DECI Tanzania: Ilivyoanza, ilipo na hatma yake

DECI Tanzania: Ilivyoanza, ilipo na hatma yake

Unalima, Unapanda, Unapalia kisha Unavuna. Hii ndiyo kanuni. Ni kweli unaweza usipalie na ukavuna lakini KUPANDA NA KUVUNA BILA KULIMA !!!.

DECI wangekuwa na miradi (kulima) sawa lakini kupanda na kuvuna tu! Wataalam wa uchumi hebu mtusaidie maana sioni ila wingu zito.

NN

NUNGU NUNGU:
Hii haitaji mtaalamu wa uchumi kupambanua ukweli,michezo ya kupeana pesa bila riba(UPATU) ipo sehemu nyingi kama makazini,kwenye biashara na sehemu nyinginezo, na hii ufanyika kwa kutambua uwezo wa kila mshiriki,mnapangiana zamu , pesa zinakusanywa na mtu mwenye zamu anachukua, Basi.

Lakini inapofika suala la pyramid scheme ni kitu tofauti sana ,Fikiria kwamba pesa haizalishwi, Hakuna Investment ya ku-generate profits, unaweka Tshs. 200,000/- unapata 200,000/- kwa misingi ipi?Maana yake ni kwamba ili mmoja apate 200000/- kuna wengi wanapoteza!

Cha kufanya ,serikali iingilie kati ,isimamishe wanachama wapya wahakikiwe wale wanachama wote walioko kwenye laini ya kuvuna,zihakikiwe amana zote zilizoko kwenye sources zote za DECI kuona kama zinaweza kuwalipa watu wanaotakiwa kuvuna katika vipindi vyote bila kuongeza mwanachama mpya ,mpaka mtu wa mwisho avune na iwapo itaonekana kwamba huo uwezo upo .DECI Waendele kupokea pesa za Watu wapya kwa maana waruhusiwe kuoperate.
 
Wezi wote siku zote huwa ni wajanja sana. Hao maaskofu au wachungaji wa Kenya wanaokiri kuwa walifanya makosa, je wamewarudishia watu waliowaibia? Hata hawa wanaojiita wachungaji wanawaibia watu na wanajua kuwa wanaiba. Ila wanataka waibe kisha baadaye wawaombe msamaha waliowaibia!!

Uzembe ni tatizo kubwa. Hawa watu wakati wanawasukumia maskini wa Tanzania kwenye nyavu zao ili wawaibie vizuri walikuwa wakisema wamesajiriwa na benki kuu. Vile vile kuna makato walikuwa wakikata watu wakidai ni kodi za serikali. Serikali imeamua kugutuka usingizini na kusema haiwatambui! Sasa wanazua visingizio vingine mara ooo inasaidia watu, watu wamenunua magari, sijui ..... taka taka gani. Kwa nini serikali haiwakamati na kuwafunga wahusika woote kwa kufanya biashara ya fedah bila leseni?? Sababu ni zile zile zinazofanya wezi wengine waendelee kuiba. Serikali inaona. Serikali ilikuwa inaona. Ilikuwa inajua kinachoendelea.

Hakuna cha kusema wachunguzwe wanatoa wapi hela. Hakuna cha kujiuliza. Huu ni wizi wa mchana kweupe na hawa wanajua kuwa wanaiba. Ila wakiisha iba watatubu kwa waumini hao hao kisha watawajengea makanisa kutokana na wizi huo na kutoa misaada 0.01% ya wizi huo.
 
Kwani hao DECI wakishapokea pesa za wananchi wanazifanyia nini?, Je ni nani anawalipa wafanyakazi wa DECI?, Je DECI wanabiashara yoyote yenye faida ya kutosha ambayo wakiishaipata wanaigawa kwa Members?. Kama siyo je Wananchi wana haki ya kupata faida kwa kuwekeza pesa zao mahali pasipofanya biashara?

DECI wameajiri wafanyakazi. Wakipokea hela hawana wanachokifanyia bali huzungusha zile zile hela na kuwapa wengine.

Huyu mama ambaye ndio yupo behind the scheme ametokea Kenya. Mtaji wake ilikuwa one billion kwa sasa wana 7 billion.

