Kaka nitake radhi kaka,
Mimi sio mshabiki wa Zitto na wala sina kundi huko na CHADEMA. Mimi ni rafiki wa Zitto. Urafiki wetu sio wa nafasi za kisiasa ama kijamii, ila ni wa kiitikadi (wote tunaamini katika ujamaa), kimitizamo (wote tunaamini katika constructive criticism/engagement), ki-ajenda (wote tunaamini katika demokrasia makini na sio bora demokrasia), Vision (wote ni waumini wakuu wa muungano wa Afrika – Panafricanism), Misingi (Siasa ni utumishi na sio uheshimiwa) na mengineyo. Sasa huko kwenye upambe kwa kweli itakuwa ni kunitusi. Una haki ya kuona hivyo lakini mimi binafsi sijioni hivyo kamwe na naamini hata Zitto pia.
Pia ni muhimu ukanikumbusha wapi ambapo mimi niliwahi kumchafulia ama kumtuhumu MBOWE ama Dr Slaa zaidi ya kusema kuwa kuna watu ambao wako karibu yake ni wafitini wakubwa kitu ambacho hata wewe unakubaliana nacho katika moja ya michango yako hapa.
Na zaidi nilichowahi kufanya hapa ni kujaribu kuondoa sumu iliyokuwa /inayoendelea kupandwa dhidi ya Zitto na watu humu na kwengineko ambao baadhi yao wanatoka CHADEMA na na wengine kutoka katika makundi mengine ya kisiasa. Sasa mimi kuja kuelezea jinsi nimjuavyo Zitto ikiwa ni tofauti na majungu na fitina hizo ndiyo nimekuwa mbaya ama muendeleza makundi. Ulitaka ninyamaze kimya ili wanajamiiforums na watanzania wengine wajenge mtazamoa/maoni hasi dhidi ya Zitto kwa mujibu wa majungu na fitina za maadui zake na sio utetezi wa marafiki zake?
Na zaidi ndugu yangu huku kunifananisha na wapambe wa hawa WAJASIRIAMALI WA SIASA uliowataja hapo juu ndio tusi kubwa zaidi…
omarilyas
Mkuu wangu kwanza nakuomba samahani kama ulivyotaka nitangulize...lakini pia naomba maelezo yangu kuyaweka wazi na uyapokee..
Kwanza ni kutokana na majibizano yenu ndio yaliyonisukuma mimi kusema nilichoandika.. Na nitarudia kusema hakuna kundi la Zitto na Mbowe isipokuwa kuna kundi la Zitto na wale wanaompinga wakitumia jina la Mbowe kuweka uzito wa utetezi wao kwani binafsi naamini kabisa kwamba hakuna uhasama wowote baina ya Mbowe, Dr.Slaa na Zitto isipokuwa ni watu wanaotafuta kukibomoa chama aidha makusudi au kwa kutofahamu wanfanya hivyo kutokana na chuki zao binafsi kwa baadhi ya viongozi hawa.
Na nimeongezea tu kusema inafanana na malumbano ya Mwakyembe na Mwakalinga kwa sababu hoja kubwa ya wananchi ni KYELA na sii Mwakyembe wala Mwakalinga. Na kile kinachosukuma great mind kuzungumzia zaidi Idea ni pale unapoweka issue at hand kuwa aidha ni CHAMA, KYELA au WANANCHI wake badala ya issue nzima kuwa Mwakyembe au Mwakalinga.. Unapoanza na Mtu kuwa the main issue ni vigumu sana kujenga mawazo mbadala nje ya mtu isipokuwa mawazo ya kumjenga au kumbomoa mtu huyo.
Sasa basi maadam mimi ni mtu mzima na mwenye kuelewa hadithi za kutunga nafahamu fika kwamba Zitto na Mbowe sii issue hata kidogo, matatizo ya Chadema kama YAPO are deeper than Zitto au Mbowe na Dr.Slaa kwani navyoelewa mimi hawa watu sii maadui wala hawana uhasama isipokuwa washabiki wake ndio wanaozusha mambo haya kuwa makubwa kiasi ambacho wanataka wananchi waanze kupima umuhimu wa Zitto vs Mbowe au Dr. Slaa ndani ya chama.
Kama sikosei kuna mwana JF Invincible, mara kibao aliwahi sema Chadema ni kubwa kuliko Mbowe, Dr. Slaa na Zitto..sijui kama nyote mlielewa uzito wa maneno yake..
Kwa hiyo kaka, maneno yangu ya kusema ushabiki umetokana na ukweli kwamba umechukua muda mrefu kumlinda Zitto na sii ideology unayo amini. Ningefurahi sana kama ktk utetezi wako ungetumia zaidi imani yako ili kuunganisha na matukio yanahusiana na Zitto. Lakini utetezi wako ulivutwa na mvuto wa kutetea soul partner wako kiasi kwamba ukaingia ktk mkumbo wa kusema Zitto is not a problem (an Issue) but someone else is!.
Ndipo napokataa na kusema sasa huu ni ushabiki kwani matatizo ya Chadema yanasukwa tu.. hakuna mtu anayesababisha matatizo ya Chadema isipokuwa kuna watu wanaotafuta kuzua matatizo hayo kwani nimemsoma vizuri Bi. Asha na yaonyesha wazi kuna uelewano mkubwa baina yao ktk sekta ambazo wengi wetu tunaziwekea mashaka. Zitto, Dr. Slaa, Mbowe wote wanaendelea kusema hakuna matatizo Chadema iweje hapa JF ndipo tunaoina matatizo baina ya viongozi hawa watatu!..Je kuna ambalo hatulifahamu na kama lipo who is telling the truth!
Mkuu wangu kweli unaweza kuwa rafiki wa Zitto kutokana na imani yako ktk itikadi na nadhani hili hata mimi nipo upande wake.. Mimi pia nimekuwa interested sana na chama Chadema kwa sababu hiyo pekee na sii mtu yeyote na nitayatetea yale tu yaliyomo ktk msahafu wa imani yangu..kwa hiyo itikadi hii inatuweka sote pamoja lakini kama Zitto atakosea nitakuwa rafiki wa kwanza kumkosoa, kumkanya, kumuasa na kumbumbusha malengo ya imani hii inavyopingana na matendo yake.
Na viongozi hawa wa Chadema kwa kuacha watu wanakivuruga chama, watu wanaongea na waandishi wa habari wakati wa kikao cha chama Dodoma kuelezea kufukuzwa kwa mtu kiasi kwamba gazeti linamtafuta mhusika na kumuuliza kama anayo habari kuhusiana na mkutano huo ndio UNAFIKI mkubwa utakao kibomoa chama.
Rev. Kishoka ameshuka na kitu na hakika TTTP ambayo ni pigo kubwa sana kwa Chadema strategically, haya ndio mambo ya kutazama kwa nini mtu kama Rev kafikia kufungua chama with new edition inachofundisha Gospel yetu..Tunafanya makosa wapi na tunaweza vipi kuweka ushawishi kwa vijana ambao wamefikia kuona kwamba hata Chadema hawana mpango wa kuchukua madaraka..Kwa mtazamo wangu kufikia mwaka 2015, Chadema haitakuwa Chadema ikiwa mambo kama haya ya Zitto vs Mbowe yataendelea kukuzwa wakasahau malengo ya Upinzani ni kuchukua madaraka na sii kuwa ranked underdog.