Declassified KGB documents: Churchill alimuua Stalin

Declassified KGB documents: Churchill alimuua Stalin

Mkuu kama sijasahau USSR na China mahusiano yao yalizorota sana ikafikia China kupeleka jeshi la watu milioni moja na hali kadhalika kwa USSR nao hivo hivo wakapeleka jeshi kubwa karibu na mpaka wao na China.

Kwamba ilifikia mivutano ya kuvamiana tena?

Uchina alivamia kabisa kambi ya jeshi la Urusi na kuua wanajeshi lakini Urusi hakufanya lolote lile.
 
Kuna sababu nyingi sana za kushinda na kushindwa vita,
Lakini kubwa sana huwa zinakuwa nne ambazo tunaziangalia:

1. Manpower.
2. Equipment.
3. Training and
4. Budget.

Sasa Bwana Amini alikuwa na masilaha mazito na ukweli wanasema wakati JWTZ @TPDF imevamia Uganda walishangazwa sana kukuta mikakati mingi ya vita ya Tanzania. Hapo tunakuja kwenye vigezo vyetu hapo juu, kwamba unaweza ukawa na masilaha mazito lakini jeshi lako lisiwe na nidhamu kabisa. Mfano Mzuri tu tokea miaka ya 1919 hadi kufika 1940 Ufaransa ndiyo ilikuwa inaaminika kuwa ni moja ya nchi zenye nguvu kubwa za kijeshi Barani Ulaya lakini Ujerumani ya Hitler ilimvamia Ufaransa na kumpiga ndani ya Mwezi mmoja na siku kumi tu.

Upande mwingine wa shilingi,
Urusi ya Kisovieti ilikuwa haina silaha za kutisha sana kama zile za Adolf Hitler,
Lakini MANPOWER ndiyo iliwabeba, walikuwa wanatumia mikakati ya kufanya Conscription ya vijana wadogo na wanakuvamia katika namba kubwa sana ili kukuchosha. Hitler alikuwa anatumia Strategy ya The Blitzkrieg, ambapo anakuvamia kwa haraka halafu anavunja defense line yako anaenda nyuma halafu anageuka na kuanza kukupiga mgongoni mwako na mbele huku akitegemea msaada wa anga. Mkakati huu lengo lake ni kushinda vita haraka iwezekanavyo na bila kuwa na Casualties nyingi.

Lakini sasa Warusi walikuwa ni wengi sana,
Wanahistoria wa kivita wanasema kwenye Vita ya Stalingrad ilfikika kipindi wajerumani waliangamiza sana warusi lakini jamaa bado wakawa wanaendelea kuja tu. Warusi kwenye ile vita walikufa zaidi ya milioni 26, lakini wingi wao ndiyo uliwabeba. Hitler alitumia zaidi ya Asilimia 80% ya silaha zake zote Urusi ya kisovieti lakini alishindwa kuwaangamiza wote. Sasa hapa ni lazima ujue kulikuwa na wanajeshi vitani pia kulikuwa na watu wanaofanya kazi kwenye viwanda vya silaha wakiwa maelfu kwa maelfu.

Jingine ni hili la mafunzo,
Humu ndani tunaangalia vitu kama nidhamu na mikakati ya kivita.
Hili ndilo linaiangusha jeshi la Marekani hadi leo: Ukisoma historia hadi Raisi wao wa Kwanza General George Washington aliwahi kulalamika kwamba wanajeshi wa Marekani hawana nidhamu na mambo mengi wanayafanya kimazoea sana. Ndiyo maana hata kama walimpiga mwingereza wenye vita nyingi lakini walikuwa wanaumizwa sanaaa. Mfano hai kabisa ni hii Vita ya Vietnam 1955-1975, ambapo inasemekena wanajeshi wengi sana wa Marekani Maelfu kwa Maelfu walitoroka uwanja wa vita (Defected) na kukimbilia nchi kama Canada, Israel na Ulaya. Na hii ndiyo moja ya sababu ambazo zilichangia Marekani kushindwa vita hadi Raisi Richard Nixon alimwambia Henry Kissinger kwamba "The Harvard Hebrew Boys are defecting from the field and i don't know how they do it" .

Sasa Waganda tu wenyewe walikuwa kinyume na Field Marshal Amini, jeshi lake lilikuwa limegawanyika kidini na kikabila.
Wanajeshi walikuwa wakivamia sehemu wanaiba na kuua mateka bila huruma (No Quarter) na TPDF ilipovamia Uganda badala ya kuanza kupigana wakaiba mali na kuanza kukimbia hovyo. Hii ni sababu tosha ya kushindwa vita, ndiyo maana Sun Tzu Wu kwenye The Art of War anasema wanajeshi ni lazima wafundishwa nidhamu hata kwa makali ya Upanga ili mkuu wao akisema hata watembee juu wa moto au watumbukie kwenye korongo wanatii. Mfano Ernesto Che Guevara anasema alikata tamaa sana kuwasiadia wakina Mzee Laurent Desire Kabila kwasababu kila walipochukua jimbo walinyang'anywa tena na Mobutu; Anasema kazi yake kubwa Mzee Kabila ilikuwa ni Wanawake na wanajeshi wake walikuwa wanatafuta sana mali kuliko nchi. Na hili lilikuja thibitika walivyomuua yule Mzee na hakuna aliyefanya lolote nchini Congo DRC (Acute Lack of Discipline)

Hili la Bajeti nalo lipo sana,
Japo historia imethibitisha hauhitaji kuwa na bajeti kubwa kushinda vita kama hutakuwa na Manpower, Equipment na Training (Discipline). Ndiyo maana Mfalme Dario wa Uajemi alivyovamia Ugiriki na jeshi kubwa sana alipigwa na Athens peke yake kwenye The Battle of Marathon...Tena Spartans wakiongozwa na Leonidas wakampiga Mfalme Xerxes wa Uajemi kule Thermopylae na Wakalimaliza jeshi lake lote la majini kwenye The Battle of Salamis. Ndiyo maana Warumi walikuwa na nguvu sana kwasababu wanajeshi wao walikuwa siyo watu wa mchezo mchezo; walikuwa na uwezo wa kutembea na kilo hamsini mgongoni kwa mwendo mkali wa kilomita ziaidi ya ishirini (This is no Easy), na ndiyo maana walitawala Ulaya yote (Walikuwa na Budget kubwa, Vicious Training, Manpower and Heavy Equipment)

Mussolini na masilaha yake alivamia kisiwa cha Crete lakini alitumia miezi kama nane hivi,
Alikuwa akituma wanajeshi na parachutes wanatunguliwa na wakitua chini wanapewa kipigo mpaka kufa.
Jiulize ni kwanini kakisiwa kale kadogo kalimshinda Mussolini mpaka alivyosaidiwa na Ujerumani ya Hitler ndiyo wakashinda.

NB 1: Kuna mambo mengi sana hapa na tukiangalia upande wa Silaha na Bajeti tu, tutakosea sana.
Kupigwa kwa Iddi Amini kulitegemea sana vitu vingi sana kwenye udhaifu wa Amini ambao Nyerere alitumia kama Mwanya japo Amini alikuwa na masilaha mengi mazito. Halafu kuna factors nyingine ambazo zilisaidia sana Tanzania:
SECRET ALLIANCES, kwasababu ile vita hatukupigana peke yetu kuna Mkono wa nchi kama Algeria na Uchina pamoja na makundi ya wahuni wa Kitutsi wa Uganda kama Musseveni na Kagame.

