Mungu ashukuriwe kwa lipi ndugu yangu? 1) Ashukuriwe kwa ufisadi waliofanyiwa watu maskini, ambao sasa wanalia na kusaga meno, wakiwa na hofu kuu juu ya usalama wa fedha zao? au 2) Ashukuriwe kwa ufisadi waliofanyiwa watu maskini, ambao kila uchao wanadanganywa na wanasiasa (soma Watawala) kwamba wataletewa maendeleo, ambayo mpaka leo yamekuwa ni ndoto. Nafasi pekee waliyoipata wananchi ya kujipatia maendeleo ya kweli imezimwa kama mshumaa uliozimika kwa upepo mkali... Upepo hauna muamana na kila kilichoko kwenye njia yake... Wanasiasa nao vile vile, hawana muamana na yeyote yule aliyeko kwenye njia yao, wanamuona kila anayetaka kuleta maendeleo ya kweli kuwa hatari kwa uhai wao, kwani, maendeleo yakija, wanasiasa watakosa kazi... watamwambia nani juu ya maendeleo ambayo tayari YAPO? Mmeshabikia kufutwa kwa DECi bila kupambanua kwa kina nini kinachoendelea. 1) Mwaka 2007, PRIDE Tanzania ilichukua mkopo wa USD 1.2 million kutoka Hivos-Triodos Fund. Kwa mujibu wa taarifa zilizoko kwenye Internet (nenda uka-google utapata), PRIDE Tanzania "is the largest microfinance institution in Tanzania". Haya, hii taasisi ya microfinance iliyo kubwa kuliko zote, iliyoanzishwa miaka ya 90, ina wanachama 75,000 (takriban), mpaka sasa. DECI, iliyoanza shughuli zake 2006 ina takriban wanachama 500,000! Mjiulize: Kwa nini DECI imefanikiwa mapema haraka kiasi hicho? Ina maana watu wote hao ni wajinga na mbumbumbu, wasiojua kwamba wanatapeliwa? 2) Kuanzia 2006, wakati DECI ilipoanzisha Tushikamane Revolving Fund, haikukopesha, lakini mwaka 2007 ilipoomba kibali cha kuwakopesha wanachama wake huko Wizara ya Biashara na Viwanda ILIKATALIWA. Haya, LEO hii Gavana Benno Ndulu anasema DECI isajiliwe ili IWAKOPESHE wanachama wake. 3) Mojawapo ya kundi la wanachama wa DECI ni wafanyakazi wa Benki (kama vile NMB, CRDB na nyinginezo...). Hawa, baada ya kuona hawatapata faida ya maana kwenye benki zao, wamekuwa wakichukua mikopo ya muda mfupi, wakipanda mbegu zao na kuvuna, kisha kurejesha mikopo hiyo na kuendelea na kupandikiza mbegu hizo, kwenye mfumo huo wa revolving fund. Wale walioanzia 2006 sasa wamekuwa wakivuna zaidi ya Shs. 10 million kwa mara moja. 4) Matatizo ya upatikanaji wa pesa yameanza tu mara Serikali ilipoingilia kati mpango huu, kwa kuwa nia ilikuwa kuhakikisha kwamba DECI INAKUFA KWA HALI YOYOTE ILE. Mikakati iliyopangwa ilikuwa ni pamoja na (i) kujenga hoja potofu kwamba DECI ni utapeli, bila hata ya kutaja ni aina gani ya utapeli unaofanyika, (ii) kujenga hoja kwamba wasimamizi wa DECI ni watu matapeli, bila kusema ni watu wa aina gani (ukweli ni kwamba hawa ni watu wa Kanisa, kama sikosei, Kanisa la Kibaptisti... MIMI NI MUISLAM, na si mwanachama wa DECI... lakini kama ningejua kuhusu undani wa DECI singeangalia UDINI wa walioianzisha, ningejiunga nao...), (iii) kujenga hoja kwamba DECI itakufa, bila hata ya kusema itakufa kwa namna gani. 5) Kuna tofauti kubwa kati ya "Pyramid Scheme" na "Revolving Fund". Mkitaka niwafafanulie, hiyo ni mada pekee, inayojitosheleza. BOT, kwanza ninashangaa, jinsi ilivyojazwa na ufisadi inapataje uhalali wa kusema kwamba DECI ni matapeli, imetoa tangazo kwamba DECI inakwenda kinyume na sheria. Mbona