DECI Tanzania: Ilivyoanza, ilipo na hatma yake

DECI Tanzania: Ilivyoanza, ilipo na hatma yake

Hapa kuna ishu kubwa sana ambayo inabidi ichambuliwe kwa kiina kwani ni:
- Uzembe wa vyombo husika vya serikali - CMSA na BoT
- Greed and ignorance of wananchi wanaotaka kutajirika kirahisi
- Ujanja na unyama wa viongozi wa DECI ambao wanaendelea kuwadanganya wananchi

Kazi ni kubwa na ni vyema hatua zichukuliwe mara moja!
 
Maaskofu wa Kipentekoste kwa kawaida ni watu wenye elimu ndogo sana. Hata hivyo nadhani wanaelewa hii ni pyramid scheme, na kwamba ikiachwa kuendelea basi itafika mahali watu wengi sana watapoteza fedha zao. Ni uchu tu wa fedha ndio unafanya wapiganie kuendelea kuweko hii scheme.

God made man,
Man made money,
Money made man mad.

Wako wapi wenye elimu kubwa? Na waliishafanya nini?
Kigezo kipi ulichotumia kupima upeo wao wa elimu?
kama hauna hoja ficha pumba zako.
Maaskofu wana elimu na ufahamu na hekima ambazo Mungu kawapatia
 
MKJJ unaweza kutuletea PDF ya Cheche hapa; habari mzuri naona hii;

All in all; serikali haipo tena; au ipo lakini haijui wajibu wake; mie naona DECI ni ubunifu ambao unatakiwa kutengenezewa documentation ya uhakika kisera tena kwa kusaidiana na serikali ili hata ile mikopo midogo midogo hata zile pesa za JK zipitie huko kuwawezesha wananchi wengie zaidi;
Jana ilibidi nitembelee eneo hilo kujionea; ilikuwa mapumziko muda huo nilibahatika kukutana na akina mama wachache wengi wao ni wajane na yatima na akina mama niwekee (mama lishe); wanapata mikopo hata walikuwa hawaamini na jinsi muda ulivyokwenda wakaona kuna mafanikio; wanajichotea hela nzuir na kuweza kuishi

Haya yote ni kwa sababu;
Wananchi hasa wa kima cha chini hawana mahala pa kukimbilia ( kama serikali ina sehemu basi iwaonyeshe sio kupiga marufukubila kutoa mbadala)
 
Hapa kuna ishu kubwa sana ambayo inabidi ichambuliwe kwa kiina kwani ni:
- Uzembe wa vyombo husika vya serikali - CMSA na BoT
- Greed and ignorance of wananchi wanaotaka kutajirika kirahisi
- Ujanja na unyama wa viongozi wa DECI ambao wanaendelea kuwadanganya wananchi

Kazi ni kubwa na ni vyema hatua zichukuliwe mara moja!

Hatua gani hapo mkuu unayotaka? watu kwa ujinga wao wameweka vijisenti vyao bila kulazimishwa na wanavuna kwelikweli, leo unataka serikali iingilie kati halafu hao DECI wawaambie kuwa Serikali ndio iliyotutia hasara nendeni mkadai hukohuko? kwani serikali ikiingilia tu basi DECI atakuwa kapata pa kutokea na kutokomea na mihela yote na kusubiri kesi laini mahakamani,DECI wabarikiwe!
 
Haya yote ni kwa sababu;
Wananchi hasa wa kima cha chini hawana mahala pa kukimbilia ( kama serikali ina sehemu basi iwaonyeshe sio kupiga marufukubila kutoa mbadala)

Exactly, this what I always say.

WASOMI wetu wako mstari wa mbele kutwambia mazuri na mabaya ya vitu kama DECI..its easier kwa wao maana ni wasomi na wana uwezo. Lakini katika hao wote hakuna anayetoa njia mbadala ya kumsaidia huyu huyu anayekimbilia DECI. Maana wewe kama msomi..unakimbilia Capital MARKET NA KUNUNUA HISA....mwananchi wa Kimanzichana huo utaalam na resources za kununua hisa hana. Sasa aende wapi? au ndo akae chini amsubiri chini aliye juu? Asiposhuka je?

