CUF sasa wawapigia magoti CHADEMA

CUF sasa wawapigia magoti CHADEMA

.....!!!!!!!!!!!!????????????? tuna maswali mengi ya kujiuliza kuhusu CUF, moja kubwa, si wapinzani kweli kweli, CCM B, hii ipo waziii,
they are not serious with opposition, BUT, BUT, BUT, let us allow Mbowe & CDM wawaruhusu waingie upinzani, no problem, wakubali ombi la Rashid
we will monitor them with magnified lenses Microscope, wakiwa hawaeleweki, as usual makamanda wa CDM FUKUZA CUF no discussions



Hivi kanuni zinasemaje kuhusu kuwafukuza wakionekana wanaasi, maana kisije kikawa kitanzi kwa CDM kwamba labda mpaka maamuzi ya Spika. Spika akikataa kwamba hakuna kufukuzwa basi wanaweza kubaki milele. Nakumbuka incidence ya Cheyo mpaka Speaker Sita alivyoitolea ufafanuzi kuwa jamaa amekyuka ndio alitemwa kama waziri kivuri baada ya kuunga bajeti ya ccm. Lakini pia ilifuatana na hekima na maono ya Speaker Sita. Hebu kumbuka mwaka 2005 Mrema alitangaza kumtema uanachama wa TLP bwana Ngawaiya, na kwa kanuni ilipaswa atemwe na Ubunge pia, lakini Speaker wa wakati huo, mzee Msekwa alikataa na akipangana na kanuni za bunge na Ngawaiya aliendelea kuwa Mbunge. Sasa hilo pia la kuliangalia kwa watalaam wa Sheria na huyu Speaker kuwadi wa Mafisadi Anna Makinda, kinaweza kuwa kitanzi kwa Chadema. Kuwa katika Safe side ni kuwakataa kabisa
 
CUF... they green snake in green grass watchout!!!!!!!!!.................CDM
 
Makokoto kweli mpo wengi. Mwenyewe unaikubali UD eeh? Usiposoma pale basi wewe sio msomi. Kaah![/QUOTE
RANKING UNIVERSITY IN AFRICA TOP 100.
13.UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
90. SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE 4 International Colleges & Universities | World Universities Web Ranking
kama Tanzania kwenye vyuo 100 bora Africa tuna vyuo wiwili tu unadhani wasomi wapo tanzania? mnasoma vyuo vya kata mnataka muitwe wasomi waliofanya utafiti wakaweka Ranking Tanzania tukapewa vyuo viwili sio wajinga wanaosoma hivyo vyuo ni wasomi, wewe unasoma Journalism pale Ilala unataka tukuite msomi..kweli makokoto wapo wengi na vyuo vyao vya KATA

Kwa taarifa yako Graduate wa UD na SUA wananafasi kubwa ya kupata International Scholarship nyingi zaidi ya hivyo vyuo vingine vilivyoko huko Tanzania. We speaking through experience. Ni ukweli usipingika kuwa cream ya form six kwa asilimia kubwa imekuwa ikienda, UD, SUA na MZUMBE kwa muda mrefu labda miaka ya sasa baada ya kuongezeka idadi ya wanafunzi na vyuo vya kata
 
Hivi kanuni zinasemaje kuhusu kuwafukuza wakionekana wanaasi, maana kisije kikawa kitanzi kwa CDM kwamba labda mpaka maamuzi ya Spika. Spika akikataa kwamba hakuna kufukuzwa basi wanaweza kubaki milele. Nakumbuka incidence ya Cheyo mpaka Speaker Sita alivyoitolea ufafanuzi kuwa jamaa amekyuka ndio alitemwa kama waziri kivuri baada ya kuunga bajeti ya ccm. Lakini pia ilifuatana na hekima na maono ya Speaker Sita. Hebu kumbuka mwaka 2005 Mrema alitangaza kumtema uanachama wa TLP bwana Ngawaiya, na kwa kanuni ilipaswa atemwe na Ubunge pia, lakini Speaker wa wakati huo, mzee Msekwa alikataa na akipangana na kanuni za bunge na Ngawaiya aliendelea kuwa Mbunge. Sasa hilo pia la kuliangalia kwa watalaam wa Sheria na huyu Speaker kuwadi wa Mafisadi Anna Makinda, kinaweza kuwa kitanzi kwa Chadema. Kuwa katika Safe side ni kuwakataa kabisa

remember no rules that can override opposition selection, once opposition selected shadow minister(s) and the shadow minister seems
to misbehave is only opposition will kick him out, not Speaker, hakuchaguliwa na speaker ni kambi ya upinzani itamfukuza, speaker
hana power hapo, RULE OF THUMB, waliokuweka if u go against them wanakutoa period
 
Wapinzani wamsihi Mbowe

Kambi ya upinzani isiyo rasmi bungeni imemuandikia barua Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuomba wachaguliwe kuunda Baraza la Mwaziri Kivuli kwenye Bunge ili waweze kushirikiana kwa dhati kama kambi ya upinzani.

