#COVID-19: Tuwajibishane

#COVID-19: Tuwajibishane

Copy and Paste Anti-Covid 19 Measures hit Hard East African Countries

By: Kimathi Njoroge, Mombasa
April 20,2020

There is an old saying that a falcon cannot bear the falconer. The saying is compared to some East African countries that have copied and pasted Western countries anti-COVID 19 measures. Specifically, I write in the view of my lovely country, Kenya. In academic sphere, Copy and Paste is academic suicide. This is no difference with copied and pasted measures against anti- COVID-19 measures in the World. In East African Context, each country opted her measures against COVID-19. But most countries in the region excluding our neighbours Tanzania copied and pasted Lockdown Western style. It is unfortunate that there has been no single coordinated formula in these countries to fight COVID-19. Now western styles against COVID-19 in Eastern countries have started to backfire. For example, Kenyan government has today told the public that it plans to re-open domestic flights and other travels to save the economy. The statement posted by BBC news stated clearly that Kenyan economy has been badly hit by total lockdown. The statement went further by stating that the country is also set to open up local tourism to save its economy. It should be noted that - Kenya is a middle income country that will not benefit the debt relief provided by World Bank and IMF to poor African countries. We have addresses this many times to Kenya government. In our neighbours Rwanda, the situation is the same. Yesterday, the country lamented for lockdown effects while pledging to continue with it. The government said it was becoming tough to feed all Rwandese on the pretext that the number of needy people is too high compared with the government's capacity In Uganda the situation is not different, Ugandans have been hit bitterly and hardly economically by the total lockdown. I spoke to my friends in Uganda - the majority are asking the government to re-open up businesses. President Kaguta Museveni has resisted his peoples call telling them that if you were poor before COVID-19 you will remain poor after COVID-19. It should be noted that last week the World Bank warned some African countries including Kenya against their copy and paste anti-COVID 19 behaviours. These countries were advised to use their think-tanks to plan best measures that suits their environment. Few countries in Africa have not copied and pasted Western countries. These include among others our neighbours Burundi and Tanzania. I researched over Tanzania’s measures and found despite the allegations against our neighbours, all World Health Organisation's anti- COVID-19 measures are in place but has not closed its borders. The country has neither halted domestic flights nor businesses shut down. It is possible that Tanzania analysed anti western COVID-19 measures and concluded that they will not bearfruits in the region. Recently, President John Magufuli told the congregation in the church that Tanzania is surrounded by eight countries that depend on it to survive adding that if we close the borders citizens in these countries will die. What kind of lovely gesture in our regional friendship! 8This was a strong statement coming from the leader whose country is also fighting COVID-19. If this is not enough, President Magufuli asked Tanzanian to hold three days prayers against Covid-19. Prayers lifted the souls and minds of many people despite the existing stressing virus. It is said in Latin that _Gaudele cum gaudentibus_ meaning that enjoy with those who enjoy. In my opinion, God through Tanzanians prayers will cover all of us in the region so long as we are attached to them. It seems, Tanzanian style is bearing fruits and interests other countries in Africa and World at large. Today, President Nana Akufo Ado has ordered the lock down meaningless and told his citizens come out and work to save the economy. At the same time, things are jumping from the pan to the fire in the US. Americans have flocked in the streets demanding the lock down orders in states to be lifted because they have badly hit them economically. In Sweden, the government has ordered people to come out and work to save the economy while taking measures against COVID-19. These are symptoms that most countries in the world will open up their economy while taking measures against COVID-19 because lockdown will no longer be a permanent solution. I think, this should be the lesson to us, especially the East African countries that whenever something bad happens we must be united and put our efforts towards the solution that works for us and serve our region.

Sent using Jamii Forums mobile app

Huyo Mkenya anayewasifia ki Pascal P ambao kwao wana lockdown unadhani karibu wakenya sasa wanaenda makanisani?

"Recently, President John Magufuli told the congregation in the church that Tanzania is surrounded by eight countries that depend on it to survive adding that if we close the borders citizens in these countries will die. What kind of lovely gesture in our regional friendship! "

You must be a nut to believe in this statement from your competitor.

Wajinga ndiyo waliwao.
 
Sorry to differ with you, Lakini Tanzania sio North Korea kwamba kiongozi asipoonekana hadharani au kutajwa kwenye TV basi nchi inatetemeka na watu kuulizana kuna nini. We are mature than that, kitendo cha sisi to keep our cool while the other in the region wanamalizana Kwa vita, inaonyesha ukomavu wetu.