Cha kufanya..tujadili ni namna gani..hii DECI inaweza badilisha na kuwasaidia wananchi wetu. Yes it might be a ponzi scheme..lakini hilo analijua Mwanakiji na Ndullu na wengine ambao ni ma analyst. Mwananchi anajaribu kuona kama elfu ishirini yake inaweza kuzalisha akapata arobaini..apeleke moto shule...ni kutomtendea haki. Perhaps Ndullu akae na wasomi wake..wajaribu kuona hiyo DECI inavyoweza kuboreshwa au hata humu JF..watu jadilini alternative ya DECI na mwananchi wa kawaida atai afford vipi.....siyo kuja na hadithi za mifano lukuki wakati wananchi wanahangaika tuu...kila siku wasomi hapa JF wanalalamika ugumu wa kupata mkopo Benki zetu..iwe mwananchi wa kawaida?

Wasomi shughulisha bongo zenu..acha kudismiss....miradi inayowasaidia wanyonge....leteni miradi mbadala..
 
Hiyo si biashara wala kitega uchumi ni mbinu wajanja wanata kuishi kwa kutumia jasho la wengine ni sawa kabisa na karata tu .Tuachane na wanaoshawishi kuendeleaza DECI.
 
Kwani hao DECI wakishapokea pesa za wananchi wanazifanyia nini?, Je ni nani anawalipa wafanyakazi wa DECI?, Je DECI wanabiashara yoyote yenye faida ya kutosha ambayo wakiishaipata wanaigawa kwa Members?. Kama siyo je Wananchi wana haki ya kupata faida kwa kuwekeza pesa zao mahali pasipofanya biashara?
 
Mkuu naomba nitangulize pole zangu za dhati kwani naona we umewekeza katika DECI. Kama uko tayari naomba nikujibu kwa kutumia facts pia:

Fact: DECI wamegundua njia ya kufanya kazi nje ya mfumo wa kibenki wa Tanzania, jambo ambalo limewatisha watawala na wamiliki wa mabenki haya. Watu wakizidi kuhamisha pesa zao kutoka kwenye benki hizo, na kuzipeleka DECI, uhai wa benki hizo utakuwa mashakani. Hakuna benki yenye uwezo wa kuwapa watu faida ya 125% kwa muda wa miezi 4. HAKUNA!
Mfumo nje ya benki: Sheria ya Tanzania iko wazi kama unaendesha benki unasimamiwa na BoT, kama unaendesha mpango wa fedha nje ya mfumo rasmi wa benki, unasimamiwa na CMSA. Mfano mzuri ni mpango wa Umoja Fund, ambao mpaka leo unaendelea na haijafungiwa.
Faida ya 125% katika miezi 4: Ni kweli hiyo ni fact na nimefurahi umeliona. Hakuna benki, hakuna mpango wa fedha unaoweza kukuahidi hilo. Je DECI wanafanya shughuli gani ya uzalishaji utakaoweza kuzaa faida hiyo? Hakuna, kwa hiyo ni kitu gani kinachofanyika? Unapoweka 40,000 na kulipwa 100,000 baada ya miezi 4 ina maana umepata faida ya 60,000. Je hiyo 60,000 imetoka wapi? Ni pesa za wenzako waliokufuata - watu 3 waliowekeza 20,000. Na baada ya miezi 4 watachukua faida inayotokana na uwekezaji ya wengine 6 au hata 8. That is what a pyramid scheme is. Kwa hiyo kama umewekeza mapema utapata 'faida' lakini wanaofuata ni lazima wapate wenzao wa kuwekeza pesa ili wapate 'faida' This is useless, na si uzalishaji.


Kama DECI wamekiuka sheria, na kama kweli wamewatapeli au wana nia ya kuwatapeli Watanzania, wafungiwe, lakini kama sivyo, ndugu zanguni mnapiga vita nafasi ya kuachana na umaskini, tena kwa pupa bila kuchuja pumba na chuya! Kalaghabaho! Wenzenu wanavuna wanachopanda, nyie mnakalia, matapeli... nani ametapeliwa?
DECI wamekiuka sheria, tena ni kesi ya jinai walichokifanya. Sasa ukiendelea kushikilia bango ujue kuwa hata KUSHIRIKI katika Pyramid scheme ni kosa na unaweza kuchukuliwa hatua za kisheria. Kwa nini? Kwa sababu ulipochukua 'faida' ulichukua pesa za watu.

Kilichotokea Kenya si lazima kitokee hapa nchini... kumbukeni, Kenya wao ni rahisi sana kushika silaha na kupigana... si mnakumbuka yaliyotokea hivi majuzi, baada ya uchaguzi mkuu wao kufanyika? Sisi hapa tunaweza kweli kukatana mapanga kwa sababu ya tofauti za kisiasa? Sisi ni wapenda amani, na kamwe hatuwezi kuwa na mfumo wa kitapeli nchi nzima.

