Dar Tambarare: Mvua, mafuriko na Usahaulifu!

This is another business opportunity kwa wajasirimali kama mimi, nanunua kaboti kangu kawe kanapiga Mwenge-Posta!!!
 

TOTALLY UNACCEPTABLE: The ditch on the side of Shaurimoyo Street in Dar es Salaam is pictured in a state of overflowing slime yesterday.

Huyu Kandoro, Mkuu wa Mkoa wa Dar ni wa kufukuza kazi mara moja. Dar uchafu unazidi kukithiri kila kona, taa za barabarani hakuna. Mashimo barabarani yanazidi kuongezeka kila kukicha sehemu za kupumzikia wananchi kama vile pale Mnazi mmoja zinafungwa wakati wote na nyingine kama kwenye fukwe za bahari ya hindi ni marufuku kwa wananchi kupumzika. Kuna ushahidi wa kutosha kwamba kazi imemshinda.
 
Hakuna cha utambarare wowote no wonder kipidupindu nje nje...Hivi hao vijana wanakimbilia mjini kuuza maji wana akili timamu kweli?
Ni kivipi unaenda mjini kufanya kazi ya kuuza maji ya chupa...?Nakumbuka kipindi cha nyuma ilikuwa ni glasi ya maji baridi tshs 10 wakati huo Maji ya chupa hayajaanza kuwa popular ama kuteng'enezwa.
Hivyo vibanda vyote havina mantiki ya kuwepo hapo kabisa...Kama viongozi wetu wangekuwa na ubinadamu na wakweli basi ile Kagoda Agriculture ingesaidia sana...Mlundikano wa watu na wafanyabiashara holela ndio umechangia hayo yote..Si unaona ni nylons everywhere...Bila ya kuweka mkakati wa kuendeleza vijijini kweli hatuendi mahali
Ndugu zangu tunahitaji mabadiliko si kidogo na uchafu kama huu unachangiwa na overpopulation,ukosefu wa mikakati bora ya mipango miji,ufisadi na kutoweka kipaumbele vijijini especially kwenye kilimo.
 
heshima mbele. Hii sidhani kama ni kazi ya Kandoro, nafikiri hili ni jukumu la Meya kama sikosei.Tatizo kila mtu anasubiri mheshimiwa atoe maagizo. Zile semina za Ngurdoto hazijasaidia kabisa.
 
heshima mbele. Hii sidhani kama ni kazi ya Kandoro, nafikiri hili ni jukumu la Meya kama sikosei.Tatizo kila mtu anasubiri mheshimiwa atoe maagizo. Zile semina za Ngurdoto hazijasaidia kabisa.

....true,lakini kandoro hana sababu ya kuvumilia upuuzi kama huu maana ndio mkuu pale,hata meya anaweza sema diwani anahusika hapo,hii culture ya uchafu ina athari mbaya sana kwenye jamii....hivi hakuna sheria za kushtaki wahusika wanaotakiwa kusafisha maeneo kama haya ili sisi wananchi tuwawajibishe mbele ya sheria?
 
heshima mbele. Hii sidhani kama ni kazi ya Kandoro, nafikiri hili ni jukumu la Meya kama sikosei.Tatizo kila mtu anasubiri mheshimiwa atoe maagizo. Zile semina za Ngurdoto hazijasaidia kabisa.

Nakumbuka mwanzoni mwa miaka ya 90 wakati Mrema alipokuwa Waziri wa Mambo ya ndani. Alilivalia njuga swala la usafi Dar na kuwaambia wenye maduka waweke mapipa ya taka nje ya maduka yao, wananchi waache kutupa uchafu hovyo hovyo wahakikishe wanatupa uchafu kwenye mapipa, akahakikisha soko la kariakoo kwa nje na ndani linasafishwa na kweli likasafishwa. Dar ikaanza kung'ara na umaarufu wa Mrema Dar ukazidi kuongezeka. Wakti huo Mkuu wa mkoa wa Dar alikuwa Mary Chipungahelo maarufu kwa mama Chipps.

Siku moja pale Karimjee wakati wa kikao cha bunge Mama Chipps akaropoka kwamba Mrema kaingilia kazi isiyomuhusu basi mama akanunua vita na wakazi wa Dar kwani kila walipomuona walimrushia matusi ya nguoni na wengine hata kulipiga mawe gari lake la RC DSM, Mzee rukhsa akaamua kumuondoa pale na kumpeleka katika moja ya balozi zetu.

Ninachotaka kusema mameya wa Dar wako chini ya mkuu wa mkoa, hivyo kama hawatendi kazi zao inavyostahili basi Kandoro awapeleke puta kila kukicha ili kuhakikisha jiji linakuwa katika usafi unaokubalika ili kupunguza magonjwa ya kipindupindu, malaria, kuharisha n.k. yanayosababishwa na uchafu uliokithiri na siyo kusubiri Mrema mwingine aje kufanya kampeni ya usafi Dar.
 
Nakubaliana kabisa kuwa msisitizo kwenye usafi upewe kiapaumbele ili kuepekana na uchafuzi wa mazingira na magonjwa...Lakini bottomline hapa ni overpopulation...Especially kwenye picha uliyoitumia kama kielelezo, hivyo vibanda vilivyojipanga hapo kuna atakayejali pipa la taka na hapo utaweka mangapi wakati hakuna utaratibu wowote...?Hayo maji machafu kigiza kikiingia hata kukojoa rukhsa.

Idadi ya watu ni kubwa sana hapo bongo na kuwadhibiti ni shida..Kila mahali ni biashara tu..everywhere...Hata hivyo vibanda inawezekana kabisa vinauza bidhaa za aina moja na kila mtu na riziki yake...Kila mahali ni sokoni,na vibanda hivyo viko hapo kwasababu ya kituo cha daladala...Sasa jiji ambalo halijajengwa kwa mpangilio na bado hakuna mpango wa kulinusuru tutafika kweli?

Kulibadilisha jiji inahitaji mipango madhubuti waulize wanaofahamu kuhusu kuna Livingstone aliyekuwa meya wa London, hata Giuliani alikwenda kujifunza kwake...Ukiwa London hata haja ya kuendesha gari huna na tabia ya kutumia dust bin "trash cans" ni kawaida...Sasa sisi Mrema alipoondoka na wao wakaacha kuzingatia usafi as if walikuwa wakimfanyia Mrema favor.

Mikakati mbinu ni lazima iwepo na kabla ya kufikira kuweza kuwahudumia wananchi walio overpopulate....Ni vyema kwanza kuanza kufikiria namna ya kuwapunguza mijini na kupunguza uhamiaji wa mijini...Tz ardhi kubwa kila mtu mijini ni dili, na ufisadi ndo utamaduni badala ya kuwekeza kwenye kilimo ni kununua tu nyumba ughaibuni na kuweka pesa kwenye benki za nje...Mabilioni ya pesa ambayo wao wanasema ni vijisenti.
Mimi siamini kama Tanzania na waafrika tumelaaniwa...Nadhani tunaweza kubadilika na kuibadilisha nchi yetu....Ni muhimu sana....Ila tuanze na ufisadi kwanza maana watu wanadhani madaraka ni misifa na pesa tu na si uwajibikaji.
 
Kuhusu usafi uzembe unapofanyika ktk sheria na utimizaji wa hizo sheria basi kumanage uchafu inakuwa ngumu.

Niko Singapore hapa kila kituo cha daladala kuna dust bin la kutosha na kila maeneo ya makazi( of course makazi yamepangiliwa ipasavyo sio holela kama bongo) kuna the same kind of dust bin la kutosha maeneo hayo. Kila nyumba (apartiments) kuna shute maalum jikoni kwa ajili ya kutupa taka, then kila chumba na hata sebule wanajitahidi kuweka dust bin. Kuna makampuni maalum ya kuondoa uchafu huo huwezi kuta dust bin limejaa ovyo na hata hao wafanyakazi wa taka wana vifaa maalum kulinda afya zao. Kwa hiyo usafi kwao unaanzia chumbani je bongo usafi unaanzia wapi? ( for most of the people)

Nafikiri kama kila nyumba ikiamuliwa kuweka japo dust bin na recyle bin nje ya nyumba tunaweza kupunguza huu uchafu kwani maramoja waweza kuona mahari pa kutupa uchafu ulionao. Then halmashauri ya mji ijitahidi kuondoa uchafu huu kila siku ili kuepuka mrundikano wa uchafu.

I think yes we can.
 
Watendaji wa manispaa ndio wanapaswa kuwajibishwa kwa hili la usafi. Kila manispa inatoa tenda kwa kampuni za kufanya usafi... hapo ndipo ulaji ulaji unapoingizwa na matokeo yake ndiyo haya.
 
Kandoro will be resposible..rais kachagua watu wa kumsaidia...kama kandoro hawajibiki sie lazima tupige kelele...

Jiji Halina Nidhamu hata kidogo...Wizi kila Eneo....Uchafu kila eneo...Madanguro kila eneo...leo hii usafiri tabu lkn Wahusika wanasafiri Nje ya TZ kila siku..lkn Hawajifunzi...kazi kufanya shopping ktk ..... idols!!!! Ukienda Miji ya wenzetu wizi wa kipuuzi kama bongo huwezi kuukuta...
 
Friday, March 6, 2009
uporaji dar mchana kweupeeeeee

Leo asubuhi, nikiwa kwenye foleni maeneo ya jangwani, saa 1.20 asubuhi, gari la tatu kutoka gari langu kwa nyuma lilivamiwa na vibaka, wakafungua milango, ndani ya kama dakika 3 wakapora kila walichoweza kupora.
Ilikuwa ni kwenye foleni, jamaa wana visu, na kila mtu akawa anaangalia kama sinema hivi. HAKUNA MSAADA!
Watu kwenye daladala la karibu, wakawa wametulia kimyaaaaa. Na walio kwenye saloon cars wakawa wanafunga vizuri vioo ili wasiwe next target. Siku zote hizi WARNING nilikuwa sizipi uzito unaostahili, leo nimekubali. Naomba munielewe, Sizungumzii mtu kupora cheni au simu dirishani.
Jamaa wamefungua milango, na kunyang'anya kila walichokifikia.
Tafadhali sio tu ufunge vioo, lakini hakikisha milango imefungwa ( LOCKED) BONGO TAMBARAREEE!
Mdau OCTAVIAN ‘OC'

© Michuzi | Friday, March 06, 2009 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako |



Maoni: 38



Tarehe March 06, 2009 10:11 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

Octavian, lakini wewe ulifanya nini kusaidia?


Tarehe March 06, 2009 10:25 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

Itabidi sasa tuanze ku-drive na pistol mfukoni. Unamumwagisha mtu ubongo barabarani tu.


Tarehe March 06, 2009 10:34 AM, Mtoa Maoni: Ralph

Hapo ni bastola tu, fully loaded! halafu hao vibaka uchwara ndio watalijua jiji.....


Tarehe March 06, 2009 10:48 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

Jamani, zile difender zimeishia wapi, Tukubaliane kitu kimoja, mambo mengi yanayofanyika Tanzania yanasababisha madhaama sehemu nyingine, mfano, tukimuuliza Muheshimiwa IGP- Mwema, atasema hana askari na vitendea kazi, kang'ang'ania community policing weee mpaka basi, mabilioni yanayopotea kila siku kwenye, Radar, Richmond, Dowans, EPA na nyingine nyingi, zingetosha kabisa kumpa IGP uwezo wa kudhibiti hawa wahuni wachache. Hili tatizo halipo tu Jangwani jamani, lipo Salander Bridge pia, nimeshashuhudia mwenyewe mara mbili mtu akiporwa side mirrors na Handbag. Watanzania tushikamane kuishinikiza serikali kuthibiti hii hali.


Tarehe March 06, 2009 10:50 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

Mdau bora umelitoa hili wadau waweze kuchangia. Hili jambo lipo sana hapa Bongo sielewi ndio life style ya wabongo au vipi. Unaweza ukawa unaibiwa na hata kupigwa mchana peupeee lakini hakuna anayejitokeza kukusaidia hata kama kunawatu wanaopita karibu tena mwenye gari kama yupo karibu ndio anafunga vioo kabisaaa. Kwakweli wabongo tunakosa upendo kabisa kwa wenzetu.

Nao vibaka siku hizi kutokana na tabia hiyo ya kuachwa wakimuibia mtu hakuna basi ndio wamezidisha hasa. Hayo maeneo ya hapo Magomeni ni kama kawa kwa kitendo hicho kwa wewe ndio mara ya kwanza kuona mimi nilishaona tena vitendo kama hivyo. Inakuwa kama watu wa Magomeni wanawajua vibaka hao na nijamaa zao.

Hii polisi jamii sijui itaimarika lini ikiwa sisi wenyewe tunaangalia tu hatushiriki kusaidia kupunguza hivi vitendo viovu vikiendelea. Hii inaonyesha wazi huko tunapoelekea tutakuja kuchinjana hivi njiani hakuna pia atakayesaidia.

Kwa maoni yangu naona pia vibaka wamejiamini sana kutokana na wakimwibia mtu hakuna anayeingilia kumkamata pia hata wanapokamatwa wakienda polisi wanafungwa tu hauzidi mwaka wanatoka msamaha wa Rais ukipita. Hii imepelekea kufanya uporaji kuwa ndio ajira yao. (Mimi nitaiba nikikamatwa poa nitafungwa kwanza gerezani nitakuwa napata chakula cha bure kutofautisha na uraiani na pia muda si mrefu nitatoka kwa msamaa wa Rais au nikikamatwa nitatoa chochote nitaachiwa)

Pia Kinondoni yani msamaa wa Rais ulipopita yani vibaka wote unawaona uraiani bora maeneo ya studio sio mabaya sana lakini maeneo ya manyanya na Mkwajuni ukipita tu katika mitaa mida ya asubuhi basi wewe ujue utabananishwa na vibaka wakupore vitu vyote.

Nilinyanganywa simu mchana kweupee, nilipita mtaa mmoja nitokee Kinondoni Stereo nikakutana na kibaka ikawa tunapambana nikijiamini kwani niliona watu kwa mbali kidogo wananiona kuwa watanisaidia huku napiga kelele lakini hakuna aliyekuja zaidi ya kunishangaa hadi kibaka akaning'ata na kuchukua simu.

NAOMBA WATANZANIA TUBADILIKE..NCHI YETU NI NCHI YENYE AMANI..TUPENDANE, TUSHIRIKIANE, UKIONA MWENZAKO ANAPATA TATIZO KAMA HILO BASI ASIJITOKEZE MMOJA KUMSAIDIA TUJITOKEZE KWA WINGI TUMSAIDIE NDIVYO TUTAKAVYO TOKOMEZA MAOVU HAYA...TUITUNZE AMANI YETU YA NCHI SASAHIVI TUNAPOELEKEA PABAYA...MWENZIO AKIFANYIWA KITU KIBAYA JIHISI KAMA NI WEWE AU NDUGU YAKO KWANI IPO SIKU YATAKUFIKA NA WEWE..

Mdau H


Tarehe March 06, 2009 10:52 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

du sasa bongo kunatisha naogopa hata kurudi kama mambo yamefikia hivo ndugu zetu huko watapona ndo mana mdogo wangu anataka kununua bunduki nikamkataza ya nini bongo kumbe ni muhimu kuwa nayo kwa mambo kama haya nchi inaenda kubaya


Tarehe March 06, 2009 11:01 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

Hii michuzi ni kweli au kamba kali tu kwa bongo yetu hii mambo kama hayo wapi na wapi kwanza sio tamaduni zetu au ulikuwa unaota donto ya mchana kaka


Tarehe March 06, 2009 11:34 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

tuache utani bwana serikali inaweza kushughulikia hili


tunaomba serikali ifannye kazi yake


Tarehe March 06, 2009 11:56 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

Ahsante kwa kutuhabarisha. Naelewa usingeweza kufanya chochote maana wao walikuwa na silaha na wewe huna. Pia ungetoka wangekuvamia na wewe.
Cha msingi tukumbuke ku lock milango ya magari yetu


Tarehe March 06, 2009 12:06 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

Nimekusoma OC .inabidi wanausalama wa yaangilie sana haya maeneo ya Jangwani ,Salender bridge pia maeneo ya Daraja la Ubungo yamekuwa na matukio mengi sana ya uharifu.

Afande Kova changamoto hiyo


Tarehe March 06, 2009 12:06 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

Nimekusoma OC .inabidi wanausalama wa yaangilie sana haya maeneo ya Jangwani ,Salender bridge pia maeneo ya Daraja la Ubungo yamekuwa na matukio mengi sana ya uharifu.

Afande Kova changamoto hiyo


Tarehe March 06, 2009 12:13 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

mbona na wewe hukusaidia kitu?


Tarehe March 06, 2009 12:20 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

Hii mimi inanishangaza, walikuwepo watu kwenye daladala, na maeneo mengine wameona, halafu wote wameuchuna, kwakuogopa visu na mapanga, hamjui munawapa vichwa hawa watu. Ilibidi watu wajitose, kwasababu na wao walikuwa wanawapima, kwa kujua wengi ni waoga.
Tusidanganyike, kama hatutajitolea wenyewe tusitegemee polisi watakuwepo kila mahali. Inabidi kujitolea muhanga ili kuinusuru hii hali. Hayeni wachekeeni, kwani leo kwa yule kesho kwako.
M3


Tarehe March 06, 2009 1:50 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

Hii ni dalili ya baadhi ya wananchi (na hasa wananchi wa chini kabisa kimapato) kukata tamaa na kufikia hali ya kusema, "liwalo na liwe". Hii inatokana na Upumbavu, Ujinga, na Uzembe wa Serikali na watendaji wake (pamoja na Rais) kutumia mida wote wa uongozi wao katika kujinufaisha wao na familia zao binafsi bila ya kujali nchi na wananchi wake.

Sitetei wezi, na ningependa sana kama hawa vibaka wangeelekeza uharamia huu kwa watendaji wa serikali, na familia zao.


Tarehe March 06, 2009 2:26 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

wewe unaetaka kumumwagisha mtu ubongo naomba nikuulize swali ulishamwaga wangapi??
angalia utaishia kunyongwa na ufisadi wenu..
mnataka wenzenu wafe na njaa?? na ufisadi wenu

hii ni trela bado picha kamili mtaiona


Tarehe March 06, 2009 2:29 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

hakuna msaada wa story ukitaka kutoa msaada wape hela hiyo ni njaa tu inawasumbuwa ni ndugu zetu wanahitaji kuishi na kuishi ni kula sasa mnataka wao wafe na njaa.

waende na nyumbani kwa mkapa watapata hela ya kula mwaka mzima.


Tarehe March 06, 2009 2:34 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

je ungelikuwa wewe unanjaa na nyumbani kwenu mzazi wako yuko hosp na hakuna hela ya matibabu je ungefanyanini???
au utamwacha ndugu yako afe na njaa kwa ajili ya mafisadi au utawakaba ili umtibie mzazi wako???
mimi naona hawanakosa ni kosa la selikali ya mafisadi kuifisadi nchi na kuleta ungumu wa maisha kwa walio wengi.


Tarehe March 06, 2009 2:37 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

bora mtu ufe kwa kutafuta ridhiki kuliko kufa na njaa poa tu tumieni hizo bastora zenu kama mnaona kuuwa watu ni ufahari wenu mafisadi

ila azabu zenu za kuibia walala hoi zinaongezeka.


Tarehe March 06, 2009 2:42 PM, Mtoa Maoni: Mzee wa Zeze

Hayo yaliwahi kunikuta mwaka 2001 pale kwenye taa za barabarani za Ubungo. Walifanikiwa kunikomba kila kitu nilichokuwa nacho garini na kunijeruhi kwenye bega la upande wa kulia.
Kwa bahati nzuri mmoja alikamatwa nanatumikia kifungo chake cha miaka 30


Tarehe March 06, 2009 2:55 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

Wadau, anachosema huyu Mdau mwenzetu ni kweeeeeeli kabisa. Wiki iliyopita wameninyang'anya hereni zangu ivi ivi hapo hapo jangwani maeneo ya Kwa Macheni!! Ilikuwa ni saa moja dakika ishirini na tatu (07:23am) nikiwa kwe foleni. Watu walikuwa wameshangaa na kunipa pole tu. Vijana wako Smart huwezi amini wala kudhania. Nawahimiza watu wote mlock milango ya magari yenu na kufunga vioo. Na kwa wale watembea kwa miguu umezuka wizi wa waendesha pikipiki kukwapua pochi za kina dada na kutokomea nazo. Hilo lilitokea mwishonimwa mwezi wa pili maeneo ya Ubungo. Jeshi letu la polisi tunaomba litusaidie kucheki katka maeneo tajwa ili kutunusruru maana itafika mahali sasa wataanza kuchinja watu wakienda Kulijenga Taifa!!!! Sharly


Tarehe March 06, 2009 2:56 PM, Mtoa Maoni: narsis mboya

hi wadau
this is just the beginning
ngoja watu waanze kupungwa makazini kutokana na hili lirecession linalokuja
watoto wanamaliza mashule ajiri haba
sekta binafsi nazo zitajibu mapigo kwa kutokuajiri
bidhaa haziuziki labda za china!
nakwambia ni kasheshe tupu
askari wa doria wapo siku hizi?
Mdau


Tarehe March 06, 2009 3:13 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

Ni juzi tu niliona katika blog moja ya MR. BOBOS CLASS imetolewa tahadhari baada ya dada mmmoja kuvamiwa hapo jangwani majira ya saa3. Ninachojiuliza mimi ni kwamba, nikiwakama mtumiaji wa njia hiyo kilasiku, huwa naona askari wanapatrol katika eneo hilo. Je, wanakuwa wapi au ndo vibaka wanawa-time?Inatia hofu hofu sana. Je, ukimfyatua na bastola mtu kama huyo inasimama vipi?


Tarehe March 06, 2009 3:16 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

SAFI SANA.
Hao jamaa mi nawafagilia sana, maana ni kielelezo kizuri cha hali tuliyiofika najua naweza kueleweka vibaya lakini aliye na macho haambiwi tazama. Hata MUNGIKI waliianza hivi leo wanakaribia kuwa insurgence


Tarehe March 06, 2009 3:23 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

Watanzania wengi ni wagumu sana kuwasaidia wenzao wanapopatwa na matatizo. hivi ni kweli uwingi ule wa magari katika foleni na daladala zote hizo watu wanashindwa kuwa na umoja na kushuka na kukabiliana na majambazi ama wahuni? si pati jibu. hivi kama watu wangeshuka katika madaladala kama matatu hao vibaka wengeweza kufanya unyama huo?
Tuache uoga wa kihindi wa kujifungia ndani.


Tarehe March 06, 2009 3:38 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

waacheni jamaa nao wajilipe washaburuzwa sana na mafisadi hao


Tarehe March 06, 2009 4:17 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

hayo mambo ni kweli kabisa na yanatokea maeneo ya jangwani wakati wa foleni. wiki iliyopita pia dada wawili wafanyakazi wa muhimbili(nurses)waliporwa kwa staili hiyo hiyo. hakuna aliyewasaidia, kwa kuwa vibaka walikuwa na mapanga na visu. walichukua simu, pochi na kila walichoweza kubeba, asubuhi kweupeee


Tarehe March 06, 2009 4:17 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

hayo mambo ni kweli kabisa na yanatokea maeneo ya jangwani wakati wa foleni. wiki iliyopita pia dada wawili wafanyakazi wa muhimbili(nurses)waliporwa kwa staili hiyo hiyo. hakuna aliyewasaidia, kwa kuwa vibaka walikuwa na mapanga na visu. walichukua simu, pochi na kila walichoweza kubeba, asubuhi kweupeee


Tarehe March 06, 2009 4:17 PM, Mtoa Maoni: Waefeso

Nadhani ndo kilichobakia, kuwa na bastola, nadhani serikali ilegeze masharti ya watu kununua silaha, itaongeza discipline.


Tarehe March 06, 2009 4:42 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

Duh e bwanaeeeee...Kova atakuwa anayo habari hii na lazima kutakuwa na askari wa doria walipangwa eneo hili!! Mara kibao huwa inatokea pale Jangwani nyakati za foleni haswa asubuhi!Huwa wanafuatilia kilichomo na aina ya abiria waliomo kuanzia magomeni! wakishaona kwamba milango haitawapa shida kufunguka na abiria si mapande ya watu/mabaunsa basi wanali-mark hilo gari na ku-set ambush pale chini Darajani, sehemu ambayo wao kukimbia bila kufukuzwa na umati wa watu wenye hasira inakuwa rahisi!Sasa sijui tufanyeje?maanake pale hakuna ujanja na ni lazima mtu uende kazini saa hizo...KOVA SAIDIA BANA!!


Tarehe March 06, 2009 5:38 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

mkiwa kwenye magari yenu msitegemee msaada kutoka kwenye daladala kwani saiz kuna chuki kati ya watumiaji wa daladala na wenye magari.tunapoelekea sio pazuri jamani!


Tarehe March 06, 2009 5:47 PM, Mtoa Maoni: mgogo muuza kahawa!

WANACHOFIKIRIA ABIRIA WALIOBANA KWENYE DALADALA NI KUWA"ENDAPONITASHUKA KUSAIDIA BASI NI WAZI KABISA KUWA SITOIPATA TENA NAFASI YA KUKAA KWENYE KITI HADI POSTA MPYA PALE NITAKOPORUDI KWENYE DALADALA"WATANZANIA TULIANZISHA KAMTINDO KAZURI KABISA KA KUSAIDIANA NA HATA KUCHOMANA MOTO,ILA SASA NAONA ULE UPENDO UMEANZA KUPOTEA NA WATU TUNETAWALIWA NA HAKA KANENO"fisadi" AMBAPO KILA ALIYEJITAHIDI KIDOGO KUWA NA KAGARI AU MAISHA YA KULA MATATATU KWA SIKU BASI NI FISADI;HEBU JAMANI TURUDIE ZILE ZAMA ZA KUSHIRIKIANA KAMA ZAMANI ITAPENDEZA!


Tarehe March 06, 2009 6:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

'Hii sasa ni kamba ngumu, uchumi tunao tunaukalia'- maneno ya Xplastaz.

Maana yake ajira hakuna, walionacho wanazidi kupora, soma magazeti ya siku hizi 'mabilionea' ndio wanaanza kufikishwa mahakamani.

Njia za kupunguza uhalifu sio raia kubeba bastola au kumwaga polisi. Maana hizo bastola pia zitaibiwa ili kupora simu za mikononi, briefcase au mikoba.

Jibu ni serikali kupanga mikakati endelevu ya kupanua wigo wa kuwezesha raia wenyewe kama vijana kupata ajira, kufanya kilimo cha kisasa au mikopo na mafunzo ya kuendesha biashara.

Ikiwa masuala hayo niliyosema hapo juu haitafanyiwa kazi, basi tutegemee kuona uhalifu wa kutumia mabavu/nguvu ukiongezeka kwa kasi kulingana na kasi ya wizi wa 'kalamu' unaofanywa na 'mabilionea.


Tarehe March 06, 2009 6:01 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

Hao waliokuwa kwenye daladala waliona shida kutoka kusaidia kwa sababu sasa hivi sio kila mwenye gari ni jirani mwema. Kuna mafisadi humo humo.


Tarehe March 06, 2009 6:22 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

Katika hali hiyo msaada utautoaje? hata kama una bastola maana ukikosea na kumpata mtu mwingine utaozea jela, hakuna mtu yuko tayari kupambana na kundi lenye visu na mapanga kwa kuwa wao kwa kawaida huwa wamelewa bangi au unga kwa hiyo hata wakiona pistol wataendelea kuvamia. Hapa ni polisi kufanya kazi yao tu kwa kuwa wao wanaogopwa.


Tarehe March 06, 2009 7:13 PM, Mtoa Maoni: Nshimimana aka Dumisane

hivi kwanini watu wanaendelea kuishi hapo Jangwani!?

si mnatafuta matatizo lakini wenyewe!?

recession hii hiyo, ohooo..

Anyway, sijui kwanini hamuwachomi!?

I Luv You Bongo, Japo Sijafika?

= = =
Buffalo,
New York


Tarehe March 06, 2009 7:33 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

Hivi kweli tumeshindwa hata kuzuia vibaka....
Mimi sikubaliani na kwamba recesssion ndo inasababisha haya majanga.
Hawa vibaka wanajua kwamba serikali yao siku zote iko likizo siku zote kwahiyo wanafanya wanavyotaka..
Mimi nina jamaa yangu alivamiwa nyumbani kwakwe Mbezi saa nne usiku.Akapiga simu polisi mara nyingi tu..wakipokea wanasema hawana usafiri kwahiyo hawawezi kusaidia.
Tell me, how u gonna feel when you are facing death and law enforcement are telling you..just die man we ain't coming over....this is BS


Tarehe March 06, 2009 10:12 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

Kuna wimbo 'Tusibweteke' ktk Youtube. Kwa kuwa sasa mtoto bongo anazaliwa na madeni na aliyekopa siyo anayelipa......

Hili suala ni 'systemic problem' (mfumo-mzima) siyo la Kamanda Kova wala Polisi. Hapa ni mfumo mzima wa nchi iliyokosa mkakati wa kuwawezesha wale walio watoto wa wakulima/wafugaji/wavuvi/wafanyakazi masikini na ndio maana uhalifu wa kupata hela ya 'kuganga njaa' utaendelea kuongezeka kwa sana.


Tarehe March 07, 2009 1:14 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

mimi sishauri wafanywe chochote kumpiga mtu bastola kwa ajili amekuibia simu sio haki, huku uk ukiiba unaambiwa stop stop kama kuna polisi karibu wanakutoa mbio.
lakini ukifisadi chamoto utakiona.

kwa hiyo wakupigwa bastola ni hao mafisadi wanaowaibia kila siku na sasa hivi wameanza kuwarithisha watoto wao uwizi wanaiba kuanzia milioni tshs mpaka $£.

azabu lazima iendane na kosa, sio mtu anapora elfu 50 anauliwa, mtu anaiba mabilioni anatembea, hizo bilioni ndio zingeweza kuajiri askari wengi huyo wa elfu hamsini asingeweza kusogea

michuzi usiibane hii kama kawaida yako
mdau uk
 
Bubu, unafikiri jama angileta ubishi kutoa kile ambacho vijana wakazi walikuwa wanataka ingekuwaje? nadhani ingekuwa habari nyingine "mauaji''. Mkuu, hii ni vita, kama watu wanakuja na visu kupora na wako tayari kuvitumia mapambano sahihi kwao ni kwenda full armed too, Nakumbuka Omary Mahita aliwahi kutoa order kwa wali vijana askali wa chuo cha wanayama poli kutokusita kuua maharamia, maana wakisita watauwawa wao. And it worked very fine. I bet that is the only solution. Mtanzania anakosa amani katika nchi yake kama mkimbizi, sasa hata kudrive alone mtu ataogopa nini hiii?
 
bm 21, nakubaliana na wewe kwamba hao vibaka wanaweza kuua. Pamoja na hayo serikali ina wajibu wa kulinda uhai na mali za raia wake. Maeneo yote ambayo yanajulikana kwamba yana matatizo ya hao vibaka kama pale jangwani, salendar bridge n.k. wangewekwa polisi hata 10 wakiwa na bunduki tayari kwa lolote lile dhidi ya vibaka hao. Hii itasaidia sana kupunguza matukio kama hayo vinginevyo si muda mrefu tutasikia vibaka hao wameua mtu aliyeamua kujitetea dhidi ya vibaka hao.
 
Mods, nafikiri hii thread inajirudia ingawa katika kichwa cha habari tofauti. Naomba kama inawezekana ziunganishwe. Tizama thread ya jana, Uporaji dar kweupeee!

Shadow.
 
wkuu, unajua kuna mvua imenyesha leo hapa mjini kwa kweli sio utani, imeonyesha jinsi gani tuna matatizo mengi zaidi ya hata tunavyojifikiria..... Wenzetu wakifikiria kujenga "space shuttles" etc sisi inabidi turudi darasani na kujaribu kujenga mitaro ya maji ya mvua, storm water systems. Kwa kweli pamoja na kwamba inatia aibu, ni hatari sana na hasara ni nyingi kutokana na mvua hapa kwetu... Imagine that is Dar es Salaam, je Lindi na mikoa mingine?

mpaka wafikirie suala la mitaro.. wenzio wanafikiria "barabara za lami", majengo marefu yenye vioo vinavyomeremeta, madish ya setalaiti n.k Likija suala la mitaro ni usumbufu mkubwa wa wananchi, linahitaji utalaamu na usimamizi wa karibu na linaweza kuchukua muda mrefu.

So, kwa sababu maji ya mvua pia yanakauka haraka hakuna sababu ya kujenga mitaro.
 
mpaka wafikirie suala la mitaro.. wenzio wanafikiria "barabara za lami", majengo marefu yenye vioo vinavyomeremeta, madish ya setalaiti n.k Likija suala la mitaro ni usumbufu mkubwa wa wananchi, linahitaji utalaamu na usimamizi wa karibu na linaweza kuchukua muda mrefu.

So, kwa sababu maji ya mvua pia yanakauka haraka hakuna sababu ya kujenga mitaro.

.........Mkuu Mwanakijiji.......kwi kwi kwi kwi..........pamoja na kwamba point hiyo hapo ni kweli....lakini nimepata majibu meengi zaidi na kunifanya nicheke sana

Mkuu Morani75,
hili tatizo tumeshalizungumzia sana hapa na solution zilitolewa............tusichoke kuwakumbushia......
 
.........Mkuu Mwanakijiji.......kwi kwi kwi kwi..........pamoja na kwamba point hiyo hapo ni kweli....lakini nimepata majibu meengi zaidi na kunifanya nicheke sana

Mkuu Morani75,
hili tatizo tumeshalizungumzia sana hapa na solution zilitolewa............tusichoke kuwakumbushia......

Unajua watu wa Dar, wameshazoea maneuvering kwenye mafuriko ya aina hii.. wamebuni njia mbalimbali za kukabiliana nayo miongoni mwao ni kuweka matairi, kuvua viatu na kuvifisha mikononi na kwa wale wenye akili za kiujasiriamali wanaweza kuvusha watu kwa kuwabeba mgongoni na kuwacharge capacity fee ya aina fulani.
 
Na bado utaambiwa kina cha maji kimeshuka ,waacheni waendelee kusema uwongo mwisho Mwenyezi Mungu atazamisha hata mabwawa ila kwa hawa mafisadi wataendeleza msimamo wao kuwa kina cha maji kimeshuka maana waTz wengi hawayajui hata hayo mabwawa yanayotumika kutoa umeme yako wapi ,ni balaa tu mwizi kupewa feza awagaie masikini.
 
Kwakweli hii issue ya storm water ni tatizo kwenye jiji letu hili. Na siyo hapo na baadhi ya mikoa inayoanzakukua. Barabara nyingi zinajengwa bila mitaro madhubuti ambayo haitoshelezi na pia uchafu unaotupwa na watu kwenye hii mitaro kwa asilimia fulani inachangia kuleta mafuliko.

Kuna kitu kingine unajua yale maeneo ya mills tower, shoppers plaza etc zile sehemu zilikuwa njia za maji wakazuia sasa inaponyesha mvua kubwa maji yanakosa pa kwenda. Kwenye ujenzi wetu tunajua tu kusimamisha magholofa lakini vitu vingine kama maji machafu yataenda wapi, jengo limezuia njia ya maji je maji yakija yaendeje hayo yote si ya muhumu.

Inabidi tubadilike ili kuondoa hizi kero. Hizo picha hapo juu zinasikitisha sana. Wengine wenye vifaa vya electronic hakuna kitu hapo pia hata umeme unaweza kulipuka. HII HATARI JAMANI....
 
Back
Top Bottom