Huwezi kumjua huyu mama maana yupo behind the scene, soon nadhani ataondoka. kama sikosei ni mnyakyusa.
 
Huo ni wizi uliopangwa vizuri. Hiyo limit ya laki mbili waliyoweka ilikuwa na lengo la kuhakikisha hawachukui hela nyingi kutoka kwa mtu mmoja. kama biashara yao ingekuwa kweli biashara, kusingekuwa na masharti ya kiwango cha mwisho. Wataalam wa wizi hawataki wamwibie mtu mmoja hela nyingi. Wanataka wawaibie watu wengi hela kidogo kidogo ili hatimaye mambo yakibumburuka, watu hawatakuwa wakali sana. Kila mtu ataona amepoteza hela kidogo tuu. Lakini hiyo principle walishaanza kuivunja wenyewe kwa kuruhusu mtu mmoja kwa majina tofauti tofauti kupanda mbegu nyingi. Hapo inaonyesha jinsi wezi wasivyokuwa na principle. Flow ya hela ilishawafanya wajisahau.

Kwa uwekezaji wa laki mbili, wiki kumi na sita unapata laki tatu faida, mtaji uko pale pale, wiki nyingine kumi na sita uende kuchukua laki tatu tena!!! Mhhhh, hapa nahisi wahindi ndo wangekuwa wateja wa kwanza!!!

Huo wizi plan yake ni kuwa-hit watu maskini wasio na kipato. Hao maskini ndo watu wepesi kukubali watakapoambiwa bahati mbaya imetokea. Bahati nyingine ni kuwa hao maskini ndo walafi na wasiojua ugumu wa kuzalisha pesa kwa wingi hivyo. Vile vile ni wajinga.

Kwa kifupi ni kuwa wale wachache waliokwisah lipwa mavuno walikuwa wanawasaidia hao wezi kuja kuwaibia watu wengi zaidi. Hizo fedha walizochukua ni za wizi na inatakiwa wazirudishe!!! Walioibiwa ni wale ambao mbegu zao hazitazaa kwa sababu hakuna wachangiaji wapya watakaokuja.
 
Kwanza Maaskofu na Wainjilisti wana elimu ya Kiroho zaidi ambayo inapatikana kwa njia ya Roho Mtakatifu (uwezo wa Mungu) Hivyo vitu vingi kama PYRAMID SCHEMES hawajui - wanapaswa kukubali kuelimishwa

Pia ingawaje ni kweli wengi wamenufaika na DECI - lakini swala ni kuwa mwisho wake sio mzuri - kama ilivyo PYRAMID SCHEME yoyote - wanaowahi kupanda mwanzo wanavuna kutokana na wanaopanda baadaye - na UPANDAJI UTAKAPOKOMA - WATAVUNA NINI??

DECI wanapata some percent kwenye ile hela inayopandwa na hapo ndipo wanatapeli watu kwani wamejipangia wenyewe -

WANANCHI wengi pia hawajaelimishwa PYRAMID scheme ni nini - hivyo wanaingia kichwa kichwa na wanachotazama ni PESA YA KUTATUA MATATIZO - LABDA WENGINE WALIDHANI NDIO MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA - NO WAY ..............

VIONGOZI WA DECI wanajua wanachofanya na matokeo yake - WANAWADANGANYA WENGI - UCHUNGUZI - UCHUNGUZI - wa nini?? ni kiasi cha kuwachukua na kuwahoji waeleze PROJECTION YA DECI NI NINI??

ILA SI KWAMBA WATU WANASOMESHA TU WATOTO, WAMENUNUA MAGARI - WAMEFANYA SHOPPING ZA NGUVU - just like their elected MPs.

GOD HELP YOUR PEOPLE
 
Hao wanaofanya shoping, na kusomesha watoto (kama wapo kweli) wanawaibia hao waliowachangia au wanaopanda mbegu ambazo hazitazaa. Nasema kama wapo kweli kwa sababu mimi sijamuona mtu ninayemfahamu aliyenufaika kihivyo. Hizi heresay kuwa watu wananunua magari, .... sijui nini, ni sehemu ya scheme yenyewe. Mnaaminishwa kuwa watu wananufaika sana, ukweli ni kuwa wengi hizo hela wanazirudisha huko huko na hawatakuja zipata. Ile ofisi ya makaratasi itachomwa moto na kumbukumbu zote itakuwa hakuna. Hizo fedha virtual zilizoko kwenye makaratasi yanayoitwa receipts ndo utakuwa mwisho wake.

