China kwa sasa ni reference point ya EV industry duniani, imebadilisha rules za mchezo.

China kwa sasa ni reference point ya EV industry duniani, imebadilisha rules za mchezo.

Xi Jinping

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2023
Posts
9,543
Reaction score
28,807
Makampuni mengi ya kutengeneza magari yameingia kwenye production ya EVs, magari ya umeme.

Changamoto wanayokutana nayo ni kwamba tayari China's EV industry imesha-set standards.

Inachofanya sasa China ni kama Japan's auto industry miaka ya 1980 hadi 2000 mwanzoni ilivyoweka legacy kwenye magari ya mfumo wa ICE.

Kampuni nyingi kama VW, Mercedes Benz, Toyota, Hyundai n.k zinalazimika kujifunza modern features za EV kutoka China.

Haishangazi siku hizi kila kampuni kubwa ya kutengeneza magari inapounda toleo jipya lazima wawe na toleo hilohilo lakini maalumu kwa ajili ya soko la China. Lengo ni ku-meet demands za Chinese customers.

CEO wa Honda alipotembelea supply chain ya EV China.
​
“Hatuna nafasi dhidi ya hili."
— Mkurugenzi wa Honda, Toshihiro Mibe
​

Akimaanisha ni vigumu kushindana na China kwenye kasi, gharama ndogo, na ufanisi mkubwa wa uzalishaji wa magari nchini China wa magari ya umeme.

​
"Makampuni ya magari ya China ni tishio kubwa sana na yanaweza kuondoa wengine sokoni kama hawatabadilika haraka."
—Mkurugenzi wa Ford, Jim Farley
​

CEO wa VW yeye alikiri si rahisi kushindana na China wako mbele ila wana ya kujifunza.​
"We can not keep up, China makes us better."
—Oliver Blume, VW CEO
​
​

"The Chinese market is extremely competitive and fast-moving. Chinese EV competitors offer lower prices and often superior digital features and connectivity.”
—Ola Källenius, CEO Mercedes Benz

"Chinese brands are relevant competitors in the premium segment.”
—Gernot Döllner, CEO AUDI
​
Audi wanakiri wazi kuwa kampuni za EV China sasa zinashindana hata kwenye “premium/luxury level,” si tu magari ya bei nafuu.

Toyota pia imeonyesha wasiwasi kwamba bila mabadiliko makubwa, sekta ya magari ya ICE inaweza kukabiliwa na changamoto ya kuendelea kuwepo.

Makampuni ya China yana advantage kubwa katika EVs kwa sababu kadhaa:
​
  • Uzalishaji wa haraka wa magari​
  • Gharama ndogo za uzalishaji​
  • Mtandao mkubwa (supply chain) wa betri na vifaa vya EV ​
  • Teknolojia ya magari ya umeme inayokua haraka​
 
1. BATTERY
CATL na BYD wamebadilisha kabisa industry:
🔥 Blade Battery (BYD) imeweka kiwango kipya cha usalama dhidi ya moto
⚡ LFP chemistry (Lithium Iron Phosphate) imekuwa standard ya bei nafuu na salama
💰 China imepunguza cost ya betri duniani kwa kiasi kikubwa
👉 Matokeo: Watengenezaji wengi sasa wanarudi kutumia LFP kama “global baseline”.

💻 2. Software-defined EVs
China imeweka kiwango cha EV kuwa:
🧠 “smart device on wheels”
📱 screens kubwa + AI assistants
🔄 OTA (over-the-air updates) kama simu
👉 Hii imeathiri hata kampuni za Ulaya na Marekani kuiga “Chinese-style cockpit design”
​

3. Fast charging & infrastructure push
China ina:
mtandao mkubwa sana wa fast chargers
standardization ya high-power charging
integration ya EV + grid system
👉 Hii imeweka presha kwa US na EU kufuata kasi hiyo.

🚗 4. Cost + scale standard (global pricing pressure)
BYD na wengine wameweka “new benchmark” ya bei:
EV za bei ya chini lakini zenye features nyingi
scale kubwa ya uzalishaji
vertical integration (battery + car + software)
👉 Matokeo: Dunia nzima inalazimika kushindana kwenye “affordable EV standard.”
 
Kinachoibeba China saivi ni population

China is second pupulated country afyer India.

Population yao tu, Inafanya soko la ndnai la magari kuchangamka kwa kasi kabla hawajalikuta la nje yaani USA and Europe.

Vitu vinavyo zalishwa USA vinabei bila sababu za msingi, ni ngumu kucompete china.
 
Hiyo ni kweli kabisa, ila naona mfumo wao wa kibiashara unatishia uchumi mpana wa dunia, maana wao ni liwalo na liwe, sidhani kama wanalenga zaidi faida,wanamwaga kila kitu, kuanzia low end product hadi high end kwa bei za chini kabisa, sasa dunia ikipoteza competition kabisa haitakuwa na ladha tena.
 
