DECI Tanzania: Ilivyoanza, ilipo na hatma yake

DECI Tanzania: Ilivyoanza, ilipo na hatma yake

Kwa wanachama wa DECI hasa wale waliokwisha kuvuna baada ya kupanda ni ngumu kuwaeleza kwamba DECI inaweza kuwapa kilio. Kwani kila mmoja wa wanachama wa DECI anategemea kuvuna tu na hategemei kuna siku atakosa au pesa yake kupotea. Huu ni upatu lolote laweza kutokea. Wangi wanafikiri kutolewa kwa tamko kwamba DECI haina baraka za Banki kuu ni kwamba kuna mabenki na mashirika yanayotoa mikopo yameathirika kutokana na kukosa wateja kwani wengi wamekimbilia DECI. Na kweli wapo wengi waliofaidi kutokana na DECI, ambao ni ngumu kuwaeleza waachane na DECI.

Tatizo langu ni hili; DECI wanapata wapi hizo fedha watu wanazovuna? DECI inafanya biashara gani ambayo inawapa mapesa wanayowajaza watu? Hilo inabidi liangaliwe kwa umakini sana.

Naomba mchango wenu wanajamii forum.

Limeshaongelewa sana hili, angalia thread ya https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/22907-deci-tanzania-ilivyoanza-ilipo-na-hatma-yake.html

DECI haitengenezi hela yoyote, inachuka hela za B wanampa A, hela za C wanampa B, na kuendelea, kisha wao wanapiga panga lao humo humo. Hawajafikiria litakalotokea wakifika Z!
 
Heshima mbele mzee.

Wewe jamaa either una akili sana na unalipwa ghali sana na DECI kudanganya watu.

Au una uwezo mdogo mno wa kufikiri mpaka imepitiliza.

Au inaweza ikawa neither lakini ni paranoid schizophrenic with terrible^3 delusions.

Au pia inawezekana umewekeza sana DECI, sasa ukisikia kwamba inaweza kuanguka kabla hujavuna, unapanic kidogo.

Nawasiwasi kwamba inawezekana hata huelewi watu wakisema "pyramid scheme" au "ponzi scheme" wanamaanisha nini. Unadhani ni majina tu watu ambao hawapendi maendeleo yako wameyatunga ili kukuongezea umasikini. Maana ungekuwa unaelewa ungeweza kutuonyesha ni jinsi gani DECI haiko hivyo, na ungetuonyesha hizo faida wanazovuna watu zinatoka wapi.

poleni sana kwa MGOMBEA WENU KUSHINDWA VIBAYA, mwambieni ajaribu next time.....!
ila lo labda uraisi wa 'PRAIDI' na sio urais wa Tanzania....!
 
Habari zilizopo DECI wamefunga ofisi zao zote wenye habari zaidi watumwagie hapa
 
poleni sana kwa MGOMBEA WENU KUSHINDWA VIBAYA, mwambieni ajaribu next time.....!
ila lo labda uraisi wa 'PRAIDI' na sio urais wa Tanzania....!

mgombea gani unayemwongelea wewe aisee,

Jamaa anaamini kabisa kwamba Iddi Simba na PRIDE ndio walikuwa wanaichongea na kuipigia DECI propaganda hasi kwa sababu wateja wanaondoka PRIDE na kwenda DECI.

[ame=http://en.wikipedia.org/wiki/Paranoia]Paranoia - Wikipedia, the free encyclopedia[/ame]
 
Nasubiri kati ya hawa wachungaji na maaskofu wa DECI nione ni yupi baada ya sakata hili atathubutu kusema "Ni mimi peke yangu nimepona.... mimi tu kuwaletea habari" Maana wote ni wezi watupu
 
Kwa habari zinazoingia sasa hivi ni kuwa ile Taasisi ya Upatu iliyozua sintofahamu (DECI) imefungwa rasmi. Source Alasiri ya Leo.

