Hakuna Ubishi Mwabukusi ni Mwanaharakati, Je TLS Yake Iwe ya Kiharakati, Au Asilete Harakati Zake kwenye TLS Yetu, Ibaki Kuwa Profesheno Body?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
51,790
117,278
Wanabodi,
Hii ni makala yangu gazeti la Nipashe la leo
1722750065841.png

Hii ni makala yangu ya pongezi kwa Wakili Mwabukusi kuchaguliwa kuwa rais wa TLS, na kumpa ushauri wa bure, aibadili TLS kutoka kule juu ilipo, aishushe chini ground zero Ihudumie wananchi wa kawaida wanaohitaji huduma za kisheria, badala ya kuhudumia wanachama wake tuu.

Kwa vile yeye ni Mwanaharakati, namuomba sana, chonde chonde asituletee uana harakati wake kwenye TLS yetu , TLS sio chama cha siasa, sio chama cha ki harakati, TLS ni a Professional Body.

Hapa naomba kumtumia rais wangu wa TLS, rais wa r ndogo, Salaam rais wangu Mwanaharati Wakili Boniphase Mwabukusi, kutoka kwa Rais wa R kubwa, Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kuhusu TLS ya chama cha wanasheria na TLS ya chama cha kiharati
View: https://youtu.be/fZ7MWhPeyko?si=Fkur0u0qguoovPMo
Ila pia naishauri Serikali yetu tukufu na mihimili yake ya Bunge na Mahakama, sasa ikae mguu sawa, usiempenda kaja!, lazima ijifunze kusikiliza na kuwa sikivu kwa hoja za kiprofesheni za kisheria za TLS, kwasabu kwa hapa tulipo, tumeshuhudia, Serikali, Bunge na Mahakama Kiburi na Jeuri, yenye Madharau kuidharau TLS na hoja za TLS baada ya kufanikiwa kuwachomeka machawa wake kwenye uongozi wa juu wa TLS, hivyo kuiweka TLS mfukoni!.

Lakini safari hii, sisi wanasheria mawakili tunaotaka mabadiliko, tumewagomea kutupandikizia viongozi vibaraka, na kuamua kumchagua mtu independent, jasiri na mwanaharakati Mwabukusi, hivyo vyombo hivi vikiendeleza ile tabia yake mbaya ya kiburi na jeuri, this time around, watakula jeuri yao!, Mwabukusi sio mtu wa mchezo mchezo, wakileta zile za kuleta, hachelewi kuwapelekea moto na kuwawasha!.

Wiki hii, kumefanyika uchaguzi wa chama cha mawawili Tanzania, TLS, mmoja wa wagombea, alikuwa ni mtu “asietakiwa” (naomba nisiseme asietakiwa na nani), lakini zilifanyika juhudi mbalimbali kumkwamisha asigombee, Mahakama ndio ikaokoa jahazi kwa kumtendea haki, huyu si mwingine ni Wakili Msomi, Boniface Mwabukuzi, ambaye amechaguliwa kwa kishindo, hivyo sasa “usiemtaka kaja”, itakuwaje?.

Hivyo mimi mwandishi wako wa makala hizi, nikiwa pia ni mwanasheria, wakili na mwanachama wa TLS, pia nimeufurahia ushindi huu, nikiamini ni Mungu ndio amewezesha, kuna jambo la kisheria Mungu anataka kulifanya kwa watanzania, baada ya serikali yetu tukufu, kushindwa kulifanya tangu tulirejesha mfumo wa vyama vingi.

Ushindi wa Mwabukusi umepokelewa na vifijo na nderemo ukumbi mzima, hivyo unatuma ujumbe mzito kwa waliokuwa hawamtaki Mwabukusi kuwa sasa ndio yeye, ndiye kaja.

Mimi kama mwanachama wa TLS, sio mara moja au mbili, nimeeleza kupitia maandiko yangu mbalimbali jinsi TLS inavyonyamazia madudu ya kisheria yanayofanywa na serikali yetu, Bunge letu na Mahakama zetu.

Kwa vile mgeni rasmi Mkutano Mkuu wa TLS alipangwa awe Rais Samia, mimi niliwaandikia Waraka TLS, wamwambie nini Rais Samia Rais Samia Mgeni Rasmi AGM ya TLS: Wanasheria Tumweleze Ukweli Kuhusu Ubatili wa Katiba Yetu na Sheria Zetu, Turudishe Haki Kuu ya Msingi
Hii ni sehemu ya waraka huo.
Wanabodi,

Utambulisho

Japo sisi wanabodi wa jf, tunaitana wanabodi, na kutambuana kwa majina yetu ya ki jf jf, sio mbaya kunapotokea hoja ya msingi kwa mustakabali mwema ya nchi yetu, watu tukajitambulisha tena humu who we real are, hivyo mimi mwana JF mwenzenu, Pascal Mayalla, (Pasco wa JF) naomba kujitambulisha tena kwenu kuwa zaidi ya mimi kuwa ni mwana jf mwenzenu, na wengi wananifahamu kwa fani yangu ya mwandishi wa habari na mtangazaji wa kujitegemea kwa kujitolea.

Mimi pia ni mwanasheria, ni member wa TLS, na wakili wa kujitegemea pia kwa kujitolea, ila mimi sijiiti wakili msomi, wala sijaanza kwenda mahakamani, namalizana kwanza na sekta ya habari ndipo niugeukie uwakili active, hivyo kwa sasa mimi ni wakili mtangazaji, niliyejikita kwenye utoaji wa elimu ya katiba, sheria na haki, kupitia makala zangu kwenye magazeti ya Nipashe kila Jumapili, na Mwananchi kila Jumatano, na pia nina kipindi cha TV on Channel Ten kinachoitwa KMT kinachorushwa kila siku za Jumapili, saa 3:00 usiku. Kikizungumzia, katiba, sheria na haki.

Leo asubuhi nimeamka na habari njema sana kuhusu Mkutano Mkuu wa TLS. Habari yenyewe ni hii
Dear Members,

We hope this message finds you well.

As previously communicated, our 2024 Annual General Meeting (AGM) will be held in Dodoma from 1st through to 3rd August, 2024.

We are thrilled to officially announce that the Guest of Honor for our AGM will be Her Excellency, Dr. Samia Suluhu Hassan, the President of the United Republic of Tanzania. This is a significant milestone for us as the Bar Association of the Tanzania Mainland. We are honored to have our dear President officiating our AGM.

During the AGM, Her Excellency, Dr. Samia Suluhu Hassan will inaugurate the celebrations marking 70 years of the existence of the Tanganyika Law Society (TLS). Additionally, she will present awards and trophies to recognize and honor outstanding advocates in various categories. Her Excellency presence makes this event truly special and memorable.

We encourage all members to participate in honor of our dear President. Please register your attendance through Wakili database at your earliest convenience.

Hii maana yake ni Chama cha Mawakili Tanzania, TLS, kinaadhimisha miaka 70!, hiki ni moja ya vyama vikonge kabisa vilivyoanzishwa hata kabla ya Tanganyika kupata uhuru.

Chama cha Mawakili TLS ni nini na majukumu yake ni yapi?

Nimetembelea website yake.

1. Kitu cha kwanza nilichokutana nacho, ni lugha ya kimombo!. Naomba na mimi niende nao hivyo hivyo, ila kiukweli wakoloni wametufanya vibaya kwenye eneo la indoctrination!, Tanzania lugha yetu ya taifa ni Kiswahili ambacho ni lugha adhimu, lakini TLS wao ni kimombo tuu!, wale wenzangu na mimi wa St. Kayumba, mtanisamehe.

Ukiingia website yao, Tanganyika Law Society – TLS unapokelewa na makaribisho ya utambulisho wa TLS
WHO WE ARE
The Tanganyika Law Society (TLS) is the Bar association of Tanzania Mainland, founded in 1954 by an Act of Parliament – the Tanganyika Law Society Ordinance 1954. The Tanganyika Law Society is currently governed by the Tanganyika Law Society Act, Cap 307 R.E. 2002.
Integrity and Transparency
Assist the Public to access justice.
Legal Aid to Public.
24/7 Members Support

Kisha inakuja idadi ya wanachama wao, ambao na mimi nimo. Tanzania tuna mawakili 8,514 wanaofanya uwakili, mawakili 1,007 wasiofanya uwakili na mawakili 387 Waliotangulia mbele ya haki.

2. Our Vision
To become an independent bar association for a just society. (Kuwa chama huru kisichofungamana)
3. Our Mission
To create a conducive environment for the legal fraternity, facilitate the acquisition of legal knowledge, represent, promote and protect Members; to support the State Organs in legislation and administration of rule of law; and assist the Public to access justice in sustainable professional standards.
4. Our Goal
To promote professional excellence for efficient legal service delivery to ensure access to justice and rule of law.
5. Ndipo tunapata makaribisho ya rais wa TLS Wakili Harold Sungusia.

Kwenye Majukumu ya TLS, mimi naomba kujikita kwenye jukumu moja tuu, "to support the State Organs in legislation and administration of rule of law" kuisaidia serikali kwenye utungaji wa sheria na utawala wa sheria.

Kabla sheria yoyote haijatungwa, TLS kama wadau wa sheria, inapitishwa kwao, TLS wanatupa wanachama wao wote, fursa ya kutoa maoni, kisha TLS, wanapeleka maoni yake ya kisheria, ndipo sheria onatungwa.

Tangu nimejiunga TLS kuwa mwanachama wao, nomekuwa nahudhuria vikao vya kukusanya maoni ya TLS kuhusu ule mkataba wa IGA ya DPW na Bandari zetu, nikaipongeza TLS kwa maoni yake, lakini pia nikawatwanga na swali Kwa la Bandari, Pongezi TLS. Katiba yetu imenajisiwa. Bunge limetunga Sheria batili. Haki za Watanzania zimeporwa. Kwanini TLS wamenyamaza kimya?

Kiukweli kabisa maoni ya TLS yalikuwa solid!, serikali na Bunge, ilipigwa na kitu kizito!. Wito: Hoja za Kisheria za TLS, Prof. Shivji na wengine wote kupinga IGA, zisijibiwe Kisiasa kwa maneno matupu!, zijibiwe Kisheria kwa Vifungu! Hoja hizo za kisheria za TLS, zilipuuzwa!, hazikujibiwa, na TLS, ikanyamaza!

Yakaja mabadiliko ya sheria ya uchaguzi, kama kawaida TLS ikatoa fursa kwa sisi wanachama wake kutoa maoni yetu, siku ya siku serikali ikaitisha kikao kupokea maoni, TLS wakatoa maoni yake, serikali ikayapuuza na TLS wakanyamaza!.

Ubatili wa Katiba na Ubatili wa Sheria, na Kilio cha Haki
Kwa muda mrefu, nimekuwa nikipigia kelele ubatili wa katiba yetu, na ubatili wa sheria zetu uliopoka haki. kuu ya mzingi, haki ya kuchagua na kuchaguliwa iliyotolowe na ibara ya 5 ya katiba, inayompa kila Mtanzania haki na uhuru wa kuchagua viongozi anaowapenda kwa kuwapigia kura, na ibara ya 21 inayompa kila Mtanzania haki na uhuru wa kushiri kwenye kwenye serikali, toka serikali ya mtaa hadi serikali kuu kwa haki ya kugombea uongozi, lakini haki hizo kuu mbili, zikaja kupokwa na ibara ya 39 na 63, zilizochomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu, ambazo zinakwenda kinyume cha katiba ya JMT ya mwaka 1977.

Kwa mujibu wa katiba yetu hii yenye ubatili, ile haki ya kuchagua yaani haki ya kupiga kura kumchagua kiongozi yoyote unayempenda imepokwa na kukasimiwa kwa vyama vya siasa, kuwa Mtanzania hayuko huru tena kumchagua kiongozi anayemtaka, analazimishwa lazima amchague kiongozi aliyepitishwa na chama cha siasa. Na kwenye kugombea uongozi, Mtanzania hana haki ya kugombea kwa mujibu wa ibara ya 21, ili Mtanzania kugombea uongozi, analazimishwa, lazima ajiunge na chama cha siasa, hicho chama kimdhamini ndipo aruhusiwe kugombea!

Marais Sio Wanasheria, Wanaijua Katiba
Japo Marais Wetu Sio Wanasheria, Lakini Katiba Wanaijua, Kati ya Marais wote watano wa Tanzania, ni Rais Mwalimu Nyerere Pekee, Ndiye Aliitambua Haki hii imepokwa, Wanasheria Tumweleze Rais Samia, Airejeshe na kutuondolea ubatili huu ndani ya Katiba yetu.

Mimi Mwenyewe Tuu Binafsi Nina Mabandiko Humu zaidi ya 100, nikizungumzia jambo hili hili, nimezungumza kwa
  1. Humu JF kwa members wetu
  2. Kwa Kikosi Kazi -
    View: https://youtu.be/3a4SjkV46JY
  3. Nimezungumza kwa Wadau wa Siasa-
    View: https://youtu.be/Q2A65MLBLws
  4. Nimezungumza kwa Waheshimiwa Wabunge wetu.
    View: https://youtu.be/lBC3xKODSvY?si=f1B7XUdmfYvsk4nJ
  5. Ujio wa Rais Samia kwenye AGM yetu, hii sasa ni fursa adimu na adhimu ya kulizungumza hili, kwa Rais Samia.

Hili la ubatili wa katiba ni jambo kubwa na very serious, kabisa ambalo TLS ilibidi, wa deal nalo toka pale mahakama kuu iliutamka ubatili huo wa katiba na sheria hiyo.

Siku TLS, wametuita wadau wao, kututaka tuchangie maoni yetu kwenye mkataba wa DPW na bandari zetu, mimi niliwapongeza TLS

Nimelizungumza sana kwenye awamu hii ya 6 ya Rais Samia
  1. Haki, Haki, Haki! Serikali, Bunge na Mahakama hazina uwezo wala mamlaka ya kupora haki ya kuchagua na kuchaguliwa. Je, jicho ona litaliona hili?
  2. Mabadiliko ya Sheria Bila Mabadiliko ya Katiba,Sawa na Kula Bila Kunawa!. Je Watanzania Tuna Haraka Sana na Uchaguzi Hadi Tukimbilie Kula Bila Kunawa?
  3. Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi. Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!
  4. Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
  5. Ombi kwa Rais Samia: Sheria Mpya ya Uchaguzi Bado ina Ubatili. Haki ya Kuchagua na Kuchaguliwa imeporwa! Irejeshwe kwa Mujibu wa Katiba!
  6. Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa! Sheria ya Uchaguzi ni kosa. Kwanini tunarudia kosa? Haki si hisani, ni stahiki. Bunge tutendeeni haki!
  7. Japo Wengi Wamepania Kumzawadia Mwezi October 2025, Mimi Zawadi Yangu Nimemuaa Kuitoa Mapema, Kusubiria 2025 Will Be Too Little Too Late!
  8. Mabadiliko ya Sheria Bila Mabadiliko ya Katiba,Sawa na Kula Bila Kunawa!. Je Watanzania Tuna Haraka Sana na Uchaguzi Hadi Tukimbilie Kula Bila Kunawa?
  9. Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?
  10. Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
  11. Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
  12. Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
  13. Je, kuna kazi za kike na za kiume? Fupa hili lililowashinda wanaume wanne, mwanamke mmoja ataliweza?
  14. Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!
  15. Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?
  16. Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?
  17. Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?
  18. Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga. Kuzuiwa bila kifungu, kuruhusu bila Kifungu. Ni hisani ya Rais Samia. Haki kuhisaniwa hadi lini?
  19. Kwa la Bandari, Pongezi TLS. Katiba yetu imenajisiwa. Bunge limetunga Sheria batili. Haki za Watanzania zimeporwa. Kwanini TLS wamenyamaza kimya?
  20. Asante Rais kuruhusu mikutano, tunakuomba uruhusu haki nyingine ambayo imeporwa ya Watanzania wote kuchagua na kuchaguliwa
  21. Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
  22. Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!
Sasa maadam imejitokeza fursa ya TLS kuhutubiwa na Rais Samia, hii ni fursa adhimu na adhimu, kwa TLS tumweleze Rais Samia kuhusu ubatili wa katiba yetu unaonyima haki ya Watanzania kuchagua na kuchaguliwa! ambao wasaidizi wake hawamwambii, serikali yake imetutungia muswada batili wa sheria ya uchaguzi, Bunge likapitisha muswada huo, hivyo kukutungia tena sheria batili, na yeye akaisaini ianze kutumika na ubatili wake hivyo hivyo.

Sisi hatumlaumu Rais Samia kusaini sheria batili, kwasababu yeye sii mwanasheria kuujua ubatili huo, lakini wasaidizi wake ni wanasheria wanaujua fika ubatili wa katiba yetu na sheria zetu, , lakini hawamwambii, hivyo hii ni fursa, kwa TLS kutimiza wajibu wake kikamilifu kwa kumweleza ukweli Rais Samia, kuwa ni lazima tufanye kwanza mabadiliko madogo ya katiba, minimum reforms, ndipo twende kwenye uchaguzi.

Tumshauri Rais Samia kuwa Uchaguzi wa serikali za mitaa uhairishwe kwanza, tuondoe kwanza ubatili wa katiba, tufanye marekebisho ya sheria, ndipo twende kwenye uchaguzi, na uchaguzi huo wa serikali za mtaa, ufanyike siku moja na uchaguzi Mkuu na kusimamiwa na Tume moja huru na Shirikishi ya Uchaguzi!.

Paskali.

Hii maana yake ni Chama cha Mawakili Tanzania, TLS, kinaadhimisha miaka 70!, hiki ni moja ya vyama vikonge kabisa vilivyoanzishwa hata kabla ya Tanganyika kupata uhuru.

Kwenye Majukumu ya TLS, mimi naomba kujikita kwenye jukumu moja tuu, "to support the State Organs in legislation and administration of justice and the rule of law" kuisaidia serikali kwenye utungaji wa sheria na utawala wa sheria.

Kabla sheria yoyote haijatungwa, TLS kama wadau wa sheria, inapitishwa kwao, TLS wanatupa wanachama wao wote, fursa ya kutoa maoni, kisha TLS, wanapeleka maoni yake ya kisheria, ndipo sheria inatungwa.

Ushauri wangu wa kwanza kwa Wakili Mwabukusi, kwa vile hakuna ubishi kumhusu yeye kuwa ni mwanaharakati, ombi la kwanza, asiigeuze TLS kuwa TLS ya kiharakati, TLS ni profesheno body, lazima ifanye mambo yake ki profeshenali na sio kiharakati.

Kitu cha pili, aibadili TLS kutoka kuwa chama cha mawakili wasomi, kugeuka ni taasisi ya kuwahudumia wananchi, hivyo aishushe TLS took huko juu ilipo, aiteremshe chini kwa wananchi ikiwemo matumizi ya lugha yetu adhimu ya Kiswahili kwenye tovuti yake, kw asana ni kimombo tuu!.

Tangu nimejiunga TLS kuwa mwanachama wao, nomekuwa nahudhuria vikao vya kukusanya maoni ya TLS kuhusu ule mkataba wa IGA ya DPW na Bandari zetu, nikaipongeza TLS kwa maoni yake mazuri ya kisheria kwa mkata ule, , lakini pia nikauliza swali Kwa la Bandari, Pongezi TLS. Katiba yetu imenajisiwa. Bunge limetunga Sheria batili. Haki za Watanzania zimeporwa. Kwanini TLS wamenyamaza kimya? . TLS ya Mwabukusi, hili sio la kulinyamazia.

Yakaja mabadiliko ya sheria ya uchaguzi, kama kawaida TLS ikatoa fursa kwa sisi wanachama wake kutoa maoni yetu, siku ya siku serikali ikaitisha kikao kupokea maoni, TLS wakatoa maoni yake, serikali ikayapuuza na TLS wakanyamaza!. TLS ya Mwabukusi, tukitoa maoni ya kisheria kwa serikali yetu, isipotusikilize, tusinyamaze, tuibananishe kisheria.

Ubatili wa Katiba na Ubatili wa Sheria, na Kilio cha Haki
Kwa muda mrefu, nimekuwa nikipigia kelele ubatili wa katiba yetu, na ubatili wa sheria zetu uliopoka haki. kuu ya mzingi, haki ya kuchagua na kuchaguliwa iliyotolowe na ibara ya 5 ya katiba, inayompa kila Mtanzania haki na uhuru wa kuchagua viongozi anaowapenda kwa kuwapigia kura, na ibara ya 21 inayompa kila Mtanzania haki na uhuru wa kushiri kwenye kwenye serikali, toka serikali ya mtaa hadi serikali kuu kwa haki ya kugombea uongozi, lakini haki hizo kuu mbili, zikaja kupokwa na ibara ya 39 na 63, zilizochomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu, ambazo zinakwenda kinyume cha katiba ya JMT ya mwaka 1977.

Kwa mujibu wa katiba yetu hii yenye ubatili, ile haki ya kuchagua yaani haki ya kupiga kura kumchagua kiongozi yoyote unayempenda imepokwa na kukasimiwa kwa vyama vya siasa, kuwa Mtanzania hayuko huru tena kumchagua kiongozi anayemtaka, analazimishwa lazima amchague kiongozi aliyepitishwa na chama cha siasa. Na kwenye kugombea uongozi, Mtanzania hana haki ya kugombea kwa mujibu wa ibara ya 21, ili Mtanzania kugombea uongozi, analazimishwa, lazima ajiunge na chama cha siasa, hicho chama kimdhamini ndipo aruhusiwe kugombea!

Marais Sio Wanasheria, Wanaijua Katiba
Japo Marais Wetu Sio Wanasheria, Lakini Katiba Wanaijua, Kati ya Marais wote watano wa Tanzania, ni Rais Mwalimu Nyerere Pekee, Ndiye Aliitambua Haki hii imepokwa, Wanasheria Tumweleze Rais Samia, Airejeshe na kutuondolea ubatili huu ndani ya Katiba yetu.

Hili la ubatili wa katiba ni jambo kubwa na very serious, kabisa ambalo TLS ilibidi, wa deal nalo toka pale mahakama kuu iliutamka ubatili huo wa katiba na sheria hiyo ya TLS yetu ilinyamaza, TLS ya Mwabukusi, hili sio la kulinyamazia.

Naiomba sana TLS ya Mwabukusi iwe makini sana kwa kujipusha na uanaharakati, rudia tena kuusikiliza huu msimamo wa Rais Samia, kwa wanasheria wanaharakati wakileta za kuleta, na yeye atatumia sheria hizo hizo kuwabananisha.
Rudia kumsikiliza
View: https://youtu.be/fZ7MWhPeyko?si=Fkur0u0qguoovPMo

Tunaomba TLS ya Mwabukusi isiturudishe huko. Tunaomba tujikite kwenye profeshenolizimu Hivyo ujio wa rais Mwabukusi hii miaka 70 ya TLS ni fursa, kwa TLS kutimiza wajibu wake kikamilifu kwa kuwawezesha Watanzania wapate haki zao zilizoporwa kipindi kirefu.
Kwa heri Wakili Harold Sungusia, Karibu Wakili Mwabukusi

Mungu Mbariki Mwabukusi,

Mungu Ibariki TLS

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali.
 
Harakati zina tatizo gani?
Hakuna tatizo lolote kwa mtu kuwa mwanaharakati kwasababu harakati hazina tatizo kwa taasisi za ki harakati, TLS sio taasisi ya kiharakati, its a professional body. Professional bodies zinaendesha mambo yake professionally na harakati ndio zinaendeshwa ki harakati.
Mwana harakati kama Mwabukusu anapochaguliwa kuendesha a professiona body, there is a very thin line kati ya professionalism and activism!.
P
 
Sema we jamaa una kaujuaji Fulani ka kishamba.
Kuhusu ushamba, sisi watu wa kanda ile ni washamba sana.
BAK is far better than you.
Kwani kuna mashindano humu who is good, better and best? kila mtu ana maeneo yake ya kujidai, ni kila mtu is good, better and best depends ni kwenye nini, yes anaweza kuwa better than me, lakini na mimi ni better kuliko mwingine!, hata kwenye top ten, wa kumi ndie wamwisho but is better than wa 11 etc,
P
 
Wanabodi,
Hii ni makala yangu gazeti la Nipashe la leo
View attachment 3060994
Hii ni makala yangu ya pongezi kwa Wakili Mwabukusi kuchaguliwa kuwa rais wa TLS, na kumpa ushauri wa bure, aibadili TLS kutoka kule juu ilipo, aishushe chini ground zero Ihudumie wananchi wa kawaida wanaohitaji huduma za kisheria, badala ya kuhudumia wanachama wake tuu.

Kwa vile yeye ni Mwanaharakati, namuomba sana, chonde chonde asituletee uana harakati wake kwenye TLS yetu , TLS sio chama cha siasa, sio chama cha ki harakati, TLS ni a Professional Body, ila pia naishauri Serikali yetu tukufu na mihimili yake ya Bunge na Mahakama, sasa ikae mguu sawa, usiempenda kaja!, lazima ijifunze kusikiliza na kuwa sikivu kwa hoja za kiprofesheni za kisheria za TLS, kwasabu kwa hapa tulipo, tumeshuhudia, Serikali, Bunge na Mahakama Kiburi na Jeuri, yenye Madharau kuidharau TLS na hoja za TLS baada ya kufanikiwa kuwachomeka machawa wake kwenye uongozi wa juu wa TLS, hivyo kuiweka TLS mfukoni!.

Lakini safari hii, sisi wanasheria mawakili tunaotaka mabadiliko, tumewagomea kutupandikizia viongozi vibaraka, na kuamua kumchagua mtu independent, jasiri na mwanaharakati Mwabukusi, hivyo vyombo hivi vikiendeleza ile tabia yake mbaya ya kiburi na jeuri, this time around, watakula jeuri yao!, Mwabukusi sio mtu wa mchezo mchezo, wakileta zile za kuleta, hachelewi kuwapelekea moto na kuwawasha!.

Wiki hii, kumefanyika uchaguzi wa chama cha mawawili Tanzania, TLS, mmoja wa wagombea, alikuwa ni mtu “asietakiwa” (naomba nisiseme asietakiwa na nani), lakini zilifanyika juhudi mbalimbali kumkwamisha asigombee, Mahakama ndio ikaokoa jahazi kwa kumtendea haki, huyu si mwingine ni Wakili Msomi, Boniface Mwabukuzi, ambaye amechaguliwa kwa kishindo, hivyo sasa “usiemtaka kaja”, itakuwaje?.

Hivyo mimi mwandishi wako wa makala hizi, nikiwa pia ni mwanasheria, wakili na mwanachama wa TLS, pia nimeufurahia ushindi huu, nikiamini ni Mungu ndio amewezesha, kuna jambo la kisheria Mungu anataka kulifanya kwa watanzania, baada ya serikali yetu tukufu, kushindwa kulifanya tangu tulirejesha mfumo wa vyama vingi.

Ushindi wa Mwabukusi umepokelewa na vifijo na nderemo ukumbi mzima, hivyo unatuma ujumbe mzito kwa waliokuwa hawamtaki Mwabukusi kuwa sasa ndio yeye, ndiye kaja.

Mimi kama mwanachama wa TLS, sio mara moja au mbili, nimeeleza kupitia maandiko yangu mbalimbali jinsi TLS inavyonyamazia madudu ya kisheria yanayofanywa na serikali yetu, Bunge letu na Mahakama zetu.

Kwa vile mgeni rasmi Mkutano Mkuu wa TLS alipangwa awe Rais Samia, mimi niliwaandikia Waraka TLS, wamwambie nini Rais Samia Rais Samia Mgeni Rasmi AGM ya TLS: Wanasheria Tumweleze Ukweli Kuhusu Ubatili wa Katiba Yetu na Sheria Zetu, Turudishe Haki Kuu ya Msingi
Hii ni sehemu ya waraka huo.

Hii maana yake ni Chama cha Mawakili Tanzania, TLS, kinaadhimisha miaka 70!, hiki ni moja ya vyama vikonge kabisa vilivyoanzishwa hata kabla ya Tanganyika kupata uhuru.

Kwenye Majukumu ya TLS, mimi naomba kujikita kwenye jukumu moja tuu, "to support the State Organs in legislation and administration of justice and the rule of law" kuisaidia serikali kwenye utungaji wa sheria na utawala wa sheria.

Kabla sheria yoyote haijatungwa, TLS kama wadau wa sheria, inapitishwa kwao, TLS wanatupa wanachama wao wote, fursa ya kutoa maoni, kisha TLS, wanapeleka maoni yake ya kisheria, ndipo sheria inatungwa.

Ushauri wangu wa kwanza kwa Wakili Mwabukusi, kwa vile hakuna ubishi kumhusu yeye kuwa ni mwanaharakati, ombi la kwanza, asiigeuze TLS kuwa TLS ya kiharakati, TLS ni profesheno body, lazima ifanye mambo yake ki profeshenali na sio kiharakati.

Kitu cha pili, aibadili TLS kutoka kuwa chama cha mawakili wasomi, kugeuka ni taasisi ya kuwahudumia wananchi, hivyo aishushe TLS took huko juu ilipo, aiteremshe chini kwa wananchi ikiwemo matumizi ya lugha yetu adhimu ya Kiswahili kwenye tovuti yake, kw asana ni kimombo tuu!.

Tangu nimejiunga TLS kuwa mwanachama wao, nomekuwa nahudhuria vikao vya kukusanya maoni ya TLS kuhusu ule mkataba wa IGA ya DPW na Bandari zetu, nikaipongeza TLS kwa maoni yake mazuri ya kisheria kwa mkata ule, , lakini pia nikauliza swali Kwa la Bandari, Pongezi TLS. Katiba yetu imenajisiwa. Bunge limetunga Sheria batili. Haki za Watanzania zimeporwa. Kwanini TLS wamenyamaza kimya? . TLS ya Mwabukusi, hili sio la kulinyamazia.

Yakaja mabadiliko ya sheria ya uchaguzi, kama kawaida TLS ikatoa fursa kwa sisi wanachama wake kutoa maoni yetu, siku ya siku serikali ikaitisha kikao kupokea maoni, TLS wakatoa maoni yake, serikali ikayapuuza na TLS wakanyamaza!. TLS ya Mwabukusi, tukitoa maoni ya kisheria kwa serikali yetu, isipotusikilize, tusinyamaze, tuibananishe kisheria.

Ubatili wa Katiba na Ubatili wa Sheria, na Kilio cha Haki
Kwa muda mrefu, nimekuwa nikipigia kelele ubatili wa katiba yetu, na ubatili wa sheria zetu uliopoka haki. kuu ya mzingi, haki ya kuchagua na kuchaguliwa iliyotolowe na ibara ya 5 ya katiba, inayompa kila Mtanzania haki na uhuru wa kuchagua viongozi anaowapenda kwa kuwapigia kura, na ibara ya 21 inayompa kila Mtanzania haki na uhuru wa kushiri kwenye kwenye serikali, toka serikali ya mtaa hadi serikali kuu kwa haki ya kugombea uongozi, lakini haki hizo kuu mbili, zikaja kupokwa na ibara ya 39 na 63, zilizochomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu, ambazo zinakwenda kinyume cha katiba ya JMT ya mwaka 1977.

Kwa mujibu wa katiba yetu hii yenye ubatili, ile haki ya kuchagua yaani haki ya kupiga kura kumchagua kiongozi yoyote unayempenda imepokwa na kukasimiwa kwa vyama vya siasa, kuwa Mtanzania hayuko huru tena kumchagua kiongozi anayemtaka, analazimishwa lazima amchague kiongozi aliyepitishwa na chama cha siasa. Na kwenye kugombea uongozi, Mtanzania hana haki ya kugombea kwa mujibu wa ibara ya 21, ili Mtanzania kugombea uongozi, analazimishwa, lazima ajiunge na chama cha siasa, hicho chama kimdhamini ndipo aruhusiwe kugombea!

Marais Sio Wanasheria, Wanaijua Katiba
Japo Marais Wetu Sio Wanasheria, Lakini Katiba Wanaijua, Kati ya Marais wote watano wa Tanzania, ni Rais Mwalimu Nyerere Pekee, Ndiye Aliitambua Haki hii imepokwa, Wanasheria Tumweleze Rais Samia, Airejeshe na kutuondolea ubatili huu ndani ya Katiba yetu.

Hili la ubatili wa katiba ni jambo kubwa na very serious, kabisa ambalo TLS ilibidi, wa deal nalo toka pale mahakama kuu iliutamka ubatili huo wa katiba na sheria hiyo ya TLS yetu ilinyamaza, TLS ya Mwabukusi, hili sio la kulinyamazia.

Naiomba sana TLS ya Mwabukusi iwe makini sana na Rais Samia, aliishawahi kutangaza msimamo wake kuwa wanasheria wakileta za kuleta, nay eye atatumia sheria hizo hizo kuwabananisha, tunaomba tujikite kwa profeshenolisim. Hivyo ujio wa rais Mwabukusi hii miaka 70 ya TLS ni fursa, kwa TLS kutimiza wajibu wake kikamilifu kwa kuwawezesha Watanzania wapate haki zao zilizoporwa kipindi kirefu.
Kwa heri Wakili Harold Sungusia, Karibu Wakili Mwabukusi

Mungu Mbariki Mwabukusi,

Mungu Ibariki TLS

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali.
Harakati ni nin?
Mwanaharakati ni mtu wa aina gani?
Naomba msaada
Pia ntafarijika nikijua faida na hasara za kua mwana wa harakati kwa jamii...
 
kama ulikuwa haujui, wanasheria wote ni wanaharakati, na hawana mwanaume wala mwanamke.wote ni wanaharakati. ndio maana walipigiwa kampeni na pengine kupewa hadi pesa wapige kinyume na mwabukusi wakawa wanawazoom tu, pesa walichukua na kura wanajua watakakozipeleka. usifanye mchezo na mwanasheria, tunajuana sisi wenyewe.
 
Kwahiyo na huyu kumbe alimpa boss kura yake
 
Back
Top Bottom