DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

Kwahiyo mlifuta utaratibu wa kadi ili mvune hizo hamsini hamsini zinazobaki mikononi kwenu? Utaratibu wa malipo ya kadi ulikuwa rafiki sana na ulipunguza msongamano kwenye vituo vya tiketi..!
 
Kwahiyo mlifuta utaratibu wa kadi ili mvune hizo hamsini hamsini zinazobaki mikononi kwenu? Utaratibu wa malipo ya kadi ulikuwa rafiki sana na ulipunguza msongamano kwenye vituo vya tiketi..!
Overload rebound, damping factor in advance
 
mwanza mtahitaji kampuni yenu, kama ilivyo kila mkoa una mamlaka zake za maji, ndivyo itavyokuwa kwa mabasi ya aina hii kila jiji litakuwa na kampuni yake ya usafirishaji

Sent from my TECNO KI5k using JamiiForums mobile app
 
ushauri wa bure, uwapo kituoni kama una haraka, na huna mahitaji maalum, ni mzima wa afya na nguvu zako, panda basi lolote linaloekea uelekeo wako, simama usitake siti, ukifika mbele shuka pamda lengine hadi ufike uendako

mwendokasi ukidharau kupata siti, na kusimama, na kupansa basi lolote mradi lin uelekeo uutakao na upande basi la kituo chako mbele kwa mbele, hutakaa ulalamike unacheleweshwa, kwasababu mabasi yenyewe yanakufikisha haraka uendako, shida ni wingi wa watu uliozidi mabasi

Sent from my TECNO KI5k using JamiiForums mobile app
 
Mkafie mbali huko wezi sana nyie mmepewa mabasi 100 ya kuanzia saiz yamekufa yote
 
Nyakati za asubuhi na jioni watu hujaa Sana vituoni,inakua Haina tofauti na Banda la mbuzi,magari machache,halafu inakuaje hata kutangaza vituo imeshindikana,si wote wenyeji,mpaka tuchungulie kila kituo utadhani twiga anapelekwa mbuga za chato-burigi
😂😂😂
 
Mimi naona ni kama kupotezeana mda tu,..hata tutoe maoni hamtobadilika sababu ya urasimu na upigaji mwingi.
Maoni yanapokelewa na yanafanyiwa kazi ni kwa vile tu watanzania wengi hatupendi kuwa na subra wakati huu ambao serikali inatatua changamoto ya uchache wa Mabasi.
 
Acha vichekesho. Kuna watu wanaochagua magari na uchache huu wa mabasi!? Gari zimajaan mpaka zote zinageuka express!
 
Naomba kujua huu mladi wa mwendo kasi kutoka JKT Mibulani to Magomeni mikumi umekwama wapi ?,
hasa iki kipande cha kutoka MSIMBAZI CENTER to NJIA PANDA YA KIGOGO.
Hiki kipande kimeachwa kama kilivyo na mkandarasi hatumuoni akiendele na kazi.
Kingine zile Bomba za kutiririsha Maji katika Baazi ya vituo zimeanza kubomoka kabla hata ya Mradi kuanza shida ninini?
Mf: Kituo cha KEKO na VETA
 
Kuna. Basi Kimara Kariakoo limewapeleka abiria Muhimbili badala ya Gerezqni
 
 
Kwahiyo mlifuta utaratibu wa kadi ili mvune hizo hamsini hamsini zinazobaki mikononi kwenu? Utaratibu wa malipo ya kadi ulikuwa rafiki sana na ulipunguza msongamano kwenye vituo vya tiketi..!
Kweli hata Mimi nilikua nikifarijika sana na matumizi ya kadi ili kupunguza msongamano usio wa lazima
 
Mimi naona changamoto pale Mbezi Louis. Wake askari hawafanyi kazi sawasawa, hawaangalii mistari ya abiria mpaka inavurugika ndo utawaona na pia hawana kauli nzuri ya huduma kwa wateja. Pili naona ni muda muafaka wa kurudisha kadi na Sisi tuwe tunachanja maana tumezidiwa na TERESA wao wana kadi kwenye vivuko vya kigamboni
 
Hao askari unawalaumu Bure TU. Ni kama hapo Kimara, gari zikishachelewa sana na abiria kuwa wengi askari waliopo hawatoshi wala hawawezi kudhibiti vurugu mechi gari zinapokuja .

Binafsi nilikuwa napanga mstari kila niingiapo kituoni ila nikaja kushtuka kuwa napoteza muda kwani kila basi likija wanaofanikiwa kupanda ni wale wa pembeni baada ya abiria kuwa wengi. Sasa hivi sipangi foleni, nasubiria TU ku_force kama wengine. Ujinga wakati wa kwenda TU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…