Achana na
Genereal Yuri Drozdov wa Illegal Program.
Huyu alikuwa ni Counter Intelligence Officer based in Japan.
Yaani yeye alikuwa ni msomi wa Chuo Kikuu na alikamata sana majasusi wa CIA na MI6 kwa wingi.
NATO walichanganyikiwa sana wakawa wanahisi labda kuna watu wanatoa siri za CIA na MI6; kumbe jamaa katembelea nchi zote za Warsaw Pact na zile za Kikomunisti duniani akafanya utafiti mkubwa kuhusu tabia za kipekee (Peculiara Human Behavior) za majasusi wa CIA na MI6 na akatengeneza Bango-Kitita (Matrix) kubwa kweli akawapelekea KGB.
Hivyo mle ndani kukawa na somo kabisa wanafundishwa majasusi wa KGB-Counter Intelligence kuhusu CIA behaviour. Wanakwambia zaidi ya asilimia 85% ya tabia zilizoorodheshwa mle zilikuwa ni za majasusi wa CIA na MI6. Baada ya kuanguka Urusi ya kisovieti CIA walimfuata awaeleze alitumia mbinu gani kuwakamata wengi vile. Baadae wakaja kuambiwa ni kutumia Peni, Karatasi na kuangalia kwa jicho la tatu tu......!
NB 1: Tafuta kitabu cha Oxford kinaitwa "
Near and distant neighbours: A new history of soviet Intelligence (The Extraordinary achievements of Yuri Totrov Page 251 na Page 252)" kimeandikwa na Jonathan Haslam. Sasa huwa najiuliza sana maswali kama: Hivi miaka ya 70's na 80's KGB walikuwa wanafanya hivi unategemea leo ndiyo nchi yenu inakutana na majasusi wa namna hii hivi kuna kupona kweli ???
NB 2: Yuri Totrov ni uthibitisho tosha kwamba hakuna silaha kubwa duniani kama Ubongo wa mwanadamu, pia hakuna kitu chenye nguvu kama Human Intelligence. Aliweza kufanya ujasusi kwa kutumia
COMMON SENSE na kuweza kushindana na CIA ambayo ilikuwa iko mbele sana kwenye swala la teknolojia na fedha.
Watanzania tuna nini cha kujifunza hapa ???
Tunaweza tusiwe na pesa nyingi na teknolojia kubwa sana lakini tukafanikiwa kwa kiasi kikubwa mno katika kulinda maslahi mapana ya nchi. Japo ni kweli kwa dunia ya sasa tunahitaji pesa na teknolojia lakini hili halitakiwi kutufanya tulemae na kutegemea kuomba msaada wa taarifa au kununua vyombo vya kijasusi kutoka nchi za nje: Ni hatari sana kwetu.......
CC:
Consigliere,
Red Giant ,
zitto junior ,
chige ,
mng'ato