Juzi walikuwa wanatangaza mfumo wa mita mpya za malipo ya Prepaid[Mfumo kama wa malipo ya LUKU] Sijui utaanza mwaka gani, lakini walizindua tarehe 23.07.2018. Huuu ndio utakuwa mwarobaini. Wasoma mita za maji wahuni wataondoka ktk system, na itasaidia ukusanyaji wa mapato wale wasoma mita watabaki kukagua kuna utoroshwaji wa maji wapi? Maana kampuni ina wafanyakazi wengi lakini ufanisi mdogo sana na watu wanaiba sana maji na wakifunga izo mita mpya ziwe zina uwezo wa kutoa report ya kuanzia bomba kubwa ulipoungwa na mpaka kwy mita yako, tatizo linaloikumba Dawasco kuna wafanyakazi wenye umri Mkubwa ambao kasi ya technology imewatupa na wapo kitengoni, ndio iyo unakuta MTU ana diploma yeye ndio boss anasimamia sehemu alafu wasoma mita wana degrees, sasa apo kwy kugawanya madaraka inakuwa ngumu sana. Unakuta kunakuwa na ubishani na ukwamishaji ukwamishaji,. MTU ana degrees ya uhandisi wa maji lakini ataki kuchafuka na kuchimba ili kuweka bomba la maji sawa. Mimi hii ilishanikuta mtu, anakuja kurekebisha bomba muda wote yupo kwy simu Mara uku Mara Kule mpaka, nikamtafutia MTU wa kuchimba ndio akaaunganisha bombaKuna tatizo kuhusu mfumo MPYA wa kulipia bili kwa kutumia reference number yenye tarakimu 12. Mfumo haukubali kulipia kwa Simu kama tunavyoambiwa. Nilijaribu Mara NNE kulipia kwa tigo pesa! Unafuata hatua zote mpaka kuweka mamba ya siri lakini bado malipo hayafanyiki. Mpaka nikalazimika kwenda kulipia CRDB kwa kupoteza pesa kwa kulipa nauli na kupoteza muda kwenye foleni!! Huu mfumo haufai!!!
Pili reference number ingekuwa ni moja tu kwa kila MTEJA kwa muda wote kuliko hii ya kupewa reference number MPYA kila mwezi.
Tatu, pamoja na kuwa wana namba Yangu nilisubiri reference number kwa miezi miwili bila mafanikio mpaka nikalazimika kwenda ofisini kwao!!!!
Warudishe mfumo wa mwanzo uliokuwa rafiki zaidi wa kutumia akaunti namba ambapo tulikuwa tunalipia kwa Simu bila matatizo.
Sent using Jamii Forums mobile app
heri hata mliyounganishiwa huduma mm nipo kiwalani maji dawasco nayasikia tu sijui yanafananajeDAWASCO ; Kwa muonekano huu wa kuchelewesha kujibu hoja za wateja, inaonyesha hii Special Thread haijakuwa assigned kwa mtu specific wa kushughulikia kujibu kero za wananchi. Kama mmenuia kutumia njia hii kuwa karibu na wateja wenu, ni vyema mkamu-assign mtu 'informed' wa customer service awe na kazi ya kujibu kero za wananchi mmoja mmoja na ku-coordinate na wahusika ili kuleta tija kwa jamii.
Kuwa na special thread kusiwe fashion, kwa sababu taasisi nyingine wanayo. Ni fursa ambayo mkiitumia vema mtapata taarifa nyingi za kusaidia kuboresha huduma zenu, kulinda miondo mbinu yenu, kupunguza foleni ndefu (zisizo na tija) kwenye maofisi yenu na kupunguza rushwa na vishoka.
Iyo mifumo kama itakuwa na uwezo kujua maji yanayokuwa yanamwagika kuanzia maungio makubwa mpaka kwa mteja. Itakuwa nzuri lakini kama aitaweza kugundua kiwango cha maji yamwagikayo basi, watu wengi wataiba sana majiNaomba kuuliza hyo kampuni inayofunga mita za, maji za luku inaitwaje? Na je wameanza maeneo gani?
Je plan yao kufikia jiji zima upoje
Mikocheni karibu na Club 327, barabara ya rose garden kuna bomba lina karibu mwezi sasa linamwaga maji. ni bomba kubwa la Dawasco. tumesharipoti mpaka tumechoka. tunawaachia wenyewe siku mkipita mlione maana na nyie mmezidi. kujituma ni janga la kitaifa