UMEKIPIMA KWA KIGEZO KIPI?
Asante mheshimiwa, Inawezekana mumelewa sifa sasa, kwa hiyo hamfikirii njia mbadala za kusolve matatizo ya CHAMA kwa amani bila kutoa ufa wa kukikosesha nafasi yakuvuna wanachama wengine na pia kupata wabunge wengi bungeni. Umesoma post zangu tatu za nyuma kwenye hii thread? Mumebeba ajenda za watanzania, Mumebeba matumaini yetu, tunawajadili kwa kuwa tunaawamini kuwa ninyi ndio ukombozi wa kweli kujadili kwetu huku ni kutokana na kuwa upepo unaovuma unaonyesha mwelekeo usio kuwa sio. Tunajaribu kuwakumbusha msilewe sifa za kuwa na washabiki wengi, kuweni na mkakati madhubuti wa kuweza kuabadirisha hali ya nchi, nayo ni kuliteka bunge, ndoto inayoweza kutimia kirahisi kabisa (bila hata bajeti ya helkopita,)maana kwa kufanya hivyo mtaibeba ajenda ya watanzania sawa sawa. Umenipata?