NB 2: Saudi Arabia na Israel wana
silaha nzito kuliko Iran lakini kwanini hawamvamii ??? Au NATO wana silaha na Uchumi mkubwa kuliko Urusi lakini mbona bado Putin anawatesa sana mpaka leo ??? Au North Korea ni masikini kuliko Korea Kusini na Japan lakini hawamiwi tu ??? Kuna mambo siku hizi kama Asymmetric Warfare (Low Investment High Profit War) kama Urusi alichofanya nchini Ukraine na Syria, au Marekani alichowafanyia Wasovieti kule Afghanistani kwa kupitia The Mujahedeen. Wewe unakazana na Size, Budget and Conventional Warfare, mwenzako anafanya Terrorism, Cyberwarfare, Information Warfare and other irregular tactics na anakushinda vibaya sana tu...!
Kudos [emoji106] [emoji106]
 
Asiejua hawezi kuchangia hapa
Mnajua historia fundisheni wale wa kwetu makumbusho
 
Uchina alivamia kabisa kambi ya jeshi la Urusi na kuua wanajeshi lakini Urusi hakufanya lolote lile.


Alaaaa, nimewavulia kofia wachina aisee!

Niliwasikiliza baadhi ya wachambuzi kipindi Obama yupo madarakani wakisema kuwa Obama anaiogopa China na sasa nimeamini kuwa waChina ni watu ambao sio waoga waoga na kama wana calibre hii kweli mpaka leo basi Westerners waangalie sana kwamba choko choko zao ziishie kwa Mrusi tu. Wakijichanganya kwa mChina Dunia itaandika historia mpya aisee. Kwa hali waliokuwa nayo wachina in 1960's kijeshi ni walijitoa mhanga kupiga kambi ya jeshi ya 1960's Soviet red army ukilinganisha hali ya 1960's Chinese red army versus 1960's Soviet red army
 
Heshima yako mkuu, naamini mkuu wewe kama mimi ni wafuatiliaji wazuri wa history. Na kama unakumbuka vizuri huyo Leonid Brezhnev hakuwa solid leader kama Stalin.

Yeye(Brezhnev) na Khrushev ni viongozi wa USSR waliokuwa waoga kweli kweli pamona na mwenzao Gorbachev.

Katika History, kiongozi wa USSR aliekuwa anaogopwa na US kupita maelezo ni Joseph Stalin. Alikuwa ni mtu pengine unaweza dhani ni wa ovyo katika vitendo, kama pia una kumbukumbu nzuri Chairman Mao kabla hajafa, alisema kuwa kiongozi aliemheshime pekee USSR ni Stalin pekee.

Chini ya uongozi wa Stalin tulishuhudia Marubani wa USSR red army wakiwa pamoja na marubani wa Chinese red army jointly wakiwa vitani na wanajeshi wa Marekani walioongozwa na General Douglas McArthur (kama sijasahau jina la General).

Baada ya hapo sidhani kama USSR red army wamewahi engage in battlefield na US/Allied directly/live. Viongozi waliofatia baada ya Stalin wote walikuwa waoga

Waoga kwa sababu hawakuua watu sana kama Stalin? Nikita sawa alitishwa na Kennedy Cuban Missile Crisis akaogopa. Brezhnev Je? Nadhani wakati wao nguvu ya Kisovieti ilianza kuporomoka.
 
Ikurudie na wewe mkuu,
Ni kweli hatujui mengi lakini taratibu ndiyo tunaanza kujifunza.
Hatua kwa hatua naamini ipo siku tutajua endapo tutaweka bidii kwenye kujifunza kwa unyenyekevu mwingi.
Umekuwa darasa bora kwangu kuchota MAARIFA ambayo si rahisi kuyapata kirahisi, keep it up
 
Alaaaa, nimewavulia kofia wachina aisee!

Niliwasikiliza baadhi ya wachambuzi kipindi Obama yupo madarakani wakisema kuwa Obama anaiogopa China na sasa nimeamini kuwa waChina ni watu ambao sio waoga waoga na kama wana calibre hii kweli mpaka leo basi Westerners waangalie sana kwamba choko choko zao ziishie kwa Mrusi tu. Wakijichanganya kwa mChina Dunia itaandika historia mpya aisee. Kwa hali waliokuwa nayo wachina in 1960's kijeshi ni walijitoa mhanga kupiga kambi ya jeshi ya 1960's Soviet red army ukilinganisha hali ya 1960's Chinese red army versus 1960's Soviet red army
Kilikuwa ni kikosi kidogo cha mpaka, na Uchina alimtegea sana Mrusi akijua hatafanya lolote kwasababu Mkakati wa vita wa Urusi kwa wakati huo ulikuwa umeelekea Ulaya. Hivyo vikosi vingi vya Urusi vilikuwa viko Ulaya hivyo kama angetaka kumpiga Uchina basi ilimbidi atoe baadhi ya vikosi Ulaya, na endapo angefanya hivi basi ingemgharimu sana.

Brezhnev alitaka kuwashawishi Wamarekani ili washirikiane kutumia Nyuklia kuwalipua Wachina lakini Wamarekani wakakataa na wakaamua kutumia huu mwanya kuwavuta Wachina upande wao.
 
Nimewasikia wameraki wanataka kuishambulia tena Syria sababu ya matumizi ya chemical weapons, wakati wao ndio walianzisha huo mchezo kwa kuyatumia vietnam.
 
Mkuu umeitoa wapi hii ???
Halafu kama KGB ndiyo imefanya ku-declassify hizi nyaraka utasemaje kwamba Counter=Intelligence ya Urusi ya Kisovieti ilikuwa dhaifu, wakati walikuwa wanajua mpango wote ??? (Hapa pana ukakasi sana)
Hizi nyaraka zingetolewa na MI6 ndiyo zingekuwa na uhalisia kidogo, kuna mengi yana walakini hapa.

Siwezi kukupinga sana lakini tukitumia Common Sense tutabaki na maswali mengi sana:
1. Kwanini walisubiri wamuue Joseph Stalin wakati ameshakuwa mzee na miaka 73 ??
2. Kwanini mnawasahau maadui zake wakubwa wa ndani kama Nikita Khrushchev ??
3. Kwanini hao MI6 hawakuwaua Leonid Brezhnev na Yuri Andropov ??

NB: Kama KGB walikuwa na Intelijensia kinzani dhaifu basi hujawahi kumsikia mtu anaitwa Yuri Titrov (The most ruthless spy catcher in KGB history)..CIA walimfuata kumhonga mabilioni ya pesa baada ya kuanguka Urusi ya Kisovieti ili kujua alikuwa anatumia mbinu gani kukamata CIA na MI6 wengi vile.....
Naomba historia ya huyo jamaa wa kirus a'm interested
 
Kilikuwa ni kikosi kidogo cha mpaka, na Uchina alimtegea sana Mrusi akijua hatafanya lolote kwasababu Mkakati wa vita wa Urusi kwa wakati huo ulikuwa umeelekea Ulaya. Hivyo vikosi vingi vya Urusi vilikuwa viko Ulaya hivyo kama angetaka kumpiga Uchina basi ilimbidi atoe baadhi ya vikosi Ulaya, na endapo angefanya hivi basi ingemgharimu sana.

Brezhnev alitaka kuwashawishi Wamarekani ili washirikiane kutumia Nyuklia kuwalipua Wachina lakini Wamarekani wakakataa na wakaamua kutumia huu mwanya kuwavuta Wachina upande wao.

Kumbe aliekuwa Kremlin wakati inatokea hii issue ni Brezhnev! Sitashangaa sababu wachina walimheshimu sana Stalin na hakuna Dictator mwingine wa USSR aliyepewa heshima na wachina zaidi yake,,,,,,,, na nadhani pia ni wakati huo huo wa Brezhnev mpaka USSR inatukanwa na viongozi wa China kuwa ni ''Toothless Dragon''
 
Back
Top Bottom