Binafsi naamini katiba huendana na nyakati na kumsema Nyerere kwa nyakati alizoongoza na sasa pengine tunaweza tusimtendee haki sana
Yawezekana kweli alikuwa na uwezo wa kubadili katiba wakati wa Mwinyi na Mkapa, lakini kipindi hicho hakuwa Rais. Yawezekana kweli angeweza kubadili katiba kipindi chake, lakini hali ya wakati ule na sasa imekuwa tofauti sana. Kwa kipindi kile mapungufu ya katiba yalijificha ficha kwasababu ya aina ya viongozi waliokuwepo lakini sasa yako wazi
Kwa mapungufu kuonekana wazi wazi ndio muda sahihi wa kufanya marekebisho. Hata nguo iliyotoboka unaweza kuvumilia kuivaa kama tobo haliko sehemu inayoonekana ila tobo likishakuwa sehemu inayoonekana kutoliziba au kununua shati lingine huo ni upuuzi