Comparing: Lowassa vs Pinda

Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda ndiye Rais wetu mtarajiwa hapo mwaka 2015 baada ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kumaliza muda wake.
 
Kwa kigezo cha UMAHIRI na UFISADI ni Lowassa, Kwa kigezo cha UMAKINI na UAMINIFU ni PINDA.

Chagua moja......

Tanzanianjema
 
Unajua mkuu mimi swali hili najiuliza kila siku,kwani magufuli amemkosea nini kikwete au ni kwa sababu yuko karibu sana na che Nkapa,au inawezekana hayumo katika mtandao!Maana naona kikwete amezamilia kabisa kumpoteza,lakini mie kila siku nasema kipaji hata siku moja akipotei.Si mnaona kampeleka uvuvi kumechangamka,najua ataipa jina wizara ya uvuvi mwisho wa siku watamnyang'anya,lets wait and see.pamoja na mapungufu yake,jamaa anafaa kuwa kiongozi wa watu.

Serikali iliyokuwepo ni ya kiswahili na Magufuli siyo mswahili unafikiri wataiva vipi wakati magufuli anataka kazi hataki longo,JK anamuogopa Magufuli anajua kwa vyovyote atamfunika kama mrema alivyomfunika H mwinyi,hongera tanzania kwa kumpata raisi mtalii na mpenda misiba,
 
kwa kigezo cha umahiri na ufisadi ni lowassa, kwa kigezo cha umakini na uaminifu ni pinda.

Chagua moja......

Tanzanianjema

hatutaki kiongozi yeyote goi goi na fisadi tanzania kwa sasa kwani muda wao umeshapita tunahitaji kiongozi mchapakazi na mwenye future
 
Jamani huyu Lwassa anakipi cha ajabu mpaka tumlinganishe na mwingine? igekuwa busara kama tugekuwa tunalinganisha embe kwa embe na pilipili kwa pilipili na sio embe kwa pilipili, nasema hivyo kwa misingi ifuatayo:
-kulinganisha fisadi na mwadilifu hiki siyo kipimo sahihi cha mlinganyo bali ni kitendo cha kusafishana mchana kweupe.
-Shule zinazo sifiwa ndicho kilikuwa ugomvi wa shilika la haki elimu na serikali hadi kutishiwa kufungiwa mala kibao, kwani hao jamaa waliona mapema wizi uliokuwa ukifanywa na wakuu wa shule na kamati zao za maendeleo, kwa kuwa na bei za kifisadi na kujenge madarasa ambayo yako chini ya kiwango
- Maamuzi ya fisadi Lwassa yalikuwa ya kukulupuka na kutofuata ushauri wa wenzie kwani pale Mwanza aliwahi kutolewa nishai na mkuu wa wilaya ya Ilemele.
Nahitimisha kwa kusema kuwa hakuna zambi mbaya ka kufisadi nchi yako na watu wengine kujidai wanakusafisha, tuige ya wanatarime mawe tu kwa mafisadi na wapambe wao mpaka wakome.
 
Tatizo la Lowasa ni ufisadi but jamaa ni mchapakazi kuliko Pinda
Huyu Pinda namuona kama ROBOT linaloendeshwa kwa remote

Lowasa ana tamaa zinazomfanya awe papara.Hajatulia. Mizengo mwoga kuact.
 
Ukweli nimeuona.

Japokuwa Lowasa alituhumiwa kuwa alishiriki sakata la RIchmond, Lowasa ni chapakazi. I can see the difference in short time.

Nachukia mafisadi, lakini Nahisi Lowasa ameshajifunza. Kama ni mtu mwenye utashi na akili atakuwa makini katika maamuzi ya Tenda.

Naomba au Nashauri apewe Unaibu Uwaziri Mkuu. Hii inawezekana. Hata Kipindi kile Mzee Ruksa alimpa Mhe Lyatonga Mrema Unaibu.

Hapo vipi wadau


Hoja kama hizi ni za kulipuuza taifa na kujitengezea mazingira ya kuamini kuwa Tanzania haina watu wenye uweza wa utawala. Utaratibu wa kuwabadilisha watu kutoka sehemu moja kwenda nyingine pale walipoharibu ndipo kulikozifikisha nchi nyingi masikini kuwa masikini zaidi.

Wapo Watanzania wengi zaidi ya Pinda wenye uwezo. Wapo wengi wenye uwezo kuliko Lowasa na waliowasafi wasiokula bila kunawa.

Tujifunze kuipenda nchi yetu na kuona kuwa tunaweza kuitawala na kuiendeleza bila kuangalia tu kuwa huyu ni Mwezetu au La.

Nahitimisha kwa kusema kuwa suala la kupwaya kwa Pinda kisiwe kisingizio cha kumtafuta Lowasa yuko wapi.

Tusifanye makosa kama haya!
 
Wote hakuna kitu.

Shule alizohimiza Lowassa ni ujinga mtupu. Nashindwa kuelewa mtu wa ngazi ya waziri mkuu anaposhindwa kuelewa kwamba shule alizokuwa anazishabikia ilikuwa kama kufukuza upepo,kwa maana kwamba si kitu,ni upuuzi mtupu. Shule zisizo na maabara, maktaba, mabweni wala mazingira mazuri ya kusomea ni shule gani.Hebu waza kidogo tu,ni wahitimu wa aina gani wanaotoka kwenye shule hizo,kama sio uozo tu.

Zaidi ni kwamba hata udikteta wake ulikuwa wa kijinga. Nahisi alikuwa anautumia kuficha madhambi yake. Nashindwa kuelewa kwa nini mtu kama yeye alishindwa kuelewa kwamba udikteta ule ungeathiri utendaji kazi wa wale waliokuwa chini yake. Watendaji wangetekeleza kama 'robots',na hata kama katika maagizo mengine wangeona kuna makosa ya dhahiri, wangetekeza tu,na matokeo yasingekuwa mazuri.

Kwa hiyo 'to me they are swimming in the same boat.'
 
Lowasa ana tamaa zinazomfanya awe papara.Hajatulia. Mizengo mwoga kuact.

Pinda ata act vipi wakati hao hao kina Lowassa bado wanaongoza nchi 'kimtindo'

Huwa najiuliza hivi watanzania ndio tumeumbwa kuwa wepesi wa kusahau kiasi hiki? Hivi leo tumesahau kwamba LOWASSA ni MWIZI, FISADI asiyestahili huruma ya aina yeyote! Ptuu! Tuliambiwa EL anatumia magazeti kumjenga nadhani hata mwanzilishi wa thread hii alikuwa na malengo hayo hayo! Kama EL alijenga shule hizo za Kata ni bora akazibomoe na tuendelee kuwa wajinga hadi siku tutayopata mtu wa maana wa kusimamia ujenzi wa shule huku koti lake likiwa safi.

Huyo Magufuli mnayemsifia na yeye ni FISADI la nguvu! Si ndio huyu alisimamia kwa 'ufanisi' zoezi la kuuza Nyumba za Serikali. Waulize Makandarasi namna alivyokuwa anawapa masharti magumu hadi watoe 'milungula' ili wapewe kandarasi! Si ndiye huyu huyu alikuwa KILA KITU pale Wizara ya Ujenzi. Yeye ndiye alikuwa Waziri, Katibu Mkuu, Mkurugenzi wa TANROAD, CEO wa Wakala wa Majengo ya Serikali. Tumesahau kuwa huyu ndiye alikuwa akigawa nyumba za Serikali kwa ndugu zake kama pipi akiwemo 'Malaya' wake aliyezaa naye mtoto mmoja. Hivi ule ugomvi wa Mawaziri wawili ndani ya Serikali moja tumeshasau chanzo chake? Mwandosya kwa kutumia wataalam wa Wizara yake walitoa kibali cha kusafirisha zile meli, akaja huyu huyu Magufuli 'wenu' na kutamka zile boti zitapita kwenye barabara "over my dead body" kisa ETI kina Dewji walimpa Mwandosya PESA za kumsaidia kwenye uchaguzi kwa hiyo nayeye akaweka masharti lazima apewe. Zile boti zilisafirishwa kwa kupitia Kenya mbona hatujasikia hizo barabara za Kenya kama zimeharibika? Unataka kumpa uPM mtu ambaye hajui hata collective responsibility!

Kumzomea Pinda sasa hivi ni 'kumuonea' Hana meno yoyote ya kung'ata. Hivi kigugumizi alichonacho JK cha kushindwa kushughulikia ufisadi wa EPA, Richmond, UVCCM. Hivi ile hotuba yake ya masaa manne kasorobo pale Dodoma aliongea nini cha maana zaidi ya kuonyesha kuwa hakuwa na majibu kwa maswali wanayojiuliza Watanzania! Nilikuwepo pale Kilimanajaro Hotel siku RA anatoa tamko kuhusu ule msaada aliotoa kanisani na fedha alizompa Mtikila. Huwezi amini lakini huyo RA aliongea na JK kwa simu sio chini ya mara tano kwa kipindi kisichozidi nusu saa. Leo mnataka Pinda aamke asubuhi aseme weka ndani MAFISADI wote. ATAUPATA WAPI HUO UBAVU. Siku ile anaongea kuhusu mradi wa Meremeta pale bungeni, 'body language' ilikuwa ikitutamkia Watanzania kuwa, "Huku nilikoletwa najuta kwa nini nilikubali na ningeweza kutoka ningetoka ila mlango wa kutokea haupo" JK angekuwa na NIA SAFI ya kuisafisha SERIKALI yake naamini PINDA ni chaguo sahihi. Kama alivyotamka mwanzoni wakati wa kukubali wadhifa wa uWM, Pinda alisema kuwa yeye si mwanasiasa! Kimsingi yeye ni mtendaji zaidi. Sasa atatenda nini wakati Bosi wake ndio kawekwa madarakani na hao Mafisadi! HAJIPENDI?!

Mwalimu wakati akimnadi Mwinyi mwaka 1985 alisema kuwa, "Mwinyi hana makundi" akimaanisha ni hatari sana kwa Rais kupelekwa Ikulu na makundi. Sasa kinachomtafuna JK leo ni kundi lake la 'mtandao' ambalo kwalo kama si mwanachama huna nafasi kwenye mfumo mzima.

Ukiangalia nyuma utaona kuwa Mwinyi na Mkapa walivurunda sana katika kipindi cha pili cha uongozi wao. Sasa huyu mwuungwana, filimbi pyeee! Madudu! Hivi atakaporudi madarakani awamu ya pili! SIPENDI KUWA MTABIRI lakini nikifikiria NAHISI HAJA KUBWA!

Mungu ibariki TANZANIA (Sina imani kama na 'nchi' ya Zanzibar imo humu)
 
WOTE HAWAFAI!!!!!. WALA HAWATAFAA! WHAT IF PINDA ANAFANYA KAZI BILA VYOMBO VYA HABARI(HATAKI POPULARITY)?. HUYU MWINGINE(LOWASA) NI MUUAJI NA IMETHIBITIKA HIVYO!

WOTE HAWAFAI-PINDA KASHINDWA KUFANYA LOLOTE KUHUSU UFISADI

waberoya
 
Wote watu wazima hovyo tu. Mmoja kuna ushahidi tosha kwamba ni fisadi na mwingine bado tunaufanyia kazi ushahidi wa kuthibitisha naye ni fisadi maana kishatoa kauli chungu nzima ambazo zinaonyesha anawatetea au kuwaogopa mafisadi.
 
kubadili mtu mmoja hakuwezi kusaidia kwani watu aliokuwa anafanya nao kazi EL ndo wale wale anaofanya nao kazi Pinda, hivyo kuona mabadiliko ni vigumu sana ndio maana wote wanaonekana hawafai.
 
WOTE HAWAFAI!!!!!. WALA HAWATAFAA! WHAT IF PINDA ANAFANYA KAZI BILA VYOMBO VYA HABARI(HATAKI POPULARITY)?. HUYU MWINGINE(LOWASA) NI MUUAJI NA IMETHIBITIKA HIVYO!

WOTE HAWAFAI-PINDA KASHINDWA KUFANYA LOLOTE KUHUSU UFISADI

waberoya


..you analysis..is perfect...mimi nilitaka kumlaumu pinda lakini umenikumbusha point moja muhimu sana..kuwa kwa miaka zaidi ya kumi...mtandao utendaji wao umetawaliwa na ukaribu na wana habari......lowassa kwa mfano tangu akiwa waziri wa ardhi alikuwa hafanyi any big announcement kama watu wa press hawajafika....

kwa pinda najua anatawaliwa na ethics..kwani amekuwa clerk kwennye cabinet tangu enzi za mwalimu..na anajuwa namna prime minister anavyotakiwa ku behave..nchi hii rais ndio mtendaji..waziri mkuu unatekeleza maagizo yake na kusimamia serikali.....waziri mkuu hatakiwi kuwa na ambition za wazi za urais...utendaji wa kimya wa waziri mkuu pinda ndio sifa za kufanya waziri mkuu kudumu...kwani anakuwa na nidhamu..na kuwa tayari kubeba lawama zisifike kwa rais...angalia utendaji wa warioba,kawawa,sumaye..pinda...unashabihiana..kwa karibu....

rais populist kama kikwete anayehusudu umaarufu wa bei nafuu kwenye magazeti anapokuwa na waziri mkuu kama lowassa....inafanya nchi inakuwa ina ROADSIDE DECLARATIONS nyingi[maagizo mengi]...hadi watendaji wanachanganyikiwa......tofauti na sasa ambapo PINDA ANASUBIRI MAELEKEZO YA RAIS ..LAIKINI BAHATI MBAYA RAIS ATOE MAELEKEZO YEYOTE ZAIDI YA MISAMAHA.....SASA PINDA ANABAKI HANA KAZI ...ZAIDI YA ILE YA KIKATIBA YA KUSIMAMIA UTENDAJI WA SIKU HADI SIKU WA SERIKALI......AMBAYO NI YA KIKATIBA NA HAIHITAJI..KUWA WAZI KWA VYOMBO VYA HABARI......

KWA USHAURI TU KWA PINDA ...NADHANI HII HALI ITAMUUWA KISIASA....NA SASA KUNA VACUUM OF POWER KWA KUWA INAONEKANA RAIS ANATAKIWA KUSAIDIWA BAADHI YA MAJUKUMU MAZITO AMBAYO ANAKUWA MZITO..KUYAFANYA...NI JUKUMU LA PINDA NA SHEIN KUINGILIA KATI NA KUTEKELEZA BAADHI YA MAJUKUMU YA KIRAIS...BADALA YA KUKAA KUSUBIRI MAELEKEZO YA RAIS...

TULIKUWA TUKIFIKIRI KUWA MWINYI ALIKUWA MZITO KUTOA MAELEKEZO ....LAKINI ALIKUWA MZURI KUJUA ANAHITAJI WATU WA AINA GANI WA KUWAPA MENO ILI SERIKALI IONEKANE..NDIO MAANA ALIPOGUNDUA WARIOBA ...NI MTENDAJI LAKINI ASIYEPENDA UMAARUFU..or something like that..ALIWEKA WATENDAJI AMBAO WANGEWEZA KUFUNIKA UPOLE WAKE KAMA ..MALECELA NA MREMA ..na akawaacha wafanye kazi.....sasa kikwete hili hataweza kwa kuwa anataka mtendaji aonekani ni yeye...sifa apewe yeye...LAKINI LAWAMA ..ziwaendee wengine.....hili anahitaji watendaji DODOKI.....
 
..kuhusu john pombe magufuli anafaa kuwa waziri mkuu au rais baada ya kikwete...nchi hii inataka mtu authorative..si mtu kama george michael.....

Tatizo ni lile lile na huyu naye anapenda kaumaarufu..na hapendi kupewa lawama sizizo zake...hataweza kabisa kuwa waziri mkuu wa kikwete wakaelewana...hawaongei lugha moja.....[kiutendaji]
 
Nadhani ukitaka kuwalinganisha vizuri mawaziri hawa wakuu unatakiwa pia kufuatilia utendaji wa mawaziri wakuu wastaafu.... mfano... Sumaye, Malecela, Msuya, Salim A. Salim. Warioba.

Kwa kifupi sana utendaji wa kuongea na kusikika kwenye vyombo vya habari... nimeuona kwa Lowassa na Malecela.

Utendaji kupitia kwa mawaziri na Goverment system bila kupiga makelele mengi while wengi wakidhani waziri mkuu muhusika hafanyi kazi nimeshuhudia kwa Msuya na Warioba.

Mpaka sasa sina hakika... maana kwa hakika muda ni mfupi sana.... sijajua kama Pinda anafiti vizuri kwenye kundi la Msuya na Warioba au vipi...

Lakini kwa hakika mtoa hoja anatoa ujumbe mzuri tu kwamba Pinda hayuko kwenye kundi la Lowassa na Malecela.

Nilichosema ni kushabihiana kwa utendaji sisemi... Lowassa na Malecela wako sawa, kwa nidhamu zao, au kwa mitizamo yao etc. etc. etc...

Mwisho Magufuli hana sifa za kuwa waziri mkuu mzuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania... nawashangaa watu wanaodhani huyu bwana anafaa...
 
Nadhani ukitaka kuwalinganisha vizuri mawaziri hawa wakuu unatakiwa pia kufuatilia utendaji wa mawaziri wakuu wastaafu.... mfano... Sumaye, Malecela, Msuya, Salim A. Salim. Warioba.

Kwa kifupi sana utendaji wa kuongea na kusikika kwenye vyombo vya habari... nimeuona kwa Lowassa na Malecela.

Utendaji kupitia kwa mawaziri na Goverment system bila kupiga makelele mengi while wengi wakidhani waziri mkuu muhusika hafanyi kazi nimeshuhudia kwa Msuya na Warioba.

Mpaka sasa sina hakika... maana kwa hakika muda ni mfupi sana.... sijajua kama Pinda anafiti vizuri kwenye kundi la Msuya na Warioba au vipi...

Lakini kwa hakika mtoa hoja anatoa ujumbe mzuri tu kwamba Pinda hayuko kwenye kundi la Lowassa na Malecela.

Nilichosema ni kushabihiana kwa utendaji sisemi... Lowassa na Malecela wako sawa, kwa nidhamu zao, au kwa mitizamo yao etc. etc. etc...

Mwisho Magufuli hana sifa za kuwa waziri mkuu mzuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania... nawashangaa watu wanaodhani huyu bwana anafaa...

Ndugu umemsahau sokoine na Nyerere wote hawa wameshawahi kuwa mawaziri wakuu...Sijajua pia kumuweka Malecela na Lowassa kwenye kundi moja?... for what .(kupenda vyombo vya habari)..nieleze chombo cha habari cha wakati huo ambacho kilikuwa kinambeba Malecela. Lowassa -mkurupukaji, Malecela siyo mkurupukaji thet dont fit in one bucket list..unless nieleweshe zaidi.

waberoya
 
Pamoja na faults zake Lowassa is a hands on leader tafsiri ambayo pia itamletea shida anaposema hajui yalioendelea kuhusu Richmond.
 
Pinda hakuwekwa hapo ili abadilishe kitu...Hivyo kudai kuwa anashindanishwa na Lowassa na huku mwenyewe akisema wazi kuwa hakuja kubadilisha chochote bali kuendeleza yale ya Lowassa.

Kwa mwanzisha mada hii...Ni wazi kuwa kwake yeye ni halali kuwafananisha na kuwashindanisha hawa watu.

Kwangu mimi kufanya hivyo ni sawa na kusema kuwa nani mwenye uwezo mkubwa zaidi wa kulinda ule ufisadi uliokwisha fanywa.

Kwa style ya ufanyaji kazi wa Lowassa..Ni wazi kuwa kama ni fisadi basi hata kuulinda ataulinda kwa nguvu zake zote...Licha ya kwamba ni mchapa kazi...Bado ana tamaa na huruma kwa masikini inahitaji BIG HEART.

Kwa upande wa Pinda...Hapo bado mjadala huu ni wazi umeanza kwasababu ya karata ya kisiasa za ccm ambazo ni kama zile za Saddam na baath party pale ambapo walikuwa mabingwa wa kubuy time na kumanipulate news...Nadhani mnakumbuka hata yule waziri wao wa mambo ya nje na mawasiliano alipokuwa akidai hakuna wanajeshi wa marekani iraki.

Na viongozi wetu wanadai hakuna rushwa....Na wananchi wanaamini.....Mwingine ni RICHMOND NA MWENZAKE ANADAI ISSUE HIZO NI USALAMA WA TAIFA...Sasa wanataka kuwalinganisha Lowassa na Pinda kuwa nani ni mchapa kazi kama vile yale matatizo tuliyokuwa tukiyazungumzia miezi na hata miaka kadhaa iliyopita nayo yamepita na kumalizwa na sasa tunaendelea vyema tu.

Wameshasahahu EPA ,RICHOMD, KIWIRA NK...Sasa mambo ni shwari na wanataka kuona kama Lowassa anaweza kumpindua Pinda again....

Halafu mada hii ipo hapa jf...Tena inafurahiwa tuuu.
 
Huwezi kufananisha kizima na kilichooza,
Hapo hapana adhima, watu watakupuuza,
Utajivunjia heshima, na wengi watakubeza,
Kizima na kilichooza, vigumu kufananisha!

Uongozi sio sura, wala kujifagilia,
Uongozi ni hijra, ubinafsi kukimbia,
Ukawa mtu wa shura, umma kuutumikia,
Kizima na kilichooza, vigumu kufananisha!

Uongozi si ukubwa, ukawa Kilimanjaro,
Kwa kugawa ubwabwa, na hao ng'ombe wa Njoro,
Vya kwako vikabebwa, vya wenzako kuwa kiporo,
Kizima na kilichooza, vigumu kufananisha!

Uongozi si akili, bali yataka pia roho,
Sawa kuthamini mwili, ila moyo uwe joho,
'siwe kuabudu mali, Jeta na mkubwa mroho,
Kizima na kilichooza, vigumu kufananisha!

Uongozi si hasira, yako yakifichuliwa,
Kutuma kina majura, mtu wakamshambulia,
Hapo waonesha si bora, hufai kutoa daawa,
Kizima na kilichooza, vigumu kufananisha!

Uongozi kutumikia, sio tu kutumikiwa,
Ukubwa kunyenyekea, sio mali kunyemelea,
Cheo dhamana ikiwa, fukara huwa bora,
Kizima na kilichooza, vigumu kufananisha!
 
Back
Top Bottom