haikutangaza ni sheria gani (na vifungu vyake) iliyokiukwa? Unapomshtaki mtu, tena kosa la jinai, ana haki ya kujua anashtakiwa kwa kosa gani. DECI hawakuambiwa wameshtakiwa kwa kosa gani, mbaya zaidi, wananchi/wanachama wa DECI wametishwa na BOT waondoe fedha zao kule, au wasiwe na imani na DECI, ili DECI ife! 6) Kama DECI - na hiki ndicho kiini cha matatizo - ingeachwa iendelee, watu wangeendelea kuvuna, na kuvuna, kiasi kwamba benki za kawaida zingekosa uhalali wake. Watu wangeondoa amana zao kwenye benki (NMB, CRDB, NBC, BARCLAYS, STANBIC, etc.), kisha kuzipeleka DECI, ambapo wangepata faida kubwa zaidi, kwa kuwa DECI HAIKOPESHI. Wote mnajua (na hili si kwa Uislam pekee) kwamba vitabu vya Mungu vimeharamisha RIBA! Mikopo yote inayotolewa kwa minajili ya kutoza RIBA ni haramu. Lakini tumezaliwa na kukuukuta mfumo huu, ambao ndio umeanza kuhatarisha mfumo wa kiuchumi wa dunia... si mmeyaona wenyewe? 7) DECI haikuanzishwa ili IKOPESHE wanachama wake, kwani waanzilishi wake, ambao ni watu wa KANISA, walitambua kwamba kufanya hivyo kungekuwa ni kuzidi kuwakandamiza watu maskini, mafukara, wasiokopesheka, wasio na hata hati ya kibanda, ambao wakienda benki wanarudishwa nyuma, na wakienda PRIDE na FINCA wanaambiwa wajiunge vikundi vya watu 5 kila kikundi, na wanageuzwa kuwa watumwa wa kufanya kazi kwa bidii ili WALIPE RIBA ya mkopo, hatimaye kushindwa kulipa mkopo! Kama ninayoyasema ni uongo, waulizeni PRIDE na FINCA wawambie wana wanachama wangapi mpaka sasa na DECI wana wanachama wangapi? Benki huwa zinaikopesha Serikali ili iweze kuendesha shughuli zake za kiserikali (soma kifisadi), na kama watu wakitoa amana zao kwenye hizo benki, hakutakuwa na pesa za kuikopesha Serikali, hatimaye Serikali itaporomoka na kukosa uhalali wa kuitwa "Serikali", kwani, kadri jinsi watu wanavyoneemeka na kuwa na uwezo mkubwa wa kiuchumi, viongozi wa kuchaguliwa wanakosa watu wa kuwasimamia. Wananchi wakijenga Shule zao wenyewe, Hospitali zao wenyewe, mifumo yao wenyewe, na (asilani!) mitambo yao wenyewe ya kuzalisha nishati ya umeme, ili waweze kuwa na (a) nyumba bora, (b) lishe bora, (c) elimu bora, (d) afya bora, hapo ndipo kutakuwa na MAENDELEO! DECI waliwapa nuru Watanzania wanyonge - maskini - walio wengi. Lakini Serikali yetu hii - ya kifisadi - imediriki kwenda kuwakandamiza na kuizima nuru hiyo ya matumaini! Kumbe zile ahadi za "Maisha Bora kwa Kila Mtanzania" zilikuwa danganya toto? Sasa mmeamini wenyewe! Mmeshabikia DECI kufungwa, haya, nendeni, kama kondoo mnaotaka kuchungwa, mkaweke pesa zenu kwenye benki (NMB, NBC, CRDB, BARCLAYS, STANBIC, PRIDE, FINCA, etc.) tuone kama mtayapata hayo "Maisha Bora"! Kumbukeni, PRIDE ilikuwa na wanachama 75,000. Sasa wamepungua, na kuwa takriban 50,000! Ina maana, 25,000 waliondoka na kwenda DECI. Sasa Iddi Simba aliona hatari, atarudishaje mkopo wa USD 1.2 million huko kwa Wadachi wa Hivos-Triodos Fund? Ukitaka kusoma habari hizo, just Google "Pride Tanzania", utaona link mojawapo! Wala si siri! Ama kweli, wajinga ndio waliwao! Nimetoa somo... atakayekwazwa, aniwie radhi! Sasa kilichobaki, Uchaguzi Mkuu! 2010 ni keshokutwa! Tutaona itakavyokuwa, au sio? Umejiandikisha kupiga kura? ./Mwana wa Haki