Kama kuna kipindi Muhimu katika siasa za CHADEMA Basi ni hiki, Uamuzi wa CUF, NCCR,TLP,UMD wa Kumuandikia Baruwa Mhe Mbowe na Kumuomba awashirikishe katika Kambi ni Ujasiri na Ukomavu wa Kisiasa wa Vyama hivyo nasema Hongera hAMAD rASHID na Viongozi wa Kambi ndogo, Ushauri wangu kwa Mhe Mbowe kuwa jasiri yasahau ya Nyuma weka Maslahi ya Kambi Mbele ubinafsi utupe mbali, nyosha Mikono yako uwapokee wenzako kwania safi ufanmye nao kazi kwaaslahi ya Watanzania Wanyonge walio wengi waliokandamizwa na CCM, vyenginevyo ukiwapuuza na Kuwakatalia wenzako ukasahabikia Utengano na kusaikiliza Kiburi cha Wapambe wako basi majuto yatakuja baadae. nchi hii haiwezi kukombolewa na Chama Kimoja bali vyama vyote dhidi ya CCM.
Nakuomba tena Mwenyekiti Mbowe tujengee historia Mpya ya Upinzani ndani ya Mkutano Huu unaoanza sasa ndani ya Bunge. DAMU za Mashujaa waliodhulumiwa ARUSHA zinataka Kutetewa na zile zilizopotezwa kila palipo na wanamageuzi nazo zinataka Kuenziwa.