Some references za Tanzania kwenye National Archive:
na hapa:
wanakiita Checklist of African Problems:
The Americans took a lead from Nyerere:
National Security Estimates Oct 21, 1976
Miaka mitano kabla yake, Wamerekani katika hicho hicho wanachokiita National Security Estimates waliandika hivi:
Na kuhusu Political Stability waliandika hivi, wakiwa wanafuatilia vinavyoendelea Tanzania:
hivyo ni vichache tu...
MKJJ hayo uliyoandika hapo juu ni inteligensia declassified....Zetu bado hatujafanya hivyo na kwa hiyo kama kuna wanaojuwa siri za nchi ndio wanaoelewa kinachoendelea...Lakini watu kama sisi tuna common sense na kwahiyo tuna uwezo wa ku connect the dots.
Honestly maelezo yako yote kama ukipitia michango yangu kuanzia ule mjadala wa Zimbabwe...Utaelewa pamoja na maswali niliyouliza kwenye posting yangu ya kwanza kwenye mjadala huu....Na ndio maana simlaumu Nyani kwasababu anataka maelezo...Na kwasababu umetowa upande mmoja wa CIA...Then towa na upande wa UWT.
Leo Kweli,Mag3 na Isaya Mwita....Issue ya Isarael imekaa hivi:
1)Kuna mitizamo ya tofaut pale inapokuja kwenye historia ya Taifa la Israel...Nayo ni kama ifuatayo kwenye vipengele a,b na c..
a)Mtizamo wa Wakristo:Mtizamo wa wakristo ni kuwa Israel belongs to the middle east na jerusalem ni mji mtakatifu. Jambo hilo pia linaaminiwa na Jews wenyewe....Hapa pamekuwa na gogoro kubwa kwani historia ya darasani haisemi kuwa wayahudi hapo Palestina ni kwao.
b)Muslim people; wao nao wanaamini pia kuwa jerusalem ni mji mtakatifu kwani hapo ndipo mahali ambapo kuna historia muhimu kwao wao na mtume wao....Na msikiti wao maarufu na mtakatifu uko hapo...
Na pia kuna mchanganyiko...
Jerusalem imegawanyika mara nnne....Wajews, wakristo, waislam na warumi...Wote hao waliitawala Jerusalem kwa vipindi tofauti kwenye historia yetu....Na kwa hiyo Obama yeye anataka waishi pamoja kama vile tunavyotaka tuishi kwa usawa na umoja baina ya weupe, weusi,waoriental, waarabu na jews...Kamwe mwafrika asichaguwe BWANA!
c)Modern History:Kwa historia ya dunia ya kwetu ya sasa...Israel imefikisha miaka 60 juzi tu toka izaliwe....Na kiukweli...Mtu aliyesaidia uanzishwaji wa Taifa hilo ni muingereza...Kwani ilikuwa ni territories zake..Na hilo alilifanya mara baada ya kusaidiwa na mmarekani kwenye vita ya pili ya dunia...Ni Churchill kama asingepewa msaada na mmarekani basi HITLER alikuwa amchukue mwingereza kiulaini kabisa.
Ni wazi kulikuwepo na makubaliano kati ya Churchill na Roosevelt...Na labda Hoover kabla ya hapo wakati wa The Great Depression.
Ila sasa matatizo ya Hitler...Kama wanavyodai waarabu na waislam wengine...Wapalestina hawakuwafanya chochote wa jews huko Ujerumani kiasi cha kupelekewa ngarambe hiyo...Kwani mara baada ya holocaust...Wale Jews walipakizwa kwenye meli kubwa za wanigereza na wamarekani wakamwagwa Huko middle east maeneo ya Palestine territories ambayo yalikuwa chini ya mwingereza.
Na wapalestina wakapambana na Yasser Arafat na yeye pia...Baadae kafa kifo cha utatanishi sana....Na aliyekuwa akimminya naye akafa...Sijui nasikia bado yuko hai...Ni huyo Sharon ambaye kwa kweli na yeye historia yake si nzuri hata kidogo pale inapokuja kwenye ubinadamu.
Hivyo Uingereza wana part kubwa ya kuplay kwenye mgogoro huu kwa kufanikisha hao watu waweze kuishi pamoja na si kuchaguwa upande hata mara moja...Hilo litakuwa hatari..Kwasababu mtu kama mchina yeye hana dini wala nini...Kwa hiyo mwarabu akimuonyesha historia ya dunia halafu na yeye akamwambia kuwa na sisi tunataka mtetezi kama vile mmarekani anavyomtetea muisrael...Halafu kwasababu mchina si mkristo wala musilam...Anaweza kumsadia mwarabu nyuklia na hapo ndipo penye tabu...Maana walisema jeshi la waisraeli ndio kiboko zaidi duniani...Sasa sijui la mchina nalo vipi....Tuombe Mungu aepushie mbali..Ni balaa!
Kwa sasa ngoja nifikie hapa kwa ujumbe huu kwako Leo Kweli...Si kweli kuwa Jews wote ni wabaya...Na ndio maana Yitzak Rabin Aliuwawa na wale ma extrimist...Nilishawahi kusema too much of anything is harmful hata kama ni medicine...You overdose it kills you.
Hata waislam si wote wabaya...Tukiwa na sterio type hatutaweza kuepuka mapigano kwani hatutaweza kukaa mezani na kuongea kama kutakuwa na chuki mbaya baina ya wanadamu.
Na ndio maana namsapoti Obama badala ya Clinton kama unavyofanya wewe...Na hao kina Young ambao ni movement corrupt na siyo ile halisi ya MLK NA JFK.
Kwa upande wa Tanzania chini ya mwalimu tumeweza kuona kuwa uchumi na kila kitu tuliwategemea uchina..Na bado tunafanya hivyo..Kwani ni wazi mchina anaogopeka toka kitambo na ndio maana alimsaidia Mwalimu na Uingereza wakagwaya kumsaidia Amin licha ya kwamba hawakumpenda Obote na huku walijuwa ni Obote nayerudishwa na mchina kwa kupitia Mwalimu.
Lakini sasa ndio maana nakwambia kuwa...This time ni mwafrika kwanza..Na tusianze chuki dhidi ya west kwani kama kweli west na wao wakibadilika na kutusikiliza...Basi hata uchina nao wataacha kutupa yale masharti ya kulazimishia kuturundikia raia wake nchini mwetu simply kwasababu eti wanatusaidia kiuchumi na kivita!
Cha muhimu NI UHURU KWANZA.
Kwasasa naishia hapa..Ila mjadala uendelee na pia mnapoleta hizo declassified..Mfanye pia jitihada za kumwelisha Nyani badala ya kum dhihaki.
Ahsanteni.
NB:Tuhakikishe tunajibana maswali yetu kwani ni muhimu...Na kama hatujaelewana na kuna maswali..Basi tujibiane kistaarabu na kwa kuelemishana...Lakini haina maana ku ignore maswali ya watu halafu kinachoandikwa ni kama kilitakiwa kielezewe ili Nyani wa watu asighafirishwe na kufungiwa tena na wanamtandao.