Hizi habari kuwa watu wananunua magari, sijui wanasomesha..... ni part ya scheme yenyewe! Hakuna kitu cha namna hiyo!!
 
toleola33.jpg
 

Attachments

Kusema kuwa hakuna walionufaika kusomesha na kununua magari utakuwa unapotosha maana mimi nawajua baadhi, ila ni kwamba ni wachache kulinganisha na watakao poteza fedha zao
 
Du tukimbilie wapi maana tulifikiria DECI ndio mkombozi wetu sisi wanyonge.....twafwaa...nami nilikuwa mbioni kwenda kupanda...mbegu...tunaomba ushauri sasa je ni riski kupanda????
 
Du tukimbilie wapi maana tulifikiria DECI ndio mkombozi wetu sisi wanyonge.....twafwaa...nami nilikuwa mbioni kwenda kupanda...mbegu...tunaomba ushauri sasa je ni riski kupanda????

Pole mkuu, huwezi kupanda mbegu kwenye kopo tupu halafu baada ya miezi minne ukute limekua na kutoa mazao. Hilo huitwa mazingaombwe kwani linapingana na sheria zote za kisayansi tunazozijua.

Ukitaka faida ya haraka namna hiyo ni bora uanzishe mchezo wa Kibati na wenzako wanne, ili kila mwezi uwe unapata fedha zaidi ya zile ulizoingiza. Mkiwa watu zaidi ya wanne, mtalia.
 
Mkuu, mi naomba ukae utafakari na ujue ya kuwa kama ulishiriki katika DECI basi wewe ni mnyonyaji na umekula pesa za wenzako hao unaodai ni maskini watanzania. Na ninaomba urudishe hiy 'faida' feki uliyopewa kwani ni pesa za mvuja jasho mwamnifu aliyedanganywa na hivi sasa hawezi kurudishiwa pesa zake.

Kaa utafakari hilo alafu kwa majibu zaidi soma jibu ndefu niliyotoa katika thread ile ya mwanzo ya DECI.

Naweza kukuelewa; lakini kamuulize swali hilo mlalahoi aliyeweka 20,000 ( aliyoipata kwa kufanya kibarua siku 5) then akapata 50,000 na akaendelea kufanya hivyo hatimae akafungua mama lishe kama atakuelewa; toa alternative ndg yangu; swala sio makala marefu; toa alternative maisha magumu waende wapi; watakula hayo makala zenu za kikandamizaji?
 
Benk riba huwa wanajadili na mteja??? kama uko finca/nbc/crdb/chartered/pride lazima upigie debe tawi lako ndg; nani kalalamika kuwa amepata shida na hilo; pyramid hili unalijua vema au unatumia mapokea ya historia kutoa jibu usilolijua?
 
watapoteza lini? can you prove in court? au unaishi kwa hisia; toa mbadala wa DECI Tanzania; au kuwanyima wananchi DECI ndio maisha bora kwa kila MTZ; walau DECI wamethubutu
 
Naweza kukuelewa; lakini kamuulize swali hilo mlalahoi aliyeweka 20,000 ( aliyoipata kwa kufanya kibarua siku 5) then akapata 50,000 na akaendelea kufanya hivyo hatimae akafungua mama lishe kama atakuelewa; toa alternative ndg yangu; swala sio makala marefu; toa alternative maisha magumu waende wapi; watakula hayo makala zenu za kikandamizaji?

Sorry mkuu, ukimwibia mtu alafu ukazitumia kujiendeleza bado unaitwa mwizi.
Next to story ya mama nitilie huyu ninaweza kukuwekea possible story ya watu angalau 10 ambao wamepoteza pesa zao na hazirudi tena na waliweka akiba zao zote katika Deci - wengine watajinyonga, wengine watapigwa na waume zao kwa ajili ya kupoteza pesa hizo, wengine wataishia kusota na njaa.