Hivi leo hii ukiambiwa urudishe ile 'faida' uliyochukua na kuitumia, utakuwa tayari kufanya hivyo? Hapana! Mfano wako huu wa Kenya si sahihi na kumbuka kuwa hata huko Philippines na Columbia na kwingne, wananchi ni wapenda amani lakini mbele ya pesa, hakuna uvumilivu amani na upendo.

DECI inawasaidia Watanzania wasiokopesheka, maskini wanaolala kwenye nyumba za udongo, tena wasio na uhakika wa hata mlo mmoja. Leo mnasema IFUNGWE? Ina maana wao hawana haki ya kuachana na umaskini? Acheni ROHO MBAYA!

Kama wewe una uwezo, ni wewe, waacheni wasio na uwezo wawezeshwe. Hii ni Maisha Bora kwa Kila Mtanzania KWA VITENDO! Msiungane na MAFISADI!

Kama kuna atakayechukia, basi, namwomba radhi, lakini binafsi siungi mkono Serikali kuifungia DECI, kwa sababu, hii ni REVOLVING FUND, sio PYRAMID SCHEME! Kwenye PYRAMID SCHEME unaambiwa nenda ulete wanachama wengine, kwenye DECI ni wewe mwenyewe na mtaji wako. Wapi na wapi ndugu zanguni?

Kama kuna ambaye amelizwa na DECI hapa Tanzania, vyombo vya sheria viko wazi, aende akashtaki. Hajazuiwa. Lakini kama mnasema tu, bila kuchuja, bila kufikiria, mnawasaidia mafisadi kuwakandamiza Watanzania wanyonge, walio wengi, maskini, fukara wa kufukarika!

./Mwana wa Haki

Umeongea vitu vingi lakini naomba nigusie vitu 2 muhimu:
Revolving Fund: hii ina maana gani? NI kuwa hamna kinachofanyika kama uzalishaji bali ni kuzungusha pesa za watu. Katika mzunguko huu lazima itafikia tamati maana watu wa kuwekeza wakiisha ni lazima mpango uta-collapse. Hawa DECI wamejisuta wenyewe kwa kutumia neno hili na kuonyesha dhahiri kuwa ni pyramid scheme. Unasema katika pyramid scheme unaambiwa ulete wanachama wenzako na hii haipo katika DECI, lakini si ndivyo unavyofanya? Kwani ulipopata 'faida' si ulienda kutangaza kwa majirani wawekeze kwa kuwa kuna faida kubwa? Unakataa si ndicho ulichofanya? Recruitment siyo lazima iwe kwa fomu, inaweza kuwa word of mouth. Pia makanisa yametumika kutangaza kusifia na kuhimiza watu kuwekeza katika DECI, kitu ambacho ni dhambi kubwa sana, ukiachilia kuwa ni kosa la jinai.
Mafisadi: ujue ya kuwa hata washiriki wote wa DECI ni mafisadi tena wale wabaya maana wameibia maskini watanzania alafu wanaifanya kama vile ni mpango wa kuwasaidia. Wewe binafsi umeonyesha ni jinsi gani umekuwa 'brain washed' Naomba uamke na uachane na ufisadi huu mara moja. Tena rudisha 'faida' uliyopewa ili wenzako warudishiwe pesa zao.
Kama una maswali au unahitaji ushauri niandikie katika inbox
Pole tena na uwe makini!
 
Kuna askofu alikua TBC sasa hivi, anatetea DECI kwa nguvu mno, akibanwa na swali anasema sio msemaji! kazi ipo.

Sio ASKOFU nu muinjilisti, kashindwa kujibu maswali kapeleka lawama kwa taasisi za kifedha eti wamewaonea wivu, PATAMU HAPO.
 
Mimi nafuatilia suala la historia ya ponzi schemes duniani.

Inaonekana sehemu nyingi duniani hizi ponzi schemes zimekuwa zinaanzishwa na kuendeshwa na kuenezwa na makanisa ya kipentekoste. Hivyo si ajabu hata Tanzania Maaskofu wa kipentekoste wanatetea.

