blackstarline
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 3,517
- 8,872
Bora umesema huyu mvuta bangi alikua na nini haswa kiasi cha kufuatiliwa na CIA , watuw ajinga sana kwa kuamini kila lisemwalo kwnye internet .
Jamaica ilikuwa ni nchi yenye upinzani mkali wa kisiasa.Vyama viwili vikubwa vya kisiasa nchini humo wakati huo vilikuwa ni Jamaica Labour Part(JPL) kilichoongozwa na Edward Seaga na chama cha Peoples’National Part kilichoongozwa na Michael Manley.Ghasia za kisiasa zilitokea mara kwa mara. Michael Manley na chama chake cha Peoples’National Part wakiwa madarakani chama chao kilikuwa kinaeneza ujamaa na wa kisaidiwa na Fidel Castro wa Cuba, wakiwa na lengo kueneza ujamaa visiwa vyote vya Caribean Hii haikuwa habari njema kwa adui mkuu wa ujamaa Marekani, kwa kulitumia shirika lake la ujasusi, CIA Marekani ikapanga kumdhibiti Michael Manley kwa njia mbili; kumwandalia mpinzani watakae msapoti kwa kila kitu. Akaandaliwa Edward Seaga kupitia chama Jamaica Labour Party, Wakamwezesha kwa kila kitu wakati ukikaribia uchaguzi mkuu uliokuwa ukifuata 1976. Pili; kumchonganisha Michael Manley na wananchi, wakatengeneza mazingira ya vurugu, Jamaica ikashuhudia mauaji makubwa mitaani, vurungu mateso na kila aina ya ubabe, Nchi ikawa inaelekea kutotawalika. Ili mkakati huo ufanikiwe zaidi ni lazima wananchi wawe upande wa mpinzani mkuu kibaraka wa Marekani Edward Seaga hivyo CIA wakapanga kumtumia Bob Marley kwa namna yoyote, Bob alikuwa ni habari nyingine kwa wa jamaica kwao alikuwa ni super star mkubwa kabisa. CIA waliamini kuhusika kwa Bob kwenye harakati zao kungesaidia kuwavuta watu kuwa upande wao. Kwanza wakataka kumuua ili kuwaminisha wananchi serikali iliyo madarakani imeshindwa kuwalinda raia wake, hivyo wamkatae Michael Manley na wamchague Edward Seaga kwenye uchaguzi ujao. Wakamvamia Bob nyumbani kwake na kumpiga risasi, lakini kwauwezo wa Mungu alinusurika kifo. yeye mwenyewe alishtukia ule ulikuwa mchezo mchafu wa CIA alipotoka hospitali, akawatungia wimbo wa AMBUSH IN THE NIGHT
Ambush in the night all guns aiming at me, Ambush in the night They opened fire on me now, Ambush in the night, Protected by his majesty
Walinivamia usiku wa manane bunduki zote zilielekwezwa kwangu, wakanifyatulia risasi nikalindwa na aliye mkuu Mungu Mara nyingi Bob hakuwa akiwataja majina anaowalenga kwenye mashairi yake ila alitumia mafumbo rahisi ambayo watu wakawaida waliweza kuyafumbua na kuelewa alicho maanisha. Hata kwenye AMBUSH IN THE NIGHT, Bob hakutaja majina ya aliowatuhumu kujaribu kumuua bali alielezea sifa zao. See them fighting for power,
But they know not the hour,
so they bribing with their guns, spare-parts and money, trying to belittle our integrity now .
they say what we know
is just what they teach us;
And we’re so ignorant
Cause every time they can reach u
through political straterg.
But they know not the hour,
so they bribing with their guns, spare-parts and money, trying to belittle our integrity now .
they say what we know
is just what they teach us;
And we’re so ignorant
Cause every time they can reach u
through political straterg.
Waone wanavyopigania madaraka,
Hawajui saa yenyewe watakayoyapata hayo madaraka
Hivyo wanatoa hongo na bunduki zao vipuri na pesa,
Wakijaribu kutushushia heshima yetu ,
Wanasema kile tunacho kijua ni kile tu walichotufundisha,
Na kwamba eti sisi ni wajinga kwa sababu wakati wowote
Wanaweza kutufikia kwa mikakati yao ya kisiasa.
Sifa hizi ni za Marekani na Wakala wake mkuu CIA , Wao ndiyo waliokuwa wakihonga silaha kwa magenge ya wahuni kufanya vurugu. Wao ndiyo waliokuwa wakitoa pesa kufadhili harakati za kuidondosha serikali ya kidemokrasia ya Michael Manley .
Baada ya kushindwa kumuua Bob Marley CIA wakamshawishi awe upande wao ili kuwavuta wananchi , walijua wakifanikiwa kupata uungwaji mkono na Bob watakuwa wamepata uungwaji mkono na wajamaica kwa sababu wajamaica walimsikiliza na kumwamini sana Bob, Bob akakubali kwa sharti la kuwapatanisha kwanza Michael Manley na Edward Seaga Bob aliamini wanasiasa hao wakipatana mtaani kutakuwa hakuna vurugu tena .
Baada ya wanasiasa hao kupatanishwa Bob akatunga nyimbo ya RAT RACE nyimbo ambayo iliwalenga wabaya wake CIA. DON’T INVOLVE RASTA IN YOUR SAY SAY RASTA DON’T WORK FOR NO CIA. Bob Marley alikuwa habari nyingine aliimba vitu vingi ambavyo vinatoke na vitazidi kutokea.