Usituonyeshe only success story, talk about wale watakaoathirika. Unaomba proof ya watakaoathirika, subiri kidogo upate update nzima. Hatuogopi kwenda kuwaeleza wawekezaji wote wa DECI kuwa wameibiwa na walio'vuna' ndiyo waliokula pesa zao (soma makala nzuri sana ya Mzee Mwanakijiji). Mbona tulifurahi wake wa Vigogo waliopkamatwa na polisi miaka ya nyuma? Niliambiwa kuwa hata vyombo vya habari viliandika na juzijuzi tu humu kulikuwa na thread ya kuwaponda akina mama hao ambao ni wake za vigogo. Hakuna tofauti kama ni wake za vigogo au ni walokole, wote ni wezi tu.

Unasema tunaandika makala za kukandamiza, well, maybe so lakini ungekuwa makini ungeona elimu tunayotoa ni kubwa sana. Elimu ambayo ingekuwa wajibu wa serikali kuitoa.
Alternative ya DECI hamna kwa sababu DECI ni wizi mtupu. Ungeniuliza alternative ya kumwendeleza mwananchi ningekupa mifano mingi.

Hao FINCA na Pride unaowaponda mbona wamesaidia wengi? Umoja fund mbona imesaidia wengi? Kitu amabcho unakitaka wewe na hakiwezikani ni eti utengenze faida ya 200% bila ya kutoa jasho. Eti unavuna ulichopanda. Umepanda 40,000 utavunaje 60,000? Nijibu hilo ndipo uendele kubisha. Usitumie umaskini wa watanzania kama sababu kwa sababu mchezo wenu huu wa DECI umeONGEZA umaskini wa watanzania tena ndo mmefanya unyama wa hali ya juu kwani mmewa-exploit wananchi. Usitake kutuletea indignation instead of an apology! The only thing you can do as mshiriki wa DECI ni kuomba radhi kwa wenzako uliochukua pesa zao na kuwarudishia. I bet, wewe siyo mama nitilie uliyemzungumzia!
 
Ingekuwa MASHEKHE naona nchi ingewaka moto lakini uzuri ni kuwa mashekhe wenyewe waliopo ni akina Gorogosi na elimu yao ni ndogo na akili zao ni finyu sana

BOT na jamaa wa Capital Markets waliachia vipi hili liendelee muda wote huo

Je tutasikia lini kelele za GAVANA AJIUZULU?
 
Benk riba huwa wanajadili na mteja??? kama uko finca/nbc/crdb/chartered/pride lazima upigie debe tawi lako ndg; nani kalalamika kuwa amepata shida na hilo; pyramid hili unalijua vema au unatumia mapokea ya historia kutoa jibu usilolijua?

Wewe unajua piramidi? Hebu toa maelezo yako tuyaone yanatofautiana vpi na DECI?
 
Nasikia huwa wanaanza na sala (kuwachota wadanganyika akili) kabla ya kupanda/kuvuna. Na kwa jinsi wabongo walivyozama katika imani za dini, that is a perfect match.

Mungu anashusha muujiza, kama Yesu alivyoongeza mikate enzi zileeee. Kazi ipo.
 
Ingekuwa MASHEKHE naona nchi ingewaka moto lakini uzuri ni kuwa mashekhe wenyewe waliopo ni akina Gorogosi na elimu yao ni ndogo na akili zao ni finyu sana

BOT na jamaa wa Capital Markets waliachia vipi hili liendelee muda wote huo

Je tutasikia lini kelele za GAVANA AJIUZULU?

Usisubiri ndugu yangu ukiona kitu ambacho hakistahili au kinakukera take a position. Kama u naamini Gavana ajiuzulu anzisha hoja na as a matter of fact mimi nitakuunga mkono. Go for it. Au unasubiri mwingine ndiyo aanzishe?
 
Ingekuwa MASHEKHE naona nchi ingewaka moto lakini uzuri ni kuwa mashekhe wenyewe waliopo ni akina Gorogosi na elimu yao ni ndogo na akili zao ni finyu sana

BOT na jamaa wa Capital Markets waliachia vipi hili liendelee muda wote huo

Je tutasikia lini kelele za GAVANA AJIUZULU?

Sure GT
Kama chama la DECI lingekuwa chini ya masheikh kibali mida kingekuwa kishatolewa biashara kama kawa
 
Back
Top Bottom