Hivi nikuulize swali toka Trump amekuwa anasimama na kuongea na waandishi wa habari, kuna cha maana umeokota au ndio kutukana watu your fake na kusema Chinese virus. Hata huyo Kenyatta, mara ya mwisho ulimuona lini jukwaani tena anaingilia maamuzi ya madaktari na washauri wa mambo ya kiafya? Lakini huku kwetu watu wanataka wamuone Magufuli kila kona, huku anaongea mambo kuingilia wataalamu ili watu wapate cha kusema. Hao wengine sijui wakuu wa mikoa, mawaziri kila mtu anaongea to their capacity, wote hao wanawashauri wao wa mambo ya afya, iwe mkoa au wizara.
Kwani alipotoa ushauri wa maombi watu walilalamika anaingilia wataalam? Kwani Rais naye hana washauri wa kiafya kabla ya kujitokeza na kutoa strategy mpya?

Nachosema ni kwamba kuna controversy nyingi muda huu na coordination unayosema haipo kabisa ndio maana unaona Ma RC, DC wanaamua strategy ambazo zinacontradict na bodies zingine za serikali kma wizara. Sasa nani wa kuondoa hii controversy zaidi ya Rais?

Alafu mkuu kuhusu maturity hapo sikubaliani na wewe, mara ngapi mambo hayaendi moaka Rais ajitokeze? Imagine mpaka anasolve kesi za ardhi na mwanamke kutapeliwa kiosk? Hivi zile ziara maduku duku anayoambiwa na wananchi ina maana Dc na wakurugenzi hawapo?

Ukweli ni kwamba coordination hamna na kwa nchi yetu maamuzi magumu yote yanamsubirigi Rais na ushahidi upo mwingi tu kwahiyo maturity unayosema hapa haipo kabisa otherwise kungekua na clear intergrated course of action kuliko hizi sintofahamu za sasa.

Huwezi fifisha role ya Rais nyakati kama hizi kwa kisingizio cha serikali inafanya kazi kokote, wakati unajua kabisa yeye ndio ana mamlaka ya juu zaidi kutoa maamuzi magumu na dira ya taifa katika kipindi hiki.
 
Hivi nikuulize swali toka Trump amekuwa anasimama na kuongea na waandishi wa habari, kuna cha maana umeokota au ndio kutukana watu your fake na kusema Chinese virus.
Mkuu tuache bias na cherry picking, ina maana kuwatangazia wamarekani updates za ugonjwa, cutafuta cure, kutoa relief package, kuongelea possibility ya chloroquine, kuwaambia crucial sectors za uchumi zitafunguliwa taratibu, kuongelea peak days za vifo vya corona watu wajiandae hukuzisikia ila umeona Matusi yake tu?? Are we serious

Hoja yangu ni hii iwe museveni au Kenyatta lakini sauti ya Rais ndio final kwa nchi zetu huku kwahyo alipaswa kuweka sawa hizi contradicting statement za bunge,wizara na viongozi wa mkoa maana kila mtu ana lake.

Hyu anazuia wasafiri, mwingine afunge biashara, mara hyu anataka mask A hku wizara inataka mask B!! Sasa superior voice ni ipi hapo?? President has to lead from the front sio kusema eti washauri wa afya wapo kma ndio hivyo basi hta haina haja ya kuwepo taasisi ya Rais sababu afterall watendaji si wapo so Rais wa nini sasa!!?

Tuache cherry picking
 
Rais yuko safe (at least that is what he thinks).

Rais hana watu wa kumshauri, sidhani hata kama anao huwa anapokea ushauri.

Tuendelee kupambana at personal level, ila at National Level ni tatizo. Imagine hali ilivyo Dar lakini bado watu wanasafiri kwenda mikoani bila kizuizi.
mm pia nashangaa hii hali..
 
2. Ahutubie Taifa mara moja na kuwataka Wananchi kuacha shughuli zao za kila siku na kwa kutumia Sheria ya Bunge kuifunga Nchi (partial lockdown). Wananchi wasaidiwe kwa mujibu wa mapendekezo tuliyoyatoa, kila kaya ipatiwe shs 300,000

tangu tulipotapeliwa NOAH zetu.... baadae wakasema BALIMI.... Nazo zikayeyuka.... sina hamu
 
#COVID-19: TUWAJIBISHANE

Mnamo Tarehe 28/3/2020 niliwaeleza Watanzania kuwa nimemwandikia barua Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumshauri mambo makubwa 8 ili nchi yetu iweze kukabili maambukizi ya virusi vya Korona. Tarehe 4/4/2020 Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa Maalim Seif Sharif Hamad alizungumza na Wananchi kuwataka kujihadhari na virusi vya Korona. Hadi siku Mwenyekiti anazungumza Tanzania ilikuwa na wagonjwa 20 tu. Leo Tanzania ina wagonjwa 257 na Serikali imeripoti vifo vya watu 10. Kati ya Aprili 1 na Aprili 20, maambukizi yaliyotangazwa yamefikia 1,170%.

Kama Viongozi wa Upinzani nchini kwa wiki kadhaa sasa tumekuwa tunatoa ushauri kwa Viongozi wa Serikali na kuelimisha umma kudhibiti #COVID19TZA. Tumejitahidi kuunganisha Nchi yetu dhidi ya Virusi hivi. Sasa umefika wakati wa KUWAJIBISHANA.

Wakati Nchi ikiwa katika maambukizi mtu mwenye Mamlaka ya Juu kabisa katika Nchi yetu, Rais John Pombe Joseph Magufuli haonekani kuendesha mapambano kama tunavyoona kwa mataifa jirani kama Kenya, Rwanda, Uganda, Afrika Kusini nk. Mara chache ambazo Rais amejitokeza ametoa kauli zinazoonyesha kuwa COVID 19 sio tatizo na hivyo kushawishi watu kuendelea na shughuli za mikusanyiko ambazo zinakuza maambukizi. Pia tumeona Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na baadhi ya watu wa karibu na Rais wakihamasisha mikusanyiko ya watu.

Mwalimu Julius Nyerere alitafsiri Kitabu cha Shakespeare Merchants of Venice (Mabepari wa Venice). Kundi hili la Viongozi walioendelea kushawishi Watanzania kuendelea na shughuli za mikusanyiko, Mwalimu Nyerere angewaita Mabepari wa Vifo (Merchants of Deaths). #MerchantsOfDeaths ni watu ambao wakielekezwa kutofanya matendo fulani ili kuepuka maafa wao hufanya. Pia watu wenye Mamlaka ambao wanashindwa kutumia mamlaka yao kuzuia maafa. Vile vile watu wa imani ambao wanaaminisha waumini wao mambo ambayo husababisha maafa. Wanashtakika

Kutokana na maandalizi mabovu ya Serikali kwa Watumishi wa Afya - Madaktari, Manesi, Watumishi wa Maabara - maambukizi yamesambaa miongoni mwao na hata wengine kuanza kupoteza maisha. Licha ya Serikali kukusanya mabilioni ya Fedha kutoka Sekta Binafsi na yenyewe kutotenga Bajeti Maalumu ya kupambana na Korona, watumishi walio mstari wa mbele kwenye vita wanaachwa bila vifaa (PPE). Nchi yetu ipo kwenye hatari ya kupoteza wataalamu wengi wa Afya ambao wamesomeshwa kwa gharama kubwa na kwa muda mrefu. Watumishi hawa pia wanahatarisha familia zao.

Namna Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyokabili mlipuko wa Korona inathibitisha kauli kuwa Tanzania imekuwa na miaka 5 ya uholela, yaani 5 Years Of Incompetence. Mgawanyo wa Kazi wakati huu umekuwa;

- Naibu Waziri Afya: kuelimisha Umma maana ya Corona na kuvaa Barakoa

- Waziri wa Afya: Kutangaza Idadi ya visa vya Corona na vifo na kuelezea maamuzi mbalimbali ya Serikali

- Waziri Mkuu: Kukusanya michango ya Wadau (Serikali yenyewe haijaweka wazi Bajeti yake ya Corona

- Makamu wa Rais: Hajulikani alipo

- Rais: Kajificha Kijijini Chato huku akitaka Wananchi waendelee kwenda Kanisani na Misikitini

Hatuwezi kuendelea namna hii huku wagonjwa wanaongezeka, Watanzania wanapoteza maisha, huduma za Afya zinazidiwa na kupoteza wataalamu muhimu na uchumi unaanguka. Itabidi kuendelea kupambana na Korona huku tunawajibishana.

