CLOUDS FM warusha live clip ya Lwakatare

CLOUDS FM warusha live clip ya Lwakatare

Status
Not open for further replies.
Wewe unaewashangaa clouds fm inabidi tukuulize uraia wako kwakuwa walichokifanya ndicho wamekuwa wakikifanya siku zote.
Kwangu mimi hii si habari ya kushangaza ama kushtua kwa viwango vya habari.
 
Hiyo clouds ijiandae mapema kabla ya 2015 kuhamishia shughuli zake Msumbiji. Pumbav kabisa.
 
mimi pale nilikuwa nawakubali masoud kipanya na fina mango toka walivyoondoka hao basi waliobaki wote 0714 zimeharibika kasoro braza G tu!
 
Na hili nalo litapita, 2015 tutafika.
*Long live Dr Slaa*
 
CCM nchi hii imewashindwa tena kwa haya mnayoyafanya nina imani hata mkifanya zuri mtaonekana wabaya tu mmekuwa na tabia mbaya sana na sisi watanzania tumeshagundua kwani kila likitokea jambo ambalo ni aibu kwa taifa haraka mnatafuta kijimambo au kiloja cha upande mwingine ili kuwafanya watu wasahau jambo kubwa ambalo limetokea sasa endeleeni sana laana kubwa inawasubiri just time will tel, na katika hili mtaumbuka tu soon,

[h=5]"mtu anapokaribia kufa hawezi kuona wala kusikia tena mambo ya ulimwengu huu".
this is CCM.[/h]
 
Safi sana,na ngoja iwekwe ITV kabisa ili watanzania wajue ukweli,wauaji wakubwa hawa. Wameenda kumua kijana wa morogoro,wamemtia kilema kijana wa igunga na sasa wamemtoa jicho kibanda

akili za kimagamba. subiri muumbuke na video yenu inayosikika mpaka honi za bodaboda.
 
Muda huo huo wa jahazi kuna Sundowner MagicFM wako critical and ethical. Pia radio one FM nao wanakueaga na kipindi kizuri muda huo huo kinachambua mambo yaliyojiri kwa siku. Kuanzia saa kumi jioni mimi magic wakiweka tangazo nahamia radio one and vice versa. Nilishasahau jahazi na propaganda zao za ccm
 
yaan hata hujui...ni jf au goutube?..km hujui video ukisha upload huwezi kuizuia mana kila mtu anakuwa na acces nayo..ungemlaumu aliyeupload...ni makosa kwa clouds kucheza video kwa kisingizio eti iko youtube..nia ni kuchafua si kutoa habari na kujenga chuki dhidi ya anayetuhumiwa...

wangeweka na ile ya shehe ilunga.
 
Anayetaka kuiskia hyo video aende kwenye thred inayoenda kwa taito chadema hapa lwakatare alikuwa anamaanisha nini?
 
Great Thinkers wanashangilia hii video kuwekwa hapa JF lakini wanataka Clouds FM wasiitangaze?

That's a double standard. Kama haifai kutangazwa na Clouds ina maana haifai kuwekwa JF pia.

JF unaweza kutumbukiza humu utumbo bila hata kufanya utafiti, ndio maana Usernames nyingi ni fake. JF pia haijasajiliwa kwa sheria zetu hapa nchini. Chombo kama CLOUDS FM ambacho kinapaswa kuwa na wahariri na wataalamu mbalimbali. Hili ilitakiwa walione, juzi tu wamekumbana na adhabu kali kwa kuruhusu kipindi kinachoshabikia ndoa za jinsia moja!
 
Nimefungulia radio na kumsikia Kibonde akiwa anasoma taarifa iliyoandikwa katika gazeti la Mwananchi juu ya polisi kumkamata Lwakatare. Muda mfupi wakaweka audio ambayo iliwekwa humu jamvini. Hivi ni sahihi CLOUDS FM kuiweka public hii audio? Je itakuwaje kama itathibitika hii video and audio ni fake?.
Huyu Kibonde si anatafuta u-dc!!
 
Hivi ile Ya Dr Uli. Nayo ilirushwa hewani na vituo vya redio?
 
Hao ndio clouds fm super brand. Kipindi cha maana ni sports extra tu, labda na top twenty na Njia Panda.
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 14 MACHI, 2013
Ndugu waandishi wa habari,
Tumewaita hapa leo, ili kupitia kwenu tuweze kutoa taarifa inayohusu kukamatwa kwa mmoja wa
viongozi wa chama chetu, Wilfred Lwakatare, Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama, aliyekamatwa jana
tarehe 13 Machi 2013, ofisini kwake makao makuu ya CHADEMA.
Jeshi la polisi linasema limemkamata Lwakatare likimtuhumu kuhusika na mashambulio ya watu
mbalimbali kutokana na ushahidi uliopo kwenye walioita, viedo ambayo pia imesambazwa kwenye
mitandao ya kijamii.
Kwanza, tunapenda kuwaambia umma wa watanzania na watu wote duniani kwamba, CHADEMA
hakina nia yoyote ya kuzuia polisi kutenda kazi zake, iwapo watakuwa wanafanya hivyo kwa mujibu
wa sheria.
Bali, tunachoeleza hapa ni jinsi polisi na vyombo vingine vya dola vinavyoshiriki katika
kutengeneza paropaganda chafu dhidi ya CHADEMA za kuwahusisha viongozi wa CHADEMA na
unyama unaoendelea nchini wa kutesa watu, kupiga, kung’oa kucha na baadaye kuwatekeleza
wakiwa nusu mfu.
Mpango huu ulianza katika tukio la kutekwa kwa Dk. Steven Ulimboka, ukaenda kwa Mwandishi wa
habari, Daudi Mwangosi na baadaye kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda; na
kwa bahati mbaya sana, kwa namna moja au nyingine, mkakati huu umekuwa ukilihusisha jeshi la
polisi katika hatua za utekelezaji wake.
Kuweka kumbukumbu sawa, tunaweza kurejea suala la kuuawa kinyama kwa Mwangosi, unyama
uliosimamiwa na kufanikishwa chini ya uangalizi wa kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael
Kamuhanda.
Mara baada ya tukio hilo, jeshi jeshi la polisi kupitia kamishana wake, Paul Chagonja lilitoa kauli
kuwa Mwangosi alilipuliwa na kitu alipokuwa anawakimbilia polisi kujisalimisha akitokea kwa
wafuasi wa CHADEMA, jambo ambalo limethibitika kuwa halikuwa na ukweli hata kidogo.
Mpaka sasa, jeshi la Polisi halijamchukulia hatua zozote za kisheria Kamhanda aliyesimamia na
kufanikisha kifo cha Mwangosi, pamoja na ushahidi wa kuhusika kwake kuwepo wazi.
Aidha, pamoja na ukweli uliobainishwa na tume zote zilizotumwa kuchunguza suala la Nyororo
Iringa, kusema Polisi walivunja sheria, walitumia nguvu isiyohitajika, bado mpaka leo hii
wanachama 42 wa CHADEMA wanashikiliwa na polisi mkoani Iringa kuhusika na vurugu za Nyololo,
Mufindi, Iringa. Waandishi mtakumbuka kuwa Taarifa ya Kamati ya Nchimbi ilitofautiana kabisa na
Taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu nay a MCT. Baada ya kazi ya Tume na Kamati hizo hakuna
Taarifa hata mmoja imetolewa na Polisi, walsa hakuna watu waliohojiwa tena
2
ukiaachawaliokamatwa kabla ya Taarifa za Tume hizo. Wala sijaona kwa bahati mbaya vyombo vya
habari vikichambua Taaarifa hizo kwa kina,
Katika nyakati mbalimbali, CHADEMA tumefungua jalada Polisi, na nyingine amezifungua Mhe.
Lwaklatare mwenyewe akilalamikia mchezo mchafu tunaofanyiwa ikiwa ni barua kuandikwa kwa
majina yetu, yenye sura ya kutuchafua. Mojawaopo ikidhaniwa kuandikwa na Rwakatare mwenyewe
akiomba Tshs 200 millioni kwa ajili ya vijana anaodhaniwa kuwaleta toka Tarime kwa ajili ya Igunga.
Hadi leo Polisi hawajamhoji Lwakatare mwenyewe, wala hatujasikia upepelezi wowte ukifanyika.
Aidha tulitoa Taarifa ya mtu aliyepewa bunduki wakati wa uchaguzi wa Igunga akituhumu kuwa
amepewa bastola hiyo kwa lengo la kudhuru wakati wa Kampeni ya Igunga. Tumetoa mpaka nay a
Bastola husika na mahali ilipotengenezwa. Polisi hadi leo hawajatoa Tamko lolote kama Bastola
hiyo iliyotengenezwa China imesajiliwa kwa jina la nani, na hivi sasa ipo kwa nani. Lakini kwa tukio
tu la Lwakatare na picha yake kubandikwa kwenye Mtandao, Polisi tayari wameisha kumkamata. Ni
dhahiri kuna mchezo unachezwa dhidi ya CHADEMA, na Polisi kuiingizwa au kwa kujua au
kutokujua katika mtego huo.
Sasa hapo mnaweza kujiuliza, hapo haki ipo wapi? Yaani waliotajwa na tume yaani polisi – wapo
huru, lakini wanaCHADEMA 42 ambao hawakutajwa popote na tume wanasota gerezani.
Hata katika suala la Dk. Ulimboka, jeshi la Polisi halikutelekeza wajibu wake kikamilifu. Jeshi hilo
limekataa kumhoji Dk. Ulimboka na wala kuwahoji baadhi ya watuhumiwa wakuu wanaotajwa
kuhusika moja kwa moja katika kumteka Dk. Ulimboka, akiwemo Naibu Mkurugenzi wa Usalama wa
Taifa, Jack Zoka, Afisa wake Ramadhani Ighondo mwengine anayeitwa Nzowa.
Vilevile, kwenye tukio la kutekwa kwa Kibanda, ambalo linafanana kwa kiasi kikubwa na lile la Dk.
Ulimboka, Afisa Mtendaji Mkuu wa New Habari Corporation, Hussein Bashe, ametaja kuhusika kwa
polisi katika utekaji wa Absalom Kibanda, na baadaye akamtaja Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, lakini mpaka sasa, jeshi la Polisi halijachukua hatua
zozote ama kwa waliotajwa au kwa aliyetaja.
Lakini katika hili la Lwakatare CHADEMA kilipata taarifa mapema kuwa upo mkakati unaoratibiwa na
kufanikishwa na Naibu Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Jack Zoka na genge lake lenye wajumbe
mashuhuri, Ramadhani Ighondo na Nzowa linalotaka kukihusisha CHADEMA na njama za
kumdhuru Kibanda ili kukidhoofisha kisiasa. Lilipotokea hili la Lwakatare tukasema, sasa kile
tulichoambiwa ndiyo hicho kimekuja.
Bahati njema gazeti la Mwananchi la leo linasema Lwakatare anatuhumiwa kupanga njama za
kumdhuru Mhariri wa gazeti hilo, Denis Msacky, na kwamba Lwakatare amekamatwa baada ya
kuonekana kwenye video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii haraka inayomuonyesha
Lwakatare akipanga njama hizo hatujui baadhi ya taarifa zingine ingwa kwa hiki kilichopo kwenye
mtandao hakuna popote alipotajwa Msaky. Si nia yangu kuingilia upelelezi wa Polisi, lakini
nimesema CHADEMA tumefurahi kwa kuwa iwapo kwa utaratibu huu au wowote ule fursa
3
itapatikana na ukweli wote kutolewa hadharani. Ni imani yangu kuwa zoezi hili litafuata sheria na
taratibu zote zilizokwa na Katiba yetu kulinda haki za mtu.
Sasa kutajwa kwa Msacky inawezekana hilo la Kibanda halijaiva, au pengine liko njiani; ama
wameona aibu kuliingiza kwa sasa.
Lakini Waandishi wa Habari, mnajua kuwa mara baada ya Kibanda kutekwa, Ridhiwani Kikwete na
Nape Nnauye walivyoshangilia kutekwa kwa Kibanda katika mtandao huo huo uliotumika
kumkamata Lwakatare bila kuwakamata wahusika hao ambao waliingia kwenye mtandao kwa ID yao
wenyewe. Akiandika katika mtandao wake wa face book Ridhiwani alisema: “Na hili la Kibanda
mtasema ni kazi ya Ramadhani Ighondo, afisa usalama pale Ikulu?”
Kwanza, kauli hii ya Ridhiwani ilikuwa inathibitisha kwamba aliyepanga njama za kumteka Dk.
Ulimboka, ni Ramadhani Ighondo wa Ikulu.
Pili, Ridhiwani alikuwa anataka kuaminisha jamii kwamba katika hili la Kibanda, yeye na kundi lake
hawahusiki, bali wanaohusika ni CHADEMA; hivyo akawa anachokoza mjadala ambao
ulishapangwa ili baadaye vyombo vya dola viweze kuuchukua, na hivyo ndivyo ilivyotokea.
Tunazo taarifa kutoka vianzio vyetu vya ukakika ndani ya Usalama wa Taifa kuwa baada ya
Ridhiwani kuweka andishi lake kwenye facebook, aliingia kiwewe sana hasa baada ya Hussein
Bashe kuja juu. Ridhiwani anafahamu nguvu ya Bashe kwenye kufuatilia suala la kutekwa kwa
Kibanda na hivyo amemuomba baba yake kuvitumia vyombo vya dola kumuokoa. CHADEMA
haijawa na haitakuwa, lakini tuliyoambiwa yametimia, na mengine zaidi yanakuja, kwani kwa Taarifa
zetu hiyo yaliyotokea “ni cha mtoto”. Na wala hatutaki kutabiri mbinu zitakazotumika kumwokoa.
Ndugu waandishi wa habari; katika mlolongo wa kuwakamata viongozi wa CHADEMA, yumo
Mbunge wa Iringa, Mchungaji Msigwa. Mheshimiwa Msigwa tunaambiwa na watu wetu wamemtafuta
kwa muda mrefu sasa. Wanasema sumu anazotema bungeni na kwengineko dhidi ya idara ya
usalama ya taifa juu ya tuhuma za kuhusishwa na wizi wa nyara za serikali, zinawanyima usingizi na
hivyo wanataka wamnyamazishe.
Wanataka kujua kutoka kwa Msigwa ni nani aliyevujisha na kumpa taarifa zile za ujangiri wa
wanyama pori zinazohusisha CCM, usalama wa taifa, polisi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ). Msigwa anaonekana kuwa ni jasiri kusemea udhaifu wa idara ya usalama, wanaamini
anavyo vitu vingi na wao wangependa wajue ana nini na anapewa na nani.
Tayari Mchungaji Msigwa ameondolewa kwenye kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira
na kupelekwa Kamati ya Kilimo ili kulinda uchafu wa serikali, wakati yeye ni waziri kivuli wa
Maliasili na Utalii na Waziri kivuli anatakiwa kuwa Kwenye Wizara ya Sekta anayoisemea, na wala
hajaomba Wizara ya Kilimo.`ni dhahiri syndicate ya mfumo huu wa kutaka kuisambaratisha
CHADEMA. Huhitaji kwenda chuo Kikuu chochote, kuelewa hili.
4
CHADEMA kinafahamu kwa undani, kwamba uzushi huu wa Tape ya “Bukoba Boy”.Tunajua huu
umeanzishwa na kuhusisha Usalama wa Taifa, akiwemo Ighondo na wenziwe pale Ada Estate. Huyu
Ighondo ambaye anafahamika pia kwa jina la “Rama” tunamfahamu vizuri sana. Aliwahi kufanya
kazi ya katibu wa UV-CCM wilaya ya Singida Vijijini, kati ya mwaka 2006 na 2008 na ndiye aliyekuwa
akitumia simu na 0713760473 katika mawawsiliano yake na Dr. Ulimboka kwa simu na 0713731610
mpaka takriban dakika 3 kabla ya Ulimboka kutekwa. Gazeti la Mwanahalisi liliandika taarifa ya
uchunguzi ya kina ya Jambo hilo.
Rais wetu amenukuliwa na magazeti ya Serikali Addis Ababa akisema kuwa Mwanahalisi ilifungiwa
kwa sababu ya ‘kuchochea uasi katika majeshi yetu’ au maneno Kama hayo. Sitaki kumwita Rais
wetu wwongo leo lakini kwa kuwa Taarifa hiyo haijakanushwa wala na Rais, wala na Ikulu,
tunaamini maneno hayo ni kweli ametamka. Tunamtaka Rais Kikwete atamke maneno hayo hayo
hapa nchini. Kwa njia yeyote ili ili Watanzana wengi na hasa wasomaji wa Mwanahalisi, na hata
majeshi yetu amba kimsingi ninafahamu walilipenda Gazeti la Mwanahalisi wamsikie kwa masikio
yao wenyewe. Taifa linawekwa pabaya sana Rais anapofikia kutoa matamko ya upotoshwaji
mkubwa kiasi hicho tena nje ya nchi.
Ndiyo maana tunaposema Idara ya Usalama wa Taifa, ni tawi la CCM, tunaushahidi. Kwa mfano,
tunajua jinsi baadhi ya watendaji wajuu wa idara hiyo kama vile, Zoka na vibaraka wake wadogo
akiwamo Ighondo, ni radical wa CCM, wenye ushabiki uliopitiliza.
Hata ukiangalia jinsi walivyotekeleza mpango wa utekaji wa Dk. Ulimboka, kwamba walifanya hivyo
mbele ya macho ya Dk. Deogratias Michael, haraka utabaini kuwa utekaji huu ulifanywa kwa
ushabiki wa kulinda CCM.
Ndugu waandishi wa habari, kutokana na yote hayo hayo sasa tunasema ifuatavyo: Kwamba jeshi
la polisi lifanye kazi yake bila ushabiki wa kisiasa au shinikizo la wanasiasa.
Ndugu Waandishi,CHADEMA haiko tayari kuruhusu watu wenye maslahi binafsi kutuchafua mbele
ya jamii. Katika hilo, tutapambana na yoyote bila kujali cheo chake, madaraka yake serikalini, fedha
alizonazo au madaraka mengine.
Wakati polisi wakitekeleza hilo, tunamtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi,
ajitokoze hadharani kueleza umma juu ya mgogoro wake na Kibanda. Tunavyofahamu sisi, Kibanda
aliteuliwa kuwa mjumbe katika kamati ya kubuni vazi la taifa. Lakini alijitoa na kusema aliyemteuwa
yaani - Nchimbi - ambaye wakati huo, alikuwa waziri wa habari, utamaduni na michezo, ndiye
aliyeshinikiza polisi kumfungulia kesi ya uchochezi mahakamani.
Hadi sasa hatujapata taarifa za wazi zinazoonyesha kama uadui wa wawili hawa uliisha, na kwamba
Nchimbi sasa ndiye waziri wa mambo ya ndani, ambapo polisi wanawajibika kwake. Tuna mashaka
kuwa uchunguzi wa tukio lililomkuta Kibanda unaweza kudhoofika.
Kutokana na hayo yote CHADEMA tunasema nini sasa:-
5
i) CHADEMA katika hatua hii ya awali, tunafuatilia kwa karibu sakata lote la ukamataji wa
Lwakatare na kuona kama sheria za nchi, taratibu mbalimbali na misingi ya Haki za
Binadamu inafuatwa kuikamilifu.
ii) Tunarudia tena madai yaliyotolewa mara nyingi na CHADEMA, kwa Rais kuandikiwa
barua na Mwenyekiti wetu, Iundwe Judicial Commission of Inquiry (Tume Huru ya
Kimahakama kuchunguza vifo vyote vyenye utata na sura ya kisiasa). Serikali inaogopa
nini kuunda Tume hii huru ili ukweli Ujulikane? Iweje CHADEMA inayotuhumiwa
Kupanga njama wanaishinikiza Serikali kuunda Chombo huru na Serikali ndiyo
inayopata kigugumizi?
iii) Kwa wale walioumizwa na kujeruhiwa kama kina Ulimboka Kibanda na wengine,
tunarudia Tamko letu la kuwa hatuna Imani na uchunguzi unaofanywa na Jeshi la Polisi
kwa kuwa viongozi wa Jeshi hilo ni sehemu ya watu tunaowatuhumu kwa kuhusika kwa
njia mbalimbali, na Ushihidi wa wazi na Taarifa mbili za Serikali kupingana yaani Taarifa
ya Kamati yqa Nchimbi na Tume ya Haki za Binadamu. Tutaiaminije Polisi na Serikali
kwa Taarifa ya Kamati ya Nchimbi? Mwendawazimu tu anaweza kuwa na imani baada ya
Taartifa zile 3.
iv) Kuokana na upotoshwaji mkubwa, na kutokana na uhakika tulionao mkubwa
Mwanahalisi ilifungiwa si kwa sababu yeyote ile, bali kutoka na kukomalia swala la Dr
Uliomboka na hasa uhusika wa Ighondu, Afisa Usalama anayefanya kazi Ikulu chini ya
Raisi mwenyewe. CHADEMA sasa tunaitaka rasmi Serikali ifungulie Gazeti nla
Mwanahali kwa sababu hatuwezi kuendelea kuvumilia uikandamizaji huu wa uhuru wa
Habari, ambao sasa unaelekea kuota mizizi nchini kwetu. Na kweli ninawaomba na
kuwataka waandishi wote msimame imara, bila kujadili itikadi, au tofauti zetu zozote zile
na kusimamia uhuru wa Habari. Tunataka vivyo hivyo, kwa wanaharakati mbalimbali.
Waache hofu, eti wanaogopa kuhusishwa na vyama vya Siasa! Haki ni haki na haina
rangi ya bendera ya chama chochote.
Ndugu Waandishi Nawashukuru sana
Imetolewa Makao Makuu ya CHADEMA
KATIBU MKUU - CHADEMA
 
Jamani Kibonde anaumwa, na wenye ugonjwa huo WANAONGEA HAO kama nini!!!

ha ha ha, kuna mgonjwa mmoja mwenye ugonjwa huo sikumoja akiwa mahututi hospitalini basi ndugu na jamaa walivyokwenda kumsabahi akasema "tokeni hapa nitawagalagaza, mara akanyanyuka toka kitandani kufukuza watu ghafla akapiga kichwa chini" kwisha kazi.
 
Hakuna ubaya wowote Clouds kurusha hiyo Clip mimi kama Mtanzania mpenda amani nawapa pongezi sana uhalifu haukubaliki Tanzania ni nchi ya amani.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom