CUF sasa wawapigia magoti CHADEMA

Mmhhh! Huu ushirikiano ni wa mashaka sana, maana hawa CUF hawaeleweki vizuri, muda flani kama kweli muda kama sio!!!
 
Wewe Chadema ni nani mpaka mimi nikuite msomi wala mimi siitaji kujua umesoma wapi. mimi sijakujibu wewe nashangaa unafata post yangu mimi kama sina akili timamu sawa nadhani wewe ndani ya Chadema ni loose ball Meretricis..unataka kufokea watu utadhani JF ya baba ako.
Hivi kuwa msomi kama unavyosema amesoma UDSM hadi niwe kiongozi CDM, toka usingizini hujui hata ku-argue na hoja zako za usomi.
 
Mkuu,
Hapo red
Ushabiki mwengine hauna maana.
Lugha hii haisaidii katika kuwaunganisha wananchi.
Hata kama wewe ni CHADEMA, huisaidii CHADEMA kwa matumizi ya lugha kama hii.
CDM wanahitaji kila nguvu itakayokuja upande wao.
Fikirieni kabla ya kuandika, kusema. Busara wana chadema.

Nakubaliana na wewe kiasi fulani. Wasi wasi wangu ni kwamba hivi ni kweli wanataka kuunganisha nguvu na sio ku-divide? Why now? Nini ambacho wame-learn baada yakupinga mawazo yao kwa muda mrefu e.g. kumpigia kura spika etc. Kila kitu kina consequences jamani, kama umeshindwa kuonyesha uaminifu kwenye maamuzi yaliyopita nafikiri hauwezi kulaumu kama wenzako hawatakuamini kwenye maamuzi yajayo". In other words, whatever CDM decides nakifikiri CUF na TLP hawawezi kulaumu kwasababu ya misimamo yao walioonyesha before.
 
Originally Posted by ritz:
Kweli Chadema viongozi wake ni
wasomi? ni viongozi wawili ndio
wasomi ZITTO na LISU ndio
wamesoma UNIVERSITY OF DAR ES
SALAAM wengine kama watakuwa
wamesoma basi vyuo vya kata

CCM Wamesoma wapi?! Sio palepale SHAMBA LA BIBI!?
 
Kuna haja ya kuchangamana nao bse lengo ni kujenga nchi sio kubomoa
ni kweli mkuu ila sio kuchangamana na CUF ya leo ambayo imeshaonja hatamu.hivo kila kitakachojadiliwa upinzani CUF wanaweza toa siri kwa greenguard.
 
1.Ibrahim lipumba UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
2.Juma Duni UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
3.Ismail Jussa UNIVERSITY OF HULL CITY. UK
4.Hamad Rashid UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
5.Julius Mtatiro UNIVERSITY OF DAR ES SALAA
6.Maalim seif UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
hiyo ndio safu ya viongozi wa CUF sasa sijui utasilimu dini kama ulivyosema..basi kama uwezi kusilimu nipe tig...unadhani watu wote wajinga kama wewe kwanza na wasiwasi na Elimu yako kama umesoma chuo basi chuo cha kata kama viongozi wako kina mbowe na wenzake..Viongozi wasomi Chadema ni wawili tu ZITTO na LISU..UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM.

Makokoto kweli mpo wengi. Mwenyewe unaikubali UD eeh? Usiposoma pale basi wewe sio msomi. Kaah!
 
Wewe unajua kwa nini SABODO kada CCM anawapa Chadema pesa? Muhindi mtu hatari mtakuja juta. Watch out!!

ndugu,
yaelekea wewe ni mdogo sana wa mawazo, au hujui unaloelea hapa.
utambue kuwa SABODO na RA ni watu wawili na tofauti kabisa na wala dhamira zao haziwezi kutumika kuionya CDM hata chembe na unatakiwa utambue yafuatayo:
* RA ni haramia, mafia na fisadi anayedhamini kundi lenye mwelekeo kama yeye na faida kwake -yaani CCM. hili halihitaji malaika au digrii kulielewa.
* SABODO ni mdhamini wa demokrasia ya umma na kutetea haki, na hili amelifanya toka enzi za Nyerere, -ndio maana amekuwa pia rafiki wa karibu sana wa baba wa taifa, alimtengenezea hadi sanamu!
* wakati RA anapambana na umma ili kupora rasilimali, uhai na ustawi wa taifa, kama DOWANS, madini nk, SABODO anapoteza rasilimali zake kustawisha taifa.
* RA ni tapeli, RABODO ni mwadilifu.

bila shaka umepata picha halisi.
CDM kama chama chenyd dira makini, vikao ndo vitaamua, ni tafauti na CCM inayokufa na RA wao.
 
Wapinzani wamsihi Mbowe

Kambi ya upinzani isiyo rasmi bungeni imemuandikia barua Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuomba wachaguliwe kuunda Baraza la Mwaziri Kivuli kwenye Bunge ili waweze kushirikiana kwa dhati kama kambi ya upinzani.

Katika barua ya kambi hiyo iliyosainiwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Hamad Rashid na katibu wake David Kafulila kwenda kwa Mwenyekiti wa Chadema wamesema wanaomba ushirikiano huo uanze kwenye Mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza Februari mwaka huu.

Kambi hiyo ilimsihi Mbowe kuunda kambi ya upinzani imara ikishirikisha vyama vyote vya upinzani ili kuimarisha nguvu ya upinzani bungeni na kuibana serikali ya CCM kwa pamoja.

Vyama vilivyotoa ombi hilo ni CUF chenye wabunge 33, NCCR Mageuzi chenye wabunge wanne, TLP mbunge mmoja na UDP mbunge mmoja wakati Chadema kikiwa na wabunge 47.

Chadema ambacho ndicho chama kikuu cha upinzani kimeunda kambi ya upinzani peke yake huku mwenyekiti wake akichaguliwa kuwa kiongozi wa kambi hiyo na nafasi nyingine za mawaziri kivuli zikijazwa na wabunge wa chama hicho pekee…..

Habari zaidi katika Mwananchi Jumapili.

Je Huyo Hamad Rashid ameishavunja hiyo kambi yake?

Amakweli siasa hazina adui wa kudumu.

Mbowe mimi ni chadema sugu. Nakuomba wakubalie vyama vyote vya upinzani muunde upinzani wenye nguvu ili muwa na sauti hasa inje ya nchi na ndani ya nchi pia. Kumbuka umoja ni nguvu utengani ni dhaifu.
 
ndugu,
yaelekea wewe ni mdogo sana wa mawazo, au hujui unaloelea hapa.
utambue kuwa SABODO na RA ni watu wawili na tofauti kabisa na wala dhamira zao haziwezi kutumika kuionya CDM hata chembe na unatakiwa utambue yafuatayo:
* RA ni haramia, mafia na fisadi anayedhamini kundi lenye mwelekeo kama yeye na faida kwake -yaani CCM. hili halihitaji malaika au digrii kulielewa.
* SABODO ni mdhamini wa demokrasia ya umma na kutetea haki, na hili amelifanya toka enzi za Nyerere, -ndio maana amekuwa pia rafiki wa karibu sana wa baba wa taifa, alimtengenezea hadi sanamu!
* wakati RA anapambana na umma ili kupora rasilimali, uhai na ustawi wa taifa, kama DOWANS, madini nk, SABODO anapoteza rasilimali zake kustawisha taifa.
* RA ni tapeli, RABODO ni mwadilifu.

bila shaka umepata picha halisi.
CDM kama chama chenyd dira makini, vikao ndo vitaamua, ni tafauti na CCM inayokufa na RA wao.

umjui SABODO wewe kaa kimya (WHITE SUGAR) madude
 
waacheni waje kwani cdm ni watu makini kama usalama walinywea waliporushiwa dongo la kuchakachua wamefyata mkia hao cuf na nccr,TLP waje tu
 
Kama kuna kipindi Muhimu katika siasa za CHADEMA Basi ni hiki, Uamuzi wa CUF, NCCR,TLP,UMD wa Kumuandikia Baruwa Mhe Mbowe na Kumuomba awashirikishe katika Kambi ni Ujasiri na Ukomavu wa Kisiasa wa Vyama hivyo nasema Hongera hAMAD rASHID na Viongozi wa Kambi ndogo, Ushauri wangu kwa Mhe Mbowe kuwa jasiri yasahau ya Nyuma weka Maslahi ya Kambi Mbele ubinafsi utupe mbali, nyosha Mikono yako uwapokee wenzako kwania safi ufanmye nao kazi kwaaslahi ya Watanzania Wanyonge walio wengi waliokandamizwa na CCM, vyenginevyo ukiwapuuza na Kuwakatalia wenzako ukasahabikia Utengano na kusaikiliza Kiburi cha Wapambe wako basi majuto yatakuja baadae. nchi hii haiwezi kukombolewa na Chama Kimoja bali vyama vyote dhidi ya CCM.
Nakuomba tena Mwenyekiti Mbowe tujengee historia Mpya ya Upinzani ndani ya Mkutano Huu unaoanza sasa ndani ya Bunge. DAMU za Mashujaa waliodhulumiwa ARUSHA zinataka Kutetewa na zile zilizopotezwa kila palipo na wanamageuzi nazo zinataka Kuenziwa.

Pamoja na maneno yako matamu lakini viongozi wa CDM wakidaganganyika na kuwasikiliza watu wenye maoni kama yako watafanya makosa ambayo watakuja yajutia. Hivi hawa wapinzani wakiungana wote watapata idadi ambayo itawazidi CCM? jibu ni hapana. Sasa wanaungana ili iweje? Jambo ambalo watanzania wanataka kuona ni viongozi watakao watumika ili kutetea maslahi yao basi. Sasa haijalishi watetezi hao watatoka chama gani cha siasa. Chama au mbunge atakaye tetea maslahi ya wananchi ndiye mwenye umuhimu kwa siasa za sasa za nchi hii. CDM wakiungana na hawa wapinzani wengine kwa mtazamo wangu watakuwa wanafanya upumbavu tena wa mwaka.
 
Makokoto kweli mpo wengi. Mwenyewe unaikubali UD eeh? Usiposoma pale basi wewe sio msomi. Kaah![/QUOTE
RANKING UNIVERSITY IN AFRICA TOP 100.
13.UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
90. SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE www.4icu.org
kama Tanzania kwenye vyuo 100 bora Africa tuna vyuo wiwili tu unadhani wasomi wapo tanzania? mnasoma vyuo vya kata mnataka muitwe wasomi waliofanya utafiti wakaweka Ranking Tanzania tukapewa vyuo viwili sio wajinga wanaosoma hivyo vyuo ni wasomi, wewe unasoma Journalism pale Ilala unataka tukuite msomi..kweli makokoto wapo wengi na vyuo vyao vya KATA
 
Wapinzani wamsihi Mbowe

Kambi ya upinzani isiyo rasmi bungeni imemuandikia barua Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuomba wachaguliwe kuunda Baraza la Mwaziri Kivuli kwenye Bunge ili waweze kushirikiana kwa dhati kama kambi ya upinzani.

Katika barua ya kambi hiyo iliyosainiwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Hamad Rashid na katibu wake David Kafulila kwenda kwa Mwenyekiti wa Chadema wamesema wanaomba ushirikiano huo uanze kwenye Mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza Februari mwaka huu.

Kambi hiyo ilimsihi Mbowe kuunda kambi ya upinzani imara ikishirikisha vyama vyote vya upinzani ili kuimarisha nguvu ya upinzani bungeni na kuibana serikali ya CCM kwa pamoja.

Vyama vilivyotoa ombi hilo ni CUF chenye wabunge 33, NCCR Mageuzi chenye wabunge wanne, TLP mbunge mmoja na UDP mbunge mmoja wakati Chadema kikiwa na wabunge 47.

Chadema ambacho ndicho chama kikuu cha upinzani kimeunda kambi ya upinzani peke yake huku mwenyekiti wake akichaguliwa kuwa kiongozi wa kambi hiyo na nafasi nyingine za mawaziri kivuli zikijazwa na wabunge wa chama hicho pekee…..

Habari zaidi katika Mwananchi Jumapili.

[/QUOT]
Mimi naunga mkono wazo la Mh. Rashid la kuunganisha nguvu ili wapinzani tuweze kuibana kisawasawa serikali wala sioni hatari yoyote kwa CHADEMA katika hili. Ni lazima nikiri kuwa mimi, licha ya kuwa CHADEMA damu namheshimu sana Mheshimiwa huyu hasa alipokuwa akitoa hoja zake zilizokuwa zikisheheni mantiki katika Bunge lililopita kwa hiyo kurejea kwake katika kambi rasmi ya upinzani Bungeni kutachangamsha kwelikweli mijadala. He is the right person at the wrong place (CUF) na kabla ya uchaguzi nilikuwa naombea across CHADEMA kumpa tafu Dr. Slaa katika harakati za kuibomoa CCM na nilisikitika kweli niliposikia alikataa. I can't imagine scenario ya Bunge la safari hii upinzani ukiwa na vichwa kama Mbowe, Tundu Lisu, Hamad Rashid, Kafulila, Zitto, Godbless Lema na wengine. Naona patakuwa hapatoshi.
God Bless Tanzania
 
Hawa CUF wameshapoteza muelekeo pale walipoamua walioamua kuunda Serikali ya mseto na Chama Cha Mafisadi sasa hivi CUF ni kitengo cha CCM kama ilivyo UWT na vitengo vingine vya CCM. Wanataka wapewe nafasi hii ili waendelee kuivuruga CHADEMA na kuipa jina baya mbele ya Watanzania. CHADEMA msifanye makosa ya kuwashirikisha CUF, NCCR Mageuzi na TLP katika baraza lenu la Mawaziri kivuli Bungeni.
 
CUF waogopeni kama ukoma, Hilo n granade la CCM. They will use you (CDM) mkishalikoroga watarudi kwa bwana zao CCM
 
.....!!!!!!!!!!!!????????????? tuna maswali mengi ya kujiuliza kuhusu CUF, moja kubwa, si wapinzani kweli kweli, CCM B, hii ipo waziii,
they are not serious with opposition, BUT, BUT, BUT, let us allow Mbowe & CDM wawaruhusu waingie upinzani, no problem, wakubali ombi la Rashid
we will monitor them with magnified lenses Microscope, wakiwa hawaeleweki, as usual makamanda wa CDM FUKUZA CUF no discussions
 
.....!!!!!!!!!!!!????????????? tuna maswali mengi ya kujiuliza kuhusu CUF, moja kubwa, si wapinzani kweli kweli, CCM B, hii ipo waziwe will monitor them with magnified lenses Microscope, wakiwa hawaeleweki, as usual makamanda wa CDM FUKUZA CUF no discussions

Nilikuwa na jaribu kujiuliza hivi hawa CUF wanatakiwa wafanye kipi zaidi ya haya waliokwisha ya fanya ili wawe wakiwa hawaeleweweki?

Wasipewe kwanza kwa sasa, tuwaone kwenye bunge la mwezi wa pili mijadala yao, inabase wapi na wanachangia vipi kwenye hoja muhimu, especially hoja zitakazokuwepo kama dowans na mabadiliko ya katiba. Tayari wamefanya uchafuzi kwenye uchaguzi wa meya Mwanza kwa kusurpport CCM na pia kama walivyoungana na CCM kozomea na kureplace seat za CDM walivyotoka bungeni. Hawa watu wametumwa ili kudhoofisha nguvu ya chadema kwa sasa. Tunaomba clarification ya kikao walichokaa mpaka kufikia kuandika hiyo barua, au mtu mmoja tu ameamua kwa niaba na hiyo ni hatari kwa CDM kama haitaangaliwa kwa mapana.
 
Back
Top Bottom