David Kafulila ajivua uanachama CHADEMA

David Kafulila ajivua uanachama CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Sisi ni wamoja, zaidi ya JF hatuna pakusemea. Hongera JF. Heri akina Kafulila wanauwezo wa kuwakusanya waandishi wa habari kibao na kusema watakavyo, nasi tukaamini.

Idumu JF!!!!
Umenifurahisha sana kwa hii conclusion
 
well said, He was supposed to step down even before he was fired

So, next is Zitto? how come is one of the top leaders?
Nashangaa, hivi ni wangapi wabovu huko?

Nini hasa kosa la Zitto chamani, mbona anatajwatajwa sana. Au kutaka kugombea u-wenyekti CHADEMA ndio kosa lake.

Siku zote nilikuwa nadhani kuwa Zitto Kabwe ni Mfano wa kuigwa kama kiongozi shupavu asiyetetemeshwa hata na vingunge wa chama tawala. Na si hivyo tu, bali nilidhania kuwa, yeye ni mtetezi wa wanyonge bila ya kujali chama.

Hebu wana CHADEMA tupeni siri za huyu kijana, Zitto Kabwe. Maana hapa kwetu Magomeni, huyu kijana ndio tegemeo letu. Na kila kijana anayetaka kuingia katika siasa, matarajio yake ni kuwa kama Zitto Kabwe.
 
Dhahabu safi hupita katika moto mkali. Lets see if Chadema will survive the test of time!!
 
No hapa anaongelewa - Kolimba, Kabeho, Kibona, Mama Mbatia, Kombe, mkemia mkuu wa serikali, Stan Katabalo, na wengine wengi waliopitia chinja chinja ya ccm.

Hapo hujaweka wale waandamanaji wa pemba au mauaji ya Jan 2001.

No,

Wale waandamanaji wa pemba (kama wale wa mwembechai) walivunja sheria za nchi na hivyo jeshi lilifanya kazi yake ya kutuliza fujo na kuleta amani.
 
1) Alianguka kutoka ghorafani..kwahiyo inawezekana ana matatizo ya akili..swali mbona sasa hivi? mbona chadema ilimfanya kiongozi muda wote?
2) Hajamaliza shule ame-disco..gosh? mbona sasa hivi? mbona alikuwa kiongozi wenu muda wote?
Akiondoka ndio mnapekua historia yake na siyo kabla ya kumpa nafasi hiyo kwa muda wote huo ni unafiki na sizitaki mbichi hizi lol.

Heshima kwako.

Si wote walioshtukia propaganda uchwara.Wengi wameingia kwenye mtego wa kumshambulia kafulila kwasababu kajaribu kutueleza udhaifu wa CHADEMA.
 
kamwaga damu????? mi sijamuelewa..huyu ni wa kukamatwa na polisi ahojiwe alimwaga damu ya nani?
 
Kinachofanyika sasa na vyama vya upinzani ni sensitization na advocacy u kutokana na size ya vyama hivyo!!

Upinzani wa kweli uko ndani ya CCM na kuna siku utajitokeza

Haya ndiyo aliyoyasema Baba wa Taifa. Ila nami nakubaliana na wewe we really needs advocacy na sensetization mpaka tufikie mahalimshindi anachaguliwa kwa merits na sio kwa ki-imla kamailivyo sasa.

Sensetization ikifanyika, the wind of change will sweep accross Tanzania, CCM itangoka bila hata kumeguka.

Kwa upande wa haka kajana kalikofulia, kametoa tafsiri mbovu kuhusu kumwaga damu, watu wakifikiri damu iliyomwagika kuifia Chadema, kinaja anamaanisha ile michubuko ya mikiki mikiki ya kampeni za Tarime, Busanda na Biharamulo, kuna wanaChadema wengi yakuwakuta yaliwakuta, na vijidamu vikatiririka kwa vipigo, vurugu nk lakini hakuna damu iliyomwagika, ukiondoa hizo za kwenye ajali.
 
Huyu kijana amekurupuka na inaonyesha ana uroho sana na madaraka kwani akiwa mwanachama wa kawaida atapungukiwa na nini? Kwa hiyo huko aliko enda wasipo mmpa madaraka maanake nako atakimbia na kuhamia TLP sasa!
 
Big Brother is watching.
Hivi naomba kujuzwa.
Kiongozi wa kuteuliwa ana haki ya kugomea au kuhoji kutenguliwa uteuzi wake?????

