libeneke la DECI: Wajinga ndio waliwao???
Warning Guys!
That's known as pyramid scheme. Very few people get rich, the ones who run this idiotic scheme. It has made a lot of people more poor. It operated in South Africa, Zimbabwe, Germany and UK. In actual fact its a criminal offence in UK and if caught you end up in Jail.
Unaweza google au nenda wikipedia na search Pyramid scheme. Mchongo wenyewe wa kuingizana mjini inakuwa kama ilivyoelezwa hapo chini
--------------------------------------------------
1: Kijiji kina watu 10000
2. Watu wa 10 wa kwanza wasio na fedha wanaanzisha mradi wa DECI. Wanasema kujiunga nao ni Shs. 200,000Watu 1000 wanajiunga kwa kutoa Tsh200,000 kila mmoja. (Kijiji kinabakia na watu 8990. Kwa kiyo Mtaji wa kwanza ni: Tsh. 200,000,000 (za wale watu 10)Hawa wanaambiwa wasubiri miezi minne ili wavune faida.
3. Wanatangaza na watu wengine 1500 wanajiunga kijiji kinabakiwa na watu 7490Watu wale 1500 wanaleta mtaji mpya wa milioni 300,000,000 Miezi minne inapopita wale 1000 wa kwanza wanalipwa fedha yao milioni 200, na kila mmoja anapata faida ya laki moja moja hivyo kila aliyeingia na laki mbili miezi minne anatoka na laki tatu!
4. Wanaingia watu wengi zaidi sasa nao wanafikia 2000 nao wanataka haya mavuno! Kijiji kinabakiwa na watu 5490 ambao sio wanachama.
5. Wale watu 2000 wanaingia na mtaji wa 400,000,000. Sasa hapa ndipo kuna kitu cha kuangalia vizuria. kuna watu 1500 ambao wanatakiwa kulipwa laki mbili zao (kwa jumla ya milioni 300 za mbegu). Lakini pia wanatajia kupata kila mmoja laki moja zaidi kama faida.b. Hivyo pamoja na kiasi hicho unatakiwa mradi wa milioni 150 zaidi kama faida ya kundi lile la pili.c. Kiasi hicho kinatolewa kwa wale waliokuwa na milioni 400 na hivyo kufanya wale wanaoingia na milioni mia nne kimsingi kuwa wamekingia na milioni 250! (hilo si tatizo kwa sasa). d. So wale wa kundi la pili wanaondoka na wao na laki tatu tatu kwa furaha ya mvunaji
6. Hivyo kampuni yetu inaanzisha recruitment drive nyingine na watu wengine 3000 wanajiunga na kampuni yetu hii ya mavuno. Kijiji kinabakiwa na 2490 ambao wengi wao wanaonekana kuwa ni wanachama wa JF!! Hao nao wanaingia na mtaji wa 600,000,000!
7. Hivyo muda umefika wa kuwalipa walioingia na milioni 400! So wale milioni mia nne kwanza wanalipwa seed money yao) ambayo ni kiasi hicho hicho. Lakini wanataka faida yao ya laki moja moja kila mmoja. - Hivyo zinahitajika milioni 200 nyingine na hivyo kuchukua kabisa mtaji wa wale wa milioni 600, kuwalipa wao na hivyo wale wa milioni 600. So wale wa milioni mia nne wanaondoka kwa furaha kwani wamepata fedha yao.
8 Wale wa milioni mia sita (ambao ni wengi zaidi 3000) na wenyewe wanaambiwa wasubiri fedha zao hadi mwisho wa miezi minna. 9. Sasa recruitment inaenda na kuwashawishi wale 2490 waliosalia kijijini kujiunga ili wavune. Nao wanaingia na mtaji wa 498000! (mara moja tunaona kuwa wanaingia na kiasi pungufu. Kampuni yetu ifanye nini basi; 10. Kampuni inawashawishi wale waliokwisha pewa mavuno yao kuzizungusha fedha hizo hizo tena kwenye mfumo huo. Kwa hiyo wale wa 1000, na wale 1500 na wanatakiwa kuzungusha fedha zao humo kwa humo.
NOW THIS HOW THE SYSTEM COLLAPSES
SCENARIO ONE:
a. Baada ya wale 2490 kuingia na kulipa milioni 498 wale wa milioni 600 watajikuta wanapungukiwa Sh 102! Bila ya fedha kuzungushwa tena kundi la milioni 600 wataanza kulalamika.
b. Wakati hao wanaanza kulalamika kundi lile la 2490 linasubiri kiasi walichoingia nacho (kwa maana angalau waliokwishalipwa awali idadi kama yao wawe wamzungusha tena fedha). Na pia wanasubiri milioni 249 kama faida! (kwa maana ya kwamba wanahitajika watu wengine kama 50 hivi kujiunga kuweza kuzalisha hiyo faida.
SCENARIO TWO:
a. Hii inategemea idadi ya watu ambao wako tayari kuzungusha fedha zao ndani kwa ndani. Kinachofanyika hapa ni saikolojia ya fedha. Wakikupa laki moja faida na wakakuambia uziingize tena kwenye system itabadi urudishe laki mbili kwao tena, na wewe unabakiwa na laki moja! Katika mfano halisi wa DECI ni kwamba wanakulipa laki tatu, na unaweza kuzirudisha kwa mafungu laki mbili mbili, hivyo utarudisha kwao zile za kwako (laki mbili) za kwao (laki mbili) na wewe unabakia na laki moja! Ulichofurahia kimsingi ni wewe kuwa na laki tatu kwa muda fulani, siyo kuzitumia.
b. Hili hata hivyo linatabia ya kuchosha huwezi kuwa na fedha usiyoitumia! Hivyo collapse ya pili itatokea pale watu ambao wamekuwa wakizungusha fedha zao huko kwenye kampuni watakapoamua kuziondoa kwenye mzunguko! Kwa maneno mengine wale 1000, na wale 2000 na wale wa 3000 watakapoamua kuondoka na fedha zao wale wa mwisho 2490 watajikuta wameliwa karibu milioni 500!
Hahahahaaa, Hapo wadau mkilizwa kwa kuingia mkenge huu kicha kichwa msianze oooohh hamkutustua mapema, mara ooooohh JK mbaya kuruhusu haya, mara oooooohhh kwa nini serikali isipige marufuku kama ilivyokuwa Kenya. Eh Kalagheni baho, ila mnaambiwa hii ni kanyaboya mwenye macho asikie na mwenye masikio na aone!