#COVID-19: Tuwajibishane

#COVID-19: Tuwajibishane

Mkuu umesoma bandiko langu kuelewa?

1. Bandiko langu limegawanywa sehemu mbili kuonyesha nini serikali haikufanya au haifanyi.

2. Points zile tatu ambazo serikali haikufanya zingezuia ugonjwa kuingia. Hizo hazihusiani na lockdown.

3. Nimeandika kifupi kukuonyesha kuwa lockdown si kufungiwa watu vyumbani wala watu kuhangaika ba njaa.

Labda angalia hapa lockdown ni nini:

View attachment 1426000
Sidhani kama kuna nchi yoyote duniani ilikuwa na uwezo wa kutabiri wimbi la ugonjwa wa COVID-19, sio China, sio EU, sio USA na wala sio Africa. Kila nchi imeupokea huu ugonjwa kivyake na wala na magnitute ya huu ugonjwa haufanani kutokana nchi moja kwenda nchi nyingine. Kila nchi inajitahidi kutokana na hali ya health care system iliyopo.

Ukija kwenye point yako kwanini serikali haikusitisha mambo yasio ya lazima toka mwanzo. Nadhani umejionea mwenyewe kuwa hata zile nchi zilizo funga hizo shughuli, wamejikuta kama walifanya jambo ambalo halikuwa na ulazima kama vile wangelazisha watu kuvaa masks na personal hygiene. China ni moja ya hizo nchi, mwanzo na wao walijaribu kila njia walifunga kila kitu lakini speed ya kupunguzwa ugonjwa ilikuja kuoneka baada ya kulazimisha watu kuvaa mask wanapokuwa nje ya nyumba zao au wanatolewa social points.(Google Social Credit System kuilelwa zaidi). Fahamu kama ugonjwa huu unapata pale unapokuwa karibu na muathika na chembe chembe za mate yabo au makamasi yao au hata machozi yao yatakapo fanikiwa kuingia kwenye mdomo, pua au macho yako. Mask inazuia kwa asilimia kubwa.

Tanzania Corona ipo, na wengi wanatembea wakiwa nao bila ya wao kujijua wanayo, wanaambukiza wengine na wengine wanaambukiza wengine tena. Dawa ni nini wear a mask. "I wear mask to protect you, and you wear mask to protect me". Simple.
 
Acha kutetea upumbavu! Kiongozi gani anayeenda mapumzikoni wakati wa janga??mnavyomtetea sijui anawalipa nini? Na mwenzako hapo juu eti ni safe yeye kukaa Chato...huyo prince Charles mwenyewe ali test postive ndio itakua yeye???

Ofisi ya rais iko kila mahali hata chini ya mwembe. Ndio maana unaona picha zake ziko kila kona ya nchi. Kazi ya urais sio kama receptionist ambaye lazima awepo pale alipoajiriwa ndio kazi iendelee.
 
How can we stand United as one while the ones who were suppose to lead and unite us against the disease are no where to be seen in the scene?
No 1 has isolated him self in his village.
No 2 is no where to be seen.
How can this be possible if we are realy serious in fighting against this pandemic
This is not infantry war zone, wanajeshi wanapigana kwa kujipanga mistari, adui unamuona mbele yako, mashambulizi yanafanywa na askari wa mstari wa mbele wakiongozwa na Kamanda!, no!, this is invisible war fighting an invincible enemy hivyo Kamanda anaweza kuongoza mapambano remotely from an invisible location.
P
 
Acha kutetea upumbavu! Kiongozi gani anayeenda mapumzikoni wakati wa janga??mnavyomtetea sijui anawalipa nini? Na mwenzako hapo juu eti ni safe yeye kukaa Chato...huyo prince Charles mwenyewe ali test postive ndio itakua yeye???
It's a wrong mentality kufikiri kuwa kwa vile Chato ni kwao, kwa hiyo kila akiwa Chato basi ni lazima atakuwa mapumzikoni!. No!. Wewe unaizungumzia Chato ya zamani enzi zile, hii Chato ya sasa ni Chato nyingine ina 4G internet service connectivity hivyo Kamanda waitu anaweza kuongoza mapambano remotely akiwa popote!.

