David Kafulila ajivua uanachama CHADEMA

David Kafulila ajivua uanachama CHADEMA

Status
Not open for further replies.
nimesikiliza mahojiano ya kafulila mlimani tv...kwa kifupi ni kijana ambaye hata kwa mpangilio wa hoja zake ..anaaonyesha bado anahitaji malezi ya kisiasa....nadhani haukuwa wakati muafaka kwake kuhama ....nitamshauri tu asifanye kosa kwenda CCM ..kwani hatapata cheo anachotarajia.....ni vema akaenda chama kidogo kama NCCR ambacho kule kigoma kinajulikana ..ili aendelee kujijenga kisiasa..au la afikirie upya msimamo wake na kubakia CHADEMA.

Nadhani tubadilike kifikra ...kuhama vyama kwa tofauti ya kimtazamo kumepitwa na wakati ...internal power strugle kwenye association yeyote ni jambo la kawaida......na unatakiwa upiganie mabadiliko ndani ....kabla ya kutaka umaarufu nje..ya kundi au chama chako...that is normal political evolution....

ndio maana unaona hata rebels wa CCM wanapigana wakiwa ndani....ninafurahisha hata muheshimiwa zitto ..anakubaliana na dhana ya kupigania mabadiliko ndani ....kwa ndani...hiyo ndiyo siasa...historia haiwapi nafasi nzuri sana rebels wanao ditch boat...kwani angalia looosers kama kina kabourou,hiza tambwe na wengine...zaidi ya kupata pesa ya kununua mkate kurudi nao nyumbani jioni...they lack a really constituets as of now......ndani hawaaminiki ..na nje hawaaminiki....

na si vema mwanasiasa kujijengea legacy ya kutoaminika.....bora uwe na msimamo hadi mwisho....

Akipigana ndani kwa ndani..mchochezi...anatumiwa...amepewa pesa kuvuruga chama...

Akitoka chama...Hajafikia muda wa kuhama chama...anatakiwa alelewe kisiasa....!!!
 
Lwakatare=Kufulila=kabouro=tambwe=masumbuko==list go on ni tamaa ya vyeo, madaraka ulafi wa fedha nk..pamoja na kwamba akiondoka tuhuma za vyama vyao baada ya mtu kuondoka huwa sikubaliani nayo...kabisaa.
 
Ila pamoja na kuchemka kwa kafulila, pia CHADEMA kuna waka moshi na moshi huu ulianza kufuka toka kwa Wangwe, na kwa bahati mbaya hawakuuzima, sasa moto umeanza kushika nyasi kavu. Kuna kitu hakiko sawa CHADEMA, lazma wakae chini wajiangalie tunaelekea kipindi kigum mwakani na cha muhim Tanzania.
 
Hii stage ni muhimu sana kwa ukuaji wa demokrasia, hasa kwa nchi kama tanzania!!!

CCM wenyewe bado wanakuwa ndio maana hakuishi shughuli kule!!
 
CCM kutoka madarakani kwa sasa ni ngum sana, labda kundi moja lijigawe, ila tatizo likijigawa, lina funds za kutosha kujiendeleza?We angalia CCM inavijitawi almost zaidi ya 80% ya vitongoji na vijiji Tanzania. Ni rahisi kukitoa chama hiki kweli?Nahisi mpaka wajitenge wenyewe na watakaojitenga wawe na funds nyingi za kuji expand.
 
Kinachofanyika sasa na vyama vya upinzani ni sensitization na advocacy u kutokana na size ya vyama hivyo!!

Upinzani wa kweli uko ndani ya CCM na kuna siku utajitokeza
 
Jamani kumwaga damu mbona iko simple, si anamaanisha ame-invest nguvu yake nyingi Chadema,

kama kuna mtu ana tafsiri tofauti aandike
 
kiswahili sana anatakiwa kusema alimwaga Jasho na sii damu..pengine ile siku ya uchaguzi wa vijana ndo alimwaga damu, nasikia zilitokea ngumi sii mchezo.....
 
Tetesi za kufukuzwa uanachama, bwana Kafulila zilijitokeza toka kwa wana Paparazi siku nyingi tu kabla hata ya yeye mwenyewe kukutana na waandishi wa habari.

