Mkuu una nondo muruwa. Endelea kuleta mambo.
Btw nasikia wakati wa vita yetu na fashist alikuwa na hizi MiG-21. Je sisi tulikuwa nazo au tulikuwa na mitambo gani ya kuaminika wkt huko kiasi cha kumpa mchonga jeuri ile?
Kuna sababu nyingi sana za kushinda na kushindwa vita,
Lakini kubwa sana huwa zinakuwa nne ambazo tunaziangalia:
1. Manpower.
2. Equipment.
3. Training and
4. Budget.
Sasa Bwana Amini alikuwa na masilaha mazito na ukweli wanasema wakati JWTZ
TPDF imevamia Uganda walishangazwa sana kukuta mikakati mingi ya vita ya Tanzania. Hapo tunakuja kwenye vigezo vyetu hapo juu, kwamba unaweza ukawa na masilaha mazito lakini jeshi lako lisiwe na nidhamu kabisa. Mfano Mzuri tu tokea miaka ya 1919 hadi kufika 1940 Ufaransa ndiyo ilikuwa inaaminika kuwa ni moja ya nchi zenye nguvu kubwa za kijeshi Barani Ulaya lakini Ujerumani ya Hitler ilimvamia Ufaransa na kumpiga ndani ya Mwezi mmoja na siku kumi tu.
Upande mwingine wa shilingi,
Urusi ya Kisovieti ilikuwa haina silaha za kutisha sana kama zile za Adolf Hitler,
Lakini MANPOWER ndiyo iliwabeba, walikuwa wanatumia mikakati ya kufanya Conscription ya vijana wadogo na wanakuvamia katika namba kubwa sana ili kukuchosha. Hitler alikuwa anatumia Strategy ya The Blitzkrieg (The Lightning War), ambapo anakuvamia kwa haraka halafu anavunja defense line yako anaenda nyuma halafu anageuka na kuanza kukupiga mgongoni mwako na mbele huku akitegemea msaada wa jeshi la anga. Mkakati huu lengo lake ni kushinda vita haraka iwezekanavyo na bila kuwa na Casualties nyingi.
Lakini sasa Warusi walikuwa ni wengi sana,
Wanahistoria wa kivita wanasema kwenye Vita ya Stalingrad ilfikika kipindi wajerumani waliangamiza sana warusi lakini jamaa bado wakawa wanaendelea kuja tu. Warusi kwenye ile vita walikufa zaidi ya milioni 26, lakini wingi wao ndiyo uliwabeba. Hitler alitumia zaidi ya Asilimia 80% ya silaha zake zote Urusi ya kisovieti lakini alishindwa kuwaangamiza wote. Sasa hapa ni lazima ujue kulikuwa na wanajeshi vitani pia kulikuwa na watu wanaofanya kazi kwenye viwanda vya silaha wakiwa maelfu kwa maelfu.
Jingine ni hili la mafunzo,
Humu ndani tunaangalia vitu kama nidhamu na mikakati ya kivita.
Hili ndilo linaiangusha jeshi la Marekani hadi leo: Ukisoma historia hadi Raisi wao wa Kwanza General George Washington aliwahi kulalamika kwamba wanajeshi wa Marekani hawana nidhamu na mambo mengi wanayafanya kimazoea sana. Ndiyo maana hata kama walimpiga mwingereza wenye vita nyingi lakini walikuwa wanaumizwa sanaaa.
Mfano hai kabisa ni hii Vita ya Vietnam 1955-1975, ambapo inasemekena wanajeshi wengi sana wa Marekani Maelfu kwa Maelfu walitoroka uwanja wa vita (Deserted) na kukimbilia nchi kama Canada, Israel na Ulaya. Na hii ndiyo moja ya sababu ambazo zilichangia Marekani kushindwa vita hadi Raisi Richard Nixon alimwambia Henry Kissinger kwamba "The Harvard Hebrew Boys are deserting the field and i don't know how they do it" .
Sasa Waganda tu wenyewe walikuwa kinyume na Field Marshal Amini, jeshi lake lilikuwa limegawanyika kidini na kikabila. Wanajeshi walikuwa wakivamia sehemu wanaiba na kuua mateka bila huruma (No Quarter) na TPDF ilipovamia Uganda badala ya kuanza kupigana wakaiba mali na kuanza kukimbia hovyo. Hii ni sababu tosha ya kushindwa vita,
Sun Tzu Wu kwenye
The Art of War anasema wanajeshi ni lazima wafundishwe nidhamu hata kwa makali ya Upanga ili mkuu wao akisema hata watembee juu wa moto au watumbukie kwenye korongo wanatii.
Ernesto Che Guevara anasema alikata tamaa sana kuwasiadia wakina Mzee Laurent Desire Kabila kwasababu kila walipochukua jimbo walinyang'anywa tena na Mobutu; Anasema kazi yake kubwa Mzee Kabila ilikuwa ni Wanawake na pombe, huku wanajeshi wake wakitafuta sana mali kuliko nchi. Na hili lilikuja thibitika walivyomuua yule Mzee na hakuna aliyefanya lolote nchini Congo DRC (Acute Lack of Discipline)
Hili la Bajeti nalo lipo sana,
Japo historia imethibitisha hauhitaji kuwa na bajeti kubwa kushinda vita kama hutakuwa na Manpower, Equipment na Training (Discipline). Mfalme Dario wa Uajemi alivyovamia Ugiriki na jeshi kubwa sana alipigwa na Athens peke yake kwenye The Battle of Marathon...Baadae tena kikosi cha wanajeshi kutoka Sparta wakiongozwa na Leonidas wakamtwanga mtoto wa Dario, Mfalme Xerxes wa Uajemi kule Thermopylae (Japo walishindwa lakini walisababisha madhara makubwa) na baadae jeshi la Ugiriki yote wakalimaliza manowari zote za Uajemi kwenye The Battle of Salamis. Warumi walikuwa na nguvu sana kwasababu wanajeshi wao walikuwa siyo watu wa mchezo mchezo; walikuwa na uwezo wa kutembea na kilo hamsini mgongoni kwa mwendo mkali wa kilomita ziaidi ya ishirini (This is no Easy), na ndiyo maana walitawala Ulaya yote (Walikuwa na Budget kubwa, Vicious Training, Manpower and Heavy Equipment)
Mussolini na masilaha yake alivamia kisiwa cha Crete lakini alitumia miezi kama nane hivi,
Alikuwa akituma wanajeshi na parachutes wanatunguliwa na wakitua chini wanapewa kipigo mpaka kufa. Jiulize ni kwanini kakisiwa kale kadogo kalimshinda Mussolini mpaka alivyosaidiwa na Ujerumani ya Hitler ndiyo wakashinda. Huku Ufaransa yenye nguvu kubwa ikipigwa kwa mwezi na siku kumi tu (Think About it)
NB 1: Kuna mambo mengi sana hapa na tukiangalia upande wa Silaha na Bajeti tu, tutakosea sana. Kupigwa kwa Iddi Amini kulitegemea sana vitu vingi sana kwenye udhaifu wa Amini ambao Nyerere alitumia kama Mwanya japo Amini alikuwa na masilaha mengi mazito. Halafu kuna factors nyingine ambazo zilisaidia sana Tanzania:
SECRET ALLIANCES, kwasababu ile vita hatukupigana peke yetu kuna Mkono wa nchi kama Algeria na Uchina pamoja na makundi ya wahuni wa Kitutsi wa Uganda kama Musseveni na Kagame.
NB 2: Saudi Arabia na Israel wana silaha nzito kuliko
Iran lakini kwanini hawamvamii ??? Au NATO wana silaha na Uchumi mkubwa kuliko Urusi lakini mbona bado Putin anawatesa sana mpaka leo ??? Au North Korea ni masikini kuliko Korea Kusini na Japan lakini havamiwi tu ??? Kuna mambo siku hizi kama Asymmetric Warfare (Low Investment High Profit War) kama Urusi alichofanya nchini Ukraine na Syria, au Marekani alichowafanyia Wasovieti kule Afghanistani kwa kupitia
The Mujahedeen. Wewe unakazana na Size, Budget and Conventional Warfare, mwenzako anafanya Terrorism, Cyberwarfare, Information Warfare and other irregular tactics na anakushinda vizuri sana tu...!