Naunga Mkono Uwanja wa Ndege wa Chato, Una Justification, Utakuwa kama Ggabolite, au Yamoussoukro, Watalii Watamiminika! - JamiiForums
P
 
Sidhani kama kuna nchi yoyote duniani ilikuwa na uwezo wa kutabiri wimbi la ugonjwa wa COVID-19, sio China, sio EU, sio USA na wala sio Africa. Kila nchi imeupokea huu ugonjwa kivyake na wala na magnitute ya huu ugonjwa haufanani kutokana nchi moja kwenda nchi nyingine. Kila nchi inajitahidi kutokana na hali ya health care system iliyopo.

Ukija kwenye point yako kwanini serikali haikusitisha mambo yasio ya lazima toka mwanzo. Nadhani umejionea mwenyewe kuwa hata zile nchi zilizo funga hizo shughuli, wamejikuta kama walifanya jambo ambalo halikuwa na ulazima kama vile wangelazisha watu kuvaa masks na personal hygiene. China ni moja ya hizo nchi, mwanzo na wao walijaribu kila njia walifunga kila kitu lakini speed ya kupunguzwa ugonjwa ilikuja kuoneka baada ya kulazimisha watu kuvaa mask wanapokuwa nje ya nyumba zao au wanatolewa social points.(Google Social Credit System kuilelwa zaidi). Fahamu kama ugonjwa huu unapata pale unapokuwa karibu na muathika na chembe chembe za mate yabo au makamasi yao au hata machozi yao yatakapo fanikiwa kuingia kwenye mdomo, pua au macho yako. Mask inazuia kwa asilimia kubwa.

Tanzania Corona ipo, na wengi wanatembea wakiwa nao bila ya wao kujijua wanayo, wanaambukiza wengine na wengine wanaambukiza wengine tena. Dawa ni nini wear a mask. "I wear mask to protect you, and you wear mask to protect me". Simple.

Mkuu Tanzania haikuhitaji kutabiri kujua kama Corona itakuja. Tanzania ilitahadharishwa kutokea kila pembe. Hata sasa inatahadharishwa kuhusu kusambaa au mnajiandaa kuja kusema msingeweza kutabiri kuwa ugonjwa ungesambaa?

Hapa ninakuwekea kwa uchache tu tahadhari zilizowekwa wazi mno kabla ya ugonjwa kuingia. Tahadhari zipi Tanzania haikuwa nazo hadi kuhitaji utabiri wa kibwetere kwenye kuingia huu ugonjwa nchini?

Corona virus: Tunajifunza nini toka kwa wengine? - JamiiForums

IMG_20200422_062622_736.jpg

Mkuu uliwahi kuyaona hayo au ni leo tu ndiyo una yaona? Haya niliyokuwa hapa yalikuwa ni ya March 14, kabla ya ugonjwa kuingia. Yapo hata ya kabla zaidi kabla ya hapo (humu jamvini). Achilia mbali huko kwingine.

Vipi mkuu hukuwahi kuyaona, au ndiyo yale yale ya kujifanya hamnazo? Au yale ya kujifanya ndiyo kwanza mnawasili tokea sayari nyingine?

China wali lockdown Wuhan na maeneo yote yasiyokuwa na maambukizi ndiyo maana hatimaye wakaushinda huu ugonjwa. Si wao tu bali hata nchi zote zilizoonyesha mafanikio thabiti (yasiyo superficial) USA, Germany, Italy, Spain nk.

Vile vile wenzetu kama sisi Rwanda, Uganda, Kenya nk. Kupitia lockdown, sasa hivi nao maambukizi tayari ni machache kuliko wanaopona. Tayari wamesha udhibiti huu ugonjwa na taratibu sasa wanaanza kurudi kwenye maisha ya kawaida.

Tanzania ni sikio la kufa!

Aliyewatuma kuja huku jamvini na hivyo vi propaganda nendeni mkamwambie anayo nafasi fupi sana sasa iliyobakia. Mwambieni ushauri wa Zitto ni sasa ndiyo habari ya mjini. Wananchi tunasimama nao ni vyema akachagua kuutumia.

Muda sasa kama unavyoyoma kwetu na maisha yetu unayoyoma kwake kwani uvumilivu sasa kweli umetuisha kabisa. Hayuko tayari kufa tukijiona kwa uzembe wake.
 