Namtaka Rais Magufuli afanye yafuatayo

1. Amwagize Waziri wa Fedha kupeleka Bungeni Bajeti ya Dharura kukabiliana na Korona na baada ya Bajeti hiyo Bunge lisimamishe vikao vyake mpaka Korona itakapokomeshwa nchini. Bajeti hiyo ihakikishe Wataalamu wetu wa Afya wanapata vifaa vya kuwalinda ili kupambana na Korona

2. Ahutubie Taifa mara moja na kuwataka Wananchi kuacha shughuli zao za kila siku na kwa kutumia Sheria ya Bunge kuifunga Nchi (partial lockdown). Wananchi wasaidiwe kwa mujibu wa mapendekezo tuliyoyatoa, kila kaya ipatiwe shs 300,000

3. Kama hawezi kuyafanya haya ajiondoe madarakani ili watanzania wengine wafanye hiyo kazi ya kulinda Nchi yetu.

Mwisho nawaomba Wanasheria nchini kuandaa mashtaka ya kukusudia kuua dhidi ya watu wote ambao wametoa matamko ambayo yaliwafanya wananchi waendelee na shughuli za kuambukiza virusi vya Korona.

Imetolewa na:

Zitto Kabwe

Kiongozi wa ACT Wazalendo
21 Aprili, 2020

#RaisTokaChato​
Mh Zitto, matatizo yote haya yaliletwa na Kikwete kwa kuingia na majina mfukoni, mwisho wa siku akaibuka mtu ambaye hana sifa za kuwa hata Ten cell Leader, mtu huyo eti Leo ni Rais, ndo maana hali iko hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani alipotoa ushauri wa maombi watu walilalamika anaingilia wataalam? Kwani Rais naye hana washauri wa kiafya kabla ya kujitokeza na kutoa strategy mpya?

Nachosema ni kwamba kuna controversy nyingi muda huu na coordination unayosema haipo kabisa ndio maana unaona Ma RC, DC wanaamua strategy ambazo zinacontradict na bodies zingine za serikali kma wizara. Sasa nani wa kuondoa hii controversy zaidi ya Rais?

Alafu mkuu kuhusu maturity hapo sikubaliani na wewe, mara ngapi mambo hayaendi moaka Rais ajitokeze? Imagine mpaka anasolve kesi za ardhi na mwanamke kutapeliwa kiosk? Hivi zile ziara maduku duku anayoambiwa na wananchi ina maana Dc na wakurugenzi hawapo?

Ukweli ni kwamba coordination hamna na kwa nchi yetu maamuzi magumu yote yanamsubirigi Rais na ushahidi upo mwingi tu kwahiyo maturity unayosema hapa haipo kabisa otherwise kungekua na clear intergrated course of action kuliko hizi sintofahamu za sasa.

Huwezi fifisha role ya Rais nyakati kama hizi kwa kisingizio cha serikali inafanya kazi kokote, wakati unajua kabisa yeye ndio ana mamlaka ya juu zaidi kutoa maamuzi magumu na dira ya taifa katika kipindi hiki.

Lakini siku alipoliomba taifa kufanya maombi, alisema watu waombe huku kukumbatiana na kuambukizana Corona? Kitu ambacho ndugu zetu tena waupinzani mnafanya ni kuchukua jambo na kuliongezea miguu na mikono. Waziri Mkuu alishaunda kamati tatu za kupambana na COVID-19, ya kwanza inaongozwa na yeye PM, ya pili inaongozwa na katibu kiongozi office ya rais, na ya tatu inaongozwa na katibu mkuu wizara ya afya. Hizi kamati zote zina wataalamu walio bobea maswala ya afya na jamii, taarifa zote na mikakati yote ya hizi kamati zinafikishwa office ya rais na yeye mwenyewe anapewa taarifa as head of state. Sasa ukisema hakuna coordination nashindwa kuelewa ulitaka coordination ya aina gani, kwamba rais asimame pale atoe amri ndio ndio watu waamini kama serikali inafanya kazi. Mbona aliongea na taifa march 22 na kutoa update nini kinafanyika ikiwa pamoja na kuweka watu quarantine Kwa siku 14.

Course of action iko wazi na kila siku inasemwa, NAWA MIKONO, VAA BARAKOA, EPUKA MIKUSANYIKO NA PUNGUZA SAFARI ZISIZO ZA LAZIMA. Hakuna kingine kikubwa zaidi ya hapo, sasa hata hili watu mnataka rais asimame pale alitolewa tamko. Mbona ni nchi nyingi tu mda huu viongozi wao wamewapa muda wahusika kulizungumzia hili swala. Ukisema Trump anasimama na kutoa maelezo ya ventilators, madawa na mengineo, ukumbuke mwenzako yuko kwenye election year, he needs all the coverage he could get.
 
Tatizo namba waahid yupo mafichon
Mkuu Mhe. Zitto, kwenye hili, siungi mkono hoja, kwa sasa tuko katikati ya Mapambano, huu sii wakati wa kunyoosheana vidole kulaumiana, kushutumiana na kutafuta mchawi tuwajibishane. Huu ni wakati wa kusimama pamoja, stand together united as one and fight as one unified army against one common enemy.

Corona: Tusinyoosheane vidole. Kama unaweza kusaidia, please do. Usisubiri uombwe - jitokeze saidia, vinginevyo nyamaza! - JamiiForums
P

Sent using Jamii Forums mobile app
 
. Ukisema Trump anasimama na kutoa maelezo ya ventilators, madawa na mengineo, ukumbuke mwenzako yuko kwenye election year, he needs all the coverage he could get.
Mkuu hizo ndio cherry picking naziona kwako, kwani Wa kwetu hayupo election year? Naona kma una chuki binafsi na trump huoni positives yeyote ya yeye kma head of state kusimama na kutoa updates as Amiri jeshi Mkuu wakati wa crisis kama hii?

Nachoona unajaribu ku undermine role ya public presence ya Rais kwenye suala kama hili, hta sep 11 Rais Bush alienda site ili kuonyesha solidarity na wamarekani katika lile janga na kuwapa uniting factor na hope kma beacon ya nchi!! U don't undermine that.

Coordination nayosema ni ya Serikali kuu to bunge to halmsahauri/RCs yaani kila mtu na kauli yake hujui lipi uchukue lipi uache. Mkuu mmoja wa mkoa anashauri magari ya Dar yasifike huko, mikoa mingine inaruhsu bado hapo hapo wa Dar anashauri wasije huku Yaani chaos!! Kwanini hakuna directive moja juu ya inter-regional commuters?. Haya swala la barakoa tu Madaktari wakasema yao, waziri la kwake na RC la kwake?? Ssa cordination iko wapi hapo??

Coordination hakuna mkuu lazima tukubaliane hapa, ndio maana sintofahamu kila sehemu. Sasa hii inaweza kuwa cleared na formal directive ya Rais kwenye press releases za kila mara kutoa updates za hili suala na kuwa na chain of command inayoeleqeka sio hii ya sasa ambapo kila mtu amegeuka health consultant
 
Haha, ikiwa kama kigezo chako cha uwongozi ni Trump basi unanitia hofu kama siku wapinzani wakipewa nchi tutakuwa tumekwisha. Kusimama kwenye podium na kuongea haimaanishi you'll get the job done, how many time Trump ana backtrack alichokisema a day before au hata kwenye the same press conference.

Watu mmengangania hakuna coordination, Lakini ni eneo gani hilo ambalo hakuna coordination? Gov Order inatofauti kubwa na kiongozi fulani kusimama pale na kutoa matamko ya fanya hichi, usifanye kile. Kama ungeona wagonjwa wa covid wanaanguka na kufa barabarani, au hospitali zimeelewa hakuna vitamda au dawa, au hata shughuli za kila siku hazifanyiki, chakula hakuna labda mgekuwa na sababu ya kulaumu. But the system is working. Nakumbuka Wapinzani mlikuwa mnalalamika eti rais Magufuli ana husika na kila kiti kinachofanyika nchini mpaka mnasema hukumu za mahakamani anatoa yeye, leo hii mnataka aje aingilie mambo ya kitaalamu.

Mimi nadhani wapinzani itabidi msema ukweli maana hakuna namna nyingine, you guys mme-miss Magufuli, amekaa mbali sasa hakuna tena punching bag kama mliozowea.
 
Msikilize Rais wako anasema Fumigation haisaidii ilihali wizara ilisema inasaidia. Niliposema hakuna coordination ulibisha now what's this mkuu?. Je bado hujaona umuhimu wa Rais kujitokeza na kufita controversy kama hii??

2. Btw nmejitahidi sana kutokuwa partisan kwenye mjadala wetu sasa hii ya kusema wapinzani cjui madaraka inatoka wapi? Mijadala mingi ya JF inaharibiwa na hii issue ya uchama, hivi hatuwezi jadili mada bila kunyoosheana vidole kuwa ww ni CCM au upinzani?

3. Kuhusu trump pengine una chuki naye binafsi ndio maana huwezi ona zuri kwake. Tukiwa na bias opinion namna hii hatuwezi chukua positives za wenzetu licha ya mapungufu yao lukuki.
 
