Comparing: Lowassa vs Pinda

Comparing: Lowassa vs Pinda

Naona forum imeingiliwa MWIZI anasifiwa. Hivi hakuna viongozi wengine mpaka tuendelee kuwatamani hawa waliojipaka kinyesi? MWIZI ATABAKI KUWA MWIZI TU, endeleeni kuwasifia wezi wkt TZ imejaa viongozi wengi tu kuliko hawa waliopo kwenye system sasa hivi.
 
ukizungumzia uwajibikaji kwa maana ya day to day follow up mimi naona Lowassa anaiweza hiyo,ukiwa kiongozi hutawafurahisha wote kwani wengine utalazimika kuwaburuza ili mfike na hiki ndicho alichokuwa nacho yule jamaa na ndio kwa upande wa pili ilikuwa fimbo yake ya kuwadokolea watz rasilimali zao
Pinda yeye amedhihirisha ni kivuli tu kama Joka la Kibisa kwa jinsi asivyokuwa na kauli na maamuzi yenye mamlaka inayoendana na wadhifa wake
To conclude hawa ni watu tofauti sana LAKINI WOTE WAPO KATIKA DIMBI MOJA LA TOPE...WAMECHAFUKA!!!
 
Comments nyingi kwenye hii mada zinaonyesha wazi jinsi gani Wakuu walivyopiga kura uchaguzi wa juzi...

Yaani hivi kweli nchi hii haiwezi kuongozwa na watu wengine isipokuwa akina Pinda na EL tu?..:disapointed:
 
Kumbe ilihitajika sadaka kuiokoa sisiem katika sakata la richmond !!!! na kwa misingi hiyo mbuzi wa sadaka hubebeshwa madhambi yasiyo yake, tunaomba utujuze vizuri mkuu son of soil jinsi gani EL hahusiki na sakata lile na badala yake yeye a qualify kuitwa mbuzi wa sadaka ili tusiendelee kuisakama hiyo sadaka ya sisiem

UMBUZI WA SADAKA HUU HAPA SOMA HOTUBA YAKE KWA KIFUPI

Kwa kazi nzuri kwa maoni yao, wamewasilisha vizuri. Lakini nimesimama kuweka kwenye kumbukumbu kutoridhika kwangu na jinsi kazi hiyo ilivyofanywa. Mheshimiwa Dk. Mwakyembe ni Mwanasheria, tena Daktari alikuwa anafundisha Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa anafundisha ni "Natural Justice".

Mheshimiwa Spika, wewe ni Mwanasheria unafahamu suala la Natural Justice. Kwamba Kamati Teule imesikiliza watu wengine wote pamoja na wanaoita minong'ono ya mitaani, wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja kati ya watuhumiwa mle hawakunihoji hata siku moja.
Mheshimiwa Spika, nimesimama kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya Bunge mpaka ofisini kwangu hata kama wangeniita ningekwenda kwa miguu kama hamna gari na nilikuwa tayari kufanya hivyo.
 
munamuonaje PINDA-si mchapa kazi, anajiliza, analalamika maofisa kununua magari ya bei juu,hapingii rushwa kivitendo,ni ndumila kuwili (leo A kesho Z),anajifanya mtu wa kanisa,mtoto wa mkulima (bora angekuwa mtoto wa bilionea) anayechekelea nchii ikiangamia,

LOWASA-ni mchapa kazi anayeogopwa na maofisa wenzake serikalini (sifa muhimu),ana ujasiri na kujua maana ya cheo chake ni fisadi kivitendo (hana tofauti na PINDA asiyeupinga ufisadi).

