John Heche kusitisha kula kuanzia leo akiwa mahabusu

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Katibu wa familia na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mara, Mwalimu Chacha Heche, ametoa taarifa kuhusu hali ya kaka yake, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, John Heche, ambaye kwa siku 13 sasa amekuwa mikononi mwa Jeshi la Polisi, katika mahabusu ya Mtumba, Dodoma.

Kupitia taarifa hiyo, Chacha amesema Heche amemtumia ujumbe wa masikitiko kuhusu hali yake ya kiafya ambayo inaendelea kudorora, huku akieleza kuwa hajapatiwa haki zake za msingi za dhamana wala matibabu ya kina. "Amenitumia taarifa ya masikitiko kuhusu hali yake ya kiatya kuwa inaendelea kuzorota na hakuna dalili za yeye kupata haki ya dhamana ama ya matibabu ambayo ni haki ya kikatiba," amesema Chacha kupitia taarifa hiyo.

Ameeleza kuwa kwa sasa Heche anapata huduma za kwanza pekee, ambazo hazijasaidia kubadili hali yake, akihitaji vipimo na matibabu ya kitaalamu zaidi kutokana na kudhoofika kwa mwili.

Kwa mujibu wa Chacha, Heche ameshawasilisha malalamiko kwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya (OCCID) akieleza kuwa, iwapo lengo la kuzuiliwa kwake ni kumuumiza, kuanzia kesho atasitisha kula kama njia ya kupinga kile anachokiita "mateso yasiyo na msingi wa kisheria."

Juhudi za kumtafuta Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya (OCCID) Dodoma au msemaji wa jeshi la polisi ili kuzungumzia suala hilo bado zinaendelea!!

Pia Soma: Day 14: John Heche ahamishwa kituo cha Polisi, haijulikani anapelekwa wapi
1762254206053.png
 
Wanasheria wa chadema wafungue kesi ili apelekwe mahakamani au wanasubiri mpaka apotee ndo waanze kuwafunguliaa kesi polisi kwamba waseme yuko wapi.
Nchi imeshaharibika hii, siki zote 14 hakuna hata anayehangaika kufungua kesi! Chadema wajue mfumo uko against wao kila wakati wawe mbele ya muda kuweka record mahakamani. Hizo kesi za kuwatafuta akina polepole, soka zitasaidia miaka ijao dunia haisimami na pia haifuti kumbukumbu.
 
Mambo ya kuweka watu kizuizini nilifikiria yaliishia awamu ya kwanza?
 
Simshauri kwa watu hawa waliowatwanga risasi waru wasio na hatia, yeye akigoma kula ndio kwanzaa watafurahia, atakuwa kawapunguzia kazi kwa akili zao
 
Back
Top Bottom