Dada yenu nawaomba sana ndugu zangu Msaada wenu kupata kazi Nje ya Nchi

Kuwaza kwenda nje sio kitu cha kuanzia hapa, kwa ulivyojieleza inaonesha unapitia kipindi kigumu sana

Hebu tafuta namna kwanza familia yako iishii kipindi hiki kigumu kwako, kuna fursa hapa hapa nchini unaweza kuzitumia, kwenda nje ibaki kama ndoto

Nataman kukushirikisha fursa ila nadhani kila mtu ana uono wake, kwangu mimi naziona fursa nyingi sana hapa Geita nilipo, wewe umesema upo Dar

Kuhusu kwenda nje hata mimi ni ndoto yangu siku hela zikijaa nitaenda kwanza kutembea kupitia hapa www.workaway.com

Hapo unaweza pata sehemu ya kwenda kujitolea kufanya kazi nje japo wapo wanaoweza kukulipa kidogo ukiwa unajitolea
Shukran sana Kiongozi niko tayari kwa ajili ya hizo fursa ata kwa kuja huko huko Geita niko tayari Kiongozi..niko flexible enough working in any hardship environment na kuishi popote na Mkoa wowote ule ata kama mazingira yake ni magumu kiasi gani naweza kuvumilia

Kikubwa niweze kuwasimamia hawa Yatima na Mama yangu🙏

Shukran sana🙏
 
Ukweli ni huu fatmie..kua connections za kupata kazi nje zipo, ila kwa hali uliyoeleza ni kua atokee mtu akusaidie gharama zote kuanzia kuomba visa, vibali vya kufanya kazi, passport, nauli ya ndege hadi ukifika kule, na kweli nje ya nchi kuna namna ambayo unaweza kufanikiwa ndani ya muda mfupi kama utafuata miongozo fulan na zaidi uwe na angalau mwenyeji wa kufikia iwe ndugu au employer wako awe ame arrange accomodation yako..hapa tz kwakweli hali ni ngumu, bongo michosho, hadi ukae kwenye sytem lazima connections, mwenyewe unasema ushafanya application zaidi ya 200..haya, hao ndugu wa kukusaidia wako wapi, haya, nani atakukopesha hata saivi ukimwendea, lazima atataka vitu kama rehani , pia benki napo hivyo hivyo na zaidi uwe na biashara inayo run,. Watu wanakubeza kua unataka kwenda nje, pengine ndipo riziki yako ilipo, who knows, na ni kitu ambacho umekua nacho muda mrefu, na wanawake Mungu amewapa uwezo wa ajabu wa kua na instinct, shikilia ndoto yako, lakini sio kwamba connections za kazi nchi za nje hazipo, zipo, gharama

Kama una shida kweli ondoa Ulaya na Amerika weka Asia (QATAR na U.A.E-Dubai).

Why Asia? Kazi zipo pia hakuna masharti ya ajabu ya kupata VISA kama Ulaya na Amerika.
Nashukuru sana kwa mawazo yako Kiongozi

Ninashida sana yaan saana mpaka kujitosa kuandika hapa Mtoto wakike sio jambo dogo, kutokana na tafiti ndogo nilizozifanya mitandaoni Asia wanasema Waarabu wanyanyasaji sana na malipo yao ni finyu kupita kiasi, hizo ni tafiti nilizoziona mitandaoni wakisema

Na kwa upande wa Americans opportunities ziko nyingi sana kikubwa ujitume tu na ustick kwenye malengo yako

Na kama ikiwa ngumu kwa America ntaenda ata huko Asia iwe kama starting point kwangu, naweza nikiwa huko nikapata connections za kwenda America na ikawa ni kama sehem ya kutimia kwa Ndoto zangu🙏

Naomba sana MWENYEZI MUNGU amguse mtu anisaidie kwahili na tuandikishiane nikishafika na kuanza kazi Pesa zake zote nimlipe kwa maandishi kabisa ili awe huru na apate amani ya kutodhulumiwa🙏
 
Ukweli ni huu fatmie..kua connections za kupata kazi nje zipo, ila kwa hali uliyoeleza ni kua atokee mtu akusaidie gharama zote kuanzia kuomba visa, vibali vya kufanya kazi, passport, nauli ya ndege hadi ukifika kule, na kweli nje ya nchi kuna namna ambayo unaweza kufanikiwa ndani ya muda mfupi kama utafuata miongozo fulan na zaidi uwe na angalau mwenyeji wa kufikia iwe ndugu au employer wako awe ame arrange accomodation yako..hapa tz kwakweli hali ni ngumu, bongo michosho, hadi ukae kwenye sytem lazima connections, mwenyewe unasema ushafanya application zaidi ya 200..haya, hao ndugu wa kukusaidia wako wapi, haya, nani atakukopesha hata saivi ukimwendea, lazima atataka vitu kama rehani , pia benki napo hivyo hivyo na zaidi uwe na biashara inayo run,. Watu wanakubeza kua unataka kwenda nje, pengine ndipo riziki yako ilipo, who knows, na ni kitu ambacho umekua nacho muda mrefu, na wanawake Mungu amewapa uwezo wa ajabu wa kua na instinct, shikilia ndoto yako, lakini sio kwamba connections za kazi nchi za nje hazipo, zipo, gharama
Ahsante sana kwa mawazo yako yaliyonishibisha Ubongo wangu Kiongozi🙏

Niko tayari kama nitampata mtu wa kunisaidia basi niandikishiane nae kwa maandishi na mashahidi na Mwanasheria wake juu ya gharama atakazozitumia, na nitakapofika huko nifanye kazi na kumlipa gharama zake zote

Naamini katika uwezo wangu mkubwa wa kazi na bidii ya kupambana kwa mda mfupi tu kama nitapata hiyo safari ya nje basi gharama zake zote nitamrejeshea

Ahsante sana kwa kunitia moyo najua nitafanikiwa tu na nitarudi hapa kurudisha mrejesho🙏
 
Hua nikisoma baadhi ya comments ya baadhi ya watanzania mamburura kama wewe hua naishia kuwatukana tu, mana mna haki ya kutukanwa tena matusi makubwa, yamkini wewe hapo unaongea kwa dharau kubwa hivyo na kashfa umekalisha mapumbu yako mazito na manene kwa mashemeji zako, ukiamka asubuhi unakuta chai mezani, na huwazi kodi ya nyumba, bili za maji, bili za umeme, matibabu ya hospital mtu akiumwa, kifupi hauwazi chochote, na kama hauwazi chochote ndipo unapata guts za kuongea pumba na kashfa, pathetic fool !
Ndio mana ikaitwa JF sio lazima kila mtu afikirie kama unavyofikiria ww,
 
Wakubwa Shikaamooni
Wadogo zangu Habari zenu.

Mimi ni Mwanamke sijaolewa na sina watoto.

Naishi na kumlea Mama yangu Mzazi ambae ni mtu mzima ananitegemea kwa kila kitu na watoto wa Marehem Kaka yangu ambao walikufa siku moja kwa ajali na Kaka yangu hao watoto wako 3 Yatima, wananitegea kuanzia kula yao, kusoma kwao, kuumwa kwao na kila kitu Bills za maji, umeme na mahitaji mengine yote ya kibinadamu, naishi nao pamoja na Mama yangu Mzazi (extended family) mapambano yangu yote ni kwa ajili yao.

Nimeamua kuja hapa Jukwaani nikiamini kua kuna WaTanzania wengi sana wanaishi Nje ya Nchi na wao waliwezeshwa au kushikwa mkono na watu na wao pia wanaweza kutushika mkono nasisi

Katika harakati za mapambano ya Maisha Nilijaribu kulima Vitunguu Maji, Pamoja na Nyanya huku nikiwa nafanya kazi lakini kilimo hakikua na faida kwangu kilinipatia hasara sana kwakua sikua na mda wa kutosha wa kufanya closely monitoring nikachana nacho

Nianze na kuzungumza yafuatayo:-Mimi kwetu ndio nategemewa kwa kila kitu kwenye familia na niko kwenye wakati mgumu saana ndugu zangu, YAAN NIKO KWENYE WAKATI MGUMU MNOO DADA YENU😭😭😭 ITOSHE TU KUSEMA MWENYEZI MUNGU PEKEE NDIE ANAJUA NAPITIA KIPINDI GANI nawaomba saana mnisaidie najua MWENYEZI MUNGU husaidia watu kupitia watu 🙏 kwasasa sina kazi na sina pesa na ila nna uzoefu mkubwa sana wa kazi pamoja na uzoefu wa kutosha juu ya matumizi ya Computer

Nimeshasimamia miradi mbali mbali na nimeshakua Project Manager, Project Coordinator, Field Manager, Field Officer, Case Management Officer, Child Protection Coordinator,Social worker, Administrative Officer, Marketing Officer, Communication Officer, kwenye miradi mbali mbali ya miongoni mwa hayo mashirika

Elimu yangu ni Degree ya Social work nina uzoefu wa kufanya kazi kwenye mashirika mbali mbali ya Kimataifa yanayohusu juu ya Suala zima la ULINZI WA WATOTO
(Child Protection) kwa mda wa miaka 8 kwa miaka bahati mbaya mkataba wangu uliisha 31,Dec 2020 kutokana na funds kuisha hii imetokana na Athari ya Janga kubwa la Corona
( Covid-19)

Tangu November 2020, nimekua nikifanya Applications mbalimbali nionapo matangazo ya kazi lakini sijafanikiwa kuitwa popote pale. Kuomba kazi ni jambo moja na kuitwa ni jambo lingine

Tangu nilipokua mtoto nilikua na ndoto ya kwenda kuishi Nchi zifuatazo:- Switzland, UK, USA, Canada na German kwa lengo la kufanya kazi za halali zikiwemo (Black Jobs ) kikubwa nipate rizki ya halali tu na kufanya saving kwa baadae niweze kuja kuwekeza Tanzania.

Nawaomba sana, Nawaomba sana, Nawaomba saana kwa yoyote mwenye utayari wa kunisaidia kuishi Nchi mojawapo kati ya hizo tafadhali naomba sana anisaidie lengo langu ni kuishi kwa mda wa Miaka 5 tu tukijaaliwa Uhai na ndoto zangu zitakua zimeshatimia kwa target niliyojiwekea nikipata hiyo fursa ya kwenda kuishi kati ya hizo Nchi nitajituma saana na kufanya kazi kwa bidii kubwa ili kuweza kutimiliza malengo yangu

Ikiwemo kutuma Pesa nyumbani kwa ajili ya mahitaji ya Mama na hao Watoto yatima

Afya ya Mwili na Akili:- Namshukuru MWENYEZI MUNGU sina matatizo yoyote yale ya kiafya wala ya Viungo

Makazi:- Naishi Dar-es-Salaam

Kwa maswali yoyote au kama utahitaji my Personal details tafadhali naomba uni PM nitakua tayari kushare nawewe utakaenisaidia, Nawashukuru sana.

Nawaomba sana mnisaidie Dada yenu, nawaomba mnistiri jaman na MWENYEZI MUNGU atawastiri kesho Mbinguni🙏

MWENYEZI MUNGU awaguse muweze kunisaidia🙏

Ahsanteni sana.
Dah😭umeongea kwa uchungu sana mm kama mwanamke mwenzako nimeguswa sana. Connection za kazi sina ila ningekua nazo ningekusaidia

Vip umeshapata kazi mpaka sasa????ushapata yoyote aliekusaidia kupata kazi??

Ingia PM yako nikutumie ata Laki 1 niliyojaaliwa nayo kwakua uko Mama pamoja na Mayatima hiyo ni sadaka yangu kwako najua sio pesa kubwa ila kidogo itakusoheza

Uko kwenye maombi yangu, na hapa ni mahali sahihi naamini wenye nafasi za kuweza kukusaidia basi watakushika mkono na kukusaidia, JF kuna watu wenye utu sana na na wenye kujitoa kwa ajili ya watu. Usikate tamaa unaonyesha ww ni mpambanaji sana endelea kupambana usirudi nyuma na utafanikiwa Mungu ni wetu sote. Ingia PM yako Dada, Pole sana utafanikiwa na utanyanyuka tena
 
Fatmie ajira za majuu sio jambo rahisi mkuu na Zaidi kwa kukurupuka. Ningekushauri tafuta plan B kujaribu kujikwamua alau kwa sasa mengine utapanga mbeleni.
Ikiwa unaona Ajira kwenye fani yako imekua ngumu Jaribu kufikiria nje ya Box Mkuu
 
Nashukuru sana kwa mawazo yako mazuri yenye faraja, naomba nisaidie nipate kazi ata apa ndani ya Nchi maana nimeshafanya Applications saana bila mafanikio, Ahsante
Kama ni kutoitwa kwenye interview inategemea na uandishi wako wa barua ya maombi, kwa hiyo CV yako ulipopita tu ipo vizuri.
Kama upo kwenye whatsapp ingia kwenye web ya ajiraleo kisha utakutana na magroup yanayotoa taarifa za ajira kila siku. Social work nafasi huwa zinatangazwa sana.
Yawezekana uandishi wa barua na ulivyoiweandika tu CV yako, kama hadi kwenye interview huwa unaitwa ila huchaguliwi hiyo ni issue nyingine ila kama huitwi tu kwenye interview ntakuonesha sample ya barua na cv
 
Mwaka huu huwezi kwenda nje sababu ya Corona ila kuanzia mwakani na kuendelea lazima utapanda pipa tu.
Endelea kuandaa passport n.k
Corona na usumbufu wa chanjo, vikwazo vya kusafiri, uchumi kuvurugika vyote hivi vimefanya mwaka huu uwe mbaya.
 
Shukrani sana kwa faraja🙏 nitafuata ushauri wako kuhusiana na Passport Ubarikiwe sana
 
Kama ni kutoitwa kwenye interview inategemea na uandishi wako wa barua ya maombi, kwa hiyo CV yako ulipopita tu ipo vizuri.
Kama upo kwenye whatsapp ingia kwenye web ya ajiraleo kisha utakutana na magroup yanayotoa taarifa za ajira kila siku. Social work nafasi huwa zinatangazwa sana.
Yawezekana uandishi wa barua na ulivyoiweandika tu CV yako, kama hadi kwenye interview huwa unaitwa ila huchaguliwi hiyo ni issue nyingine ila kama huitwi tu kwenye interview ntakuonesha sample ya barua na cv
Shukran sana kwa mawazo yako
 
Dah😭umeongea kwa uchungu sana mm kama mwanamke mwenzako nimeguswa sana. Connection za kazi sina ila ningekua nazo ningekusaidia

Vip umeshapata kazi mpaka sasa????ushapata yoyote aliekusaidia kupata kazi??

Ingia PM yako nikutumie ata Laki 1 niliyojaaliwa nayo kwakua uko Mama pamoja na Mayatima hiyo ni sadaka yangu kwako najua sio pesa kubwa ila kidogo itakusoheza

Uko kwenye maombi yangu, na hapa ni mahali sahihi naamini wenye nafasi za kuweza kukusaidia basi watakushika mkono na kukusaidia, JF kuna watu wenye utu sana na na wenye kujitoa kwa ajili ya watu. Usikate tamaa unaonyesha ww ni mpambanaji sana endelea kupambana usirudi nyuma na utafanikiwa Mungu ni wetu sote. Ingia PM yako Dada, Pole sana utafanikiwa na utanyanyuka tena
Sijui ata niandike nini kuweza kuonyesha shukran zangu za dhati kwako, najaribu kutafuta maneno mazuri nakosa naona yote hayatoshelezi wema wako kwangu, Shukran sana kwa support yako uliyonipatia, MUNGU akulipe na akutimizie mahitaji yako na kwakila uliombalo akukamilishie nashukuru sana ndugu yangu, ur a true definition of a Lady ( Womens empowering or lifting each other ) hujui tu umenigusa kiasi gani lakin malipo yako utayapata nakushukuru sana Pesa niliipata ontime kabisa ikanisogeza kwenye Bills kama Luku na Maji pamoja na Iftari, Uzidi kuongezewa kwa pale ulipopunguza hakika haujapoteza ila umewekeza na malipo makubwa utayapata🙏
 
Fatmie ajira za majuu sio jambo rahisi mkuu na Zaidi kwa kukurupuka. Ningekushauri tafuta plan B kujaribu kujikwamua alau kwa sasa mengine utapanga mbeleni.
Ikiwa unaona Ajira kwenye fani yako imekua ngumu Jaribu kufikiria nje ya Box Mkuu
Shukran sana kwa mawazo yako
 
Habarini Wapendwa, mpaka sasa sijafanikiwa kupata kazi Nchini mwenye kuweza kuwa sehem ya msaada kwangu naomba anisaidie hali inazidi kua mbaya

Marnah nakushukuru kwa Msaada wako wa Pesa taslimu Shilingi Laki 1 ilinisaidia saana nakosa nisemeje sikujui na haunijui lakin hukutaka kuhoji chochote zaidi ya kunisaidia malipo yako utayapata na uzidi kuongezewa pale ulipopunguza🙏

Bado nahitaji kazi ndugu zangu nawaomba
 
Kama unataka kazi za Dubai, Oman, Qatar pitia hizi page zipo Facebook huwa wanapost mara kwa mara ajira zilizopo huko na kuwasafirisha wafanyakazi baada ya Interview.

1. Everlast - Recruitment Service Kenya
2. Elmvale Agency
3. The Job Centre - Malawi

Hizi zote zipo nchi jirani ila Watanzania wanaoomba pia huwa wanachukuliwa.
 
Shukran sana nazipitia kuanzia sasa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom