DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Kuna mtaa unaitwa Hondogo kwa Shija kata ya Kibamba Wilaya ya Ubungo una makazi mengi sana na yanaendelea kuongezeka lakini bomba lipo mbali zaidi ya mita 200 tunaomba mpitishe bomba ili kuwezesha uunganishaji wa maji kuwa rahisi na kwa gharama nafuu.
 
Hawa dawasco wapo nyuma sana
Mimi nimeunganishiwa maji tokea mwezi mei mbaka leo tar 28,8 ,2018 sijamuona msoma mita , wala kutumiwa sms yeyote ile
Sielewi tatizo ni nini au niendelee tu kula shushu mbaka hapo watakapo hamua kuja wenyewe
Mimi nadhani ili shirika linapigwa sana na vishoka.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dawasco ni utumbo kwa kweli kuleta maji maeneo ya kinyerezi tumechangishwa baada ya kuchanga ili tusogezewe mbinde ipo kwenye kuingiza maji ndani ya nyumba hapo ndio utawajua wao ni nani
 
Dawasco Dawasco Dawasco.
Pls njoni hapa Boko Mbweni, Kituo Masaiti. Pindeni kushoto mkitokea Boko. Hapo sasa ni mwezi maji ya bomba yanatiririka sana. Bomba linavuja sana sana sana kama hamtawahi eneo lote la uwanja wa wazi litaakuwa bwawa. Harakisheni.
 
Dawasco Dawasco Zinga kwa Hawadhi na Kwa Masister tuko na shida ya maji huu ni mwezi wa pili akuna maji wananchi tunapata shida na maji na nyie pia unakosa kipato kutoka kwa sisi wateja wenu fanyeni mpango muangalie umuhimu wa wateja wenu na nyie pia kwenye biashara yenu pia maana akuna haja ya kua na wateja wengi ambao hawawaingizii kitu
 
Dawasco nataka kujua utaratibu mpya wa kufungiwa mita mpya za luku utaratibu upo vipi???.

Nawasilisha.
 
Hizi sms za kutishia kukatia maji kutwa kutoka kwa hawa DAWASCO/DAWASA kwa kweli tumechoka nazo, ni mpaka tunakereka, kama mnakata maji kateni kwa hao wasiolipa kuliko kututumia hizo sms za vitisho, au vipi leteni meter tuwe tunalipa as we go, its too much, mpaka tunafikiria mikopo tujichimbie visima vyetu tuachane nanyi..
Mnachokifanya siyo utu kabisa, na sidhani kama mnatumia ustaarabu, its bad ethics, I wish somebody will tell them to stop this malpractice IMMEDIATELY

:mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad::mad:
 
Eneo La Kanisa Katoliki Maji Ya Dawasco Yanamwagika Usiku Na Mchana Kila Siku
Mimi Nimehamia Hapa Mwaka Hali Ndiyo Hiyo
Mitaro Ya Barabarani Imejaa Maji


Ukitoka Mwembeyanga Kwenda Kilakala Kuna Kituo Kinaitwa Kanisani Maji Yanamwagika Hadi Kwenye Barabara Ya Lami
 
Habari za kazi mimi naitwa justine nakaa mbezi beach karibu na mbezi apartments,kuna jirani yangu anaitwa mziray ukifika mbezi apartments kona ya kwanza kulia nyumba ya tatu haina geti kulia anawaibia maji usiku kwa kukata mabomba na kukinga maji na kutulelea adha ya kutuharibia ukuta,kila siku tunajitahidi kutengeneza mabomba lakini ikifika usiku uwa anayakata maji kwa msaada nipigieni nitawaelekeza ili muweze komesha kadhia hii ukifika tangi bovu katikati ya nbc bank na oilcom shell kuna barabara ya ntukamazina rd
 
Habari za kazi mimi naitwa justine nakaa mbezi beach karibu na mbezi apartments,kuna jirani yangu anaitwa mziray ukifika mbezi apartments kona ya kwanza kulia nyumba ya tatu haina geti kulia anawaibia maji usiku kwa kukata mabomba na kukinga maji na kutulelea adha ya kutuharibia ukuta,kila siku tunajitahidi kutengeneza mabomba lakini ikifika usiku uwa anayakata maji kwa msaada nipigieni nitawaelekeza ili muweze komesha kadhia hii ukifika tangi bovu katikati ya nbc bank na oilcom shell kuna barabara ya ntukamazina rd
Poleni sana Dawasco nao wamezidi kubambika bill ndio maana watu wanafaulisha maji. Hii michezo watu wengi waliokatiwa maji au wanaokuwa na matumizi makubwa huwa wanaifanya. Mbezi appartments ziko nyingi mkuu. Utakuwa uko jirani sana na Babu Rich baharia wa siku nyingi.
 
Hebu tupeni suluhisho la sisi kupata maji Mbezi Beach Jogoo, serikali za mitaa/Kerai Constraction. Tafadhali toa update kwenye huu uzi, sio kutupotezea muda !
 
Nyie dawasco mmekata maji huku Mbezi beach hadi bunju huko bila taarifa. Mtuambie sasa yanarudi lini mxieewww nna hasira.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom