DCI Manumba akata kauli

DCI Manumba akata kauli

rosemarie

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Posts
6,887
Reaction score
3,441
AFYA ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi nchini (DCI), Robert Manumba inazidi kuwa mbaya baada ya kuwapo taarifa kwamba amekata kauli na mawasiliano kwa siku tatu mfululizo, huku akiendelea kupumua kwa msaada wa mashine.
Hali hiyo tete ya afya yake imesababisha kuwapo kwa usiri mkubwa kutoka kwa maofisa wa Jeshi la Polisi, madaktari wanaomtibu na ndugu zake.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa kifupi sana, Daktari Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan alikolazwa, Jaffer Dharsee alisema kuwa atakuwa tayari kueleza maendeleo ya matibabu ya Manumba Jumatatu ijayo.
“DCI Manumba bado yupo katika chumba maalumu akiendelea na matibabu chini ya uangalizi maalum wa madaktari na wauguzi,” alisema Dk. Dharsee.
Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika viwanja vya hospitali hiyo jijini Dar es Salaam, umebaini kuwa hali ya DCI huyo inakatisha tamaa.
Hali hiyo ndiyo imeifanya serikali kushindwa kumsafirisha nje ya nchi kwa matibabu zaidi.
Hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia kumwona isipokuwa kwa baadhi ya viongozi na ndugu wachache muhimu.
Manumba aliugua ghafla na kulazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, akipatiwa matibabu kwa kile kilichoelezwa kuwa na wadudu wengi wa ugonjwa wa malaria.
Hata hivyo, Januari 14, alihamishiwa katika Hospitali ya Aga Khan kwa matibabu zaidi na kuwekwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.
Manumba aliteuliwa na Rais Kikwete kushika wadhifa huo mwaka 2006, akichukua nafasi ya Adadi Rajabu.

Mtanzania
 
Pole sana Mkuu,tunakuombea upone haraka uje uendeleee na kazi ya kulijenga taifa hili
 
mmmmmmmmmmmmmh....ngoja tusubiri.
 
Dr.akikajaga pipe za pumnzi kwa bahati nzuri biashara imekwisha
 
Natamani sana afike 2015..coz ni miongoni mwa watu ambao lupango inawahusu...
 
Aise, kumbe ikishindikana Muhimbili unahamia Aga Khan, au mi sijaelewa?

We unadhani ule mgomo wa madaktari,hasa hasa madai yao yalikuwa nini..." Mazingira bora ya kufanyia kazi" ilikuwa ina maana hiyo..
Wanasiasa wakaanza kupotosha eti helaa..helaa..
Kama wanavyopotosha ishu ya Mtwara na gas sasa hivi..
 
Naomba mchango wa huyu jamaa kwenye ujenzi wa taifa hili...mbona hamsemii..mmekazana ripii..ripii...sorry,mmekazana get well soon tuu...:majani7:
 
Kabla sijatia neno,naombeni mnikumbushe mchango wake kwenye jamìi
Muulize Samuel Sita na Mwakyembe watakueleza, wakigoma kukujibu iulize Familia ya Mwangosi, ila ana mchango mzuri tu wa kuwakamata wanaotuhumiwa walimuuwa Kamanda Liberatus Barlow wa Mwanza.
 
Amesha danja huyo, wanatupotezaea tu ili kutujenga kisaikolojia ktk kupokea taarifa ya kifo chake.
 
Pole sana Kamanda!...Mungu atakutendea Miujiza!
Its a moment whereby every citizen got to pray for him...
Do away with personals buddies, hakuna anayeomba kuugua!
Hata hivyo, Malaria HAIKUBALIKI!

Hapo ndipo biashara ilipolalia sasa.. Through malaria watu wanaingiza vpato mifukoni badala ya kupeleka kwenye malaria.. U wapi ule mradi wa kutokomeza malaria kwa kuweka dawa kwenye mazalia ya mbu na vyanzo vyake..? Zaidi ya mahekalu yaliyojengwa kwa hela za mradi ule..? Utabaki kuwa msemo na kichwa cha habari kwenye project write up za kuombea fedha toka kwa wafadhili..

Only in Tanzania..
 
[h=3]HALI YA MKURUGENZI WA UPELELEZI WAMAKOSA YA JINAI, ROBERT MANUMBA BADO NI MBAYA....HIVI SASA ANAPUMULIA MASHINE[/h]

HALI ya afya ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba ambaye hivi sasa anapumua kwa msaada wa mashine, bado inahitaji uangalizi wa karibu wa madaktari na wauguzi.

Mkurugenzi wa Tiba wa Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam, Jaffer Dharsee alithibitisha hayo jana katika taarifa yake iliyoelezea hali ya Manumba anayeendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.

“Uongozi wa hospitali ya Aga Khan unapenda kuujulisha umma, kwamba DCI Manumba bado yuko hospitali anaendelea na matibabu. Hali ya afya yake bado inahitaji uangalizi wa karibu wa madaktari na wauguzi,” alisema.

Katika hatua nyingine, ndugu, jamaa, marafiki na maofisa wa ngazi mbalimbali wa Polisi waliendelea kufika hospitalini hapo kumjulia hali Manumba ambaye amelazwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU).

DCI Manumba aliugua ghafla na kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Januari 14, kabla ya kuhamishiwa Aga Khan kwa ajili ya uchunguzi zaidi na kulazwa ICU.
 
Back
Top Bottom