Day 14: John Heche ahamishwa kituo cha Polisi, haijulikani anapelekwa wapi

Day 14: John Heche ahamishwa kituo cha Polisi, haijulikani anapelekwa wapi

Makumbele

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2009
Posts
239
Reaction score
1,055
eb80baeb-fd2f-4683-a0f2-cd6e9db81a0a.jpeg


Leo, 04 Novemba 2025, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche alichukuliwa mahabusu ya Polisi kuwa anahitajika kwa RPC Dodoma.

Heche amechukuliwa huku mke wake akishuhudia akiwa na Katibu wa Kanda ya Kati (CHADEMA) Bi ashura Masoud.

Walijaribu kuongozana na gari la Polisi lakini magari hayo yakaongeza mwendo na kuwaacha nyuma. Walipofika kwa RPC wakaambiwa hana taarifa za Heche kuhitajika hapo na hana kazi naye.

Mpaka muda huu, Mke wake amebaki hapo bila msaada wowote kuwa aelekee wapi.

Vitendo hivi vinaonyesha nia ovu kwa watanzania akiwemo ndugu Heche.

Waliopewa mamlaka ya kutulinda ndo wamekuwa tishio la usalama wetu; tufanye nini sasa?
 
TAARIFA KWA UMMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinauarifu umma kuwa leo, Jumanne, tarehe 04 Novemba 2025, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mheshimiwa John Heche, amechukuliwa na askari wa Jeshi la Polisi kutoka kituo cha Polisi cha Mtumba kwa madai kuwa anahitajika na RPC wa Dodoma.

Tukio hili lilitokea mbele ya mke wake pamoja na Katibu wa Kanda ya Kati, Bi. Ashura Masoud. Walipojaribu kufuatilia ili kujua wanapompeleka, magari yaliyombeba yaliongeza mwendo na kuwaacha nyuma.

Baadaye, walipofika kwa RPC wa Dodoma walielezwa kuwa RPC hana taarifa yoyote kuhusu kumhitaji Mh. Heche. Hadi sasa, haijulikani alipo huku familia yake na Chama kimebaki na wasiwasi mkubwa juu ya usalama wake na wapi alipo.

Tunamtaka Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Camilius Wambura, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Ramadhan Kingai, Mkuu wa Polisi Mkoa (RPC) na Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtumba watoe maelezo ya haraka kwa umma kuhusu mahali alipo na hali ya usalama wa Mheshimiwa John Heche.

Imetolewa leo Jumanne, tarehe 04 Novemba 2025.
Brenda Rupia
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi

Screenshot 2025-11-04 144120.png
 
Aliomba wakenya waje kusaidia!?..muda wa malipo
Hakuomba wakenya wala haluna sehem hiyo, ni wananchi wenyewe

Anyway hawana cha kufanya maana tayari yupo mikononi mwa polisi. So chochote kitakachotokea watakuwa responsible
 
Cha muhimu walioandamana au wale waliouliwa ndugu zao wasije wakafikiria mambo ya kujitoa mhanga,italeta taharuki sana.
 
Hakuomba wakenya wala haluna sehem hiyo, ni wananchi wenyewe

Anyway hawana cha kufanya maana tayari yupo mikononi mwa polisi. So chochote kitakachotokea watakuwa responsible
Ipo clip anaomba wakenya waje kusaidia
 
Back
Top Bottom