Darasa: Maadhimisho ya leo ni ya Uhuru wa Tanzania ila kumbukumbu ndio ya Uhuru wa Tanganyika!

Poor
 
Sahihi mkuu
 
Mkuu @mbingunikwenu , kusema ukweli kuna watu wazito ajabu kuelewa vitu vidogo tuu kama hivi. Kumbukumbu ni kuikumbuka ile siku ya tukio, hili ni ja,no moja. Maadhimisho au kusherehekea, ni tukio linalofanyika sasa.

Kama ilivyo kwa kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa, sio wote huwa wanasherehekea, wengine hukumbuka tuu kwa birthday wishi na hakuna sherehe yoyote. Ukiamua kusherehekea hiyo kumbukumbu ya siku yako ya kuzaliwa, unayefanya sherehe ni wewe na ni sasa.

Turudi kwa ule mfano wa yule Binti Mnbingunikwenu, alipozaliwa aliitwa Binti Mbingunikwenu, hivyo siku zote aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa kama Binti Mbingunikwenu, lakini baada ya kuolewa na Pasco, akabadili jina kuwa Mrs Pasco, siku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa, kumbukumbu tuu ndio ya Binti Mbingunikwenu, lakini sherehe na maadhimisho ni ya Mrs Pasco!.

Iliyopata uhuru ni Tanganyika, na kumbukumbu ni ya uhuru wa Tanganyika, lakini kwasababu sasa jina la Tanganyika halipo, anayeadhimisha, anayeshereheka, ni Tanzania Bara aliyepo!.
P
 

Hivi Pascal, kuna document yoyote ya kiserikali ambayo ilisema/inasema kuwa kuanzia sasa eneo lililokuwa Tanganyika litajulikana kama Tanzania bara?
Au tunafundisha vizazi vyetu na vijavyo mazoea yetu?

Kwa logic hiyohiyo basi subiri mapinduzi matukufu ya Tanzania visiwani.

Mkiamka tu mnabatiza ardhi ya nchi mtakavyo kama unavyobadili jina la ng'ombe, maana hata la binadamu lina taratibu zake kisheria. Au ndo kutaka kulivaa koti la Muungano vyema maana inaonekana lilikuwa oversize kuvaliwa na Tanganyika ?

Nchi mmezigeuza kuwa tofauti ni bara na visiwa. Mengine hayana maana.
 
Pasco, nadhani anastahili kufundishwa badala ya kufundisha.

Mifano anayoitoa ni tofauti kabisa na uhalisia uliopo. Ni kwa makusudi au uwezo ni mdogo.

Anatoa mfano wa mtu aliyebadili jina, lakini Tanganyika haikubadili jina kuwa Tanzania. Tanganyika iliungana na Zanzibar, ikaunda Taifa moja linaloitwa

Tan (ganyika) Zan (zibar) ia. Kama utaifanya sherehe ya uhuru wa Tanganyika kuwa ndiyo birthday ya Tanzania, basi Tanzania ina birthdays mbili. Moja ni ile ya uhuru wa Tanganyika, na ya pili ni ile ya uhuru wa Zanzibar. Kwa nini miongoni mwa wawili waliotengeneza Tanzania, aendelee kuwa na birthday yake, na mwingine birthday yake itajwe kwa jina la mwungano wa wawili?

Birthday ya Tanganyika ni 9 December

Birthday ya Zanzibar 12 January

Birthday ya Tanzania ni 26 April

Pasco ni mpotoshaji anayeamini kuwa lazima kuna watu ni wajinga watakaopokea hoja yoyote bila tafakuri.
 
Mkuu Lukonge , kiukweli somo la historia ya nchi yetu, bado linahitajika sana wakati wote, kuna Watanzania wengi tuu kama wewe hawajui historia ya nchi yetu, kifo cha jina la Tanganyika na kuzaliwa jina la Tanzania. Tulipoungana, nchi yetu iliitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ndipo kisha, likatangwa shindano la kubuni jina la nchi mpya, ndipo la Tanzania likapatikana, hivyo ule muungano ndio ulioua jina la Tanganyika likafa.

Sababu ya kifo cha jina la Tanganyika, huku jina la Zanzibar bado lipo ni kuwa huu muungano wetu adhimu ni muungano very unique, kwa upande mmoja, kimataifa, muungano wetu ni muungano wa union wa nchi mbili kuungana, kuunda nchi moja, JMT, yenye serikali moja ya yenye rais mmoja, CinC mmoja.

Ndani ya muungano, muungano wetu ni muungano wa federation, ambazo nchi mbili zimeungana, na kuunda nchi moja, yenye serikali mbili, na marais wawili, nchi moja ni Tanzania Bara ambayo ndani yake ni nchi moja yenye serikali moja na rais mmoja, rais wa JMT. Kikawaida miungano ya federation, inaunda serikali tatu, serikali ya Tanganyika, serikali ya Zanzibar na serikali ya JMT, lakini kwa vile baada ya ndani ya muungano tuna serikali mbili ya JMT na ya Zanzibar, ndani ya serikali ya JMT ndio humo humo kuna mambo ya iliyokuwa Tanganyika, hivyo there was no need for Tanganyika name, tukawa Tanzania Bara.
P
 
Paskali amekurupuka,, hotuba ya Rais, siku ile ilibainisha wazi, tunaazimisha miska 60 ya uhuru wa Tanganyika,, ambayo ndio Tanzania bara,,,
 

Pascal lengo la kuunda jina jipya lilikuwa ni kutafuta jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo ni kutokana na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. . Na si Tanzania bara.

Leta maandishi yanayosema kuwa tunatafuta jina jipya la Tanganyika.
Au sehemu inayosema kuanzia sasa ardhi ya Tanganyika itajulikana kama Tanzania bara. Unaeleza mambo ya kudhania na kufikirika tu hakuna substantial evidence.

Acha kujificha kwenye neno unique ya kufikirika bila mantiki. Acha kupotosha mambo yaliyo wazi.
 
Nawatakia maadhimisho mema ya siku ya Uhuru na Jamhuri, nikiendelea kusisitiza, kumbukumbu ndio kumbukumbu za uhuru wa Tanganyika, lakini maadhimisho ni maadhimmisho ya uhuru wa Tanzania.
P
 
Mungu endelea kuibariki nchi yetu, iendelee kuwa nchi ya amani na utulivu.

Mungu mbariki Rais wetu, Dr. Samia Suluhu Hassan.
 
Nawatakia maadhimisho mema ya siku ya Uhuru na Jamhuri, nikiendelea kusisitiza, kumbukumbu ndio kumbukumbu za uhuru wa Tanganyika, lakini maadhimisho ni maadhimmisho ya uhuru wa Tanzania.
P
Mkuu P Hivi nchi ambazo hazijawahi kutawaliwa huwa zinaazimisha.au.zina Tarehe ya kukumbuka juu ya uhuru wao? Mimi najua Tanzania tangu kuzaliwa kwake ni nchi huru
 
Mkuu P Hivi nchi ambazo hazijawahi kutawaliwa huwa zinaazimisha.au.zina Tarehe ya kukumbuka juu ya uhuru wao? Mimi najua Tanzania tangu kuzaliwa kwake ni nchi huru
Uhuru maana yake ni national day yake hivyo national day so lazima iwe ni siku ya kupata uhuru, Ethiopia, Liberia na Sierra Leone na Jamhuri ya Africa ya Kati, hazikutawaliwa lakini zina national day zake. Mfano Uingereza national day ni siku ya birthday ya Queen, na salamu yao ya taifa ni "long live the King/Queen.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…