#COVID-19: TUWAJIBISHANE

Mnamo Tarehe 28/3/2020 niliwaeleza Watanzania kuwa nimemwandikia barua Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumshauri mambo makubwa 8 ili nchi yetu iweze kukabili maambukizi ya virusi vya Korona. Tarehe 4/4/2020 Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa Maalim Seif Sharif Hamad alizungumza na Wananchi kuwataka kujihadhari na virusi vya Korona. Hadi siku Mwenyekiti anazungumza Tanzania ilikuwa na wagonjwa 20 tu. Leo Tanzania ina wagonjwa 257 na Serikali imeripoti vifo vya watu 10. Kati ya Aprili 1 na Aprili 20, maambukizi yaliyotangazwa yamefikia 1,170%.

Kama Viongozi wa Upinzani nchini kwa wiki kadhaa sasa tumekuwa tunatoa ushauri kwa Viongozi wa Serikali na kuelimisha umma kudhibiti #COVID19TZA. Tumejitahidi kuunganisha Nchi yetu dhidi ya Virusi hivi. Sasa umefika wakati wa KUWAJIBISHANA.

Wakati Nchi ikiwa katika maambukizi mtu mwenye Mamlaka ya Juu kabisa katika Nchi yetu, Rais John Pombe Joseph Magufuli haonekani kuendesha mapambano kama tunavyoona kwa mataifa jirani kama Kenya, Rwanda, Uganda, Afrika Kusini nk. Mara chache ambazo Rais amejitokeza ametoa kauli zinazoonyesha kuwa COVID 19 sio tatizo na hivyo kushawishi watu kuendelea na shughuli za mikusanyiko ambazo zinakuza maambukizi. Pia tumeona Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na baadhi ya watu wa karibu na Rais wakihamasisha mikusanyiko ya watu.

Mwalimu Julius Nyerere alitafsiri Kitabu cha Shakespeare Merchants of Venice (Mabepari wa Venice). Kundi hili la Viongozi walioendelea kushawishi Watanzania kuendelea na shughuli za mikusanyiko, Mwalimu Nyerere angewaita Mabepari wa Vifo (Merchants of Deaths). #MerchantsOfDeaths ni watu ambao wakielekezwa kutofanya matendo fulani ili kuepuka maafa wao hufanya. Pia watu wenye Mamlaka ambao wanashindwa kutumia mamlaka yao kuzuia maafa. Vile vile watu wa imani ambao wanaaminisha waumini wao mambo ambayo husababisha maafa. Wanashtakika

Kutokana na maandalizi mabovu ya Serikali kwa Watumishi wa Afya - Madaktari, Manesi, Watumishi wa Maabara - maambukizi yamesambaa miongoni mwao na hata wengine kuanza kupoteza maisha. Licha ya Serikali kukusanya mabilioni ya Fedha kutoka Sekta Binafsi na yenyewe kutotenga Bajeti Maalumu ya kupambana na Korona, watumishi walio mstari wa mbele kwenye vita wanaachwa bila vifaa (PPE). Nchi yetu ipo kwenye hatari ya kupoteza wataalamu wengi wa Afya ambao wamesomeshwa kwa gharama kubwa na kwa muda mrefu. Watumishi hawa pia wanahatarisha familia zao.

Namna Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyokabili mlipuko wa Korona inathibitisha kauli kuwa Tanzania imekuwa na miaka 5 ya uholela, yaani 5 Years Of Incompetence. Mgawanyo wa Kazi wakati huu umekuwa;

- Naibu Waziri Afya: kuelimisha Umma maana ya Corona na kuvaa Barakoa

- Waziri wa Afya: Kutangaza Idadi ya visa vya Corona na vifo na kuelezea maamuzi mbalimbali ya Serikali

- Waziri Mkuu: Kukusanya michango ya Wadau (Serikali yenyewe haijaweka wazi Bajeti yake ya Corona

- Makamu wa Rais: Hajulikani alipo

- Rais: Kajificha Kijijini Chato huku akitaka Wananchi waendelee kwenda Kanisani na Misikitini

Hatuwezi kuendelea namna hii huku wagonjwa wanaongezeka, Watanzania wanapoteza maisha, huduma za Afya zinazidiwa na kupoteza wataalamu muhimu na uchumi unaanguka. Itabidi kuendelea kupambana na Korona huku tunawajibishana.