Kenya pia DECI iliendeshwa na makanisa hayo, na maaskofu wa kipentekoste walihusika sana kueneza na kushawishi waumini wao na watu wengine. Na kwa kuwa dhamiri za waumini zinaelekea kufuata sana wanayoelekezwa na "watu wa Mungu" basi kampeni za viongozi hao wa dini zilifanya watu hata wakaidi maonyo ya serikali kama inavyokuwa sasa Tanzania.

Lakini baada ya DECI Kenya kuanguka, viongozi hao wa dini wa Kenya wametubu hadharani na kukiri KUPOTOSHA watu kuhusu kujiunga na DECI. nanukuu makala hii hapa

toka: Kenya Talk / Donde's DECI used church elders in pyramid scheme
Clergy admits to misleading flock over schemes

Some religious leaders have admitted misleading their flock into joining pyramid schemes.

Members of the clergy yesterday told a taskforce into the operation of pyramid schemes that
con artists, masquerading as religious organisations, took advantage of the Church’s influence.

Presenting their views to Francis Nyenze’s taskforce at the YMCA Hall in Nyeri, the leaders revealed
how directors of one of the schemes, called Deci, duped them.

Bishop Peter Ndegwa of Grace Chapel said the flock joined the pyramid schemes because their
spiritual leaders, like him, were fronting them.

Ndegwa who was managing Deci outlets in Central Province said those who fell to the trickery lost
more than Sh 600 million.

Bishop Erastus Njoroge also owned up, but said its proponents also duped them.

Njoroge said he even knew of some marriages breaking up as a consequence.

This is as Co-operative Development Minister Joseph Nyaga unveiled a taskforce that will investigate collapsed pyramid schemes that swindled Kenyans off billions of shillings.

Mr Nyaga launched the nine-member taskforce that will be chaired by Mr Francis Nyenze, on Monday.

Speaking during the launch, Nyaga said the taskforce would have a three-month mandate to establish who were behind the schemes.

"The taskforce will go around the country, especially the crisis regions which include Nairobi, Mount Kenya and Western province. They will seek to establish how we can resolve the problem and prosecute those involved," Nyaga said.

In 2006 and 2007, there was an influx of organisations luring innocent Kenyans to invest cash with a promise of quick returns. The market regulator, Central Bank of Kenya issued a warning that the schemes were operating against banking regulations, as they were not allowed to collect cash deposits.

"They will investigate the amount and whereabouts of funds invested into the schemes. They will also formulate and recommend strategies to apprehend operators with a view of prosecution," said Nyaga.

At the end of three months, the taskforce will present a report, which will include recommendations and mechanisms for recovery of funds invested.

Nadhani dhamiri zao zinawasuta mpaka leo.

Swali langu ni kwamba, Tanzania tuna historia ya mambo haya. Bado tunaona DECI ni kama ukombozi ulioshuka toka mbinguni. Kwa nini tuwe vipofu wa namna hiyo.

Waumini wa kipentekoste wanaoelewa hili wangewapa maaskofu wao mwanga wa historia ili wasiendelee kupotosha watu. Watakuja juta nao kama Maaskofu wa Kenya wanavyojuta sasa. Lakini pia watajibu mbele ya Mungu wanayemwamini.

Naweka attachment za mambo yaliyokwishatokea marekani ya ki-PONZI ambayo yalianzishwa na makanisa ya kilokole na source yake.

Najua bado wengi mtabisha.

Lakini ukweli ni kwamba DECI ni PONZI, na ponzi popote pale zilipoanza zimeanguka na kuleta hasara na machafuko ya kisiasa na hata mauaji.

UKWELI UTAWAWEKA HURU!!!
Someni attachment hii hapa, ina mengi zaidi ya walokole na UPATU.
 

Attachments

Last edited:
hahaha 200% ndo nini maana hapa ni kitendawili. sisi tusiojua hesabu hatukujiunga kabisa.
 
Cha muhimu ni kufahamu ni jinsi gani DECI inafanya kazi yake. Kama ina characteristics za Pyramid Scheme, basi inastahili ifungwe kwasababu watu watapoteza pesa zao. I have been through that road. Pyramid schemes zimewahi kuanzishwa hapa TZ na zote kuna watu walipoteza pesa zao nyingi tu. Kama Deci inafanya kazi katika misingi inayoeleweka basi, wabaki maana wanasaidia watu. Serekali labda iweke tu tahadhari.."Park at your own risk.."
 
