DCI Manumba akata kauli

DCI Manumba akata kauli

hivi kauli ikikatika huwa inarudi?
ah nauliza tu jamani!!!!:confused2:
 
Hapo ndipo biashara ilipolalia sasa.. Through malaria watu wanaingiza vpato mifukoni badala ya kupeleka kwenye malaria.. U wapi ule mradi wa kutokomeza malaria kwa kuweka dawa kwenye mazalia ya mbu na vyanzo vyake..? Zaidi ya mahekalu yaliyojengwa kwa hela za mradi ule..? Utabaki kuwa msemo na kichwa cha habari kwenye project write up za kuombea fedha toka kwa wafadhili..

Only in Tanzania..

Kwa kweli mkuu,inauma sana
 
Ishiiiii, ona hili nalo!!!
Ss ponda anahusika nn hapa??

Hujui Sheikh Ponda anahusika vipi enhe! wewe lala tu. Sheikh anakosa la Jinai la kuvamia Kiwanja na kuiba mali za kampuni ya Agritanza..na asipewe dhamana. aishie Segerea ang'atwe na mbu augue na afe kwa Malaria..na wengine walae vizuri nyumbani kwenye chandarua chenye dawa, na ofisi NA GARI zenye ACs.

Sheikh Ponda zidisha ubani baba...!
 
Iwakumbushe askari wote waliopewa dhamana ya kulinda uhai na mali za raia kutenda haki siku zote na kutimiza majukumu yao ipasavyo kwa mujibu wa sheria ili siku yao ya mwisho ifikapo basi wafe kifo chema.Kwa hali aliyonayo DCI Manumba hata kuomba toba hawezi,sisemi kwamba ameshiriki kufanya uzandiki uliopelekea wana wa nchi hii kupoteza maisha lakini kwa cheo alichonacho yeye yote pia yawezekana. Kila mtu ana siku yake na yawezekana kwa Manumba ndiyo siku zake zinavyokaribia,sitaki kuwa mtabiri ila ukweli ndiyo huo.Sisi wenye mamlaka tutubu sasa kwa madhambi na mauaji tuliyoyafanya kwa ndugu zetu na watanzania wenzetu ili tuendelee kufaidi mema ya nchi hii. Tusipofanya hivyo sasa,iko siku ambayo tutatamani kufanya hivyo lakini hatutaweza kama ilivyo kwa Manumba sasa




AFYA ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi nchini (DCI), Robert Manumba inazidi kuwa mbaya baada ya kuwapo taarifa kwamba amekata kauli na mawasiliano kwa siku tatu mfululizo, huku akiendelea kupumua kwa msaada wa mashine.
Hali hiyo tete ya afya yake imesababisha kuwapo kwa usiri mkubwa kutoka kwa maofisa wa Jeshi la Polisi, madaktari wanaomtibu na ndugu zake.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa kifupi sana, Daktari Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan alikolazwa, Jaffer Dharsee alisema kuwa atakuwa tayari kueleza maendeleo ya matibabu ya Manumba Jumatatu ijayo.
“DCI Manumba bado yupo katika chumba maalumu akiendelea na matibabu chini ya uangalizi maalum wa madaktari na wauguzi,” alisema Dk. Dharsee.
Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika viwanja vya hospitali hiyo jijini Dar es Salaam, umebaini kuwa hali ya DCI huyo inakatisha tamaa.
Hali hiyo ndiyo imeifanya serikali kushindwa kumsafirisha nje ya nchi kwa matibabu zaidi.
Hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia kumwona isipokuwa kwa baadhi ya viongozi na ndugu wachache muhimu.
Manumba aliugua ghafla na kulazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, akipatiwa matibabu kwa kile kilichoelezwa kuwa na wadudu wengi wa ugonjwa wa malaria.
Hata hivyo, Januari 14, alihamishiwa katika Hospitali ya Aga Khan kwa matibabu zaidi na kuwekwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.
Manumba aliteuliwa na Rais Kikwete kushika wadhifa huo mwaka 2006, akichukua nafasi ya Adadi Rajabu.

Mtanzania
 
Habari nilizozipata hivi punde, mchana huu zinasema, nanukuu
''He was in Terminal illness with Palliative care but now he is in Brain Vegetation State''
Naamini kuna wataalam hapa JF watatuelewesha vizuri.

Tunamwomba Mungu amsaidie.

Hii ina maana kuwa ubongo wake umekufa ila moyo bado unadunda, of course kwa msaada wa mashine. Unamkumbuka waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon? Mpaka wa leo yuko hai katika hali kama hii uliyoieleza.
 
Hii ina maana kuwa ubongo wake umekufa ila moyo bado unadunda, of course kwa msaada wa mashine. Unamkumbuka waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon? Mpaka wa leo yuko hai katika hali kama hii uliyoieleza.
kwa hiyo akipona na ubongo utafufuka?
 
hii dunia hii!! haya MAPENZI YA MUUMBA JUU YATIMIE, SI TUTAKAVYO SISI, BALI KWA HURUMA NA MASTAHILI YAKE JUU YETU! KIBINADAMU TUNAKUOMBEA UPONE!
 
Ewe mwenyeenzi mungu mponye manumba roho yake na mwili (ikikupendeza)
 
Natamani Upone Baba angu, ila kila nikimkumbuka Mwangosi, najikuta naku....
 
hii dunia hii!! haya MAPENZI YA MUUMBA JUU YATIMIE, SI TUTAKAVYO SISI, BALI KWA HURUMA NA MASTAHILI YAKE JUU YETU! KIBINADAMU TUNAKUOMBEA UPONE!

Hapo kwenye KIBINADAMU TUNAKUOMBEA UPONE NIMEPAPENDA........LAKINI MAPENZI YAKE ALLIYEKO JUU YATIMIE ILI KUKIOKOA KIZAZI HIKI.
 
kwa hiyo akipona na ubongo utafufuka?

Highly highly unlikely!! Mtu wa namna hiyo anakuwa CLINICALLY dead. Kifo cha mtu kinakuwa decided na moyo. Moyo ukiacha tu kudunda, mtu anatangazwa kuwa amekufa kisheria.
 
Highly highly unlikely!! Mtu wa namna hiyo anakuwa CLINICALLY dead. Kifo cha mtu kinakuwa decided na moyo. Moyo ukiacha tu kudunda, mtu anatangazwa kuwa amekufa kisheria.
aisee kama ndo hivyo hii ni hatari,Mungu amnusuru ingawa utakuwa ni muujiza
 
Back
Top Bottom