Ndoto yako inamaanisha, awamu hii yatatumika mabomu (siyo yale ya machozi), mabomu kama mabomu ndiyo maana hadi ardhi ilikuwa inamomonyoka.Ndugu zangu, niliyoyaona usiku wa leo yamenipa wasiwasi na hofu, nimeona nisikae kimya niwaambie na nyinyi, huenda kuna baadhi hapa mpo vizuri kwenye mambo ya ulimwengu ule usioonekana.
Ndoto ya kwanza niliona kundi kubwa la watu wakiwa na viongozi wa juu kabisa wakiongea na kundi hilo mara ghafla ikanyesha mvua kubwa na watu wale wakaanza kutawanyika kila mtu kwenda kujificha, cha ajabu mvua ilipokata wale viongozi wakaanza kuwaita watu warudi ili waendelee kuzungumza nikaona idadi ilikuwa ndogo sana tofauti na mwanzo.
Ndoto hiyo ikaisha hapo, NDOTO YA 2 ndiyo ilinifanya niamke usingizini maana nilikuwa naona kama kweli, TAZAMA niliona mvua kubwa sana ikinyesha ikaleta mafuriko makubwa na ardhi ikaanza kumeguka vipande vipande, nyumba zilisombwa na maji, nikawa najaribu kukimbia niweze kujiokoa, watu pia wakawa wanakimbia wengine walimezwa na ARDHI iliyokuwa inameguka.
Sijui ilikuwaje ila nikajikuta nimebahatika sehemu niliyokaa mmomonyoko na yale maji yalikoma ghafla, ilikuwa ni kama mita kadhaa tu hivyo nikawa nachungulia na kuangalia athari zilizotokea. Nikashituka toka usingizini, nimewaza na kutafakari ila sijajua maana yake nini, naombeni msaada wenu kwa mnaoelewa haya mambo.
Waandamani wote, jiandaeni kupelekwa mbinguni kwa kurushiwa mvua ya mabomu.
Ova endi auti.