Tatizo la nchi zetu wanadai tu masikini na wanapiga vita umasikini ila kwa njia gani sijui maana kila siku mwenye nacho anaongezewa na mwenzangu na mie anaambulia kuona tu neema zao. Ndo maana watu wanakamatika na DECI kwani heri nusu shari .........................😕
 
Cha muhimu ni kufahamu ni jinsi gani DECI inafanya kazi yake. Kama ina characteristics za Pyramid Scheme, basi inastahili ifungwe kwasababu watu watapoteza pesa zao. I have been through that road. Pyramid schemes zimewahi kuanzishwa hapa TZ na zote kuna watu walipoteza pesa zao nyingi tu. Kama Deci inafanya kazi katika misingi inayoeleweka basi, wabaki maana wanasaidia watu. Serekali labda iweke tu tahadhari.."Park at your own risk.."

DECI ina characteristics zote za Ponzi scheme. Hata jina ni kama la Ponzi scheme iliyokufa huko Kenya.

Hakuna biashara yoyote ya fedha iliyo wazi na halali inayoweza kutoa faida asilimia 100%.

Na kama wanapokea fedha za watu na kuzizalisha ni wajibu wao kisheria kuwa wazi wanazalishaje?

Waweke wazi biashara na vitega uchumi vyao. Vinginevyo ni PONZI tu, another pyramid.

WIZI MTUPU....
 
Locust huishi ktk uswahili wetu una haki ya kusema hayo; hujui shida; una haki hiyo; watu wanapata shida ndg; si dar/mwz/ars/na kwingineko; mie nakuhakikishia kuwa inawezekana kweli kuna huo uharibifu au upotevu wa hela mbele ya safari; lakini je; Bank zetu zimesaidia kwa kiasi gani hawa akina mama yatima na wale wasio na mbele wala nyuma; wakajivunia? ni Pride/Finca ndio wamekuwa wafilisi wa wananchi maskini mpaka sasa ni aibu hata sijui kwa nini BOT iliwaruhusu hao.

Kwa taarifa wasomi wa KITANZANIA ndio wanaongoza kubuni miradi ya kuwanyonya watanzania walio maskini au kuendeleza uchafu huo ambao hauna maslahi kwa watu maskini wasio na elimu; mwenye wazo yeyote aseme; maskini huyu; asiye na dhamana; asiye na mahala pa kukimbilia aende wapi; maana ninachoona DECI dhamana yao ni h iyo hela ndogo unayoweka kuonyesha commitment na kuiacha hela kwa kipindi hico; Nilitegemea JF ndio ingewasaidia hawa; si wakristo si waislam; si kina mama lishe si selemala ; si mafundi viatu si walalahoi wanafaidika.

Ukiwaambia wakopeshe then watataka dhamana; nani anayo dhamana? si angeenda bank ambayo pia masharti ni yaleyale; lets us stop blaming creativity; has to be developed
 
Unalima, Unapanda, Unapalia kisha Unavuna. Hii ndiyo kanuni. Ni kweli unaweza usipalie na ukavuna lakini KUPANDA NA KUVUNA BILA KULIMA !!!.

DECI wangekuwa na miradi (kulima) sawa lakini kupanda na kuvuna tu! Wataalam wa uchumi hebu mtusaidie maana sioni ila wingu zito.

NN
 
Mkutano wa wanachama wa DECI na Maaskofu umefanyika SABASABA PTA hall walioshiriki na muafaka uliofikiwa watuhabarishe
 
Locust huishi ktk uswahili wetu una haki ya kusema hayo; hujui shida; una haki hiyo; watu wanapata shida ndg; si dar/mwz/ars/na kwingineko; mie nakuhakikishia kuwa inawezekana kweli kuna huo uharibifu au upotevu wa hela mbele ya safari; lakini je; Bank zetu zimesaidia kwa kiasi gani hawa akina mama yatima na wale wasio na mbele wala nyuma; wakajivunia? ni Pride/Finca ndio wamekuwa wafilisi wa wananchi maskini mpaka sasa ni aibu hata sijui kwa nini BOT iliwaruhusu hao.

Kwa taarifa wasomi wa KITANZANIA ndio wanaongoza kubuni miradi ya kuwanyonya watanzania walio maskini au kuendeleza uchafu huo ambao hauna maslahi kwa watu maskini wasio na elimu; mwenye wazo yeyote aseme; maskini huyu; asiye na dhamana; asiye na mahala pa kukimbilia aende wapi; maana ninachoona DECI dhamana yao ni h iyo hela ndogo unayoweka kuonyesha commitment na kuiacha hela kwa kipindi hico; Nilitegemea JF ndio ingewasaidia hawa; si wakristo si waislam; si kina mama lishe si selemala ; si mafundi viatu si walalahoi wanafaidika; Ukiwaambia wakopeshe then watataka dhamana; nani anayo dhamana? si angeenda bank ambayo pia masharti ni yaleyale; lets us stop blaming creativity; has to be developed

Mkuu, mi naomba ukae utafakari na ujue ya kuwa kama ulishiriki katika DECI basi wewe ni mnyonyaji na umekula pesa za wenzako hao unaodai ni maskini watanzania. Na ninaomba urudishe hiy 'faida' feki uliyopewa kwani ni pesa za mvuja jasho mwamnifu aliyedanganywa na hivi sasa hawezi kurudishiwa pesa zake.

Kaa utafakari hilo alafu kwa majibu zaidi soma jibu ndefu niliyotoa katika thread ile ya mwanzo ya DECI.
 
duuuuuh..ebwanaeheeeeeeee..duuuhhh

Kwani...bila kuwepo deci wananchi masikini walikuwa wanaishije?...kwani hawakuwa wanaenda finca na prride na kwenye saccos zao?....hapa issue sio deci...issue ni ufuataji wa taratibu za kisheria uliowekwa na nchi katika kufanya biashara ya kutoa pesa...kama deci ni charity basi iwe imesajiliwa ki-charity ili itoe misaada...kwanini wanapokea hizo pesa(mbegu) za maskini?...pia kama deci ni chombo cha dini za kipentecostal...kwann kinatoa misaada hiyo ya mavuno au kwanin kinaruhusu wasio waumin au wafuasi wake kupanda na kuvuna shambani mwao?...(waislam na wapagani na wakatoliki na wasabato ndio wateja wakuu wa deci)...hapa naona mpango mwingine wa deci..samahani lakini kwa kuuhusisha na udini zaidi...deci naomba niuite kuwa ni mpango wa wazi wa hayo madhehebu ya kipentecoste na nahisi kwa kusaidiwa na wafadhili wa nje ya nchi kuwaingiza waumini wengine wa madhehebu mewngine kwenye hiyo jumuiya ya kipentekoste...je kwa manufaa ya nani zaidi ya huyo foreign sponsor/godfather?...hii kwa usalama wa nchi ni mbaya sana...itafika wakati wananchi watapeleka pesa yao yote ya bajeti ya serikali say 100 trilion tshs zikawa chini ya deci ambayo inatumiwa say na kina osama wa ki-pentecoste...unadhani inchi itatawalika hii?

Anyway mie sio mpiga siasa.....naomba hawa viongozi wa deci waseme hizi superprofit wanazitoa wapi??...au kama zinatoka kwa mungu twende tukazione anapozishusha...mbona hata mana kwa wayahudi ilijulikana inapotoka...leo iweje deci hawataki kuseema hayo mavuno wanayatoa wapi???

Pia viongozi wa kipentecoste(dini) naona wanajisahau kuwa hata yesu alisema ya mungu mpe mungu na ya kaisari apewe kaisari...ndo maana alimtuma petro akatupe ndoana yake baharini samaki wa kwanza atakayemvua ampasue atakuta dinari mbili aje alipe kodi ya kaisari moja yake na moja ya yesu....sasa deci na maaskofu kwanini hamtaki mkumpa kaisari iliyo yake??.....nendeni bot mkajisajili kama financial instutions nyingine- hapa ndio mtakuta kwanini watu kama kina mchungaji nabii na mtume mwingira wa efetha alivyoshindwa kufunguwa benki yake, hapa mtakuta na kujua kwanini kanisa katoliki la kirumi mpaka leo linachangisha sadaka kufungua benki yapata mwaka wa kumi hawajaweza, nendeni tra mkalipie kodi zote na muwe na leseni zote za biashara.

Hii nayo ni kwenu watu wangu..wananchi na waumini wa deci...bwana(mungu) hakuwa mjinga kusema asiyefanya kazi na asile, na aliposema anabariki kazi za mikono ya mwanadamu hakukosea.....sasa jibuni maswala haya?....pesa mnazoweka deci mnastahili kuzila?...kwani mmefanya kazi gani?..au unadhani ukishapelekaa deci wakakuandika ndio umefanya kazi unastahili kula faida 150%?.....ni maoni yangu tu na kuamua kutumia uhuru wangu wa kutoa maoni.
 
Back
Top Bottom