Namtaka Rais Magufuli afanye yafuatayo

1. Amwagize Waziri wa Fedha kupeleka Bungeni Bajeti ya Dharura kukabiliana na Korona na baada ya Bajeti hiyo Bunge lisimamishe vikao vyake mpaka Korona itakapokomeshwa nchini. Bajeti hiyo ihakikishe Wataalamu wetu wa Afya wanapata vifaa vya kuwalinda ili kupambana na Korona

2. Ahutubie Taifa mara moja na kuwataka Wananchi kuacha shughuli zao za kila siku na kwa kutumia Sheria ya Bunge kuifunga Nchi (partial lockdown). Wananchi wasaidiwe kwa mujibu wa mapendekezo tuliyoyatoa, kila kaya ipatiwe shs 300,000

3. Kama hawezi kuyafanya haya ajiondoe madarakani ili watanzania wengine wafanye hiyo kazi ya kulinda Nchi yetu.

Mwisho nawaomba Wanasheria nchini kuandaa mashtaka ya kukusudia kuua dhidi ya watu wote ambao wametoa matamko ambayo yaliwafanya wananchi waendelee na shughuli za kuambukiza virusi vya Korona.

Imetolewa na:

Zitto Kabwe

Kiongozi wa ACT Wazalendo
21 Aprili, 2020

#RaisTokaChato​
Acha utoto huu

Wewe ni mkubwa unayetegemewa

Huna hoja na husikilizwi,unapuuzwa

Sababu ya utoto wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zitto kwa kifupi unachokifanya kinaonesha dhahiri kuwa unatumia tatizo au ugonjwa wa CORONA kutaka kujipatia umaarufu wa kisiasa. Ni nani asiyejua kuwa hili ni janga la kitaifa?
Nani kakwambia kuhutubia taifa ni dawa ya CORONA?
Unataka nchi ifungwe hao wananchi mil 60 utawapakata jikoni kwako? Toa mfano wa 300,000 jimboni kwako uone kama inawezekana.
Tambua Tanzania ni kuwa sio chama cha ACT Wazalendo.
 
Mkuu Mhe. Zitto, kwenye hili, siungi mkono hoja, kwa sasa tuko katikati ya Mapambano, huu sii wakati wa kunyoosheana vidole kulaumiana, kushutumiana na kutafuta mchawi tuwajibishane. Huu ni wakati wa kusimama pamoja, stand together united as one and fight as one unified army against one common enemy.

Corona: Tusinyoosheane vidole. Kama unaweza kusaidia, please do. Usisubiri uombwe - jitokeze saidia, vinginevyo nyamaza! - JamiiForums
P
Hatua zilizokwisha kuchukuliwa katika mapambano ya Corona zinaelekea kukwama kwa sababu wataalam wa afya hawawezi kuzuia mikusanyiko bali serikali tena mkuu wa nchi. Mizaha inayofanywa na viongozi wetu imesababisha Corona kusambaa kamo moto wa nyikani kutoka Dar hadi mikoa zaidi ya 10 hadi sasa.
Kwa hiyo Paskale kama hauungi mkono hoja hii basi umeamua kumpinga Mhe. Zitto

Landson Tz
 
Ni vizuri ukweli usemwe na watu wasitake maisha ya wananchi for granted!Pascal toka uitwe Dodoma umekuaje sijui!unaonyesha kwa uwazi kabisa which side you are!!
Mkuu Mhe. Zitto, kwenye hili, siungi mkono hoja, kwa sasa tuko katikati ya Mapambano, huu sii wakati wa kunyoosheana vidole kulaumiana, kushutumiana na kutafuta mchawi tuwajibishane. Huu ni wakati wa kusimama pamoja, stand together united as one and fight as one unified army against one common enemy.

Corona: Tusinyoosheane vidole. Kama unaweza kusaidia, please do. Usisubiri uombwe - jitokeze saidia, vinginevyo nyamaza! - JamiiForums
P

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zitto, kwenye hili, sisi tuliamua kila nchi iendeshe mapambano kivyake vyake bila kuiga, kama hao marais wengine wanaendesha mapambano kwa kuonekana sio wao.

Kwanini Magufuli awaige wakati kuna njia nyingi za kuendesha mapambano na sio lazima mpaka kila mtu aone, issue ni kuona au kupambana?

P
Bwana Pascal, kwanza kumbuka hakuna jipya chini ya jua, we have a lot more literature reviews to making references, Ndui, Spanish flu etc. How did they combat? Unless tuwe na akili za Ziada zaidi ili kuandika historia kuzizidi mbinu zilizo okoa dunia then.

Labda mbinu ya maombi ya mkuu, lakini nadhani pia timeiiga Kwa Trump maana nae alifanya maombi na umeona kinachotokea huko. Pia Italy walifanya maombi na papa akawaambia wapitishe msalaba Rome! Umeona kilichowakuta!

Hebu Hata wewe bwana Pascal tuzidi kushauri Kwa kutumia akili zetu alizotupa Mungu na tuweke unafiki pembeni.

Ninachohisi ni mshauriwa anawashauri wataalamu na anatoa mawazo huku kajificha sehemu Kwa uoga, lakini taifa litaangamia! Hafanyi Kwa maksudi ila haelewi na wanaoelewa wanamuogopa na yeye anaona poa tuu!

Hebu rudi, kuwa mzalendo na shauri vizuri Kwa weledi, karipia, rekebisha na tuende tuliokoe taifa.
 
Kama corona hajaileta yeye kaileta nan?

Alipoambiwa afunge mipaka na viwanja vya ndege toka mwanzo alikubali?

Alipoambiwa afunge bar na kumbi za starehe alikubali?
Alipoambiwa azuie mabasi ya kutoka dar kuingia mikoan alikubali??

Mpaka sasa ni hatua gani madhubuti aliyochukua???

Unapimwa leo corona mwanza unasubiri vipimo viende dar mpaka virudi ushakufa,huo si ukichaa??

Think.

Sent using Jamii Forums mobile app
Africa hadi muda huu tuna case za corona 25000 kati ya hizo tanzania tuna case 254 ambayo overroll haizid hata asilimia moja ya maambukizi yalionea kwa africa nzima had sasa

wengi watasema rais amechelewa kufanya lockdown, tumeona yaliotkea kenya baada ya lockdown hao hao wanachi waligoma kukaa ndani ikasababisha hadi vifo vya watu sababu ya serikali kutumia nguvu, kama lockdown ingekuwa tanzania na hao watu wakauwawa ndo ingekuwa breaking news ya siku zote bbc london pamoja na vibaraka wao

hakuna rais ambae anapenda nchi yake iwe na majanga, yeye kichwa kinamuuma zaidi kuliko nyie ambao mmekaa mbele ya keyboard kazi yenu kubwa kulauumu huku mnakula popcorn
 
Siasa siasa siasa, kila muda ni siasa, maisha mtaishi lini?

Waache wataalamu waliobobea haya mambo wafanyekazi zao.
zito amekaa kimaslahi ya kisiasa zaid, hana uchungu wowote na wanachi
ameshaona corona ni hoja ya kumbeba kisiasa ni wa kumpuuza tu
 