Supply chain wazee, ogopa Sana hii kitu unaweza kukimbia soko Kwa Moto wa supply chain ya mwenzako...China supply chain Yao ni balaa, Kila part ya product inajulikana inatoka wapi tena Kwa competition kubwa Sana, viwanda vya kutengeneza vikorokoro vipo kibao, industrial zones Zipo za kutosha, kabla manufacturer hajatengeneza final product tayari ashajua anatoa wapi vitu vyote hivyo, unakuta Una sample za bearings zaidi ya Mia tano kutoka Kwa producers tofauti tena high quality, mzalishaji lazima uchanganyikiwe uchague kipi, cost ndogo dadeki, kwanini mpinzani usiteme kamasi.
 
Miaka ya nyuma nchi za Magharibi na Japan walitengeneza faida kubwa sana billions of dollars kwa kuuza magari kwenye soko la China.

Lakini hakukuwa na kauli kuwa nchi za Magharibi zinafanya dumping nchini China.

Ila leo China wakiuza magari kwa bei himilivu media na wanasiasa wa Magharibi utasikia "overcapacity" au "dumping"

Mpaka leo bado Marekani inaruhusiwa kuuza magari yao China lakini hawaruhusu ya China kwao, wanaogopa ushindani high quality at a reasonable price

Hii ni double standard
​
 
Vitu vinavyo zalishwa USA vinabei

Tatizo ni supply chain 👇🏼👇🏼👇🏼
Supply chain wazee, ogopa Sana hii kitu unaweza kukimbia soko Kwa Moto wa supply chain ya mwenzako...China supply chain Yao ni balaa, Kila part ya product inajulikana inatoka wapi tena Kwa competition kubwa Sana, viwanda vya kutengeneza vikorokoro vipo kibao, industrial zones Zipo za kutosha, kabla manufacturer hajatengeneza final product tayari ashajua anatoa wapi vitu vyote hivyo, unakuta Una sample za bearings zaidi ya Mia tano kutoka Kwa producers tofauti tena high quality, mzalishaji lazima uchanganyikiwe uchague kipi, cost ndogo dadeki, kwanini mpinzani usiteme kamasi.
 
Supply chain wazee, ogopa Sana hii kitu unaweza kukimbia soko Kwa Moto wa supply chain ya mwenzako...China supply chain Yao ni balaa, Kila part ya product inajulikana inatoka wapi tena Kwa competition kubwa Sana, viwanda vya kutengeneza vikorokoro vipo kibao, industrial zones Zipo za kutosha, kabla manufacturer hajatengeneza final product tayari ashajua anatoa wapi vitu vyote hivyo, unakuta Una sample za bearings zaidi ya Mia tano kutoka Kwa producers tofauti tena high quality, mzalishaji lazima uchanganyikiwe uchague kipi, cost ndogo dadeki, kwanini mpinzani usiteme kamasi.

Ni kweli Mkuu ndo maana hata makamouni makubwa yakitaka kuingia soko la china wanafunga viwanda CHINA ili wanufaike na kodi ndogo, Cheap labour, Pia accessories kama hizo.

Wanasema products nyingi za USA na EUROPE zinakua initial products zinaandaliwa CHINA finalizing kama 30% ndo Europe na USA halafu wanagonga muhuri made in USA or Europe
 
China inaelekea pazuri lakini kitu pekee kinachoikwamisha ni kwamba uchumi wao ni fragile sana....nadhani watu wenye ABC za uchumi watanielewa!!!

All in all wanajitahidi

Ni kweli, China "Social and political tension" zinamuumiza sana.
Nominal GDP ya China sasa $ 20.85 trillion in 2026. Wapo pazuri hao jamaa wa macho madogo.
 
Ni kweli Mkuu ndo maana hata makamouni makubwa yakitaka kuingia soko la china wanafunga viwanda CHINA ili wanufaike na kodi ndogo, Cheap labour, Pia accessories kama hizo.
"No supply chain in the world is more critical to us than China.
We're not in China for low labor costs....In the United States if we have a meeting of tooling engineers and we might not fill a room. In China, we would fill multiple football fields."
–Tim Cook (Apple former CEO)
​
 
Kwa mfano kampuni ya BYD wao wanafanya kilakitu wenyewe kuanzia kutengeneza chuma,parts za magari Yao , body , electronic accessories, battery na vingine vyote.
Makampuni ya ulaya na Japan unakuta radio ya gari, airbags, chassis, body , na vitu vingine vimetengenezwa na makampuni tofauti.

Kama nchini Australia magari ya BYD SHARKS 6 imeongoza Kwa mauzo na kuweza kuipiku ford ranger na Hilux sidhani kama watafaulu tena kurudi kwenye chart kama zamani
 
IMG-20260425-WA0000.jpg
 
Back
Top Bottom