#COVID-19: TUWAJIBISHANE

Mnamo Tarehe 28/3/2020 niliwaeleza Watanzania kuwa nimemwandikia barua Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumshauri mambo makubwa 8 ili nchi yetu iweze kukabili maambukizi ya virusi vya Korona. Tarehe 4/4/2020 Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa Maalim Seif Sharif Hamad alizungumza na Wananchi kuwataka kujihadhari na virusi vya Korona. Hadi siku Mwenyekiti anazungumza Tanzania ilikuwa na wagonjwa 20 tu. Leo Tanzania ina wagonjwa 257 na Serikali imeripoti vifo vya watu 10. Kati ya Aprili 1 na Aprili 20, maambukizi yaliyotangazwa yamefikia 1,170%.

Kama Viongozi wa Upinzani nchini kwa wiki kadhaa sasa tumekuwa tunatoa ushauri kwa Viongozi wa Serikali na kuelimisha umma kudhibiti #COVID19TZA. Tumejitahidi kuunganisha Nchi yetu dhidi ya Virusi hivi. Sasa umefika wakati wa KUWAJIBISHANA.

Wakati Nchi ikiwa katika maambukizi mtu mwenye Mamlaka ya Juu kabisa katika Nchi yetu, Rais John Pombe Joseph Magufuli haonekani kuendesha mapambano kama tunavyoona kwa mataifa jirani kama Kenya, Rwanda, Uganda, Afrika Kusini nk. Mara chache ambazo Rais amejitokeza ametoa kauli zinazoonyesha kuwa COVID 19 sio tatizo na hivyo kushawishi watu kuendelea na shughuli za mikusanyiko ambazo zinakuza maambukizi. Pia tumeona Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na baadhi ya watu wa karibu na Rais wakihamasisha mikusanyiko ya watu.

Mwalimu Julius Nyerere alitafsiri Kitabu cha Shakespeare Merchants of Venice (Mabepari wa Venice). Kundi hili la Viongozi walioendelea kushawishi Watanzania kuendelea na shughuli za mikusanyiko, Mwalimu Nyerere angewaita Mabepari wa Vifo (Merchants of Deaths). #MerchantsOfDeaths ni watu ambao wakielekezwa kutofanya matendo fulani ili kuepuka maafa wao hufanya. Pia watu wenye Mamlaka ambao wanashindwa kutumia mamlaka yao kuzuia maafa. Vile vile watu wa imani ambao wanaaminisha waumini wao mambo ambayo husababisha maafa. Wanashtakika

Kutokana na maandalizi mabovu ya Serikali kwa Watumishi wa Afya - Madaktari, Manesi, Watumishi wa Maabara - maambukizi yamesambaa miongoni mwao na hata wengine kuanza kupoteza maisha. Licha ya Serikali kukusanya mabilioni ya Fedha kutoka Sekta Binafsi na yenyewe kutotenga Bajeti Maalumu ya kupambana na Korona, watumishi walio mstari wa mbele kwenye vita wanaachwa bila vifaa (PPE). Nchi yetu ipo kwenye hatari ya kupoteza wataalamu wengi wa Afya ambao wamesomeshwa kwa gharama kubwa na kwa muda mrefu. Watumishi hawa pia wanahatarisha familia zao.

Namna Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyokabili mlipuko wa Korona inathibitisha kauli kuwa Tanzania imekuwa na miaka 5 ya uholela, yaani 5 Years Of Incompetence. Mgawanyo wa Kazi wakati huu umekuwa;

- Naibu Waziri Afya: kuelimisha Umma maana ya Corona na kuvaa Barakoa

- Waziri wa Afya: Kutangaza Idadi ya visa vya Corona na vifo na kuelezea maamuzi mbalimbali ya Serikali

- Waziri Mkuu: Kukusanya michango ya Wadau (Serikali yenyewe haijaweka wazi Bajeti yake ya Corona

- Makamu wa Rais: Hajulikani alipo

- Rais: Kajificha Kijijini Chato huku akitaka Wananchi waendelee kwenda Kanisani na Misikitini

Hatuwezi kuendelea namna hii huku wagonjwa wanaongezeka, Watanzania wanapoteza maisha, huduma za Afya zinazidiwa na kupoteza wataalamu muhimu na uchumi unaanguka. Itabidi kuendelea kupambana na Korona huku tunawajibishana.