Wenye taarifa zaidi na nini kinachoendelea mtufahamishe.
 
serikali itakua imeshindwa tekeleza wajibu wake kwa suala la deci,kama wanayosema kuhusu deci yana ukweli, maana si kampuni ya miezi mitatu ni kampuni mama,kampuni yenye zaidi ya 3yrs, na itabidi kwa namna moja au nyingine serikali itabidi ifidie hasara watakazopata wananchi,itakua ni uzembe usio na mfano
 
Atakayepata taarifa zaidi atujulishe, hususani hatma ya wanachama wanaosubiri kuvuna.
 
Kwa habari zinazoingia sasa hivi ni kuwa ile Taasisi ya Upatu iliyozua sintofahamu (DECI) imefungwa rasmi. Source Alasiri ya Leo.

Wenye taarifa zaidi na nini kinachoendelea mtufahamishe.

Hii ni habari njema sana mkuu. Hatimaye dawa ya ujinga huu imepatikana.
 
Atakayepata taarifa zaidi atujulishe, hususani hatma ya wanachama wanaosubiri kuvuna.

Hakuna hatima yoyote zaidi ya kuwapa pole. Watu wameelezwa sana ila walitaka kufanya majaribio. Hayo ndiyo matokea na hawana budi kuyakubali!
 
Kwa habari zinazoingia sasa hivi ni kuwa ile Taasisi ya Upatu iliyozua sintofahamu (DECI) imefungwa rasmi. Source Alasiri ya Leo.

Wenye taarifa zaidi na nini kinachoendelea mtufahamishe.
Mkuu
wamesimamisha shughuli eti kwa kuwa wanachunguzwa na serikali ili tume ikamilishe,na wamezidi kukana kule habari maelezo kuwa si upatu,na kuwa wamechunguzwa kwa siri bila kushirikishwa.
 
Kama imesimamishwa rasmi, nini hatma ya pesa za watu maana PM alisema serikali kama itafunga watu watapoteza pesa zao.
Pole kwa wale waliopanda wakitegemea kuvuna!
 
Kama imesimamishwa rasmi, nini hatma ya pesa za watu maana PM alisema serikali kama itafunga watu watapoteza pesa zao.
Pole kwa wale waliopanda wakitegemea kuvuna!

Mkuu wametoa rai ya kutaka waitwe wasikilizwe na PM au Mkulu.Ajenda yao walokuja nayo ni kuelezea shughuli zao.Wamepinga kauli ya kuwa wana akiba ya B.1.83 Bank na kusema kuwa tangu waanze huo upatu wamepokea mbegu za B.54 hadi sasa zimevunwa B.38 Na benk wana akiba ya B.11 NA HASARA YA B.5 imetokea kwa kuwa watu wang'oa mbegu.Kama si upatu hadi leo ndo waseme wakati matangazo ya kuwatuhumu yametoka many dayz.
 
Jamaa wamejieleza wapo redio kuwa wanafungua Micro finance bank na members wao watapewa nafasi kubwa , THIS ISSUE IS STILL BOILING GUYS ALOT TO COME NOT OVER YET ! i will get more details once gain later !
 
Hii ni habari njema sana mkuu. Hatimaye dawa ya ujinga huu imepatikana.


Na wapa pole watakao poteza pesa zao. Lakini wa-TZ wako desperate na maisha kiasi ambacho wanaamuamini 'muokozi' yoyote atakayetokea anaye wapromise riches, salvation from problems, you name it!

Upande mwingine ile dhana ya 'no gain without pain' haipo katika akili zetu, tunapenda utajiri wa harakaharaka. Naongea na 'wahanga' wa DECI na utashangaa wanavyotetea nakuona kwamba serekali haitambui ni jinsi gani watu wamejikwamua kimaisha. True...lakini the fact that hizo hela zilikua 'illegal' haingii akilini mwao, sisi tunawaona wajinga lakini, pesa bwana - mwanaharamu!?
 
"...watangoja milele na watakufa bila ya kelele kama walivyokufa wafuasi wa Kibwetere,..Bongo!.."
 
Back
Top Bottom