hapa ni bora nchi kuwa na lowasa fisadi mchapakazi, kuliko PINDA mpalilia ufisadi asiyechapa kazi?
Kalale naona umechoka. Utaachiwa nchi hii jangwa na mashimo. Fisadi hana huruma na mtuu bidii yake kuchumia tumbo anatumia cover ya hard work kuharalisha ujambazi wake. Fisadi hafai ndg yangu, hapo umechemsha usimfagilie mwizi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kusema kweli Pinda anaudhi. Misimamo yake haijulikani kabisa. Waziru mkuu lazima uwe na misimamo yako na wananchi waijue. Kujiita tuu mtoto wa mkulima, kukataa magari ya bei mbaya wakati ofisini kwako waka wanaoyatumia haisadii kitu. Kuhusu Lowasa huwa simfagilii. Ukishatuhumiwa kwa ufisadi, hata uchapakazi wako unakuwa wa mashaka. Trust me, wapo watu wanajifanya mbele ya jamii wachapakazi huku wakitumia nafasi zao kujinufaisha wenyewe.
 
munamuonaje pinda-si mchapa kazi, anajiliza, analalamika maofisa kununua magari ya bei juu,hapingii rushwa kivitendo,ni ndumila kuwili (leo a kesho z),anajifanya mtu wa kanisa,mtoto wa mkulima (bora angekuwa mtoto wa bilionea) anayechekelea nchii ikiangamia,

lowasa-ni mchapa kazi anayeogopwa na maofisa wenzake serikalini (sifa muhimu),ana ujasiri na kujua maana ya cheo chake ni fisadi kivitendo (hana tofauti na pinda asiyeupinga ufisadi).

hapa ni bora nchi kuwa na lowasa fisadi mchapakazi, kuliko pinda mpalilia ufisadi asiyechapa kazi?
Kwa hii thred nimekushusha kiwango balaaaaa.Yani nafkiri humjui lowassa kiundani zaidi ya mimi niliyewahi kuishi kwake.Kwa taarifa yako huyu jamaa na Rostam mpaka sasa ivi ndo wanaongoza nchi na kampuni yao inaitwa CCM na JK na Pinda ni waajiriwa wao.Samueli sita walimnyima kazi ile ya mwanzo baada ya kuona kijana anafundisha wenzake kugomagoma.Sasa basi kwa taharifa yako Lowasa ni next level au kwa jina lingine ni mojawapo wa Tanzanians Tycoons.Lowasa ni mjanja sana katika michezo michafu kwa mwavuli wa kuongoza.Lowasa haibi million ila ni mkali kusimamia vimiradi vya wananchi vya mamilioni.Jamaa akikwapua anakwapua kuanzia figure za bilions na ni mjuzi balaa wa kujisafisha tena mbaya zaidi hadi makanisani.Sasa basi hapa ni the home of great thinkers na sio great talkertives.lowassa Hafai hata marehemu baba wa taifa alituonya dhidi ya huyu mtu bora mara elfu kumi hata makamba na ukilaza wake.
 
ukizungumzia uwajibikaji kwa maana ya daily to daily follow up mimi naona Lowassa anaiweza hiyo,ukiwa kiongozi hutawafurahisha wote kwani wengine utalazimika kuwaburuza ili mfike na hiki ndicho alichokuwa nacho yule jamaa na ndio kwa upande wa pili ilikuwa fimbo yake ya kuwadokolea watz rasilimali zao
Pinda yeye amedhihirisha ni kivuli tu kama Joka la Kibisa kwa jinsi asivyokuwa na kauli na maamuzi yenye mamlaka inayoendana na wadhifa wake
To conclude hawa ni watu tofauti sana LAKINI WOTE WAPO KATIKA DIMBI MOJA LA TOPE...WAMECHAFUKA!!!

mhh unauhakika?
 
IFUATAYO ni hotuba fupi aliyoitoa Waziri Mkuu Edward Lowassa katika Bunge mjini Dodoma leo (Alhamisi Feb. 7, 2008) asubuhi, wakati wa mjadala wa Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza Mchakato wa Zabuni ya Kuzalisha Umeme wa Dharura Ulioipa Ushindi "Richmond Development Company LLC" ya Huston, Texas, Marekani mwaka 2006:

"Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru sana kwa kunifanya msemaji wa kwanza katika hoja hii.

Lakini la pili, nimpongeze Dk. Harrison Mkwakyembe, Mwenyekiti wa kamati Teule kwa kuwasilisha kwa mbwembwe nyingi sana taarifa yake, mbwembwe zilikuwa nzuri kweli.

Kwa kazi nzuri kwa maoni yao, wamewasilisha vizuri. Lakini nimesimama kuweka kwenye kumbukumbu kutoridhika kwangu na jinsi kazi hiyo ilivyofanywa. Mheshimiwa Dk. Mwakyembe ni Mwanasheria, tena Daktari alikuwa anafundisha Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa anafundisha ni "Natural Justice".

Mheshimiwa Spika, wewe ni Mwanasheria unafahamu suala la Natural Justice. Kwamba Kamati Teule imesikiliza watu wengine wote pamoja na wanaoita minong'ono ya mitaani, wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja kati ya watuhumiwa mle hawakunihoji hata siku moja.
Mheshimiwa Spika, nimesimama kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya Bunge mpaka ofisini kwangu hata kama wangeniita ningekwenda kwa miguu kama hamna gari na nilikuwa tayari kufanya hivyo.

Hawa ni watu makini sana siwezi kuamini kwamba wanaweza wakafanya oversite kama hiyo. Kwa sababu katika kila hoja walizojenga wamesema Waziri Mkuu ilikuwa hivi. Kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza Waziri Mkuu wanasema uliotoa dokezo hili ni sawa sawa kweli? Kulikuwa na shida gani kwa mfano kufuata utaratibu wa Westminster kuthibitisha hapo unaposema mwenye Richmond ni fulani uka-lay on the table records na ushahidi kuwa ni fulani.

Mheshimiwa Spika, Taifa letu ni Taifa changa, lakini chombo hiki ndiyo mahali pa demokrasia pakubwa katika nchi pote, hapa ndipo penyewe. Kama katika chombo hiki haki haitaonekana kutendeka nchi yetu haitakwenda vizuri. Hapa ndipo tunategemea tuwaonyeshe umakini wetu, umahiri wetu katika mambo ya demokrasia. Kwa nhiyo nilichofanyiwa napenda kuweka kumbukumbu sawa kwamba naona si sahihi, nimefadhaika sana, nimedhalilishwa sana, nimeonewa sana katika hili.

Maana zimechukuliwa tuhuma zikaelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo. Mimi sijauliza. Kulikuwa na shida gani kuniuliza, kwa nini muamini minong'ono ya mitaani kuliko maelezo yangu. Sisi wote hapa ni wanasiasa tukianza kuamini minong'ono ya mitaani niambieni mwanasiasa atakayesimama. Hatuwezi, Tume imepewa muda wa kutosha lakini inashindwa kumuona mtu ambaye wanamtuhumu na wanamsema kwa kirefu sana.

Mheshimiwa Spika, lakini hata pale uliponinong'oneza ukaniambia una ushahidi wowote? Nilikupa ushahidi huo wa maandishi. Katika taarifa yao hakuna hata moja ya ushahidi ambao umetoka Waziri Mkuu. Kile kitabu cha majedwali kimejaa majedwali mengi pamoja na magazeti mpaka ya Udaku lakini maelezo ya Waziri Mkuu hakuna hata moja.

Mheshimiwa Spika, naamini ingekuwa ni heshima wangeiweka halafu wakasema tunakataa kitambulisho hiki kwa sababu hii na hii, hiyo ndiyo imejengwa hoja. Lakini kujenga hoja na kuja hapa Bungeni tunahutubia nchi nzima na kusema Waziri Mkuu amefanya hiki, amefanya hiki bila ya kumsikiliza nachelea kuuliza hivi mtu wa chini itakuwaje?

Mheshimiwa Spika, lakini nimetafakari kwa makini sana jambo hili nikajiuliza hivi kulikoni mpaka watu wazima wenye uwezo wao, watu maarufu wenye heshima zao, mpaka wafike mahali waache jambo la msingi kama hilo kulikoni? Mimi nadhani there is a wish which I am going to grant, ni Uwaziri Mkuu. Nadhani tatizo ni Uwaziri Mkuu. Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndio amefanya haya, tumuondolee heshima au tumwajibishe.