Habari zilivuma huku wasomaji wakidai vyanzo vya habari hizo bila mafanikio. Leo hii kuna chanzo maalum ikwa ni yeye mwenyewe akithibitisha kufukuzwa uanachama. Kinachonisikitisha mimi ni pale anapoonyesha kuukubali uamuzi huo kwa shingo upande, pale asemapo: "Ninaondoka CHADEMA kwa uchungu mkubwa kwasababu ya lengo thabiti kwamba lazima niitumikie nchi yangu katika harakati za siasa, na. Nitaikumbuka sana CHADEMA kwakuwa nilimwaga damu katika ujenzi wa chama hiki, ninalazimika kukaa pembeni."

Huwezi kuitumikia nchi yako ipasavyo ukiwa ndani ya chama ambacho kinamapungufu mengi kama aliyoyaeleza Kafulila katika pres conf. Aidha anaendelea kusema kuwa "
".......ninawaheshimu sana viongozi wa CHADEMA." Huwezi hata kidogo ukawaheshimu viongozi wasiojua kazi yao au wanaotaka kuendeleza ufisadi ndani ya CHAMA. Kwa maneno mengine wanakiandaa chama kushika nchi ili kuendeleza ufisadi. Ni kosa kabisa kuwaheshimu viongozi kama hao. Kwanza kazi, ndio baadae heshima. Ukichemsha katika kazi hakuna heshima. Kwa upande mwingine nahisi kama vile Kafulila anajilaumu, kuwa kwanini alianzisha kuhoji utawala katika chama, kwani asingefanya hivyo bado angekuwa anakula kuku.

Katika pres conf yake, kulijaa tuhuma zifuatazo zikiwaendea viongozi wajuu wa CHADEMA wakiwemo, M/Kiti, Freema Mbowe, Dr Slaa n.k

1. Matumizi mabaya ya Ruzuku

2.Taratibu za fedha ndani ya Chama

3.Ufinyu wa Demokrasia (Mbowe vs Zitto/uchaguzi M/Kiti. Uchaguzi M/kiti vijana, yeye mwenyewe akiwa mgombea)

Kifupi yote hayo hapo juu ni mambo ya FWEZA, kazi ipo. Sasa chama kisichokuwa wazi katika mambo ya fedha, tutadiriki vipi kukipa nchi. Matatizo haya niliyajadili siku za nyuma, si mara moja bali mara nyingi tu. Lakini kwa bahati mbaya kama alivyoeleza Kafulila, kuwa wana CHADEMA ni wagumu sana kujirekebisha. NA MBISHI HAFAIDI MPAKA SIKU YA IDD.

Kafulilo ameendelea kwa kutoa ujumbe muhimu sana kama ninavyounukuu hapa chini:

"Taifa linapita katika kipindi kigumu sana chenye misukosuko ambayo msingi wake ni siasa duni ambazo msingi wake ni upinzani dhaifu kwa upande mmoja na Chama tawala kilicho choka kwa upande wa pili"

Yote hayo ni tisa, lakini kumi kama anajihisi kuwa kafulia bila kukusudia basi aombe msamaha kwa CHADEMA na arudi madarakani.
 
Tetesi za kufukuzwa uanachama, bwana Kafulila zilijitokeza toka kwa wana Paparazi siku nyingi tu kabla hata ya yeye mwenyewe kukutana na waandishi wa habari.

Habari zilivuma huku wasomaji wakidai vyanzo vya habari hizo bila mafanikio. Leo hii kuna chanzo maalum ikwa ni yeye mwenyewe akithibitisha kufukuzwa uanachama. Kinachonisikitisha mimi ni pale anapoonyesha kuukubali uamuzi huo kwa shingo upande, pale asemapo: "Ninaondoka CHADEMA kwa uchungu mkubwa kwasababu ya lengo thabiti kwamba lazima niitumikie nchi yangu katika harakati za siasa, na. Nitaikumbuka sana CHADEMA kwakuwa nilimwaga damu katika ujenzi wa chama hiki, ninalazimika kukaa pembeni."

Huwezi kuitumikia nchi yako ipasavyo ukiwa ndani ya chama ambacho kinamapungufu mengi kama aliyoyaeleza Kafulila katika pres conf. Aidha anaendelea kusema kuwa " ".......ninawaheshimu sana viongozi wa CHADEMA." Huwezi hata kidogo ukawaheshimu viongozi wasiojua kazi yao au wanaotaka kuendeleza ufisadi ndani ya CHAMA. Kwa maneno mengine wanakiandaa chama kushika nchi ili kuendeleza ufisadi. Ni kosa kabisa kuwaheshimu viongozi kama hao. Kwanza kazi, ndio baadae heshima. Ukichemsha katika kazi hakuna heshima. Kwa upande mwingine nahisi kama vile Kafulila anajilaumu, kuwa kwanini alianzisha kuhoji utawala katika chama, kwani asingefanya hivyo bado angekuwa anakula kuku.

Katika pres conf yake, kulijaa tuhuma zifuatazo zikiwaendea viongozi wajuu wa CHADEMA wakiwemo, M/Kiti, Freema Mbowe, Dr Slaa n.k

1. Matumizi mabaya ya Ruzuku

2.Taratibu za fedha ndani ya Chama

3.Ufinyu wa Demokrasia (Mbowe vs Zitto/uchaguzi M/Kiti. Uchaguzi M/kiti vijana, yeye mwenyewe akiwa mgombea)

Kifupi yote hayo hapo juu ni mambo ya FWEZA, kazi ipo. Sasa chama kisichokuwa wazi katika mambo ya fedha, tutadiriki vipi kukipa nchi. Matatizo haya niliyajadili siku za nyuma, si mara moja bali mara nyingi tu. Lakini kwa bahati mbaya kama alivyoeleza Kafulila, kuwa wana CHADEMA ni wagumu sana kujirekebisha. NA MBISHI HAFAIDI MPAKA SIKU YA IDD.

Kafulilo ameendelea kwa kutoa ujumbe muhimu sana kama ninavyounukuu hapa chini:

"Taifa linapita katika kipindi kigumu sana chenye misukosuko ambayo msingi wake ni siasa duni ambazo msingi wake ni upinzani dhaifu kwa upande mmoja na Chama tawala kilicho choka kwa upande wa pili"

Yote hayo ni tisa, lakini kumi kama anajihisi kuwa kafulia bila kukusudia basi aombe msamaha kwa CHADEMA na arudi madarakani.

Tabia hii ya kiswahili ya kuanika maovu wakati unapobanwa kwa uovu wako imepitwa na wakati. Kwa nini hakusema huo ufisadi ndani ya CHADEMA kabla hajatimuliwa???. Hana lolote, nae alihusika kwa kila kilichofanyika akiwa madarakani kwa dhana ya "collective responsibility".......
 
- well wale spinners wa huko upande wa pili, tafadhalini tusaidieni na hili la kumwaga damu kuimarisha chama, exactly ni nini unajua kwenye siasa ukweli usipowekwa mapema kuna hatari ya kubadilishwa kuwa uongo, kumbe ni uongo na sio ukweli!

respect.

fmes!
mkuu labda walimshirikisha kwenye kumtoa uanachama marehemu wangwe.amesema kuna njia mbili moja kujitoa mwenyewe uanachama na ya pili kutolewa kinguvu-roho.
 
CHADEMA lazima ipitie mkondo huu, lazima nidhamu na maadili yapewe kipaumbele kwa kuanzia kwa viongozi wa ngazi za juu, CCM waliogopana na kulindana kwa miaka mingi kisa umaarufu wa mtu leo hii JK, chama kimemshinda, nnchi inaangamia mikononi mwake, yaani Kafulila ilikua lazima alipe gharama za upuuzi wake, sasa hili ni somo kwa kina zito, kama hawatajirekebisha kimwenendo, panga litawashukia.
 
