Fact: Si rahisi hata siku moja kwa mtawala mdanganyifu (mwanasiasa fisadi) kumhadaa mtu mwenye pesa, amchague kwa kumpigia kura za ubunge au urais. Hilo haliwezekani.
Fact: Daima watawala wetu hawataki watu maskini wawe na uwezo, wa kujikwamua kutokana na lindi la umaskini.
Fact: DECI wamegundua njia ya kufanya kazi nje ya mfumo wa kibenki wa Tanzania, jambo ambalo limewatisha watawala na wamiliki wa mabenki haya. Watu wakizidi kuhamisha pesa zao kutoka kwenye benki hizo, na kuzipeleka DECI, uhai wa benki hizo utakuwa mashakani. Hakuna benki yenye uwezo wa kuwapa watu faida ya 125% kwa muda wa miezi 4. HAKUNA!
Kama DECI wamekiuka sheria, na kama kweli wamewatapeli au wana nia ya kuwatapeli Watanzania, wafungiwe, lakini kama sivyo, ndugu zanguni mnapiga vita nafasi ya kuachana na umaskini, tena kwa pupa bila kuchuja pumba na chuya! Kalaghabaho! Wenzenu wanavuna wanachopanda, nyie mnakalia, matapeli... nani ametapeliwa?
Kilichotokea Kenya si lazima kitokee hapa nchini... kumbukeni, Kenya wao ni rahisi sana kushika silaha na kupigana... si mnakumbuka yaliyotokea hivi majuzi, baada ya uchaguzi mkuu wao kufanyika? Sisi hapa tunaweza kweli kukatana mapanga kwa sababu ya tofauti za kisiasa? Sisi ni wapenda amani, na kamwe hatuwezi kuwa na mfumo wa kitapeli nchi nzima.
DECI inawasaidia Watanzania wasiokopesheka, maskini wanaolala kwenye nyumba za udongo, tena wasio na uhakika wa hata mlo mmoja. Leo mnasema IFUNGWE? Ina maana wao hawana haki ya kuachana na umaskini? Acheni ROHO MBAYA!
Kama wewe una uwezo, ni wewe, waacheni wasio na uwezo wawezeshwe. Hii ni Maisha Bora kwa Kila Mtanzania KWA VITENDO! Msiungane na MAFISADI!
Kama kuna atakayechukia, basi, namwomba radhi, lakini binafsi siungi mkono Serikali kuifungia DECI, kwa sababu, hii ni REVOLVING FUND, sio PYRAMID SCHEME! Kwenye PYRAMID SCHEME unaambiwa nenda ulete wanachama wengine, kwenye DECI ni wewe mwenyewe na mtaji wako. Wapi na wapi ndugu zanguni?
Kama kuna ambaye amelizwa na DECI hapa Tanzania, vyombo vya sheria viko wazi, aende akashtaki. Hajazuiwa. Lakini kama mnasema tu, bila kuchuja, bila kufikiria, mnawasaidia mafisadi kuwakandamiza Watanzania wanyonge, walio wengi, maskini, fukara wa kufukarika!
Maisha Bora kwa Kila Mtanzania yanawezekana! Tusiyapige vita!
./Mwana wa Haki