Mheshimiwa Spika, nimetafakari kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya Serikali yangu nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie ngazi. Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uwajibikaji lakini kutokubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya Bunge wa kumsingizia mtu.

Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kumshukuru sana Rais kwa heshima aliyonipa ya kutumikia nchi hii kwa Uwaziri Mkuu kwa miaka miwili.

Namshukuru sana Mheshimiwa Rais.

Nakushukuru wewe, nawashukuru Mawaziri na Manaibu Waziri, nawshukuru Waheshimiwa Wabunge na wanachama wa CCM tuliyosimamia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nashukuru
 
Lowasa anafaa sana kuwa raisi wa nchi hii sio pinda na kikwete
 
munamuonaje PINDA-si mchapa kazi, anajiliza, analalamika maofisa kununua magari ya bei juu,hapingii rushwa kivitendo,ni ndumila kuwili (leo A kesho Z),anajifanya mtu wa kanisa,mtoto wa mkulima (bora angekuwa mtoto wa bilionea) anayechekelea nchii ikiangamia,

LOWASA-ni mchapa kazi anayeogopwa na maofisa wenzake serikalini (sifa muhimu),ana ujasiri na kujua maana ya cheo chake ni fisadi kivitendo (hana tofauti na PINDA asiyeupinga ufisadi).

hapa ni bora nchi kuwa na lowasa fisadi mchapakazi, kuliko PINDA mpalilia ufisadi asiyechapa kazi?

mafisadi wanataka mtu anayelialia hadharani kama mtoto mdogo ndo awe PM.
 
Comments nyingi kwenye hii mada zinaonyesha wazi jinsi gani Wakuu walivyopiga kura uchaguzi wa juzi...

Yaani hivi kweli nchi hii haiwezi kuongozwa na watu wengine isipokuwa akina Pinda na EL tu?..:disapointed:

hii thread imeanzishwa kumsafisha lowasa kupitia JF.
 
Sometimes i'd rather have flu......than listening to politics!
 
inawezekana wajameni kuwa Lowassa ni mwizi mchapakazi,sawa. Ila watu wengi wenye upeo mkubwa kama wangu tunaamini kwamba huyu bwana mwizi mchapakazi ana influence kwenye chama na serikali kwa sababu ya pesa alizotuibia. Wanachama wenzie na hata maofisa wa serikali wanamuogopa kwa sababu ana pesa.Leo unamsifia kuwa ni mchapakazi hodari. Kweli inawezekana????????????????????????????????????
 
sorry!?

come again................?

ANA MSIMAMO NI SHUJAA ASIYETETEREKA SOMA HOTUBA YAKE AKIACHIA NGAZI HAPA
Mheshimiwa Spika, Taifa letu ni Taifa changa, lakini chombo hiki ndiyo mahali pa demokrasia pakubwa katika nchi pote, hapa ndipo penyewe. Kama katika chombo hiki haki haitaonekana kutendeka nchi yetu haitakwenda vizuri. Hapa ndipo tunategemea tuwaonyeshe umakini wetu, umahiri wetu katika mambo ya demokrasia. Kwa nhiyo nilichofanyiwa napenda kuweka kumbukumbu sawa kwamba naona si sahihi, nimefadhaika sana, nimedhalilishwa sana, nimeonewa sana katika hili.
Maana zimechukuliwa tuhuma zikaelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo. Mimi sijauliza. Kulikuwa na shida gani kuniuliza, kwa nini muamini minong'ono ya mitaani kuliko maelezo yangu. Sisi wote hapa ni wanasiasa tukianza kuamini minong'ono ya mitaani niambieni mwanasiasa atakayesimama. Hatuwezi, Tume imepewa muda wa kutosha lakini inashindwa kumuona mtu ambaye wanamtuhumu na wanamsema kwa kirefu sana
 
Back
Top Bottom