DCI Manumba akata kauli

DCI Manumba akata kauli

Pole sana Kamanda!...Mungu atakutendea Miujiza!
Its a moment whereby every citizen got to pray for him...
Do away with personals buddies, hakuna anayeomba kuugua!
Hata hivyo, Malaria HAIKUBALIKI!

kwa kweli naomba nikiri kwamba siwezi kupoteza nguvu zangu kufanya kazi hiyo. Simwombei afe ila kwa matatizo wanayowafanyia watz samahani sana.
 
Get well soon Manumba, japo una vimeo lukuki, lakini haki ya kuishi unayo kama human beings wengine bana!
 
Kabla sijatia neno,naombeni mnikumbushe mchango wake kwenye jamìi

Mi nakushauri we utie neno tu kwani ukiambiwa mchango wake katika jamii NENO lako linaweza kupandisha hasira za wenzake humu JF.
 
mie naona wanatukaushia tu amekwisha R.I.P hapo hakuna namna siku hizi mambo ya kawaida wala hatupaswi kushtuka
 
Atukawii kusema amekuwa "manumbaized"!!!
 
AFYA ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi nchini (DCI), Robert Manumba inazidi kuwa mbaya baada ya kuwapo taarifa kwamba amekata kauli na mawasiliano kwa siku tatu mfululizo, huku akiendelea kupumua kwa msaada wa mashine.
Hali hiyo tete ya afya yake imesababisha kuwapo kwa usiri mkubwa kutoka kwa maofisa wa Jeshi la Polisi, madaktari wanaomtibu na ndugu zake.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa kifupi sana, Daktari Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan alikolazwa, Jaffer Dharsee alisema kuwa atakuwa tayari kueleza maendeleo ya matibabu ya Manumba Jumatatu ijayo.
“DCI Manumba bado yupo katika chumba maalumu akiendelea na matibabu chini ya uangalizi maalum wa madaktari na wauguzi,” alisema Dk. Dharsee.
Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika viwanja vya hospitali hiyo jijini Dar es Salaam, umebaini kuwa hali ya DCI huyo inakatisha tamaa.
Hali hiyo ndiyo imeifanya serikali kushindwa kumsafirisha nje ya nchi kwa matibabu zaidi.
Hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia kumwona isipokuwa kwa baadhi ya viongozi na ndugu wachache muhimu.
Manumba aliugua ghafla na kulazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, akipatiwa matibabu kwa kile kilichoelezwa kuwa na wadudu wengi wa ugonjwa wa malaria.
Hata hivyo, Januari 14, alihamishiwa katika Hospitali ya Aga Khan kwa matibabu zaidi na kuwekwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.
Manumba aliteuliwa na Rais Kikwete kushika wadhifa huo mwaka 2006, akichukua nafasi ya Adadi Rajabu.

Mtanzania
Ma Dr waseme ukweli kama ni mapenzi ya allah.
 
Tunasubiri update jamani!!! Au ni siri kuu hadi mfalme arudi!! Maana alienda kumtembelea mara tatu tatu!!! Kunani?
 
We unadhani ule mgomo wa madaktari,hasa hasa madai yao yalikuwa nini..." Mazingira bora ya kufanyia kazi" ilikuwa ina maana hiyo..
Wanasiasa wakaanza kupotosha eti helaa..helaa..
Kama wanavyopotosha ishu ya Mtwara na gas sasa hivi..
Usitukumbushe wauwaji wale. Kama sio helaa ni nini, maweee???
 
Hatakufa, bali ataishi! ili ayasimulie matendo makuu ya mungu! Manumba tunakuombea upone lakini ukirudi huku mtaani, uache uovu na utende haki katika wadhifa ulionao huko serikalini!
 
Sina hakika kama Aga Khan ndio hospitali bora zaidi nchini? Wanaweza kuwa na vitanda vizuri na upepo mwanana toka baharini (japo kuna harufu mbaya) lakini kwa matibabu? sidhani! Muhimbili angeweza kupata matibabu bora zaidi.Hata hivyo namwombea apone haraka.
 
Back
Top Bottom