#COVID-19: Tuwajibishane

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,562
10,883
#COVID-19: TUWAJIBISHANE

Mnamo Tarehe 28/3/2020 niliwaeleza Watanzania kuwa nimemwandikia barua Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumshauri mambo makubwa 8 ili nchi yetu iweze kukabili maambukizi ya virusi vya Korona. Tarehe 4/4/2020 Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa Maalim Seif Sharif Hamad alizungumza na Wananchi kuwataka kujihadhari na virusi vya Korona. Hadi siku Mwenyekiti anazungumza Tanzania ilikuwa na wagonjwa 20 tu. Leo Tanzania ina wagonjwa 257 na Serikali imeripoti vifo vya watu 10. Kati ya Aprili 1 na Aprili 20, maambukizi yaliyotangazwa yamefikia 1,170%.

Kama Viongozi wa Upinzani nchini kwa wiki kadhaa sasa tumekuwa tunatoa ushauri kwa Viongozi wa Serikali na kuelimisha umma kudhibiti #COVID19TZA. Tumejitahidi kuunganisha Nchi yetu dhidi ya Virusi hivi. Sasa umefika wakati wa KUWAJIBISHANA.

Wakati Nchi ikiwa katika maambukizi mtu mwenye Mamlaka ya Juu kabisa katika Nchi yetu, Rais John Pombe Joseph Magufuli haonekani kuendesha mapambano kama tunavyoona kwa mataifa jirani kama Kenya, Rwanda, Uganda, Afrika Kusini nk. Mara chache ambazo Rais amejitokeza ametoa kauli zinazoonyesha kuwa COVID 19 sio tatizo na hivyo kushawishi watu kuendelea na shughuli za mikusanyiko ambazo zinakuza maambukizi. Pia tumeona Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na baadhi ya watu wa karibu na Rais wakihamasisha mikusanyiko ya watu.

Mwalimu Julius Nyerere alitafsiri Kitabu cha Shakespeare Merchants of Venice (Mabepari wa Venice). Kundi hili la Viongozi walioendelea kushawishi Watanzania kuendelea na shughuli za mikusanyiko, Mwalimu Nyerere angewaita Mabepari wa Vifo (Merchants of Deaths). #MerchantsOfDeaths ni watu ambao wakielekezwa kutofanya matendo fulani ili kuepuka maafa wao hufanya. Pia watu wenye Mamlaka ambao wanashindwa kutumia mamlaka yao kuzuia maafa. Vile vile watu wa imani ambao wanaaminisha waumini wao mambo ambayo husababisha maafa. Wanashtakika

Kutokana na maandalizi mabovu ya Serikali kwa Watumishi wa Afya - Madaktari, Manesi, Watumishi wa Maabara - maambukizi yamesambaa miongoni mwao na hata wengine kuanza kupoteza maisha. Licha ya Serikali kukusanya mabilioni ya Fedha kutoka Sekta Binafsi na yenyewe kutotenga Bajeti Maalumu ya kupambana na Korona, watumishi walio mstari wa mbele kwenye vita wanaachwa bila vifaa (PPE). Nchi yetu ipo kwenye hatari ya kupoteza wataalamu wengi wa Afya ambao wamesomeshwa kwa gharama kubwa na kwa muda mrefu. Watumishi hawa pia wanahatarisha familia zao.

Namna Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyokabili mlipuko wa Korona inathibitisha kauli kuwa Tanzania imekuwa na miaka 5 ya uholela, yaani 5 Years Of Incompetence. Mgawanyo wa Kazi wakati huu umekuwa;

- Naibu Waziri Afya: kuelimisha Umma maana ya Corona na kuvaa Barakoa

- Waziri wa Afya: Kutangaza Idadi ya visa vya Corona na vifo na kuelezea maamuzi mbalimbali ya Serikali

- Waziri Mkuu: Kukusanya michango ya Wadau (Serikali yenyewe haijaweka wazi Bajeti yake ya Corona

- Makamu wa Rais: Hajulikani alipo

- Rais: Kajificha Kijijini Chato huku akitaka Wananchi waendelee kwenda Kanisani na Misikitini

Hatuwezi kuendelea namna hii huku wagonjwa wanaongezeka, Watanzania wanapoteza maisha, huduma za Afya zinazidiwa na kupoteza wataalamu muhimu na uchumi unaanguka. Itabidi kuendelea kupambana na Korona huku tunawajibishana.


Namtaka Rais Magufuli afanye yafuatayo

1. Amwagize Waziri wa Fedha kupeleka Bungeni Bajeti ya Dharura kukabiliana na Korona na baada ya Bajeti hiyo Bunge lisimamishe vikao vyake mpaka Korona itakapokomeshwa nchini. Bajeti hiyo ihakikishe Wataalamu wetu wa Afya wanapata vifaa vya kuwalinda ili kupambana na Korona

2. Ahutubie Taifa mara moja na kuwataka Wananchi kuacha shughuli zao za kila siku na kwa kutumia Sheria ya Bunge kuifunga Nchi (partial lockdown). Wananchi wasaidiwe kwa mujibu wa mapendekezo tuliyoyatoa, kila kaya ipatiwe shs 300,000

3. Kama hawezi kuyafanya haya ajiondoe madarakani ili watanzania wengine wafanye hiyo kazi ya kulinda Nchi yetu.

Mwisho nawaomba Wanasheria nchini kuandaa mashtaka ya kukusudia kuua dhidi ya watu wote ambao wametoa matamko ambayo yaliwafanya wananchi waendelee na shughuli za kuambukiza virusi vya Korona.

Imetolewa na:

Zitto Kabwe

Kiongozi wa ACT Wazalendo
21 Aprili, 2020


#RaisTokaChato​
 
Trust me maamuzi mengi yanatoka humu JF, na sisi kwa sisi tuwajibishane!!!! nina uhakika 100% hili la partial lockdown lilipingwa na wanaJF wengi (tena wengine nakumbuka majina yao)...

Sijui sasa hivi wanawaza nini...ni kwa vile tu JF inazuia kuwataja members wengine..lasivyo leo ningewatajaaaaa woote...mmesababisha ugonjwa huu uenee!
 
Trust me maamuzi mengi yanatoka humu JF,na sisi kwa sisi tuwajibishane!!!! nina uhakika 100% hili la partial lockdown lilipingwa na wanaJF wengi (tena wengine nakumbuka majina yao)...sijui sasa hivi wanawaza nini...ni kwa vile tu JF inazuia kuwataja members wengine..lasivyo leo ningewatajaaaaa woote...mmesababisha ugonjwa huu uenee pumbav.u zenu!!!!!!!!!!
... huyu hapa Bia yetu mmoja wao. Hali imekuwa sio hali; mtumbwi unazama huo.
 
Zitto, siungi mkono hoja, kwa sasa tuko katikati ya Mapambano, huu sii wakati wa kunyoosheana vidole kulauniana, kushutumiana na kutafuta mchawi tuwajibishane, huu ni wakati wa kusimama pamoja, stand together united and fight as one.
P
Pascal Mayalla rafiki acha utoto, unisamehe! Utapambanaje hata gloves, mask, sabuni na maji huna? Mwenye kutoa vitu hivyo kafunga store haonekani?

Mna unite kivipi ebu twambie. Una unite wakati kauli anayo mtu mmoja hataki ushauri, how do you offer assistance? Kupanda kwenye pick up na msalaba kupita mitaani unaimba mapambio ya Bwana Yesu?

Shauri mtu afanyeje. Huyu Jiwe anaua watanzania and now we are going into millions some few days/weeks to come
 
Zitto, siungi mkono hoja, kwa sasa tuko katikati ya Mapambano, huu sii wakati wa kunyoosheana vidole kulauniana, kushutumiana na kutafuta mchawi tuwajibishane, huu ni wakati wa kusimama pamoja, stand together united and fight as one.
P
Kusimama pamoja ni pamoja na kushauri kama wanavyofanya wapinzani, Zitto na ACT wakiwemo.

Kama ushauri unapuuzwa huku madhara yanaongezeka,ni kwanini wahusika wasitakiwe kuwajibika?
 
Zitto, siungi mkono hoja, kwa sasa tuko katikati ya Mapambano, huu sii wakati wa kunyoosheana vidole kulauniana, kushutumiana na kutafuta mchawi tuwajibishane, huu ni wakati wa kusimama pamoja, stand together united and fight as one.
P
Mkuu hapo Zitto kamnyooshea nani mkono? Issue ni kwamba aliposhauri partial lockdown alipuuzwa leo ugonjwa umepaa.

Sasa yeye hana mamlaka ya kuamua chochote ndio maana ametoa wito kwa viongozi wenye mamlaka hayo kuchukua hizo hatua hilo ndio pekee anachoweza kushauri

Ila kama naye angekua na hizo authority alafu akaanza kulaumu subordinates wake au seniors wenzake ndio tungesema ananyooshea wenzie vidole.

Sasa mapambano ndio kma hayo kashauri kaya zisaidwe kiuchumi kupitia reserve tulionayo BOT ya $5 Billion kutusogeza kipindi hiki ili kuepuka maambukizi mapya. Sasa ulitaka afanyeje kama ushauri unapuuzwa na tatizo linaongezeka?? Asaidie mapambano kwa namna gani nyingine kuliko hili aliloshauri?
 
#COVID-19: TUWAJIBISHANE
Wakati Nchi ikiwa katika maambukizi mtu mwenye Mamlaka ya Juu kabisa katika Nchi yetu, Rais John Pombe Joseph Magufuli haonekani kuendesha mapambano kama tunavyoona kwa mataifa jirani kama Kenya, Rwanda, Uganda, Afrika Kusini nk.
Zitto, kwenye hili, sisi tuliamua kila nchi iendeshe mapambano kivyake vyake bila kuiga, kama hao marais wengine wanaendesha mapambano kwa kuonekana sio wao.

Kwanini Magufuli awaige wakati kuna njia nyingi za kuendesha mapambano na sio lazima mpaka kila mtu aone, issue ni kuona au kupambana?

P
 
Tumalizane kwanza na corona then tuwajibishane

Nchi ikivamiwa sio kwamba tunamtoa rais madarakani kwanza majeshi yanapambana kila mtu kwa uwezo wake then tukimaliza ndio tunaenda kwake kumwajibisha kwa uzembe.

Ila pamoja na mambo mengine yote kitendo cha Rais kwenda kukaa Chato kwenye vita kinaacha maswali mengi sana kama kweli tuna mtu mzalendo kwa taifa lake.
 
Nipo zangu Chato nimechill huku nawacheck nasema hiiiiiiii....
IMG_20200421_132652.jpg
 
Back
Top Bottom