Pia Hapa ndipo naanza kumwelewa vibaya Zitto kwamba anakivuruga chama chake akidhani anafanya anayoyafanya kwa nia njema.
 
Dhahabu safi hupita katika moto mkali. Lets see if Chadema will survive the test of time!!
Hii si tu ni test of time, bali ni mapinduzi kamili ndani ya chama yenye mwelekeo wa kufungua milango ya uwazi na uadilifu.

Ukilitimba uliopo katika chama hicho hauwezi kuendelea bila mwisho. CHADEMA kama chama chawajibika kukuza na kuendeleza Demokrasia ndani ya chama kabla ya kuinadi kwa watanzania. Na ili hilo lifanikiwe chama hakina budi kwanza kuondoa kile kiitwacho 'The top 15 faces'. Kama hili haliwezekani basi wasahau Demokrasia ndani ya Chama, na kwa maana hiyo wataokihama chama watakuwa wengi zaidi ya Kafulila na mtarajiwa mwingine Zitto.

Kuwa Zitto na Kafulila hawaridhishwi na jinsi chama kinavyoongozwa si siri. Na hapa ndio ipo test of time, kwani hatujui ni mbinu gani chama kitafuata kufuta tofauti hizo. Hapa kuna njia 2 za kufuata.
1. Kufukuza wote wanaotofautiana na 'The top 15 faces'.
2. Chama (uongozi) kujirekebisha na kurudisha imani kwa wanachama na baadhi ya viongozi.

Hili la pili ndilo suluhisho la kudumu, lakini linahitaji kubadili kabisa mtazamo wa chama toka kiliko mpaka kukiweka katika sura ya kitanzania. Je kazi hii ni rahisi? Haya ni maswali yanayotakiwa kujibiwa na Freeman Mbowe, Dr Slaa, Mtei n.k

CHADEMA bado ina nafasi katika umma wa kitanzania, na bado ni moja kati ya vyama pinzani vinavyotegemewa sana katika juhudi za kuin'goa CCM. Lakini bado safari ni ndefu, tena ndefu sana. Na katika hili waige mfano wa CUF, pale ambapo nafasi ya Mwenyekiti wa chama iligombaniwa na na kila aliyehitaji kuchukua fomu na mwenye sifa hizo. Hakukuwa na vikao vya pembeni vya mabaraza ya wazee vilivyomshawishi Prof Safari ajitoe, eti kwa kisingizio kuwa cha bado ni kichanga.
 
Kafulila nilimsikiliza kwenye taarifa ya habari TCB1. Huyu kijana ni mpuuzi sana. Hata maelezo yake ni ya kitoto. Kifupi anataka sifa asizostahili, kifupi hajai hata kwenye kiganja.
 
Humu ndani watu mna matatizo sana...
Mimi sio chadema but nafikiri chadema wana tatizo kubwa sana....
Bora zito ahame chadema.....
Sio kila anaepinga kitu ndani ya chadema ni msaliti....
Mbowe ni vichekesho vitupu....
 
Tetesi za kufukuzwa uanachama, bwana Kafulila zilijitokeza toka kwa wana Paparazi siku nyingi tu kabla hata ya yeye mwenyewe kukutana na waandishi wa habari.

Habari zilivuma huku wasomaji wakidai vyanzo vya habari hizo bila mafanikio. Leo hii kuna chanzo maalum ikwa ni yeye mwenyewe akithibitisha kufukuzwa uanachama. Kinachonisikitisha mimi ni pale anapoonyesha kuukubali uamuzi huo kwa shingo upande, pale asemapo: "Ninaondoka CHADEMA kwa uchungu mkubwa kwasababu ya lengo thabiti kwamba lazima niitumikie nchi yangu katika harakati za siasa, na. Nitaikumbuka sana CHADEMA kwakuwa nilimwaga damu katika ujenzi wa chama hiki, ninalazimika kukaa pembeni."

Huwezi kuitumikia nchi yako ipasavyo ukiwa ndani ya chama ambacho kinamapungufu mengi kama aliyoyaeleza Kafulila katika pres conf. Aidha anaendelea kusema kuwa " ".......ninawaheshimu sana viongozi wa CHADEMA." Huwezi hata kidogo ukawaheshimu viongozi wasiojua kazi yao au wanaotaka kuendeleza ufisadi ndani ya CHAMA. Kwa maneno mengine wanakiandaa chama kushika nchi ili kuendeleza ufisadi. Ni kosa kabisa kuwaheshimu viongozi kama hao. Kwanza kazi, ndio baadae heshima. Ukichemsha katika kazi hakuna heshima. Kwa upande mwingine nahisi kama vile Kafulila anajilaumu, kuwa kwanini alianzisha kuhoji utawala katika chama, kwani asingefanya hivyo bado angekuwa anakula kuku.

Katika pres conf yake, kulijaa tuhuma zifuatazo zikiwaendea viongozi wajuu wa CHADEMA wakiwemo, M/Kiti, Freema Mbowe, Dr Slaa n.k

1. Matumizi mabaya ya Ruzuku

2.Taratibu za fedha ndani ya Chama

3.Ufinyu wa Demokrasia (Mbowe vs Zitto/uchaguzi M/Kiti. Uchaguzi M/kiti vijana, yeye mwenyewe akiwa mgombea)

Kifupi yote hayo hapo juu ni mambo ya FWEZA, kazi ipo. Sasa chama kisichokuwa wazi katika mambo ya fedha, tutadiriki vipi kukipa nchi. Matatizo haya niliyajadili siku za nyuma, si mara moja bali mara nyingi tu. Lakini kwa bahati mbaya kama alivyoeleza Kafulila, kuwa wana CHADEMA ni wagumu sana kujirekebisha. NA MBISHI HAFAIDI MPAKA SIKU YA IDD.

Kafulilo ameendelea kwa kutoa ujumbe muhimu sana kama ninavyounukuu hapa chini:

"Taifa linapita katika kipindi kigumu sana chenye misukosuko ambayo msingi wake ni siasa duni ambazo msingi wake ni upinzani dhaifu kwa upande mmoja na Chama tawala kilicho choka kwa upande wa pili"

Yote hayo ni tisa, lakini kumi kama anajihisi kuwa kafulia bila kukusudia basi aombe msamaha kwa CHADEMA na arudi madarakani.

Na kweli amefulia.Watu waliokutana naye hivi karibuni wanasema ameshaanza kupauka kwani hana amani kuiacha CHADEMA lakini ujinga wake ndo umemfanya amamue uamzi wa kujivua uanachama.
 
Kafulila nilimsikiliza kwenye taarifa ya habari TCB1. Huyu kijana ni mpuuzi sana. Hata maelezo yake ni ya kitoto. Kifupi anataka sifa asizostahili, kifupi hajai hata kwenye kiganja.
Haya tuseme huyu Kafulila ni mjinga, na Zitto je? Maana kwa muujibu wa wapambe, naye anatia maji kichwa chake baada ya mwenzie kunyolewa.
 
Kafulila nilimsikiliza kwenye taarifa ya habari TCB1. Huyu kijana ni mpuuzi sana. Hata maelezo yake ni ya kitoto. Kifupi anataka sifa asizostahili, kifupi hajai hata kwenye kiganja.

Vijana wengi Chadema hawajakomaa kisiasa kuna tofauti kati ya siasa za DARUSO na siasa za chama kinachoongoza nchi. Chadema hili waweze kosonga mbele hili la kuwa na vijana inabidi walione mapema na kuwapa shule ya kutosha kuhusu chama.

Vijana hawa wanamengi ya kuzungumza, ambition mbali mbali lakini wanakosa subira. Wanahitaji elimu haraka ya kutosha na kutofautisha siasa za vyuo na chi kwa ujumla.

Kafulila angelikuwa kijana mzuri Chadema hila amekosa subira, huko aendako sidhani kama atafanikiwa kuliko alivyokuwa Chadema ningemshauri either arudi Chadema tu. Vinginevyo afanye kama vijana walioko Chama Cha Mapinduzi (ang'ate na kupuliza), akajiunge nao tu moja kwa moja.
 
Niwaridishe nyuma kidogo, hivi ni kukosa democrasia au ukiukwaji wa haki za binadamu kama msemavyo pale inpowekwa hata kwenye katiba kuwa umri wa kuwa kiongozi wa taifa au chama ni lazima uwe say 40yrs. Hapo tunde ki sayansi zaidi.
Hawa vijana wa CHADEMA wasubiri wakuzwe sio kuwahi namna hii. Intellegence ya madaraka mtu upikwa kwanza sio kusimama kwenye jukwaa na kusema nami naweza.
Umakini ndio unaolinda chama chochote. Ukilopoka kwisha. Mambo ya siasa sio kuwa kila kitu adharani, hebo!!!
Hebu nipe CV ya huyo Kafulia, anayechafua hali ya hewa, sio ajabu ajira yake ni kwenye chama na kaletwa na mtu.
Pole, uliyefulia. Vijana life is a progressive event, ZITTO awe Waziri mkuu au raisi sasa hivi akimaliza miaka yake 10 ataenda wapi kama sio kuja na mawazo ya kubadilisha katiba kwa kisingizio cha kuwa kipenzi cha watu. Vijana komaeni kwanza, maisha yapo. Mtaka yote kwa pupa .....
 
Zitto ni ngangari hafuati mkumbo. ataendelea kuwapo CHADEMA na utashangaa!!
Vizuri, na hilo ndio tunaloombea, maana kuhama chama si ufumbuzi wa matatizo.

Wangapi wamehama vyama kwa kizingizio eti wanatafuta chama makini, pale ambapo wao watawatumikia wananchi zaidi kwa uwezo wao wote. Hayo hayajatoke, kwani Tambwe Hiza na wenye mawazo kama yake, hawawezi kutueleza kuwa leo baada ya miaka eti wanatumikia wananchi zaidi kuliko alivyokuwa CUF.

Tunachoona ni kinyume, kuwa wote hawa wahama vyama, imani ya wananchi kwao inapungua kwa kiasi kikubwa sana. Leo hii Tambe ndani ya CCM hana mchango hata kidogo. Na hali kama hiyo tumeiona kwa Mrema.

Hivyo maombi yamgu ni kuona wanasiasa wanakuwa na malengo ya muda mrefu yatayowawezesha kujua toka awali kuwa katiba na muelekeo wa chama gani wapo tayari kuutumikia maishani mwao mwote. Malengo ya muda mfupi, kama kupata cheo chamani kamwe hayatamnufaisha yeyote, si watanzania, chama wala muhusika.
 
Sifikiri mtu kuhama chama ni tatizo mbali ni pengine mbinu mahili kabisa zakuweza kuwatumikia wananchi vizuri.

Mfano . Hakuna mwasiasa Afrika mashariki ambaye amebadirisha vyama vingi kama Raila Kalamanjogi Odinga.

Kama mtu ana nia ya kweli na sababu za msingi ,kuhama chama sio tatizo na wananchi wataendelea kuunga mkono tu hata ukihama mara ngapi.

Tatizo naloliona hapa watu tunajaribu ku reference kusiko. Kama mtu alihama chama kwa nia yake mbaya hakumzuii mtu mwingine kuhama chama kwa nia yake nzuri.

Watu mnaowaliference ni watu ambao wamehama kwa nia zao binafsi wenda za kinafiki ama wao wajuavyo.Na kinachowamaliza ni kwa sababu ya unafiki wao na si kuhama chama , kwa sababu kamwe Shetani huwa havumilii kukufichia siri yeye atajitahidi kukufichia siri kwa mda usio mwafaka na kuitoboa siri kwa mda muafaka.

Mimi ninachojaribu kusema hapa Kama kafulila kahama kwa unafiki basi shetani atamfichia siri hiyo kwa mda tu kwa wakati usio mwafaka, na ikifika wakati mwafaka shetani ataitoa hiyo siri na kujamaliza mwenyewe. Lakini kama hakuhama kwa kinafiki shetani hana siri ya kutoboa na Mungu hata mhukumu kwa lolote.

Kama CHADEMA ndo wanafiki basi watambue unafiki wao unafichwa kwa mda tu usio mwafaka na mda muafaka utapotimua shetani atatoboa siri na ktk mda mwafaka na sahihi na hatimaye kitawamaliza kabisa.
 
Siasa za Tanzania ni tofauti sana na Kenya, sitaingia kiundani.

Lakini Hebu turudi nyumbani, Tanzania. Kuna wanasiasa wengi toka tuanze siasa za vyama vingi wamehama vyama, tena wengine wamehama zaidi ya vyama vitatu. Tupe mfano mmoja tu, kati ya hao watanzania waliohama vyama na wakalitumikia Taifa vyema zaidi ya vyama vyao vya awali?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom