Kasheshe
JF-Expert Member
- Jun 29, 2007
- 4,694
- 793
Ndugu umemsahau sokoine na Nyerere wote hawa wameshawahi kuwa mawaziri wakuu...Sijajua pia kumuweka Malecela na Lowassa kwenye kundi moja?... for what .(kupenda vyombo vya habari)..nieleze chombo cha habari cha wakati huo ambacho kilikuwa kinambeba Malecela. Lowassa -mkurupukaji, Malecela siyo mkurupukaji thet dont fit in one bucket list..unless nieleweshe zaidi.
waberoya
Kuna kipindi Warioba aliulizwa ni kwa nini kwenye kipindi chako cha uwaziri mkuu ulikuwa hutumii majukwaa ya kisiasa... kutoa promises etc...
Majibu yake yalikuwa haya: "Kwa nchi kama Tanzania mkuu wa nchi ni rais wa Jamhuri... hivyo waziri mkuu kazi yake ni kusimamia serikali na kuhakikisha ahadi za Rais zinatekelezwa... kwa kawaida waziri mkuu sio wa kutoa ahadi tena..."
Hivyo properly waziri mkuu anatakiwa kukaa na timu yake... mawaziri, wakuu wa mikoa... wakuu wa wilaya... kuwa instruction kufanya mambo na kuripoti kwake... hii sio lazima kila siku kuwepo kwenye majukwaa ya siasa na mihadhara...
Warioba na Msuya walikuwa hivi... Malecela, Sokoine, Lowassa hawakuwa hivi...
Kwa kusema hayo... sijasema nani amekosea... bali nimesema style mbili za uongozi za mawaziri wakuu....
Nachelea kumzungumzia Nyerere kama waziri mkuu kwa kuwa nilikuwa sijazaliwa...