Haya ni sehemu ya aliyoyasema kijana kafulila kwenye press conf.
TAMKO LA DAVID KAFULILA KUHUSU UAMUZI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) ULIOZUA UTATA NCHINI.
1.0 UTANGULIZI
Kwanza niwashukuru wanahabari kwa kuchag kuja kunisikiliza mimi niliye mdogo sana kimamlaka katika siasa za nchi hii kiasi cha baadhi ya viongozi wenye heshima kuufananisha ubinadamu wangu na sisimizi. Nawashukuru kwakuwa mmethibitisha kuwa waumini wa dhana ya binadamu wote ni sawa, wanastahili heshima kwa thamani yao.Nawapongezeni kwa hilo kwakuwa hiyo ni moja ya tunu imara ambayo watanzania tulirithishwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
2.0 SABABU ZILIZOSABABISHWA KUTENGULIWA KWA MUJIBU WA CHADEMA
Mnafahamu na mmekuwa mkiripoti mwenendo wa siasa ndani ya CHADEMA kuhusu kadhia ya kinachoitwa mgogoro ndani ya CHADEMA kufuatia taarifa za kikao cha siri kilichofanyika Dodoma chini ya uenyekiti wa Freeman Mbowe. Mpaka sasa mengi yamesemwa na viongozi mbalimbali akiwemo, Mwenyekiti wa kwanza na Mwasisi wa CHADEMA-Mzee Edwini Mtei, Mwenyekiti wa pili-Mzee Bob Makani, Mwenyekiti wa sasa Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu..
Aidha, mengi pia yamesemwa na wanachama, wafuasi na wadau wa siasa nchini kwa misingi ya siasa na hata dini kuanzia mkoani kwangu Kigoma na Taifa kwa ujumla. Kwa kutambua nafasi yangu kama kijana mwenye ndoto ya kuchangia mabadiliko makubwa katika medani siasa za nchiini, naomba nichukue nafasi hii kueleza zinazoitwa sababu zilizopelekea CHADEMA kufikia uamuzi ilioufikia dhidi yangu.
Sababu inayoelezwa ni mimi kutotambua kikao cha siri kilichoendeshwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe Dodoma na baadhi ya viongozi wa chama. Binafsi nilikiri na bado ninakiri kwamba sikufahamu kuhusu kikao hicho kwakuwa hakipo kwa mujibu wa katiba, kanuni, maazimio na hata ratiba ya chama. Na nikiri pia kutotambua kikao hicho kwa msingi wa jukumu la kumvua mtu uanachama wa CHADEMA kama nilivyoulizwa na mwandishi wa habari, kwani kwa mujibu wa katiba, kikao cha kujadili uanachama wa mwanaCHADEMA sio kikao cha siri. Huo ndio ulikuwa msingi wa kwanza wa majibu yangu kwenye kikao cha sekretariet ya Novemba10,2009.
Pamoja na kikao hicho kutotambuliwa kwa mujibu wa katiba, kanuni na hata maazimio ya chama, binafsi sikuwa na fursa yoyote kufahamu kikao hicho kwakuwa; kwanza Mkurugenzi wa Habari na Uenezi ambaye ni Mkuu wangu katika idara kwa makusudi au bahati mbaya hakuniaga na wala kunikaimisha Ofisi kitu ambacho kingenisaidia kujua kwamba kuna kikao Dodoma. Hata aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu wakati huo, Mzee Victor Kimesera alikiri kwenye kikao cha sekretariet ya Novemba10,2009 kwamba hakuwa na taarifa kuhusu kikao hicho kilichohusu wakurugenzi walio chini yake,na kwamba alipewa taarifa tu kwamba kuna wakurugenzi wako nje ya mkoa kwa shughuli za chama Dodoma wakiwa wamesha ondoka Sio hapo tu, hata Novemba4, 2009 usiku nilipowasiliana na wajumbe wa sekretariet kuwakumbusha kuhusu kikao cha kesho yake (Novemba05, 2009), ambao sehemu yake walikuwa kwenye kikao hicho cha siri, bado sikujulishwa kwamba kuna wajumbe walikuwa nje ya Dar es Salaam wakiendelea na kikao kingine na kwamba wasingeweza kufika kwenye kikao rasmi cha sekretariet siku ya Novemba5,2009..
Nimeona nitoe ufafanuzi huo kwa ajili ya kuweka kumbukumbu sahihi ya nini kilichotokea kwakuwa pamekuwapo upotoshaji wa taarifa kuhusu jambo hili, kiasi cha wengine kuandika kwamba nina kosa la kutoa siri za chama. Napenda kuwajulisha kwamba sijachukuliwa hatua kwa kosa la kutoa siri za chama, bali kwa kilichoitwa kosa la kutotambua kikao cha siri chenye mamlaka ya kumvua mtu uanachama.Kwa mujubu wa katiba kikao cha kumfukuza mtu uanachama hakiwezi kuwa siri kwa mujibu wa katiba na kanuni. Na kwamba mwanachama makini wa chama makini hawezi kufukuzwa kwa vikao visivyo rasmi.
TATIZO LA MSINGI NI NINI CHADEMA ;
Kwakuwa pamekuwapo upotoshaji mkubwa kuhusu suala hili unaofanywa kupitia vyombo mbalimbali vya habari, ninaomba kuwaeleza vijana wenzangu wa CHADEMA ukweli uliopelekea hali hii;
1.AUMUZI WANGU WA KUHOJI KUHUSU UKWELI NDANI YA CHAMA.
Nilimwambia Dr Slaa, na sasa naomba niwaambie wanachadema kwamba tatizo nililoitiwa kuhojiwa halikuwa tatizo husika.Chanzo cha matatizo yote haya ni uamuzi wangu wa kuhoji ili kama chama TUJISAHIHISHE.
A.Nilihoji kuhusu matumizi ya ruzuku .
Mchakato wa kunifukuza makao makuu haukuanza leo. Nakumbuka februari 2009, wakati nilipokuwa nikihoji kuhusu matumizi ya milioni35 za mwezi desemba2008,Mkurugenzi wa Fedha alithubutu kumwambia Katibu Mkuu kwamba Huyu Kafulila sio mjumbe wa kikao, kwaiyo hapaswi kuwa anahoji kwenye sekretariet, yeye ni mwandishi tu. Hapa nilimhoji Dr Slaa ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kikao Kwanini tangu mwaka 2007 nimeruhusiwa kuingia kwenye kuandika na kuchangia hoja, iweje leo nisiruhusiwe kuchangia hoja?, kwasababu ninahoji masuala ya taarifa za fedha?.
B.Nilihoji kuhusu taratibu za fedha ndani ya chama.
Chuki zaidi iliongezeka baada ya kushinikiza kwenye vikao vya sekretariet kuhusu kuundwa kwa Kamati ya manunuzi badala ya Mkurugenzi wa Fedha kuwa muamuzi katika hatua zote za manunuzi. Hoja hii haikupendwa na ndio sababu pamoja na kuundwa kwa Kamati hiyo ya manunuzi bado masuala yote ya manunuzi yameendelea kufanywa na Mkurugenzi wa Fedha kama zamani. Ikiwa ni takribani miezi nane tangu kamati ya manunuzi iundwe, bado haijawahi kukaa kikao chochote kuamua manunuzi ya chama.
Sio hayo tu, hata mpango wa sasa wa kuchangisha fedha kwa SMS hauna usalama wa fedha hizo kwasababu watia saini(signatories) ni Mwenyekiti Freeman Mbowe na Anthony Komu ambao hawakuteuliwa na kikao chochote kuwa signatories.
C.Mwendelezo wa chuki kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa chama.
Katika kikao cha kwanza cha sekretariet baada ya uchaguzi mkuu wa chama, Katibu Mkuu alinifokea na kuniambia mlango uko wazi kwa madai kuwa nilishiriki kumfanyia kampeni Zitto Kabwe. Kwaiyo mimi nilitakiwa kuchukuliwa hatua kwa kumpigia kampeni zitto kabwe, lakini akina John Mnyika, John Mrema, Anthony Komu, Benson Kigaila hawakuchukuliwa hatua kwasababu tu walikuwa wakimfanyia Mbowe kampeni.
D.Mbowe na Slaa hawakutaka Kafulila awe kiongozi.
Baada ya kuanza kuhoji kuhusu uhalili wa masuala mbalimbali ya chama, Mbowe na Slaa walihakikisha kwamba David Kafulila hawi kiongozi wa chama. Mwaka jana wakati wa mchakato wa kumpata Mkurugenzi wa vijana, jina la David Kafulila lilipingwa vikali na wapambe wa Mbowe na Slaa. Lakini kwakuwa walijua kwamba nina sifa za kushika nafasi hiyo, kila walipotaka kupeleka majina ya wanaopendekezwa na sekretariet kwenye kamati kuu ili kumpata Mkurugenzi wa vijana, agenda iliahirishwa kwa hofu ya Kafulila kuibuka mshindi. Ni kwa utaratibu huu ajenda ya pendekezo la jina la Mkurugenzi wa vijana iliahirishwa mara tatu, mapaka tukaingia kwenye uchaguzi mkuu wa kwanza wa Baraza la vijana. Ambao nilishinda, lakini kwasababu zilezile za chuki, matokeo hayakutangazwa.
Naomba kutamka rasmi kwa nia njema kabisa , na kwa lengo lile lile nililosema hapo juu, kuanzia sasa mimi David Kafulila napenda kuutaarifu umma kuwa sio mwanachama wa CHADEMA Na bado ninatafakari kwa mazingira yangu njia mbadala ya kufikia lengo lile lile la kujenga upinzani imara nchini. Najua ni uamuzi mgumu. Najua utapokewa kwa kila sura hapa nchini, Lakini sina mbadala wa uamuzi huu. Ninawaheshimu sana wanachadema, ninawaheshimu sana viongozi wa CHADEMA.
Mwisho, ninaipenda nchi yangu, ninawapenda watanzania. Ninafahamu kwamba Taifa linapita katika kipindi kigumu sana chenye misukosuko ambayo msingi wake ni siasa duni ambazo msingi wake ni upinzani dhaifu kwa upande mmoja na Chama tawala kilicho choka kwa upande wa pili
Ninaahidi sintowaangusha katika ujenzi wa upinzani imara na hatimaye serikali madhubuti. Na ninawaonya CCM wakome kutumia migogoro katika vyama vya upinzani kujihalalishia utawala, na badala yake wanapaswa kujihalalishia utawala kwa kujenga ustawi wa watanzani. Ninaondoka CHADEMA kwa uchungu mkubwa kwasababu ya lengo thabiti kwamba lazima niitumikie nchi yangu katika harakati za siasa, na. Nitaikumbuka sana CHADEMA kwakuwa nilimwaga damu katika ujenzi wa chama hiki, ninalazimika kukaa pembeni.
Nawatakia kila la heri
. Nitaikumbuka sana chadema kwakuwa nilimwaga damu katika ujenzi wa chama hiki, ninalazimika kukaa pembeni.
yaani pasipo madaraka watu hawawezi kukaa upinzani?
hii kaliHa ha haaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Chaga Development Manifest (CHADEMA) ,mpoooooooooooooooooooooo