Namtaka Rais Magufuli afanye yafuatayo

1. Amwagize Waziri wa Fedha kupeleka Bungeni Bajeti ya Dharura kukabiliana na Korona na baada ya Bajeti hiyo Bunge lisimamishe vikao vyake mpaka Korona itakapokomeshwa nchini. Bajeti hiyo ihakikishe Wataalamu wetu wa Afya wanapata vifaa vya kuwalinda ili kupambana na Korona

2. Ahutubie Taifa mara moja na kuwataka Wananchi kuacha shughuli zao za kila siku na kwa kutumia Sheria ya Bunge kuifunga Nchi (partial lockdown). Wananchi wasaidiwe kwa mujibu wa mapendekezo tuliyoyatoa, kila kaya ipatiwe shs 300,000

3. Kama hawezi kuyafanya haya ajiondoe madarakani ili watanzania wengine wafanye hiyo kazi ya kulinda Nchi yetu.

Mwisho nawaomba Wanasheria nchini kuandaa mashtaka ya kukusudia kuua dhidi ya watu wote ambao wametoa matamko ambayo yaliwafanya wananchi waendelee na shughuli za kuambukiza virusi vya Korona.

Imetolewa na:

Zitto Kabwe

Kiongozi wa ACT Wazalendo
21 Aprili, 2020

#RaisTokaChato​
Ukitaka kutushauri watanzania au hata Serikali, tueleze mshauri wako wa mambo ya afya ni nani? Corona siyo sera ya chama ni jambo la kitaalamu. Huwezi kuamka unaanza kuishauri serikali. Taarifa za serikali zinatolewa na wizara ya afya. wewe unatoa ushauri ukitegemea TV na internet; yale unayosikia huko nawe unayaleta huku.
 
Msikilize Rais wako anasema Fumigation haisaidii ilihali wizara ilisema inasaidia. Niliposema hakuna coordination ulibisha now what's this mkuu?. Je bado hujaona umuhimu wa Rais kujitokeza na kufita controversy kama hii??

2. Btw nmejitahidi sana kutokuwa partisan kwenye mjadala wetu sasa hii ya kusema wapinzani cjui madaraka inatoka wapi? Mijadala mingi ya JF inaharibiwa na hii issue ya uchama, hivi hatuwezi jadili mada bila kunyoosheana vidole kuwa ww ni CCM au upinzani?

3. Kuhusu trump pengine una chuki naye binafsi ndio maana huwezi ona zuri kwake. Tukiwa na bias opinion namna hii hatuwezi chukua positives za wenzetu licha ya mapungufu yao lukuki.

Sasa ikiwa waziri mkuu alipewa maelekezo na maelekezo yakatekelezwa hapo wewe huoni kama kuna coordination? mara ya mwisho uliona lini fumigation inafanywa na idara yoyote ya serikali kuu au serikali za mitaa?

Kila nchi duniani inapita kwenye hili janga kwa kujaribu mbinu mbali mbali. Kama unafuatilia trend ya huu ugonjwa duniani utaona hakuna nchi inatumia mbinu moja au kutegemea mtu mmoja kupambana na huu ugonjwa. Kuna report imetoka juzi inasema hata ventilators sio chombo cha uhakika kupambana na Corona, na unaweza kuongeza uwezekano wa mtu kufa kuliko kumsaidia kupumua.

Dhana ya upinzani vs serikali, imejengwa zaidi na wanaojiita wapinzani. Kwa miaka mitano sasa nguvu kubwa imetumika kuweka utengamano hata kwenye mambo muhimu ya kitaifa. Hata Lissu aliulizwa kwenye Hardtalk, wewe ukiwa kama kiongozi wa upinzani kwanini unachochea kuni na kuleta taharuki kwa wananchi wakati ulitakiwa uwe ni kiongozi wa kuleta matumaini na kutoa watu hofu? Mifano ni mingi tu ambayo viongozi wa upinzani wanashindwa kuwa Non-partisan, tukiwaabia wananchi kuwa nchi ina chakula cha kutosha siku tatu tu, hapo tunawaambia wanachi nini? waanze punic buying na kuleta upungufu wa chakula?
 
1. Issue ya partisanship kwenye mjadala wetu umetoka wapi? Yaani tujaribu kuwa neutral kwenye mijadala ya kitaifa. Ukijibu kwa bias kwamba mimi ni mpinzani au CCM hutoweza kuwa rational kabisa kwenye mjadala ndio maana hutoona naitaja ccm kokote hapa so tuzingatie hilo.

2. Mkuu mifano ya coordination mbona mingi sana wewe umesema Rais anatoa directives hta akiwa huko chato na kwamba sio mpaka awe public. Nafikiti umesikia analalamika kwanini Data za waliopona hazitangazwi, anadai wamepona 100 ila waziri mkuu kasema ni 11 pekee sasa coordination iko wapi? Mkuu mbona unatetea kitu cha wazi kabisa? Contraction za ma-RC wa mikoa ile 3 na miongozo ya naibu waziri wa afya je huoni coordination hakuna kwenye mikakati?
 
Sidhani kama nimekulewa point yako No1, lakini niseme tu kuna muda wa kufanya siasa na kuna muda wa kuungana kwenye maswala ya kitaifa. Baadhi ya wanasasiasa wanashindwa kutofautisha hizi dhana mbili.

Point yako No.2 let's agree to disagree, mimi kwa mtazamo wangu najua changamoto kwenye kupambana na COVID-19 zipo lakini sio kama vile watu wanavyozijengea hoja mitaani. Kipindi hichi kelele zimekuwa nyingi na watu ku-punic. Mara lockdown, mara funga border, wengine mass testing na wengine rais toka Chato. Lakini ukweli ni kwamba, sio kila kitu lazima rais asimame aseme hadharani ndio watu wajuwe kama kazi inatendeka.

kwenye suala la wakuu wa mikoa na mawaziri, labda hilo swala linatakiwa uangalizi mpya hasa kwenye seperation of power. Wakuu wa mikoa wana mamlaka yao ndani ya mikoa yao ikiwa pamoja na maswala ya ulinzi, usalama na afya ya jamii. Mawaziri pia wana mamlaka yao kwenye maswala yanayohusu wizara zao. Lakini waziri mkuu yuko juu ya wote hao, na kamati za mambo ya COVID-19 ambazo zinaongozwa na huyo huyo waziri mkuu, anaweza kurekebisha kasoro zozote zinazojitokeza ikiwa pamoja na mgongano wa kauli, kama vile Wazuri mkuu alivyofafania kuhusu maswala ya Ibada na Sunday school pamoja na Madrasa.
 
kwanza naunga mkono hoja ya zitto kabwe maana kweli simuon makamu wa rais wa raisi mwenyewe zaid ya leo kusema labda aliposoma waraka wa zitto ndo kaamua kuongea yani haya mapambano bado tupo nyuma sana tena wauguzi wetu ndo wako kwenye hatari kubwa wala sijaona serikali ikitenga pesa ya dhalura kwenye jana hli wala bajeti yake kusomwa sasa najiuliza tunaelekea wapi maana hli swala hatujuai litaisha lini zaidi ya mungu peke yake sasa mkuu wa nchi naona na yy kaenda chato kukwepa maambukizi au ndo serikali imeamia huko jaman hli swala sio dogo ni mtambuka na mungu anasema jisaidie na mm ndo nikusaidie,naona sasa tudike mahali tuamue nn tufanye kupunguza kasi hii nchi yetu masikin sana uwezo wa kuwa na vitendea kazi bado havitoshi haya mapambano raisi ndo anatakiwa kuwa mstari wa mbele kwa janga hli na watu wake.
 
Wanasiasa wa Tanzania hii sijui huwa wanawaza nini. Rais ajitokeze wapi? Hivi kupambana Corona tunatumia mishale au bunduki kwamba sasa Mh Rais ajitokeze aongoze mapambano?

Wataalamu wa afya wanafanya majukumu yao hiyo inatosha. Na kuhusu ugonjwa ni jukumu la kila mmoja kujilinda huku tukifuata maelekezo ya serikali na wataalamu wake tena hata huyo Rais naye anapaswa kujilinda yeye kwanza kabla ya hajawaza kumlinda mwingine.

Suala la serikali ni bora mtu atuamabie wataalamu hawana vifaa na vitendanishi muhimu. Rais kutoka Chato haina umuhimu kwa sababu wajibu wake kama Rais anaweza kuutekeleza akiwa huko huko.

Tupunhuze maneno na kutafuta cheap popularity, yaani inakuwa al mradi tu Zitto aseme chochote ili asikike kuwa yeye anajali sana.

Ukweli usiofichika ni kwamba mfumo wetu wa maisha hauko tayari kwa hiyo lockdown inayopigiwa kelele.

Kila mtu atekeleze wajibu wake Rais kuwa Dodoma au Dar es Salaam haizuii kwa namna yeyote na hiyo hashtag ya #rais_toka_chato ni wazo la kipuuzi kutolewa na mwanasiasa mkubwa kama Zitto na inadhihirisha wapinzani bongo wapo kuongea ongea tu.
 
Back
Top Bottom