Katika barua ya kambi hiyo iliyosainiwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Hamad Rashid na katibu wake David Kafulila kwenda kwa Mwenyekiti wa Chadema wamesema wanaomba ushirikiano huo uanze kwenye Mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza Februari mwaka huu.

Kambi hiyo ilimsihi Mbowe kuunda kambi ya upinzani imara ikishirikisha vyama vyote vya upinzani ili kuimarisha nguvu ya upinzani bungeni na kuibana serikali ya CCM kwa pamoja.

Vyama vilivyotoa ombi hilo ni CUF chenye wabunge 33, NCCR Mageuzi chenye wabunge wanne, TLP mbunge mmoja na UDP mbunge mmoja wakati Chadema kikiwa na wabunge 47.

Chadema ambacho ndicho chama kikuu cha upinzani kimeunda kambi ya upinzani peke yake huku mwenyekiti wake akichaguliwa kuwa kiongozi wa kambi hiyo na nafasi nyingine za mawaziri kivuli zikijazwa na wabunge wa chama hicho pekee…..


Habari zaidi katika Mwananchi Jumapili.


Hawa CUF si ndio walikuwa wanataka kuanzisha upinzani wao bungeni? Imeishia wapi? Sasa hivi inaonekana Chadema wawe makini kwani CUF na TLP wanaweza wakawa vyanzo wa drama katika upinzani...kweli hatuwahitaji...wananchi wata judge vitendo vyao na hukumu inatolewa kila siku....
 
Msimamo wa vyama vingine vya upinzani ulijionyesha waziwazi wakati wa kumchagua spika na naibu wake na wakati wa hotuba ya jk ya kufungua bunge. Chadema msipoteze muda kuunda kambi ya upinzani na vyama vinavyobadilika kama vinyonga. Achana navyo. Sijui kama watu wanajua vizuri kwamba cuf ya sasa ndiyo ccm B? Watanzania tuna imani na kambi ya upinzani iliyoundwa na cdm.
 
huu ni mtihani mkubwa sana kwa CHADEMA. maamuzi ya kuwashirikisha CUF na wenzake inaweza ikawa faida kwa kambi ya upinzani au hasara. Ila napatwa na wasiwasi sana na CUF wakati wa uchaguzi wa spika na naibu wake walisema wamepewa maelekezo toka zanzibar kwamba kwa kuwa wameungana na CCM kwa upande wa Zanzibar basi wao ni serikali na hawana budi kuiunga CCM bara. Swali kwani ule muungano wao na CCM Zanzibar umekwisha?kama vp tuwateme labda waje na jipya litalotuingia akilini na sii kukurupuka na kutaka kuungana na washindi wa kila upande. pia ni lazima watueleze dhamira yachama chao.je wao wamelenga kuungana na washindi tu?? au ni kupigania na kutetea haki?
 
Hamad Rashid alijiharibia mwenyewe kwa jinsi alivyoonyesha jazba siku ya mdahalo na kuonyesha kwamba ana plan mbadala. Mimi niko na wasi wasi juu ya dhamira ya CUF na vile vile unahitajika ufafanuzi wa kina juu ya jinsi watakavyotekeleza majukumu yao wakati katika sehemu nyingine ya muungano wao ni sehemu ya serikali.
 
Jamani mimi mwenzenu naona hivi:
Hii hoja ya kuungana ili kupata nguvu ya upinzani bungeni ni ya msingi sana.Ila kuna mambo ya msingi ya kuamua kabla ya kufanya muungano huo. Ningeona kina CUF wameanza kuamka kama tu wangetangaza rasmi kuiua hiyo kambi yao ISIYO RASMI ya kisaliti then ndiyo waombe kujiunga na Wanaume. Huwezi kujiunga na chama kingine wakati una kadi ya chama kingine.Ni usaliti,ni makosa kisheria na unaweza kugombanisha watu! Kama wameona umuhimu wabwage msimamo wao uliolenga KUDHOOFISHA nguvu za UPINZANI then wajitwishe msimamo wa kiume wa KUIMARISHA UPINZANI.Thats it!Vinginevyo ni hatari kushirikiana na mtu mwenye misimamo miwili!........No Offence
 
Mimi naona bora wawakubalie ili wawe na nguvu kumbukeni Caf wapo 33 Cdm 44 hapo namba hizo zikiwa pamoja kwa CCM ni mwiba wa samki mkiwabwaga imekula kwenu watakuwa na CCM

Tatizo cuf bado awaaminiki,muda wowote wanaweza kuisaliti cdm,kwa hiyo sio watu wa kuwaamini sana.
 
''Mtu mbaya na aache matendo yake kisha ageukie mema''CUF kama mmefanya tathimini ya kutosha na mkaona mlipoanguka.Ungameni mtapokelewa,Kama CDM wataona Utayari wenu wa dhati.
 
mimi naona bora wawakubalie ili wawe na nguvu kumbukeni caf wapo 33 cdm 44 hapo namba hizo zikiwa pamoja kwa ccm ni mwiba wa samki mkiwabwaga imekula kwenu watakuwa na ccm
hawana lolote cuf ni wanafiki, mmesahau mnyaa alivyojitoa kugombea unaibu speaker akisema anaendeleza makubaliano ya kuunganisha vyama vyao? Tena kafulila alinukuliwa akisema yalikuwa maamuzi yake labda na chama chake si ya unofficial kambi ya upinzani? Na mnakumbuka jinsi ccm walivyompa kura nyingi mnyaa za ubunge wa sadc? Mi sidanganyiki, wana agenda ya siri hawa cuf na partner zao nccr.
 
kwani ni lazima wawemo kwenye baraza kivuli?.........kupinga au kukubali hoja za serikali huitaji kuwepo kwenye kamati rasmi ya upinzani....unaweza kupinga hoja yoyote hata kama wewe ni ni wa chama tawala pale unapoona kwamba hiyo hoja haiko sahihi.
CUF hawaaminiki hasa kutokekana na impression aliyoionyesha Hamad Rashid tangu mwanzoni, ni vema CDM wakasimama wao peke yao kama wao.........haya mambo ya kuwashirikisha kina mrema hayana maana sbb yy mwenyewe anajulikana ni supporter wa ccm......CDM na NCCR kuna maeneo ambayo hawakubaliani, so is better for CDM kusimama wao kama wao...wanachi tutawasupport, na hao wengine wasubiri kwanza sbb kwa hali ilivyo wanaokena ni wenye mashaka
 
Jamani hebu CDM wasikilizeni hao na mkiona kuna dalili ya usaliti au mkigundua wametumwa na green guard muwakatilie mbali

Tangu mwanzo tulishasema huu si muda wa kuungana na CUF na NCCR kwani wametumwa hao kuja kuidhoofisha CDM na mfano uko wazi kwa hiyo kila chama kitete wananchi wake kivyake. Mwisho wa siku ni sisi wananchi ndio tutawapima ni nani anafanya propaganda. au nani anaiunga mkono CCM,
Hawa jamaa kwenye chaguzi zote wmeiunga CCM leo ndio wanakuja kutuambia tuungane, hii haiwezekani hata kidogo, CDM tusonge mbele wananchi wanatuamini.

Peoples Power.
 
...sabodo hafadhili CDM ila aliichangia CDM. tafuta kamusi ya kiswahili utofautishe kufadhili na kuchangia. pia sabodo aliweka wazi michango yake na mdhumini yake, je RA anaweka wazi ufadhili wake kwa CUF? JESUIT acha kulazimisha facts!!!
 
Itakuwa kosa kubwa sana kama cdm wataingia makubaliano yoyote na cuf bungeni. Cuf ni sehemu ya serikali..wanataka wawe kambi ya upinzani ili wampinge nani?
 
Naamini ushirikiano utaleta positive impacts pia kuondoa utengano uliojitokeza wakati wa kuunda kambi ya upinzani bungeni. Kwani kuna dhambi gani kujiunga na chama chenye nguvu. Dear comrades, hebu tuwe na upeo wa kisiasa, siasa sio uhasama wa kudumu as long as you have common goal. In this case, CDM na CUF wote tuna one goal ambapo ni kuiondoa CCM madarakani, hivyo si rahisi kuacha chama chenye wafuasi kama CUF. Nawashauri viongizi wa CDM kukubali ombi hilo la CUF ili mradi mwenyekiti awe Mbowe, Mnadhimu awe Lissu, pia makamu mwenyekiti atoke CUF. Hii kwangu ni timu tosha kuitoa CCM. Tukumbuke Umoja ni nguvu utengano ni udahifu. Mungu ibariki Tanganyika
 
Kuna haja ya kuchangamana nao bse lengo ni kujenga nchi sio kubomoa

Siyo lazima hasa nia na malengo yao yatakapobainika,Kanuni za bunge ziko wazi hawatalazimishwa,ole wenu CCM kama mnawatumia na mtataka kubadili kanuni itakula kwenu.
 
Jamani, waacheni waje. Kama Hamadi Rashidi au Kafulila wakienda kinyume cha azma ya upinzani si Mbowe anaweza kuwatimua kutoka kwenye Bara Kivuli?

Hamadi Rashidi (mkuu wa kambi wa upinzani bunge lililopita) alisha mtimua John Cheyo wakati wa kikao cha bajeti mwaka jana pale Mbunge huyo wa UDP alipotoa kauli ya kuiunga mkono bajeti kwa asilimia 100![/QUOTE]

mdau hapo kwenye bluu umesahau kwamba cuf ya bunge lilopita sio cuf ya leo...wamefunga ndoa na watawala ccm kumbuka,..anything you discuss with them they will snitch on you...they can't be trusted anymore
 
Back
Top Bottom