"...........ndo niligundua kuwa, kumbe ilikuwa designed haswa kwa walokole, na si watu wote, walipoona watu wengine wanalalamika wakikataliwa, ndo wakaanza kuchukua watu wa dini zingine. asilimia 99% pale ni wakristo, waislam ni wachache sana, ndo maana ukienda pale mazungumzo mengi utakuta haleluya, wapendwa katika bwana, ameni ameni nakadhalika. nilijulishwa kuwa, hii ilianzishwa na mchungaji wa kilokole.
the point is, hii issue inawagusa wakristo wooote Tanzania, hasa wasio na elimu, in a very sensitive way, kiasi kwamba watu wako tayari kwa lolote kama ulishawahi kuhudhuria mkutano wao wowote. huwezi amini. watu wana gadhabu sana, kwasababu wengi walitia miguu yote pale na kuifuta ni kugusa mioyo ya wengi. wengi wamejenga nyumba nimeshuhudia, wengi waliweka viinua mgongo, wengi wameweka mishahara hasa waalimu, wanajeshi, maaskari nk kwasababu hapo ndo palikuwa panalipa.........."
******************************
Kidzogolae:
Hebu kidogo tufikirie hypothesis hii: Kwa mfano ndiyo ingekuwa masheikh wa Kiisilamu ndiyo wameanzisha na kuendesha kitu hicho....unafikiri ingekuwaje?
nadhani serikali bila kusita ingeingilia kati na kuwakamata wahusika na pia tungesikia kauli kutoka watu mbali mbali za kusema wanafanya kwa niaba ya Al-Qaeda etc etc.
Nadhani pia Marekani (yaani wapelelezi wao wa FBI/CIA wangetoa msukumo kwa serikali kufanya hivyo na hata kutoa kauli kwamba wana wasiwasi hela hizo wanazochangisha ni kwa ajili ya ugauidi etc etc!!