Masamila
JF-Expert Member
- Jun 22, 2014
- 6,506
- 7,472
- Thread starter
- #61
Mkuu tofauti na jinsi ambavyo vitabu vingi vinatudanganya,
Vietnam ziligawanyika na kuwa nchi mbili tofauti tokea mwaka 1954 baada ya kumpiga Mfaransa.
Walikuwa na nchi kabisa ya Kikomunisti iliyokuwa na masilaha mazito tokea Urusi na Uchina.
Vita vya msituni vilikuwa vinapigwa na Vietcong nchini Vietnam Kusini na ndiko walikuwa wanatuma Guerrillas Fighters!
Marekani alitawala Uwanja wa vita kwasababu sehemu kubwa ya vita imepiganiwa Vietnam Kusini na siyo Vietnam Kaskazini ambako vikosi vya Marekani na NATO vilikuwepo. Kule juu makao makuu ilikuwa ni ngumu sana kwenda kwasababu kulikuwa na maelfu ya Warusi, Wachina na Wakorea Kaskazini. Hivyo hii hoja ya kusema warusi hawakutoa silaha haina ukweli wowote ule.
NB: Hebu angalia hii ramani na uone maeneo ambapo vita zilipiganwa halafu uone kwamba Marekani alitawala vita kwasababu Vietnam Kaskazini walikuwa wanatuma wanajeshi wa Msituni wasio na silaha nzito sana. Walikuwa wanapitia nchi ya Laos ili kuingia Vietnam Kusini ambapo Marekani alikuwa ameweka kambi yake.
View attachment 695472
Inaweza kuwa kweli kama usemavyo, lakini tukumbuke majeshi yalikuwa mawili kwa upande wa Communists ambapo kulikuwa na NVA ambao commissioned officers wake walikuwa trained China na kulikuwa na Vietcong ambao walikuwa ni Guerilla fighters ambao hawa walikuwa ndani kabisa ya South Vietnam.
Achilia mbali engagements za Vietcong vs US&Allies kulikuwa na live engagements za NVA vs US&Allies. Ambapo NVA walikuwa wanavuka mpaka wanaenda kupiga inside South Vietnam(mfano Tet Offensive na mapambano mengine). Hao jamaa wa NVA ambao ni principally Standing army of North Vietnam ukiangalia tactics walizoemploy na jinsi vita ilivyokuwa kwa kweli hali ilikuwa ni mbaya!
Na naamini ni siasa tu zilizosababisha US akawa kama ameshindwa vita kutokana na kampeni, mivutano na maandamano yaliyokuwa yanaendelea in States soil. Ila Communists side in Vietnam war wangekubali mapema tu, hawakuwa na chao katika ile vita ila ni siasa chafu tu za Communist ideology maana wanajeshi upande wa Communists wengi wameuawa katika ile vita ambayo sidhani kama mtu anapinga kuwa huko ndio kupigwa kwenyewe!