Copy and Paste Anti-Covid 19 Measures hit Hard East African Countries

By: Kimathi Njoroge, Mombasa
April 20,2020

There is an old saying that a falcon cannot bear the falconer. The saying is compared to some East African countries that have copied and pasted Western countries anti-COVID 19 measures. Specifically, I write in the view of my lovely country, Kenya. In academic sphere, Copy and Paste is academic suicide. This is no difference with copied and pasted measures against anti- COVID-19 measures in the World. In East African Context, each country opted her measures against COVID-19. But most countries in the region excluding our neighbours Tanzania copied and pasted Lockdown Western style. It is unfortunate that there has been no single coordinated formula in these countries to fight COVID-19. Now western styles against COVID-19 in Eastern countries have started to backfire. For example, Kenyan government has today told the public that it plans to re-open domestic flights and other travels to save the economy. The statement posted by BBC news stated clearly that Kenyan economy has been badly hit by total lockdown. The statement went further by stating that the country is also set to open up local tourism to save its economy. It should be noted that - Kenya is a middle income country that will not benefit the debt relief provided by World Bank and IMF to poor African countries. We have addresses this many times to Kenya government. In our neighbours Rwanda, the situation is the same. Yesterday, the country lamented for lockdown effects while pledging to continue with it. The government said it was becoming tough to feed all Rwandese on the pretext that the number of needy people is too high compared with the government's capacity In Uganda the situation is not different, Ugandans have been hit bitterly and hardly economically by the total lockdown. I spoke to my friends in Uganda - the majority are asking the government to re-open up businesses. President Kaguta Museveni has resisted his peoples call telling them that if you were poor before COVID-19 you will remain poor after COVID-19. It should be noted that last week the World Bank warned some African countries including Kenya against their copy and paste anti-COVID 19 behaviours. These countries were advised to use their think-tanks to plan best measures that suits their environment. Few countries in Africa have not copied and pasted Western countries. These include among others our neighbours Burundi and Tanzania. I researched over Tanzania’s measures and found despite the allegations against our neighbours, all World Health Organisation's anti- COVID-19 measures are in place but has not closed its borders. The country has neither halted domestic flights nor businesses shut down. It is possible that Tanzania analysed anti western COVID-19 measures and concluded that they will not bearfruits in the region. Recently, President John Magufuli told the congregation in the church that Tanzania is surrounded by eight countries that depend on it to survive adding that if we close the borders citizens in these countries will die. What kind of lovely gesture in our regional friendship! This was a strong statement coming from the leader whose country is also fighting COVID-19. If this is not enough, President Magufuli asked Tanzanian to hold three days prayers against Covid-19. Prayers lifted the souls and minds of many people despite the existing stressing virus. It is said in Latin that _Gaudele cum gaudentibus_ meaning that enjoy with those who enjoy. In my opinion, God through Tanzanians prayers will cover all of us in the region so long as we are attached to them. It seems, Tanzanian style is bearing fruits and interests other countries in Africa and World at large. Today, President Nana Akufo Ado has ordered the lock down meaningless and told his citizens come out and work to save the economy. At the same time, things are jumping from the pan to the fire in the US. Americans have flocked in the streets demanding the lock down orders in states to be lifted because they have badly hit them economically. In Sweden, the government has ordered people to come out and work to save the economy while taking measures against COVID-19. These are symptoms that most countries in the world will open up their economy while taking measures against COVID-19 because lockdown will no longer be a permanent solution. I think, this should be the lesson to us, especially the East African countries that whenever something bad happens we must be united and put our efforts towards the solution that works for us and serve our region.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Africa hadi muda huu tuna case za corona 25000 kati ya hizo tanzania tuna case 254 ambayo overroll haizid hata asilimia moja ya maambukizi yalionea kwa africa nzima had sasa

wengi watasema rais amechelewa kufanya lockdown, tumeona yaliotkea kenya baada ya lockdown hao hao wanachi waligoma kukaa ndani ikasababisha hadi vifo vya watu sababu ya serikali kutumia nguvu, kama lockdown ingekuwa tanzania na hao watu wakauwawa ndo ingekuwa breaking news ya siku zote bbc london pamoja na vibaraka wao

hakuna rais ambae anapenda nchi yake iwe na majanga, yeye kichwa kinamuuma zaidi kuliko nyie ambao mmekaa mbele ya keyboard kazi yenu kubwa kulauumu huku mnakula popcorn

Kenya ipi ambayo wananchi hawakutaka lockdown? Ni wakenya wa CCM ipi mnayoongelea nyie?

Kenyans want total lockdown

Kuwa Tanzania wagonjwa hawafiki 1%? Kwani hujui kuwa mwanzo wa safari ndefu huanza na hatua ya kwanza? Kwani waliko wagonjwa wengi walianza na wengi?

Hivi huwa wanawavutisha nini akili zenu zinawatoka?

Nani asiyewajua? Sasa hivi ikitangazwa total lockdown mtatokea na mabango mkidai nyie ndiyo mlikuwa mnaitaka zaidi.

Rais huyu hadi hivi sasa anawajibika moja kwa moja kwa madhara yote ya ugonjwa huu. Yeye na hali kadhalika nyie wapambe wake, historia itakuwapo kuwahukumu.
 
Vita vinapigwana kisasa, the command post ni Chatto. Usually the command post inapaswa iwe established mahali ambapo ni safest place in the area. Safe heavens zetu kwa sasa ni Chatto.
P
Una maana gani kusema safe area? Kwani kuna tishio gani dhidi yake? Ina maana mahali na ofisi yake ya serikali si salama kwake? Nani anasababisha kukosekana kwa huo usalama?
 
Duuh mimi naendelea kuwa mtazamaji na msomaji huku nachukua vizuri kabisa tahadhari tunazoambiwa na shirika la Afya ulimwenguni na wala sio wizara ya afya ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom