David Kafulila ajivua uanachama CHADEMA

David Kafulila ajivua uanachama CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Muhtasari wa mgogoro wote huu, umefunikwa ni vitu vitatu. Navyo ni kama vifuatavyo:

1. Ruzuku

2.Taratibu za fedha ndani ya Chama

3.Ufinyu wa Demokrasia (Mbowe vs Zitto/uchaguzi M/Kiti)

Kifupi yote hayo hapo juu ni mambo ya FWEZA, kazi ipo. Sasa chama kisichokuwa wazi katika mambo ya fedha, tutadiki vipi kukipa nchi. Matatizo haya niliyajadili siku za nyuma, si mara moja bali mara nyingi tu. Lakini kwa bahati mbaya kama alivyoelezqa Kafulilo, kuwa wanaCHADEMA ni wagumu sana kujirekebisha. nA MBISHI HAFAIDI MPAKA SIKU YA idd.

Kafulilo ameendelea kwa kutoa ujumbe muhimu sana kama ninavyounukuu hapa chini:

"Taifa linapita katika kipindi kigumu sana chenye misukosuko ambayo msingi wake ni siasa duni ambazo msingi wake ni upinzani dhaifu kwa upande mmoja na Chama tawala kilicho choka kwa upande wa pili"

Kweli tutafika? Hivi ni watanzania ndio wajinga au Viongozi wa upinzani ndio waroho na majuha?
 
Haya ni sehemu ya aliyoyasema kijana kafulila kwenye press conf.

TAMKO LA DAVID KAFULILA KUHUSU UAMUZI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) ULIOZUA UTATA NCHINI.

Nitaikumbuka sana CHADEMA kwakuwa nilimwaga damu katika ujenzi wa chama hiki, ninalazimika kukaa pembeni.

Nawatakia kila la heri

- Well wale spinners wa huko upande wa pili, tafadhalini tusaidieni na hili la kumwaga damu kuimarisha chama, exactly ni nini unajua kwenye siasa ukweli usipowekwa mapema kuna hatari ya kubadilishwa kuwa uongo, kumbe ni uongo na sio ukweli!

Respect.

FMEs!
 
Chama cha Demokrasia na maendeleo kinaelekea kuzimu kwa hatua zote ambazo kimekua kikipitia hadi sasa! walianza kwa kuhitilafiana na Dr warid, Marehemu chacha wangwe, kina Mzirai na hatimaye Kafulila.
Uwezekano wa Chadema kuelekea kuzimu ni mkubwa sana kwa kuwa historia ya mparaganyiko wa vyama vya siasa ni mparaganyiko pale swala la fedha linapoguswa! Wangwe alilalamikia matumizi ya ruzuku, kina Mzirai matumizi ya ruzuku, Kafulila matumizi ya Ruzuku aagh! kwa sisi wa mikoani hasa Tabora mjini ni aibu kweli kweli hasa unapozungumzia ofisi za Chadema, wanatumia kipande cha Gogo la mnazi lililolazwa chini huku Mwenyekiti wa Chadema na katibu wake wa Mkoa wakifanya biashara ya kukodisha baiskeli 2 (mbili) kama mradi wao waotegemea wakati vigogo wao wakiishi kwa neema huku wakiitaka ubunge na Urais Aibu!

mtizamo hasi...kama mwenyekiti wa kigoma anakodisha baiskeli ni sawa ..kwani anajitafutia kipato halali ...kwani wenzake wa ccm hata kama ruzuku haifiki mikoani kwa uuwiano lakini wanayo dola ...na wanakodisha viwanja vya wazi na vile vya michezo kama ALI HASSAN MWINYI.....unategemea na wao watakuwa WAKULIMA na WAFANYAKAZI hata kama CCM ni Chama cha WAKULIMA na WAFANYAKAZI??
 
Haya ni sehemu ya aliyoyasema kijana kafulila kwenye press conf.

Nitaikumbuka sana CHADEMA kwakuwa nilimwaga damu katika ujenzi wa chama hiki, ninalazimika kukaa pembeni.

ana brein hemorrhage baada ya kuporomoka toka magorofani
 
nimesoma vizuri andiko lake David kafulila kwa vyombo vya habari iliyowekwa humu kwenye Jf, nimestushwa na kauli yake ya kusema kuwa amemwaga damu chadema, hivi kivipi jamani.mi ninavyojua nchi yetu haijamwaga damu yoyote eti kwaajili ya ukombozi, atuambie vizuri anahusika katika mauaji na anataka kuuambia nini uma kuwa chadema kimeshamwaga damu kwenye movement zake? au ni huku kutapatapa.......

kama ni kutapatap kweli umeanguka kabisa my broo.

Labda aliwahi kuvunjika mguu damu ikachuruzika churuuuu alipokuwa kwenye heka heka za kujenga CHADEMA.
 
Naona Kafulila ana ile falsafa ya Bush... "either you are with us or you are our enemy"!!!

Kafulila Amefulia kisiasa
 
1) Alianguka kutoka ghorafani..kwahiyo inawezekana ana matatizo ya akili..swali mbona sasa hivi? mbona chadema ilimfanya kiongozi muda wote?
2) Hajamaliza shule ame-disco..gosh? mbona sasa hivi? mbona alikuwa kiongozi wenu muda wote?
Akiondoka ndio mnapekua historia yake na siyo kabla ya kumpa nafasi hiyo kwa muda wote huo ni unafiki na sizitaki mbichi hizi lol.
 
Mbona Mbowe pia amedisco? AU?
 
nimesoma vizuri andiko lake David kafulila kwa vyombo vya habari iliyowekwa humu kwenye Jf, nimestushwa na kauli yake ya kusema kuwa amemwaga damu chadema, hivi kivipi jamani.mi ninavyojua nchi yetu haijamwaga damu yoyote eti kwaajili ya ukombozi, atuambie vizuri anahusika katika mauaji na anataka kuuambia nini uma kuwa chadema kimeshamwaga damu kwenye movement zake? au ni huku kutapatapa.......

kama ni kutapatap kweli umeanguka kabisa my broo.

Kajamaa ni kajinga yaani kalipo poromoka na lift mbovu pale ktk jengo la kitegauchumi kakazimia ndo kanasema kalimwaga damu?? Haoni wanaomwaga damu somalia??

Kafululu .....you are just another stupid fellow.
 
Demokrasia ni pale unapopewa nafasi ya kuchagua na/au kuchaguliwa. Hili linapokosekana una haki ya ku-commit suicide.

Rudi kwenye mada kubwajinga. Tunaongelea kuteuliwa na/au kutenguliwa sio kuchagua na/au kuchaguliwa.

.
 
Chama cha Demokrasia na maendeleo kinaelekea kuzimu kwa hatua zote ambazo kimekua kikipitia hadi sasa! walianza kwa kuhitilafiana na Dr warid, Marehemu chacha wangwe, kina Mzirai na hatimaye Kafulila.
Uwezekano wa Chadema kuelekea kuzimu ni mkubwa sana kwa kuwa historia ya mparaganyiko wa vyama vya siasa ni mparaganyiko pale swala la fedha linapoguswa! Wangwe alilalamikia matumizi ya ruzuku, kina Mzirai matumizi ya ruzuku, Kafulila matumizi ya Ruzuku aagh! kwa sisi wa mikoani hasa Tabora mjini ni aibu kweli kweli hasa unapozungumzia ofisi za Chadema, wanatumia kipande cha Gogo la mnazi lililolazwa chini huku Mwenyekiti wa Chadema na katibu wake wa Mkoa wakifanya biashara ya kukodisha baiskeli 2 (mbili) kama mradi wao waotegemea wakati vigogo wao wakiishi kwa neema huku wakiitaka ubunge na Urais Aibu!

Umesahau kuongezea ufujaji wa pesa kwa kukodishia helkopta kwa ajili ya Mbowe. Ukiuliza tu unaonyeshwa mlango maana chama sasa ni kampuni binafsi.
 
Tatizo la migogoro lipo kwenye vyama vyote vya siasa Tanzania, isipokuwa katika CCM kuna ka-uoga ka nguvu ya dola kwani mwenyekiti ambaye ndiye raisi ana weza kukudeal accordingly, lakina kwa huku kwenye upinzani ni balaa, we angalia CUF tangu multi-party inaanza mpaka wa leo wagombea na viongozi wa juu ni walewale (LIpumba na Sefu), Prof Safari hata hamu ya upinzani hana, UDP huwezi kumtoa bwana MApesa, TLP kama kawaida Mzee wa KIRARACHA, hAPA tatizao kubwa la Bwana Kafulila ni ule moyo wa kuvumilia hana,
ushauri wa bure kwa yoyote anaependa siasa ni lazima uwe kigeugeu, muongo, mjinga, mpambe kwa kufuata upepo wenye nguvu, Mwizi, laghai na sifa zote unazozijua, kwani kilichomtoa Lwakatare CUF na hiki cha KAfulila kina tofauti gani?
 
Heshima Kwako Kubwajinga

Chukua tano ndugu yangu kubwajinga yaani umemaliza kabisa sema jamaa wa CHADEMA wanapenda ligi za kitoto watakuja hapa na utetezi wa kipuuzi lakini wenye akili tayari tumeshawagundua.

Na wewe hii ligi unayoiendeleza ni ya kikubwa au kizee?

You just proved Ngongo's point. People like you, Mwafrika, are the ones messing up CHADEMA by doing and supporting nonsence.
 
mtizamo hasi...kama mwenyekiti wa kigoma anakodisha baiskeli ni sawa ..kwani anajitafutia kipato halali ...kwani wenzake wa ccm hata kama ruzuku haifiki mikoani kwa uuwiano lakini wanayo dola ...na wanakodisha viwanja vya wazi na vile vya michezo kama ALI HASSAN MWINYI.....unategemea na wao watakuwa WAKULIMA na WAFANYAKAZI hata kama CCM ni Chama cha WAKULIMA na WAFANYAKAZI??

Ndio matatizo yenu haya.... mnaambiwa kweli ili mjirekebishe mnakuwa mbogo!

Ofisi ya Mkoa haina jengo ipo kwenye gogo la mnazi ilhali wakubwa makao makuu wanatumbua pesa za ruzuku na kuzunguka na helikopta!

Watu wakihoji wanaambiwa hawana nidhamu wanafukuzwa chama. Wakati huyu msimamizi wa nidhamu Dr Slaa kamuita Kafulila kuwa ni "sisimizi" tu kwenye chama! hiyo ndio aina ya nidhamu anayofundisha padri Slaa?

Kama hamta jirekebisha chama linaelekea kubaya mwisho litatota na mtagawana mbao! Kalagabaho.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom