Dar Tambarare: Mvua, mafuriko na Usahaulifu!

Watanzania sijui tumelishwa nini?
Wepesi wa kusahau na wagumu wa kuhoji kwa nn hii inakuwa hivi.
Wananchi mpaka tuamke na kurealise we are the ones who can make the difference, hamna kitakachofanyika...tutafanya manuevering barabarani na kupanda juu ya maboneti ya magari kila masika, kiangazi kikija tunatimuliana vumbi, barabara zitavalishwa viraka for a while until another masika and the story continues...
Mungu kwa kweli azidi kutusaidia, tuanzekufunguka ufahamu wetu na hekima zetu, tunapoona mambo yanaenda ndivyo sivyo tuwetayari kusimamia sheria (kwanza tuzijue...) na kudai maadili mema kwa watendaji...
Mtu unakesha barabarani masaa manne, kisa ni barabara imejaa maji? Honestly? Kweli and we say we are moving in the right direction, a distance of 20 minutes you spend four hours? Really??
Wachumi wanchi hii wameshawahi kufanya cost efficiency or whatever they call it kujua what is lost as result of unnecessary traffice jams...among other things?
Pale May Fair plaza - is a swampy area ndio kumejengwa na watendaji wa jiji walikuwa wanaona, wananchi walijipatia vibarua (hopefully) lakini mkondo wa maji wala njia yake hawakuzingatia now its a never ending situation mvua zikinyesha...

Aaah....kwakweli we dont have a long way to go...cause as it is we are not moving at all!!!
 
mimi ni moja waliokutana na janga lajana. Ilinichukua masaa manne kufika nyumbani badala ya nusu saa yakawaida na hivyo baada yaku negociate barabara mbalimbali. Kwa kweli kuna haja ya viongozi kuchukua hatua seriously. Vibali kwa watu kujenga hovyo kwenye njia za maji na mitaro iwe ni lazima na iwe misafi kila wakati.Majumba makubwa ya Msasani na Mikocheni yameongeza sana matatizo maji hayana njia yanazagaa hovyo.
 
Tuombe uzima tatizo hii Labda linanisubiri mimi nije nipate Urais wa nji hii !!!!!!!!!!!!!! nawahakikisheni nikipata tu Urais tatizo la sewage limekwisha!!

Nipeni kura zenu 2010, lasivyo mtaendelea kuteseka hadi basi?????
 
Kwakweli hii issue ya storm water ni tatizo kwenye jiji letu hili. Na siyo hapo na baadhi ya mikoa inayoanzakukua. Barabara nyingi zinajengwa bila mitaro madhubuti ambayo haitoshelezi na pia uchafu unaotupwa na watu kwenye hii mitaro kwa asilimia fulani inachangia kuleta mafuliko.

Kuna kitu kingine unajua yale maeneo ya mills tower, shoppers plaza etc zile sehemu zilikuwa njia za maji wakazuia sasa inaponyesha mvua kubwa maji yanakosa pa kwenda. Kwenye ujenzi wetu tunajua tu kusimamisha magholofa lakini vitu vingine kama maji machafu yataenda wapi, jengo limezuia njia ya maji je maji yakija yaendeje hayo yote si ya muhumu.

Inabidi tubadilike ili kuondoa hizi kero. Hizo picha hapo juu zinasikitisha sana. Wengine wenye vifaa vya electronic hakuna kitu hapo pia hata umeme unaweza kulipuka. HII HATARI JAMANI....
Haya ni matokeo ya ujenzi wa maghorofa marefu bila kuwa na support system ya sewage.
Vimifereji ni vilevile, unaongeza idadi ya majengo katikati ya mji, lazima vizibe.

By the way hivi storm water ni kitu gani?

Maji ya mvua ya siku moja, mnayaita storm water?

SIJUI.
 
Eneo lililopona na mafuriko ya mvua ya jana ni barabara ya kilwa (kwenda mbagala). Kutoka mivinjeni hadi mbagala ilikuwa swali kabisa. Lakini kuna aina ya ufisadi katika ujenzi wa hiyo barabara. WanaJF wenye data watupatie, inasemekana KAJIMA wao jukumu lao ni kujenga barabara tu, na kuna KAMPUNI nyingine (jina halijulikani) yenyewe itajenga mitalo. kinachoonekana mpaka sasa KAJIMA jukumu lao la awamu ya kwanza limemalizika lakini KAMPUNI inayojenga mitalo inasusua na hivyo kusababisha maji kupita juu barabarani na kuharibu baadhi ya maeneo ya barabara. Kitu cha ajabu ni kwamba, kwa nini, kampuni hiyo imeng'ang'ania kujenga mitalo wakati haina uwezo? nani mmiliki wake? KWA NINI KAJIMA WASIJENGE MITALO HIYO? Wakati kajima wamemaliza ujenzi wa barabara awamu ya kwanza (mivinjeni mpaka mbagala) kampuni inayojenga mitalo haijafika hata Mgulani JKT. Wa TZ tuna kazi kwelikweli!!!
 
Hivi mnajua maana ya mafuriko hata huko ugabuni mafuriko yanatokea mnachonishangaza ninyi mnaangalia mabaya tu basi mbona hamsemi mabarabara yanayojenwa

IPOLE,
Nakupa pole sana. tunachozungumzia ni hali mbaya tunayoiona wenyewe ambayo kama tungekuwa serious matatizo hayo yangetokomea. Jana kuna watu baada ya kumaliza shughuli zao wamefika majumbani mwao kuanzia saa 4,5 mpaka 6 usiku. Muda kama huo unatosha kukufikisha Moro kama si Dom. Sasa ndani ya jiji mtu anasafiri kwa kutumia muda mwingi kama huo wewe mwenzetu unaridhika? hali kadhalika tunapokuja makazini muda mwingi tunaumalizia kwenye foleni, hivyo kudunisha utendaji kazi. Sisi tutaendelea kusisitiza ujenzi unaozingatia 'mipango miji' na wewe endelea kushangilia barabara zinazojengwa bila kuzingatia mahitaji halisi
 
Haya ni matokeo ya ujenzi wa maghorofa marefu bila kuwa na support system ya sewage.
Vimifereji ni vilevile, unaongeza idadi ya majengo katikati ya mji, lazima vizibe.

By the way hivi storm water ni kitu gani?

Maji ya mvua ya siku moja, mnayaita storm water?

SIJUI.

Mkuu Bonni...., hilo neno "STORMWATER" ni neno la kiufundi linalotumika kuelezea/kumaanisha ni maji yanayotokana na "precipitation activity", yaani mvua. Hii inaanzia kwenye vijirasharasha mpaka kule kwenye magharika kama lile la Nuhu (Angalia: [ame=http://en.wikipedia.org/wiki/Stormwater]Stormwater - Wikipedia, the free encyclopedia[/ame])

Sasa ukirudi kwenye swala la ujenzi wa maghorofa, upanuzi wa barabara etc, hebu kwanza tujiulize:
1. Je, Tanzania maji ya mvua yanachanganywa na yale ya vyoo/domestic/commercial building effluent (hii ina maana normal usage na wakati mwingine mpaka ablution effluents)??

2. Je, Tanzania imeweka utaratibu gani katika "design standards" zake kukabiliana na hivi mvua kubwa za vipindi vifupi? Tukumbuke kuwa kuna nchi hazina mvua kama za pale "Middle East" ambapo wao wameweka catchment areas/tanks ambapo zina trap maji then kunafanyika natural flow to the oceans etc. Hii inazuia kutokea madimbwi etc; pia nchi nyingine za Ulaya na kwingineko kuna ambazo zimejenga chanels accross cities ili kupokea maji kama haya lakini pia inatumika kama mapambo ya aina flani!

3. Je, kwenye "manual ya road design" (standard specs) tuliangalia geographical nature ya Tz au tulicopy yale tuliyopewa kutoka kwa wale jamaa zetu wa Norway (ambao waliitoa ile ya BS kama ilivyo)??

Kiufundi, waTanzania tunao wataalamu wa kutosha, tatizo ni kwamba wengi wao (kama sio wote) wame ajiriwa na kampuni binafsi (kazi yako staff kutengeneza faida to the fullest to your employee at times unaiumiza nchi), baada ya kupata experience wamekimbilia kwenye ulaji bora (nje), wameamua kukubali yaishe wakajiunga na "mradi tumbo" (mawizara na taasisi za kiserikali na kuamua ku "follow the trend" ni kutafuna as and when you can, wameamua kuachana na yote na kukubali yaishe!!!

Sasa wa kusaidia hili ni vile vyombo vya regulation of the engineering inductry (NCC, ERB, ACET, CRB etc).... Tatizo ya yote haya, wakubwa wake wengi (kama sio wote) ni political appointees........

Mwisho niseme kwamba wale wanaodhani kwamba hakuna wataalamu Tanzania kweli wanaishi kwenye dunia ya kusadikika manake wangekuja waone kwa macho yao ili waweze ondoa imani potofu kwamba mpaka mtu atoke nje ya nchi ndio anajua kazi........

Naomba kuwakilisha!!!
 
Hayo magari (Read: SUVs) hayafanani na hizo barabara kamwe.
 
Lakini hili ni wakazi wa jiji la Dar ambao wamezoea ubovu na uozo. Sidhani kama kuna mkoa wowote nchini ambao wakazi wake wako so content na status quo kiasi kwamba hawawezi na hawako tayari kufikiri nje ya sanduku walimo. Matokeo yake wamezoea ujanja wa kuishi na uchafu.

Dar ni Uso wa Tanzania na ilitakiwa uwe mji wa mfano. Ina idadi kubwa ya watu wenye uelewa mkubwa kulinganisha na mikoa mingine. Ilitakiwa iwe mfano na chimbuko la vuguvugu zote za kisiasa na kimaendeleo, lakini imekuwa so disappointing. Pamoja na mambo mengine kuna hili la mismanagement ya hela wanayopewa. Kuna halmashauri za miji midogo huko mikoani zinapewa budget ndogo, lakini hali ni bora kupita dar. Hizi picha ni za katikati ya mji. Huko mitaani Sinza, Kibangu, Goba, Makongo, Mbezi si kutakuwa kunatisha?

Kinachotakiwa ni serikali kuu ichukue jukumu la kuendeleza infrastructure za Dar (maji safi na machafu; na barabara). After all, asilimia zaidi ya 80 ya mapato ya serikali hiyo hiyo inakusanywa Dar. China kuwa miaka mitano ilitenga 10% ya pato lake kuendeleza Beijing. Nadhani ni mfano tunaoweza kuiga.
 
Jamani moja ya sababu zilizokuwa zinatolewa na wananchi jana ITV ni kuwa mitaro imeziba sababu ya uchafu na serikali haiji kuzoa uchafu ndio maana. Najiuliza sisi wanachi ni watoto tusiojua kuwa uchafu ukitupwa kwenye mitaro itaziba? Mpaka tungoje serikali ije ituzolee jamani!! Ama kweli mtoto umleavyo.

Kwanza serikali ni nani? Viongozi au hata sisi wananchi ni serikali?.

Mkuu tunakatwa kodi ili hao wazee wa jiji walipwe mishahara ya kufanya kazi ikiwa ni pamoja na kuzoa taka na kuliweka jiji ktk hali ya usafi. Ni sawa kunatakiwa kuwe na ushirikiano baina ya hao wazee wa jiji (hapa naamisha wafanyakazi wa jiji) na wakazi wa jiji, ila inatakiwa kwanza wazee wa jiji waliweke jiji safi halafu wawabane wakazi kwa kuendeleza uchafu ikiwa ni pamoja na kupigwa faini n.k.
 
134768.jpg

Men, women and children all wade through a road-turned-mini river at Tandale in Dar es Salaam following heavy rains that pounded the city from yesterday morning. (Photo: Khalfan Said)
 
Mbona ni hali ya kawaida kwa siku hizi,mi naona bado tumepunjwa ,kama utatizama mabadiliko ya hali ya hewa duniani ni sehemu nyingi sana zimekumbwa na hali hiyo ,huko alikokuweko Joji Kichaka mbali ya kuwa wanajilabu wapo mbele kwa maendeleo na first aid lakini wameshindwa kuzuia mafuriko ndani ya San Fransisco New Orleans na kwengineko naona ,jukumu la serikali ni kuwajumuisha watu katika kushirikiana linapotokea jambo kama hili ,aidha ilitakiwa zionekane harakati za jeshi,polisi katika kuunganana na raia ili kusaidiana kwani mshikamano madhubuti huweza kupatikana katika mambo haya ,lakini sijui kama polisi walitoka nje. Nasema tumepunjwa ukilinganisha na nchi nyengine tunajua ikipiga sunami basi Unguja hatunayo itabakia Pemba tu ndivyo wataalamu wasemamvyo.
 
shida ni kwamba WATANZANIA tumezidi mno upole - MAFURIKO - MAJI MACHAFU - TAKATAKA ZIMEZAGAA - UMEME UNAKATWA - ETI MGAO - USAFIRI SHIDA - VIONGOZI WETU WENGI NI WASHAMBA AU WANAWAZA PESA PESA PESA TU - MWAKA 2009 BADO MAFURIKO KATIKATI YA JIJI???? SHAME! SHAME! SHAME! - HIVI KODI ZETU ZINAENDA WAPI JAMANI?? KWA KWELI INAUMA SAAAAAAAAAAAANA - MUNGU TUSAIDIE WATOTO WAKO - USIRUHUSU KUNDI DOGO LA WATU KUTUTESA KIASI HIKI - WASHINDWE NA WALEGEE
 
natamani haya mafuriko yange peleka maji yote ikulu mpaka kitandani kwake pengine angeamka huyu kizururaji.
 
Mkuu BM, hili lijimradi ndile WB wameishauri serikali ifanye audit ya nguvu, so far kimya.... nadhani wanatengeneza majibu ya kama hapo juu!!!

Du hii ni hatari yaani mpaka pressure ya watoa pesa wao wameridhika kabisa na huo utendaji. Walivyo makini kutoa sababu za kizushi ngoja tusubiri majibu watakayowapa WB
 
Duh, hizi nimekuta kule kwa Magid Mjengwa, it is more than saaad, hebu angalia ki-starlet na hio bus na surf hapo, saad manake jamaa inawezekana kabisa engines ndio hivyo tena...

mjengwa

Duh, na ndio mvua zimeanza tu, haya...
 
Hii ni new york ya Afrika hizi mvuwa ni shamra shamra za kusherehekea sikuku ya pasaka basi hata hamlijuwi hilo?? na kama hamlioni basi hamsiki ??by the way nategemea serekali itafanya jitihada ya kuomba msada ili kupatiwa ufumbuzi tatizo hili.
 
Back
Top Bottom