Tabia hii ya kiswahili ya kuanika maovu wakati unapobanwa kwa uovu wako imepitwa na wakati. Kwa nini hakusema huo ufisadi ndani ya CHADEMA kabla hajatimuliwa???. Hana lolote, nae alihusika kwa kila kilichofanyika akiwa madarakani kwa dhana ya "collective responsibility".......
huo ni uongo wao, wanatafuta huruma, alipokua anashirikiana na Zito kuhujumu mikakati na siri za chama alidhani atavumiliwa, hongera Mbowe na Slaa, kwa kusafisha waasi na vibaraka hawa ndani ya chama
 
Hawa wamepigwa na kisichoonekana. Wamefanya mengi wakishirikiana na ccm (kina Zawadi Ngoda) ili kukivuruga chama. Mmoja mmoja baada ya mwingine wanaanza kujifunua jinsi walivyo na mabosi wao kina Zawadi Ngoda wameanza kuwakana.

Kaanza Kafulila ... utasikia tu mengi kumhusu.
 
mkuu labda walimshirikisha kwenye kumtoa uanachama marehemu wangwe.amesema kuna njia mbili moja kujitoa mwenyewe uanachama na ya pili kutolewa kinguvu-roho.

No hapa anaongelewa - Kolimba, Kabeho, Kibona, Mama Mbatia, Kombe, mkemia mkuu wa serikali, Stan Katabalo, na wengine wengi waliopitia chinja chinja ya ccm.

Hapo hujaweka wale waandamanaji wa pemba au mauaji ya Jan 2001.
 
Hawa wamepigwa na kisichoonekana. Wamefanya mengi wakishirikiana na ccm (kina Zawadi Ngoda) ili kukivuruga chama. Mmoja mmoja baada ya mwingine wanaanza kujifunua jinsi walivyo na mabosi wao kina Zawadi Ngoda wameanza kuwakana.

Kaanza Kafulila ... utasikia tu mengi kumhusu.
CHADEMA ni taasisi makini yenye dira , nidhamu , Chama kinahitaji watu wenye nia moja kuweza kusonga mbele, Kina kafurila walikua na agenda yao inayohusu kuimaliza CHADEMA, sasa wakakutana na mabingwa wa mikakati na siasa , wakawang'amua wakawang'oa, yuko huru aende kokote sasa
 
Hawa wamepigwa na kisichoonekana. Wamefanya mengi wakishirikiana na ccm (kina Zawadi Ngoda) ili kukivuruga chama. Mmoja mmoja baada ya mwingine wanaanza kujifunua jinsi walivyo na mabosi wao kina Zawadi Ngoda wameanza kuwakana.

Kaanza Kafulila ... utasikia tu mengi kumhusu.
Ndugu yangu, huko unakonipeleka mimi simo. Mimi ni mlala hoi tu ninayetarajia kuwa pengine siku moja ama upinzani ama chama tawala kitajuta kwa maovu wanayotufanyia.

Si umemsikia Mkapa ameshaanza kuyaacha ya Kaisari na kumgeukia Mungu. Basi huenda akina Mbowe na Kafulila nao wakafuata mkondo na kujisuta.

Sisi ni wamoja, zaidi ya JF hatuna pakusemea. Hongera JF. Heri akina Kafulila wanauwezo wa kuwakusanya waandishi wa habari kibao na kusema watakavyo, nasi tukaamini.

Idumu JF!!!!
 
Hawa wamepigwa na kisichoonekana. Wamefanya mengi wakishirikiana na ccm (kina Zawadi Ngoda) ili kukivuruga chama. Mmoja mmoja baada ya mwingine wanaanza kujifunua jinsi walivyo na mabosi wao kina Zawadi Ngoda wameanza kuwakana.

Kaanza Kafulila ... utasikia tu mengi kumhusu.
Heri wewe unayejua kila mwana JF ni chama gani? akili zingine pombe za bure balaaaaa!
 
Tabia hii ya kiswahili ya kuanika maovu wakati unapobanwa kwa uovu wako imepitwa na wakati. Kwa nini hakusema huo ufisadi ndani ya CHADEMA kabla hajatimuliwa???. Hana lolote, nae alihusika kwa kila kilichofanyika akiwa madarakani kwa dhana ya "collective responsibility".......

well said, He was supposed to step down even before he was fired

huo ni uongo wao, wanatafuta huruma, alipokua anashirikiana na Zito kuhujumu mikakati na siri za chama alidhani atafumiliwa, hongera Mbowe na Slaa, kwa kusafisha waasi na vibaraka hawa ndani ya chama

So, next is Zitto? how come is one of the top leaders?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom