This is a purely Biblical post.
Nicolaitans (Wanikolai).
Revelation 2:6 “But this thou hast, that thou hatest the deeds of the Nicolaitans, which I also hate.”
Ufunuo 2:6 "Lakini una jambo hili, kwamba wayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo mimi pia nayachukia."
Revelation 2:15 “So hast thou also them that hold the doctrine of the Nicolaitans, which thing I hate.”
Ufunuo 2:15 "Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile.
Wanikolai wa Jumamosi.
Wanikolai ni wale waliokuwa wanasema usipotahiriwa kwa utaratibu wa Musa, na usipoishika sheria ya Musa, na usipoishika sabato ya siku ya saba (jumamosi), na usipozishika siku kuu za sheria ya Musa, hautaingia mbinguni. Pia toa fungu la kumi. Pia kula wanyama wasafi tu na ndege na samaki wasafi tu. Kuzishika ina maanisha pia usifanye kazi kwenye siku kuu hizo. Kwa kifupi wanajaribu kupenyeza na kuchanganya mafundisho ya agano la kale kwenye ukristo wa agano jipya.
Wanikolai wa Jumapili.
Kuna wanikolai wengine wanaosema siku ya kwanza ya juma (jumapili), ni sabato, na ni siku ya Bwana. Toa fungu la kumi. Wanajaribu kupenyeza na kuchanganya mafundisho ya agano la kale na pia mafundisho ya kipagani kwenye ukristo wa agano jipya.
Baadhi ya mafundisho ya kipagani ni Bwana Yesu Kristo (Bwana Yahushua Mashiach) alizaliwa 25 Desemba, alibatizwa January au February, Jumapili ni sabato, na ni siku ya Bwana (the Lord's day), jumapili ni dominika, masanamu ya kidini kanisani etc.
Ukweli ni huu.
Bwana Yesu Kristo alizaliwa siku ya kwanza ya the feast of tabernacles, in 5 BC, alibatizwa siku ya pentekoste, in 26 AD, alisulubiwa siku ya pasaka (ijumaa, tarehe 14, ya mwezi wa kwanza wa kibiblia, Abib/Nisan, mwaka 30 AD. Hii ni tarehe 7th April 30 AD, kwa kalenda ya kisasa).
Kwenye agano jipya unatakiwa kuyajua haya, lakini hau amrishwi kuzishika hizi siku kuu na pia hau amrishwi kuacha kufanya kazi au biashara na pia hau amrishwi kuacha kufanya shughuli za kila siku za kidunia kwenye siku kuu hizi.
Kwenye agano jipya, ukipenda, unaweza kula wanyama wasafi na ndege na samaki wasafi. Ukipenda unaweza kula wasio wasafi, muhimu wasiwe na madhara ya kiafya. Hauruhusiwi kunywa damu ya wanyama, na hauruhusiwi kula wanyama walio nyongwa (ambao hawajachinjwa wakiwa hai), na zinaa hairuhusiwi, na hairuhusiwi kuabudu masanamu na hairuhusiwi kuabudu miungu ya uongo. Soma kitabu cha Matendo ya mitume sura ya 15. Soma pia barua mbali mbali za mtume Paulo, kwenye Biblia.
Kwenye agano jipya hau amrishwi kutahiriwa kwa utaratibu wa Musa, na hau amrishwi kuishika sheria ya Musa (soma kitabu cha Matendo ya mitume sura ya 15). Soma pia barua mbali mbali za mtume Paulo, kwenye Biblia.
Pia kwenye agano jipya, siku ya saba (jua linapo zama ijumaa hadi jua linapo zama jumamosi), ndio sabato, na pia ndio siku ya Bwana (the Lord's day).
LAKINI
Kwenye agano jipya wakristo wote kwa neema ya Bwana Yahushua Mashiach (Bwana Yesu Kristo), ni makuhani, na pia ni wana wa Mungu.
Kuhani anaruhusiwa kufanya kazi nzito au nyepesi za kidunia, kwenye siku ya sabato. Na akifanya hivyo hahesabiwi kwamba amevunja sabato.
Kwahiyo wakristo, wakipenda, wanaweza kufanya kazi nzito au nyepesi au biashara na shughuli za kawaida za kila siku za kidunia siku ya sabato. Wakipenda wanaweza kupumzika.
Wakipenda wanaweza kusali au na kufanya ibada, na kuondoka na kwenda kufanya kazi nzito au nyepesi au biashara na shughuli za kawaida za kila siku za kidunia.
Wakristo wakipenda wanaweza kukusanyika na kusali au na kufanya ibada siku yoyote ya wiki (hata jumapili), na kuondoka na kwenda kufanya kazi nzito au nyepesi au biashara na shughuli za kawaida za kila siku za kidunia.
Kwenye agano jipya, katika mbingu hii na dunia hii, wakristo wakikusanyika mahali popote duniani, kwa jina la Bwana Yahushua Mashiach, wanakuwa mahali patakatifu (holy place), pa hekalu la agano jipya.
Kwenye agano jipya, katika mbingu hii na dunia hii, mbinguni ni patakatifu pa patakatifu (most holy place), pa hekalu la agano jipya. Na Bwana Yahushua Mashiach ndie Apostle na Kuhani Mkuu wa hekalu looote la agano jipya mbinguni na duniani.
Kwenye agano jipya, katika mbingu mpya na dunia mpya, Jerusalem mpya yoote (all of new Jerusalem) ni patakatifu pa patakatifu (most holy place), na hakuna hekalu ndani ya Jerusalem mpya, Mungu Baba na Mungu Mwana (Bwana Yahushua Mashiach), ndio hekalu, na dunia mpya yoote ni patakatifu (holy place).
Utatu Mtakatifu wa Mungu Baba, na Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu, ni ukweli kabisa kabisa kabisa, na upo kabisa kabisa kabisa, kutoka milele yote hadi milele yote.
Baki kwenye dhehebu lako, usihame.