana dhahiri Hitler alikuwa anaelekea kupata ushindi dhidi ya Warussi, ukiangalia hata ushindi uliopatikana huko Stalingard ulilipiwa gharama kubwa sana ya maisha.
Mbona hata Marekani naye mwanzoni alishindwa vibaya na Wajapani ???
Tatizo liko wapi hapa ???
Kwahiyo Mkuu Masamila unataka kusema kwamba Hawaii nalo lilikuwa ni Koloni ???Mjapan alishinda mara ya kwanza sababu mpangilio ulikuwa wa kawaida maana mjapan alivamia makoloni na alikuwa ameshtukiza
Wangekutana kwenye dermarcated fronts huku kila mmoja amejiandaa ndio tungejua nani zaidi
Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app